RPC Geita, jipime mwenyewe kwenye hicho kiti

Hii inashangaza sana.. RC yupo, RPC yupo, RCO yupo, RSO yupo, Mshauri wa Mgambo yupo, DC yupo, OCD yupo, OC-CID yupo, OCS yupo, OCS-CID yupo, DSO yupo, lakini inahitaji Waziri atoke Dar Es Salaam kuliona hili..o_O
 
Rais Magufuli ana kazi kama ndo style ya viongoz hawa amewateua wamsaidie huko Geita!!! Ni tatizo LA kudumu
 
Hili li nchi huwa la kijinga sana, yaani hata linatia aibu duniani, hivi tunahaja ya kuwa na wawekezaji wachimbaji wa madini in small scale kweli? yaani wachina tunawaleta wamiliki mgodi kwa kujenga mabati na kukiita kiwanda? mchina anakuja anaanza kuchimba madini kama mchimbaji mdogo na wazawa wapo? kwa nini tusitoe fungu na vifaa vya kisasa tukawapa vijana/raia wandani ndo wakafanya hiyo kazi? kwa macho yangu mmeona kiwanda wanachosema wamekuja kuwekeza? kibaya zaidi wanakuja wengine zaidi tena kwa njia za panya pasipo ba kibari cha kufanya kazi na serikali ipo, matokeo yake mnakuwa na watu haramu wanaopiga na kunyanyasa raia. Hii ni aibu ,mtu anapigwa then baadae anatupwa lupango, mimi naona imefika wakati viongozi kama hawa mfano police/mkuu wa wilaya/ sio tu waachishwe kazi bali wapigwe ndani kwanza ili wawe na discipline.
 
Waziri kakosea sana, ilitakiwa amuulize yule kijana kakaa lupango muda gani? then awasweke RPC, RCO, OCD, OCCID, OCS ndani kwa muda aliokaa huyo kijana ndani ili wajue nini maana ya kazi, maviongozi kama haya Tanzania yanafanya nini? ,baada ya kulinda raia wa nchi hii yanalinda matumbo yao
 
Nakumbuka kuna ajali ilitokea Rwanda mpakani lorry lilianguka na kuziba njia,eneo ambalo mchina alipewa kandarasi ya kujenga barabara,mchina aliombwa crane asaidie kulinyanyua lile gari ili njia iweze kupitika,akagoma,kilichofuata ni wanajeshi wa rwanda waliingia ndani ya kambi ya hao wachina wakachukua crane wakalinyanyua gari,na kangame akawatimua hao wachina nchini mwake.
 
Foreigner mchina (tena possibly ni mhamiaji haramu) anampiga na kumtesa kinyama RAIA MZAWA! Mtanzania mwenzetu huyo pamoja na kipigo chote alichopewa, still akapelekwa gerezani na kutupwa lock-up! Mchina karateka hakuguswa, 'vyombo vya dola' vyote mkoa mzima vikashindwa kabisa kumshughulikia mchina huyo.

RPC yupo! OCS yupo! OCD yupo! CID yupo! Mkuu wa Wilaya yupo! Mkuu wa Mkoa yupo! wote hawa wanakula mishahara kwa kodi za wananchi lakini walikuwa vipofu kabisa juu ya suala hili.

Eti mpaka Waziri anasafiri to Geita kwa ajili ya suala hilo ndipo HAKI inaonekana kuanza kutendeka. Najiuliza... je kama Waziri asingekwenda huko Geita, kwahiyo hili suala ndo lingefunikwa na kupita?!!!

Mgeni mhamiaji (tena si ajabu ukute hana hata vibali vya Uhamiaji) anamnyanyasa RAIA mzawa na hachukuliwi hatua yoyote wala kuadabishwa. Only in Tanzania! Nchi hii ngumu sana walahi.

Huwa najiuliza, hivi hapa duniani, kuna nchi nyingine yenye maajabu kama Tanzania?

Heko kwako Mh Waziri husika, ndugu Mwigulu Nchemba kwa kuinuka offisini na kwenda kulinda haki na utu wa huyo mtanzania mwenzetu. Endelea hivyo hivyo mkuu. simamia na himiza criminal justice ndani ya nchi yetu.

TAKUKURU pia chunguzeni hili suala, inaonekana kuna element za rushwa kubwa !

RPC jipime mwenyewe kabla hujatumbuliwa.

-Kaveli-

Katika mambo ambayo watanzania wengi wanaumia na kunyayaswa ni kama hili. anyetendewa maovu vyombo au mamlaka za kumsaidia zinamtuhumu kwa kumuweka selo na mtesaji anakuwa mlalamikaji na mombo yanaisha kwa kifungo haramu.
Ni taswila mbaya kwa serikali ya chama chochote chenye mamlaka kamili na serikali yake.
Big shame shame shame and shame to this terrible story when a minister forced to travel all the way more than 1,000km to resume RPC responsibilities!!!!!!!!
 
Nakumbuka kuna ajali ilitokea Rwanda mpakani lorry lilianguka na kuziba njia,eneo ambalo mchina alipewa kandarasi ya kujenga barabara,mchina aliombwa crane asaidie kulinyanyua lile gari ili njia iweze kupitika,akagoma,kilichofuata ni wanajeshi wa rwanda waliingia ndani ya kambi ya hao wachina wakachukua crane wakalinyanyua gari,na kangame akawatimua hao wachina nchini mwake.

