Rtd General Mboma, Mhando wa TANESCO na Mh. Mbunge - ni Hatari!!

Na we unataka mambo ya NMC kama Mkwasa?we utaweza lkn?
Miya ndo maana nasema tatizo hilo linaleta ukiburi wa pesa na mengineyao, yuko Mbunge mmoja mzanzibari mwanamama ilibidi wamkate mapanga huko Area C Bunge lilopita
Haya kuhusu hoja ya Mh. Mbunge huyu ni kweli tuisubiri hii Wizara ya kina Simbachawene na utawaona watakavyochangia kwa kujishebedua kumtetea Mhando mm nachoombaumeme usikatwekatwe tena.
Ila Miya km unamtaka huyo msagaji nitakuelekeza ww utamuweza
 
Mie haka..nimekuuliza weye mana toka asubuh unazungumzia NMC na Mkwasa nkajua umezidiwa
 
hebu tumwangie mpunga huo hapa mkuu
Hili jukwaa halifai hamia lile lingine (MK)saa hizi saa 7 usiku watoto na vidampa hawajalala, kwani mambo yaliyomkuta kocha wa Queens ww utayaweza?
Chao g9t palalisote hebu rudi kwenye mada au subiri Bajeti ya Wizara hapa ndio Dodoma
 
Yaani bachelor of scince in electronics ni elimu ya kuungaunga wewe mbunge darasa la ngapi? usilete udaku udaku hapa kama huna taarifa za uhahika kajipange.
 
Hili jukwaa halifai hamia lile lingine (MK)saa hizi saa 7 usiku watoto na vidampa hawajalala, kwani mambo yaliyomkuta kocha wa Queens ww utayaweza?
Chao g9t palalisote hebu rudi kwenye mada au subiri Bajeti ya Wizara hapa ndio Dodoma

kwangu huku bado mchana
 
Kwa ufupi ni kwamba Mbona anajulikana kuwa na dirty deals katika serikali tangu akiwa mkuu wa majeshi. Ukweli ni kwamba William Mhando ameonekana kutishia maslahi mfu ya wakubwa ndiyo maana sasa hawamtaki. Usishangae akarudishwa Idris Rashid. Hii ndiyo Tanzania.
 
Kwa ufupi ni kwamba Mbona anajulikana kuwa na dirty deals katika serikali tangu akiwa mkuu wa majeshi. Ukweli ni kwamba William Mhando ameonekana kutishia maslahi mfu ya wakubwa ndiyo maana sasa hawamtaki. Usishangae akarudishwa Idris Rashid. Hii ndiyo Tanzania.

Rumours has it he fuelled rebels in DRC against UN embargo.
 
Lakini mtu mweusi jamani.... mimi nikifa nikifika mbele ya Mola kitu cha kwanza nitamwomba anifungulie kichwa cha mtu mweusi mbele yangu nione ameweka nini ndani yake!
 
Eng. Nsiande yu wapi atumegee footnotes? maana nchi inapoenda sasa ni vigumu sana kujua nani anasema ukweli, sisi wavuja-jasho tumebaki njia panda hatuna wa kumwamini tena..hatujui mstaq'bali wa kodi zetu..ama kweli JK ni legelege na dhaifu.
 
Kweli Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu; madili kuanzia ikulu mpaka kwenye mgao wa umeme?
Mtu unashangaa, nchi gani hii mgao wa umeme mwaka mzima?

Eng. Nsiande, njoo huku utumegee ya huko kwenu. Mnatudangana kuna mgawa wa umeme kumbe mgao wenyewe ni mafisadi made!
 
