RPC wa Mwanza ACP Liberatus Barlow auawa na wanaodaiwa ni majambazi!

Hapa kuna kitu kinafichwa, juzi juzi jamaa alikoswa koswa na risasi yeye akasema waliandaa mtego wa majambazi, aliyekoswa akasema alikuwa anatoka kikao cha harusi na anajua aliyemkosa anatembea na mkewe ambaye wana ugomvi,huyu amsema bahati mbaya, leo nae anamshusha dadake eti anauawa na majambazi, majambazi ya mwanza yanawinda polisi? Tusidanganyane kuna kitu kinafichwa, uwezekano mkubwa ni kuiba wake za watu.

Unafaa kwenda kitengo cha intelejensia,nakubaliana na wewe!! Huyo Dada sio kweli ni Dada yake atakuwa mke wa mtu! Yule Jamaa wa Uhamiaji aliyekoswakoswa kuuwawa anatishaaaaa kama mbwai mbwai,Nakumbuka nilimuona juzi tu alikua anaomba radhi kwamba lile tukio lilitokea kimakosa bahati nzuri hawajaua sasa leo bahati mbaya imemuangukia yeye!! RPC hana ulinzi? Alikuwa ametoka kwenye _________ tu sidhani kama kikao cha harusi,vikao vya harusi ni juma1 au juma2 na vinafanyika mchana mpaka jioni......Wake za watu ni nomaaaa!
 
Kikao kilikuwa bar au nyumbani kwa mtu?dereva wake yuko wapi?tunataka tuone japo kama kajikojolea otherwise aanze sasa kujikojolea na nataka awe polisi sasa hivi.kama Baro alikuwa anaendesha basi alipata pancha au dada yake anakaa uswazi na kuna ulinzi wa kijadi maeneo hayo,possibly walianza kupiga story tena pale gizani.utata ni mwingi hebu tupeni picha muache mambo ya uchunguzi bwana mbona mbagala kila kitu liko wazi jamani?
 
Kama kweli basi ni good news ingawa hatujui ni risasi ya nani. Daudi Mwangosi huko alipokuwa atakuwa anatasamu. Ingekuwa Kamuhanda nadhani wengi tungefanya sherehe ya kukata na jembe. Rest In Hell (RIH) Ballow.

Father of All baba wa wote, WAZIMA VS WABOVU, WAZURI NA WABAYA kwa bahati mbaya.nzuri POLICE MWANZA haina ugomvi na wanasiasa. Sijui nguvu ya kusema hayo unaitoa wapi. Kumbuka ni wilaya ya nyamagana iliyokuwa na waziri wa mambo ya ndani lakin pamoja na utajiri wa askari lakini askari hawakumlinda kufanikisha hujuma zake, aliangushwa na wenje wa CHADEMA. Sasa sijui wewe nguvu ya kuongea hivi umeipata wapi wakati unayemsemea hayo hana tatizo na poitical races na wanasiasa.
 
Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza Liberatus balow ameuawawa kwa kupigwa risasi usiku wa manane alipokuwa anatokea harusini.

Source: Radio one na kudhibitishwa na IGP

My take:
RIP kamanda ila sasa hivi baada ya kilio kwa raia wasiokuwa na hatia ngoma imehamia kwao.
Ingekuwa Kamuhanda ningesherehekea kwa kula Valuer na kuku wa kuchoma pale Chako-ni-Chako kwa saaaaaaana.
 
R.I.P Barlow,nadhani maziko yatakuwa Old moshi.TAARIFA YA AWALI YA POLISI ITAELEZA KUWA ALIPIGWA NA KITU KIZITO CHENYE NCHA KALI.
 
Duh! Ama kweli sasa ni dhahiri kabisa ya kwmb kuna watu wababe kushinda hata polisi lengwa kwa kazi ya kulinda raia na mali zao!
Ngoja tusubirie news zaidi kwn inaweza ikawa amejeruhiwa tu!

Hii itakuwa mbaya sana!

Na kama ni kweli nami kwamba nasema MUNGU amlaze roho ya Mareheu mahala pema peponi!

Aaamen!!
 
R.I.P liberatus Barlow na Mwanga wa milele ukuangazie....
Ila kwa akili za kawaida tu siamini kama ni majambazi...Hi mitego wanayotega imeanza kuwarudia wenyewe.kazi ipo.
 
Subirini muone jinsi gani jeshi la polisi lilivyo na ufanisi katika kusaka majambazi yanayoua polisi.

By the way, tukumbuke mpaka leo wa Ulimboka bado hawajapatikana.
 
Rekebisha heading...ACP (Kamishna Msaidizi wa Polisi) LIBERATUS LYIMO BARLOW.

RIP Kamanda...
 
Inasemekana amepigwa na kitu kizito chenye ncha kali na mwendo kasi. Poleni wafiwa
 
Baadhi ya Polisi wetu wanajihusisha kwa kiasi kikubwa na ujambazi,hili lililotokea inawezekana kabisa ni katika kudhulumiana kwenye ujambazi wao,wamemuua siku chache tu baada ya afisa uhamiji mkoa mwanza kutaka kuuliwa na polisi kwa kisingizio walidhani jambazi ili watu waamini kwamba ni ulipizaji kisasi kumbe ni kudhulumiana wenyewe kwa wenyewe.
 
Hakuna kinachomake sense hapo. Acheni kudanganyika enyi wadanganyika.

Majambazi siku zote hawapendi kuua bila sababu. Yaani wakuone tu umepaki gari waanze kukurushia risasi!!

Nendeni mkamdanganye mtoto wa Nursery school.

Anyway RIP
 
Unaweza kuta ameangukiwa na kitu kizito chenye ncha kali,kilichokuwa kinaning'inia ndani ya gari lake..tusubiri tuone
 
Sikuungi mkono kabisa mkuu huwezi kukaa ukafurahia kifo kama tukienda kwa visasi vya mtindo huu kama unavyotaka wewe sidhani kama nchi hii itatawalika kikubwa ni kurekebishana tabia tu na uchaguzi na demokrasia ndio njia pekee ya wananchi kufanya maamuzi tukimuombea kila mtu afe katika nchi hii utajikuta hata wewe kuna watu wanakuombea ufe na ukifa watafurahi kwa hiyo tujitahidi tu kurekebisha hii mifumo ya kiutawala kwa njia za kidemokrasia

huyo crashwise amepotoka
 
Back
Top Bottom