Again, it is Rwanda and Kagame in the spotlight.

No wonder Tanzania is to outsource the Rwandese ITs expatriates...
 
RUSHWA kitu kibaya sana. Mzawa unanyanyaswa/unateswa na 'wakuja' kisa anamiliki mgodi na ni ngozi nyeupe! big shame kwa police Geita.

Hili tukio lazima liondoke na mtu. Mh Magufuli ndo huwa hapendi upuuzi kama huo.

-Kaveli-
Rushwa bado ipo serikalini hasa polisi, uhamiaji.

Wageni wanatesa sana raia, Kuna kampuni inaitwa MER Telecom, yupo mnyarwanda mmoja anaitwa Simeon Habinshut, sio tu hana kibali cha kuishi hapa nchini yeye na familia yake, bali hana working permit, (na kazi anazofanya zinaweza fanywa na wa Tanzania ),
Jamaa anatukana wa Tanzania, anawatesa subcontractors, in short ana maneno machafu sana.

Kitu cha kusikitisha ni kwamba tarehe 18 May 2016 uhamiaji walienda wakachukua hela wakamuacha (na wamekuwa wakirudi baada ya muda kuchukua hela)

Uhamiaji na vyombo vingine vya kutoa haki jirekebisheni,
 
Nitashangaa Mwigulu akiondoka Geita bila kutumbua mtu!! Watakuwa wanalea mfumo wa rushwa nchini, aanze na OCD kupanda juu wote sijui wapelelezi na wenzao wooote
Kwa tukio hili kuanzia ngapi ya mkoa wanatakiwa wapishe viti walivyo kalia ili PCCB wafanye ukachero.
Mkoa:- RPC, RCO watoke
Wilaya:- OCD, OC-CID watoke
Location:- OCS atoke
Mwigulu anapaswa awashinikize watajwa hapo juu wajiweke pembeni toka kwenye ofisi za uma na kisha kazi ya uchunguzi wapewe PCCB
 
Jeshi ni tofaut na taasisi zingine za mkonge .......huku hatuna siasa hayo ya kujipima waambie wanasiasa. .........
Naomba niishie hapa tu aiseeee....
Maana umesha nijaza povu na kuiharibu siku yangu kwa huu muandiko wako
 
Inauma Sana, kamati ya into na usalama mkoa na wilaya wajitathmini.
Asingeenda waziri njamaa wangemchimjia Bahraini, what a shame!
Hongera Sana waziri kwa Hili.
 
Foreigner mchina (tena possibly ni mhamiaji haramu) anampiga na kumtesa kinyama RAIA MZAWA! Mtanzania mwenzetu huyo pamoja na kipigo chote alichopewa, still akapelekwa gerezani na kutupwa lock-up! Mchina karateka hakuguswa, 'vyombo vya dola' vyote mkoa mzima vikashindwa kabisa kumshughulikia mchina huyo.

RPC yupo! OCS yupo! OCD yupo! CID yupo! Mkuu wa Wilaya yupo! Mkuu wa Mkoa yupo! wote hawa wanakula mishahara kwa kodi za wananchi lakini walikuwa vipofu kabisa juu ya suala hili.

Eti mpaka Waziri anasafiri to Geita kwa ajili ya suala hilo ndipo HAKI inaonekana kuanza kutendeka. Najiuliza... je kama Waziri asingekwenda huko Geita, kwahiyo hili suala ndo lingefunikwa na kupita?!!!

Mgeni mhamiaji (tena si ajabu ukute hana hata vibali vya Uhamiaji) anamnyanyasa RAIA mzawa na hachukuliwi hatua yoyote wala kuadabishwa. Only in Tanzania! Nchi hii ngumu sana walahi.

Huwa najiuliza, hivi hapa duniani, kuna nchi nyingine yenye maajabu kama Tanzania?

Heko kwako Mh Waziri husika, ndugu Mwigulu Nchemba kwa kuinuka offisini na kwenda kulinda haki na utu wa huyo mtanzania mwenzetu. Endelea hivyo hivyo mkuu. simamia na himiza criminal justice ndani ya nchi yetu.

TAKUKURU pia chunguzeni hili suala, inaonekana kuna element za rushwa kubwa !

RPC jipime mwenyewe kabla hujatumbuliwa.

-Kaveli-
Wachina kwa kuhonga ni balaa, ingawake itakuwa vigumu kuthibitishahilo.
Lakini RPC ameonyesha udhaifu mkubwa kulinda raia wa Tanzania.
 
Tz bado tuna ile tabia ya" kumlamba mgeni viatu" wakati huo wenzetu hawana huo muda kabisa wa kumtetemekea mgeni, kwa mfano mdogo tu wakati timu zetu zinapoenda kucheza nje ya nchi huwa zinafanyiwa mchezo mchafu wenyewe huita (figisufigisu)kuanzia pale tu zinapotua kwenye uwanja wa ndege mpaka kipindi cha kucheza.Wakati huo hao watu wakija huku kwetu huwa tunakaa kimya mfano wa mbwa anaye weka mkia wake miguuni.Mimi nahisi huu si upendo bali ni kama la....na.
 
Ni ujinga mkuu yaani A.K.A ukondoo
 
Back
Top Bottom