Mbunge anakuwa na avatar za ajabu ajabu na ID za kihuni ? Jifunze kwa wenzako wakina mnyika kigwagallah na zito wanakuja hapa Kama wao wewe ni mla rushwa mkubwa ndio maana unajificha na Id za ajabu ajabu unaleta umbeya hapa jamvin mods piga ban hili gamba. Mbona sijawahi kusikia speaker Akisema swali la nyogeze mheshimiwa babykailama
 
Mbunge anakuwa na avatar za ajabu ajabu na ID za kihuni ? Jifunze kwa wenzako wakina mnyika kigwagallah na zito wanakuja hapa Kama wao wewe ni mla rushwa mkubwa ndio maana unajificha na Id za ajabu ajabu unaleta umbeya hapa jamvin mods piga ban hili gamba. Mbona sijawahi kusikia speaker Akisema swali la nyogeze mheshimiwa babykailama
Nakuunga mkono na miguu au mwili mzima kabisa. Kiongozi kama mbunge atajifichaje na ID za kihuni!!! Nitatofautishaje uhuni huo na thread yake iliyojaa umbeya wa vijiwe vya kahawa na kashata!! Mods piga ban mbeya huyu mara moja.
 
Na declare interest kuwa mimi ni Mbunge na nimeamua kuanzisha hii therad ili tuwekane sawa hapa baada ya kukamilisha uchunguzi wangu.

· Kuna Mbunge mmoja wa kike juzi aliniomba tupate naye chakula na tulipokaa alianza kunishawishi kwa kwa nguvu nyingi sana kuwa tuikatae kwa nguvu zote bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini itakapowasilishwa na tukiweza tumseme sana na kumkataa Katibu wa Wizara hiyo kuwa hafai. Aidha alikuwa ananisisitizia niwambie na wengine hivyo na kwamba tumpongeze MD William Mhando maana anafaa sana. Mwisho wa chakula alikataa nisilipe na akanilipia na pia kutaka kunipa fedha za mafuta kwa ajili ya gari langu kitu nilichomkatalia.


· Jana na leo baada ya hili la kuwasimamisha watumishi wa TANESCO nikaona niingie ndani kutafiti undani wa kinachoendelea na nikaunganisha zile juhudi za Mbunge mwenzangu ambaye alikuwa na mwenzake (Mh. wa kike ambaye ni shoga yake ) ikanibidi kuanza upelelezi wangu ambao sasa matokeo yake nimeamua kuyamwaga hapa wazi baada ya kupata ukweli toka vyanzo vyangu vinavyoaminika toka ndani ya TANESCO na Taasisi zingine husika za umma .
·
I. Uwezo mdogo sana wa ndg. Mhando katika kuongoza Shirika
Huyu jamaa ameshindwa kuongoza TANESCO KABISA. He lacks managerial skills and his interpersonal communication is very weak and questionable. Toka ameingia amejenga makundi kwa misingi ya ukabila, urafiki na wizi. Ushahidi pia mnaweza kuuliza yale maoni ya watumishi wa TANESCO yaliyokusanywa na Katibu Mkuu wa Wizara. Nimefuatilia hata shule yake ni ya kuungaunga na hakika ilikuwa mbovu sana aliposoma huko Cuba.
Hakika habari za ndani kabisa zinasema uteuzi wake kuwa MD alichukuliwa toka namba tatu katika ranking wakati kulikuwa na mtu wa kwanza na wa pili walioachwa wenye uwezo kwenye vetting yao.


II. Kushiriki wizi ndani ya Shirika
Huyu ni mwizi moja kwa moja kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Bodi yake Rtd. General Robert Mboma na Makamu wake. Yaani huyu Mwenyekiti wa Bodi, Afande yeye anawauzia mafuta ya kuendesha mitambo TANESCO tena kwa bei ya juu Tshs. 2000/= kwa lita wakati sokoni ni 1500/=. Kwanini Mwenyekiti wa bodi huyu mzee mstaafu wa jeshi afanye biashara na chombo anachokisimamia akisababisha a conflict of interests and zero accountability?
TANESCO wanakusanya yapata Tsh. Billioni 100 kwa kila mwezi na hakuna ajuaye hizo fedha zinafanya kazi gani zaidi yake MD, Incarge wa idara ya fedha na Gererali Mboma. Kwa sasa TANESCO wameshindwa hata kulipa madeni anayodaiwa na wako mbioni kuuza mitambo yake. Kimkakati, sasa wamemega fedha nyingi mno (nasema tena mno) na wanazisabaza kwa kuanzia kwa baadhi tu (si wote) ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge na wao bila kufikiri wameamua kichwa kichwa eti kwenda kuonana na Wizara kesho kusimamisha hatua zilizochukuliwa na Wizara juu ya huyu MD. Na kwa kudhihirisha mahusiano yake na Generali , kama mwenyekiti wa Bodi amekataa kusaini barua ya kumsimamisha MD na watuhumiwa wengine kitu cha ajabu sana kwa sababu tu ya kulinda maslahi yake ya biashara anayofanya hapo TANESCO. Mzee huyu hatosheki na pensheni na marupurupu apewayo kama posho za vikao na kutembelea Shirika n.k kila mara.


