RPC Morogoro akana polisi kutumia risasi za moto

hayo mabomu ukiligwa nalo nina kuua maana nakumbuka hapa arusha lilivunja dirisha na kuchoma vitu vilivyokuwemo huko lakini cha ajabu tuliambiwa chadema ndiyo tumechoma..
Bomu la machozi linaweza kukupiga/kukugonga, kuwaka na kuunguza lakini sio kupenya kama risasi.
 
Alikiri mbele ya Tundu Lissu kua polisi wameua kwa risasi,tena walilenga kichwani,kisheria ni kua walidhamiria kuua!kwa hiyo hayo mambo ya times fm anaji contradict tu!!
 
Hatimae yaliyosemwa na Dr Slaa na kukanushwa na Nape leo yametimia,Abood nae ni sehemu ya mpango huu
 
nani amesema? lissu?

Lissu amesema ilo mkutanoni pale,na kati kati ya mkutano iliundwa team ya kwenda kuhojiana na RPC,team iliporudi Lissu ndio akaleta taarifa ya mahojiano yao na RPC,polisi hata pf3 walitaka kuwanyima wale majeruhi,lakini baada ya Team hiyo iliyoongozwa na Lissu kumbana RPC,hatimaye walikubali kutoa PF3 haraka,tayari kuna wataalama na wanasheria wa Cdm wanatoka Dar na kuja kuhakikisha mauaji haya yanashughulikiwa kisheria!
 
Hichi nacho kichekesho cha karne.. Kama bomu la machozi linaua au kujeruhi kwanini wakayatumia Kuua haiangalii ume muuaje...mwema ndio mshitakiwa namba moja Huyu awe namba mbili napendekeza

Wana JF

Nimesikiliza sauti ya RPC wa Morogoro akiongea na Times FM sasa hivi anasema polisi haijatumia risasi hata moja Morogoro na badala yake wametumia mabomu ya machozi tu na kwamba hata aliyefariki leo hawezi kusema kapigwa na risasi maana huenda amefariki kutokana na jeraha la BOMU LA MACHOZI.

Nimepigwa na Butwaa na kauli hii ya RPC.
 
hawezi kukubali ila polisi walishazoea kuuwa na kutokuchukuliwa hatua zozote
 
Polisi leo hapa

Morogoro walipiga mabomu yakaisha wakawa wanaangalia na mwisho wake ndio kutumia risasi
 
Wana JF

Nimesikiliza sauti ya RPC wa Morogoro akiongea na Times FM sasa hivi anasema polisi haijatumia risasi hata moja Morogoro na badala yake wametumia mabomu ya machozi tu na kwamba hata aliyefariki leo hawezi kusema kapigwa na risasi maana huenda amefariki kutokana na jeraha la BOMU LA MACHOZI.

Nimepigwa na Butwaa na kauli hii ya RPC.
Namshauri tu ajue Morogoro ni moja ya mikoa migumu kama utaegemea siasa ukaacha kilichokutuma hapo, kauli kama hizo za haraka haraka zitamponza, asikurupuke, watu pale Msamvu walikuwepo na kuona kila kitu, afanye uchunguzi na kuja na majibu ya maana kuliko hilo alilotoa, bomu la machozi haliwezi umiza mtu mpaka kifo, wengi tumepitia majeshi tunajua hilo kamanda
 
kama mkubwa wao aliweza kurupukia chizi kwa mauaji ya ulimboka,sembuse kukana hilo?
police wamekua kama gari bovu hawafikirii hata kidogo kabla ya kutenda
 
Cha msingi ni kukomaa na post mortem ya huo mwili alafu waje umbuka mchana kweupee!
naona kuua raia imekuwa suala la kawaida nowdays
 
Katika hatua ya kushangaza, RPC wa Morogoro amekana askari wake kutumia silaha za moto wakati wa kuzima maandamano ya chadema yaliyofanyika mkoani Morogoro leo.Alisisitiza polisi kupiga mabomu ya machozi tu.

Source:Mahojiana ya kamanda huyo na kituo cha TV cha chanel ten wakati wa taarifa ya habari ya saa moja usiku huu.

Hakuna umoja katika nchi wakati kuna matatizo mpakani,kati ya Tanzania na Malawi.
 
Ngoja nipite kimya, maana nina hasira kweli nisije jiharibia jioni yangu.Ila iko siku kiburi cha hawa kenge kitaisha
 
Back
Top Bottom