Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,550
- 6,062
Pamoja sana Mkuu. Ila milele kwenye mambo ya ndege, kipindi kibaya huwa ni wakati wa kuruka/kupaa na kutua. Kupaa hatari yake kubwa ni kitu chochote kikiingia kwenye Engine kama ulivyoona Videos. Wakati wa kutua, huwa ni UPEPO mkali ukiwepo uwanjani na matairi yakigoma kutua. Pia kwenye viwanja vya kizamani ama siyo advanced, kama kuna giza, ukungu nk huwa ni kashehse.
Kwa nchi za wenzetu kama Russia, Sweden, Finland, Norway, Canada, nk pia wana tatizo wakati wa Winter kuwa kabla ndege haijapaa, lazima waiyeyushe barafu kwenye ndege nzima. Kama barafu imeganda na ndege ikaruka na hiyo barafu, basi huzidi kuganda na kuongezeka wakati inapaa na mwisho kuwa mzigo mzito sana kwa ndege na hiyo hupelekea ndege kuanguka. Juzi tu moja imeanguka Russia kwa kosa hilo kama uliona.
Kwa hiyo milele kumbuka kuwa ndege (BIRDS) kwenye viwanja vya ndege, NI HATARI SANA na si kama ulivyosema kuwa si kitu cha kutisha. Ndiyo maana huyo Rubani wa USA na rubani wa Poland, ilipelekea hadi kuwakutanisha na kuwapa hongera kwani mambo waliyoyafanya yalikuwa yanatisha ingawa wote walicheka na kusema "hili angeliweza kulifanya kila rubani mwenye uzoefu kama wangu......" Hongera kwa marubani wote kwa kazi ngumu waifanyayo inayohitaji Uwe na Nerves ngumu kama chuma.

Sikonge, nimeipenda hii, kiwango chako cha uelewa na kujadili jambo umepevuka. Hakuna binadamu mwenye uelewa wa kila jambo, ndio maana hapa tunajitahidi kuwaka mada za kuelimishana, kupashana habari na kutahadharisha, kwani kwa maoni mbalimbali kama yako uliyotoa yanatusaidia wengi kupanua zaidi wigo wa upeo wetu katima masuala ambayo hatujawa na uelewa mkubwa.
Sidhani hoja za mipasho zinaweza kutusaidia ila tu mradi mtu ameweka mstari ndani ya mada inayojadiliwa, haya ya uzoefu na upeo wa akina Sikonge ndiyo tunayotaka.
Thanks Sikonge.