III. Hujuma kwa Taifa kwa lugha za ' kiufundi' .
Leo nimeambiwa na Injinia mmoja mwandamizi wa Tanesco ninayemwamini sana kuwa hakika ugomvi umeanza kwa sababu kama kawaida yao, MD na kundi lake walitaka kutangaza kuwepo na mgao (kwa kubumba) wa umeme kwa lugha za kiufundi ili waendelee kufaidi kutokana na biashara zao za majenereta na mafuta. Sasa Wizara kwa kutaka kupigania maslahi ya wananchi wakawakatalia na hapo ndipo huyu kilaza anaamua kukata umeme mwenyewe kwa kiburi cha mwenyekiti wake anayetengeneza mamilioni ya fedha za nje (USD) kwa kila mwezi kupitia mgao wa kubumba.
Kilichoniuma kuliko vyote ni kwamba huyu Mh. Mwenzangu mwanadada kwa nini alinifuata na kunilisha nami chakula kichafu kama zilivyo fedha chafu bila mimi kujua, nitamshughulikia kibinafsi . Nimepata ukweli kuwa huyu mwanamama ni Mpenzi wake huyo MD na watu kibao wanalijua hili na yeye anatumia nafasi yake ya ujumbe kwenye kamati husika ya Bunge kuendelea kumfanya huyu MD buzi lake la kudumu. Tanesco . Na kwamba haikuwa tu kwangu bali kawatembelea wengi akiwa na fuko la fedha akijaribu kugawa kwa usiri sana na kushawishi eti tukatae bajeti ya Wizara na pia wamfukuze Katibu Mkuu wa Wizara (eti wanasema anajifanya kuleta ulokole wa kisabato, kitu ambacho ni kweli huyu jamaa ni wa SDA lakini kosa lake sasa nalifahamu kuwa ni kwamba amekuta ameingia katika anga za TANESCO- mradi wa watu wachache na sio wa umma.


Hitimisho:
1. Wabunge tuweni macho (Independent Committee iundwe kama ya Mwakyembe ) tuone nani anasema ukweli na awajibishwe. Suala laBajetu hatuhitaji kufundishwa sisi tunawasubiri wao waiwasilishe tutaipima na kuuliza maswali yanayopaswa.


2. Mamlaka husika, vunja hiyo Bodi ya TANESCO kabisa sasa hivi na wawekwe watu wasiohusika na mahusiano ya kimaslahi na watumishi wa TANESCO na wawe wenye uwezo wa kuisimamia vyema. Why always taking retired people? Tanzania ni kubwa sana na ina wasomi kibao na wenye uwezo wa kuongoza Bodi kibao!!



MD na Mh. mpenzi wako na shoga wako na hii Kamati ya Bunge inayosimamia Wizara ya Nishati kuweni macho na kila mnachotaka kukifanya sasa maana media, wala kusambaza barua kwa Rais, PM na kwa Waziri mhusika haitawasaidia. Umma wa watanzania leo umesha wamulika kuwa ninyi ni wahujumu wa uchumi.

Sisi wabunge wenye akili na wananchi tutawaangukia ninyi na yeyote ambaye anataka kuwaunga mkono katika upuuzi wa kuihujumu TANESCO, kutumia mhusiano ya kimapenzi kujaribu kutuhadaa na zaidi ya yote kushindwa kuongoza shirika hili la TANESCO NA KUJITUNGIA MIGAO YA UMEME ILI MFAHIDI !

Baada ya kuisoma habari hii swali langu la kwanza nililojiuliza ni kwamba mbunge mwenye mawazo ya kichovu sampuli hii anaweza kuwa nani.Mbunge anayeweza kupokea rushwa ya chakula eti baada ya kukila na kushiba anakiita kichafu!. Ana tuhuma nyingi za juu juu ambazo kwa mtazamo wangu hazina mashiko! Mbunge kenda mbali kiasi cha kuhoji elimu ya Mhando na kwamba ni ya kuungaunga! kama kweli wewe ni mbunge basi elimu yako ni ya kuunga unga. Siamini kama
ungeamua kufanya uchunguzi kama unavyodai ungekosa kuijua elimu ya mtu huyu.

Nyoosha maelezo kwamba kwa kuwa Mhando alikuwa swahiba wa Ngeleja, na kwa kuwa Ngeleja kawajibishwa basi Mhando naye aende! Kama swala ni uzinzi, tuseme nini kwa waheshimiwa Wabunge na hata mawaziri! Hata avatar yako inakushuhudia kwamba ni mhusudishaji wa maeneo hayo unayopenda kujitambulisha kwayo! Mpaka "vyangudoa" mnawatokea na wanawaumbua! Bado tuna kumbukumbu ya yaliyotokea Moro! Kanuni gani hii ya NDEGE WOTE WALIE, AKILIA BUNDI KUNA UCHURO!

Lete jina lako hapa. Waheshimiwa DR. Kigwangala, Zito, Mnyika kuwataja kwa uchache wamekuwa wachangiaji na wamekuwa wakimwaga majina yao! Acha majungu ya kwenye chama yako mbofu mbofu!
 
Baada ya kuisoma habari hii swali langu la kwanza nililojiuliza ni kwamba mbunge mwenye mawazo ya kichovu sampuli hii anaweza kuwa nani.Mbunge anayeweza kupokea rushwa ya chakula eti baada ya kukila na kushiba anakiita kichafu!. Ana tuhuma nyingi za juu juu ambazo kwa mtazamo wangu hazina mashiko! Mbunge kenda mbali kiasi cha kuhoji elimu ya Mhando na kwamba ni ya kuungaunga! kama kweli wewe ni mbunge basi elimu yako ni ya kuunga unga. Siamini kama
ungeamua kufanya uchunguzi kama unavyodai ungekosa kuijua elimu ya mtu huyu.

Nyoosha maelezo kwamba kwa kuwa Mhando alikuwa swahiba wa Ngeleja, na kwa kuwa Ngeleja kawajibishwa basi Mhando naye aende! Kama swala ni uzinzi, tuseme nini kwa waheshimiwa Wabunge na hata mawaziri! Mpaka "vyangudoa" mnawatokea na wanawaumbua! Bado tuna kumbukumbu ya yaliyotokea Moro! Kanuni gani hii ya NDEGE WOTE WALIE, AKILIA BUNDI KUNA UCHURO!

Lete jina lako hapa. Waheshimiwa DR. Kigwangala, Zito, Mnyika kuwataja kwa uchache wamekuwa wachangiaji na wamekuwa wakimwaga majina yao! Acha majungu ya kwenye chama yako mbofu mbofu!
Taratibu baba!
 
Kama ni kweli wapandishwe kizimbani kwa kosa la kuhujumu uchumi,maisha ya Watanzania wa kawaida yamekuwa magumu mno kutokana na gharama za umeue ili kufaidisha matumbo ya watu wachache na jamaa zao. TISS, PCCB mko wapi madudu yanafanyika kiasi hicho na wananchi wanaumia sana?
 
Wewe nawe inaelekea ni wale wale- kama unajua yote haya na ni mbunge kama unavyojitapa mahali sahihi pa kuwaumbua hao unaowatuhumu ni ndani ya ukumbi wa bunge-Kumbuka alivyofanya Kafulila kwa wale aliowakuta wakiomba rushwa. Hizi habari zenu za kuchafuana kwa visingizio vya uzalendo vimezidi. Tulisoma barua walizoandikiana wizara na Mhando, kutokana na mawasiliano hayo bado sijaliona tatizo la Mhando liko wapi unless utoe ushahidi kuthibitisha vinginevyo



Una undugu na mwizi Mhando nini?
 
Back
Top Bottom