Route za treni za Mwakyembe ndani ya jiji la Dar: TRL vs TAZARA

tulipiga kelele sana kuwa mradi wa mabasi hauwezekani UMEWEZEKANA.......sasa tunapiga kelele kuwa hilo la treni haliwezekani MWAKYEMBE na timu yake WANAANZA KUONYESHA WANAWEZA
Sisi TUNAONGEA wao WANAFANYA........mwisho wa siku tutasema wameiba kura kwa sababu mikutano yao haijazi watu....KUMBE WENZETU HAWAONGEI KWA MIDOMO BALI VITENDO

Mradi wa mabasi 'yaendayo kasi' umewezekana??? Nimeona bomoa bomoa maeneo kadhaa na harakati za kujenga njia (lane) za kupitisha mabasi hayo, lakini sijaona utekelezaji wake.

Kupanua au kujenga barabara ni moja tu kati ya changamoto za mradi wa mabasi. Changamoto zingine kama taa za barabarani kufanya kazi, na usimamizi wa kuhakikisha ya kuwa hizo njia (lanes) zilizowekwa kweli zitatumika kwa mabasi tu na kuzuia magari madogo, mikokoteni, bajaj, bodaboda, baiskeli za guta n.k kutumia njia hizo bado zipo. Askari wetu waliozoea kitu kidogo tutawabadilishaje mtazamo wao wasichukue pesa na kufumba macho watakapoona magari ya walio tayari kutoa rushwa yanatumia njia hizo? Na magari ya 'vigogo' wakikwama kwenye foleni wakaamua kupita njia za mabasi kuna atakayekuwa tayari kuwadhibiti, hali anajua kibarua chake kinaweza kuota nyasi?

Hayo yatakapowezekana, mabasi 'yaendayo kasi' yatakapoanza kutembea mijini na daladala, bajaj, bodaboda, mikokoteni, guta n.k zitakapoondoka kwenye barabara zetu; na pale mgao wa giza unaoathiri taa za kuongozea magari utakapokwisha ndiyo tuanze kutoa pongezi.

Kuhusu reli... makadirio yote hayo kuhusu watu wangapi watanufaika tujuzane nauli itakuwa shilingi ngapi? Na bei ya mafuta (dizeli) inayozidi kupanda kila kukicha? Tusije kupewa majibu kama ya watu wa Kigamboni walioambiwa asiyeweza nauli mpya apige mbizi!!!

Taarifa kwenye makaratasi na mbele ya TV inapendeza, lakini inawezekana?
 
Tuangalieni kwa jicho la tahadhari sana hii njia ya KIMARA na MBEZI (BEACH & LOUIS) tusipokuwa makini tutatatua msongamano katikati ya mji alhali kule mji unakopanukia tatizo linaanza pia.
Chezea Mwakyembe weweeee (hata sumu haimuwezi)
 
Hawa dawa yao ni kuweka kodi kubwa za kutembea na magari binafsi jijini.

Kuna wale wanaishi mbagala wanafanya kazi mikocheni. Watapanda treni gani? Kuwapiga kodi kubwa ni kuwaonea bure! Labda tuishauri serikali ifikirie treni ya kutoka Mkuranga to Bagamoyo.
 
kuna mpango wa kutumia bahari na kutakuwa na kivuko toka feri hadi kunduchi

Hilo ni wazo zuri sana. Tukiwa na vituo vya maboti vitasaidia sana abiria wa kigamboni, kijichi, ostabei, msasani, mbezi, kunduchi mpaka bagamoyo.
 
kwahili serekali imejitahid, tuache kuwa na hisia hasi na ktk kila jambo linalofanywa na serekali. Wanastahili pongezi.
 
Train zitasaidia sana ila serikali ijitahidi kujenga barabara za juu na kuwa na maegesho ya kutosha katikati ya miji kwani yataiingizia serikali mapato na kufanya mji uwe wa kisasa.
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Kwa hili DHAIFU wamepatia

Hawa siwaamini hadi nione wameanza .Na mabehewa mapya ama haya haya ya siku zote ? Angalieni matumizi ya mafuta heheheh maana mtahama Tanesco mnakuja train
 
Watz mko pessimistic nilidhani mngeshauri vituo viongezeke au vipungue badala yake mnaponda!
Jamani nchi yetu hii kama kuna zuri applaud for that na tutiane moyo na baya tulikandie kwa nguvu zote
 
Subway system in Tanzania..Good start.Hata Tokyo hawakuanza kwa siku moja.
 
Mabehewa yanakarabatiiwa kuna kama 800mil zitatumika kukarabati vichwa na mabehewa ya tazara cheki kwa bajeti speech
Ukarabati wa njia ya reli na mabehewa unaendelea bothways ili yaweze kuwa user friendly
 
Mimi mwenzenu naomba mnisamehe. Ki ukweli niliposikia kwamba kutakuwa na usafiri wa treni wazo langu la kwanza lilikuwa kwamba serikali imetenga fedha ya kujenga TRENI ZA CHINI YA ARDHI. hii ningeiafiki na kusema kwamba ni kweli itapunguza msongamano.

Ila kwa kutumia haya matreni mabovu ya wakoloni na mabehewa ambayo nashauri kuwa na watu wa huduma ya kwanza maana yana kutu sana watu wanaweza umia nayo, wala hujanisawishi kwamba eti ni njia ya kupunguza folenio, rather naona itaongeza foleni kwa wenye magari kusimamishwa kila wakati kupisha treni ipite, that's if watasimamisha maana most of the time mtu itabidi tu uichungulie treni kama inafika, wasimamishaji huwa hawapo.

Pili, hiyo root ya hizi treni, ni kama bora tufanye wananchi waone tumefanya bila kuzingatia is it useful or not.

Ufumbuzi wa foleni wafanye yafuatayo:-
1) Wajenge treni za chini ya ardhi kwa usawa wa barabara kubwa e.g treni ianzie mbagala kupitia town ikaishie bagamoyo na itakayotokea kibaha ku connect hii nyingine mjini na itakayotokea gongolamboto huko.

2) Waweke classic boat kutoka bagamoyo hadi posta (reliable)
3) Waboreshe bara bara mbadala (hizi za vichochorone ambazo wengi wetu tunazitumia asubuhi na jioni kupita japokuwa ni mbaya sana ndio zinazosaidia unajikuta umetokea salenda.

4) Waweke ingilio lingine mjini (apart ya daraja la salenda na daraja la magomeni)
5) Wasimamie sharia za barabarani, taa zifanye kazi wakati wote.
6) Raisi mwenye misafara ya mara kwa maara ambapo most of the time anakoenda kunajulikana, atumie helikopta na awekewe vituo huko anakoenda mara kwa mara e.g ikulu to (1) airport, (2) hapo usalama wa taifa makumbusho, (3) bagamoyo

7) Waboreshe ubora wa daladala na ziwe classic daladala zitakazowashawishi watu tuache magari yetu na kupanda hizo dala dala (sio kwa kugembea kama ninavowaona hapo posta, mmmmh)

8) Magari yakaguliwe kweli sio watu wakate tu stika ya wiki ya usalama barabarani na kupewa kicheti eti umekaguliwa wakati wala hata gari hawajaliona hao wanaokuandikia stika ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani, this way magari vimeo yaondolewe njiani na yabaki mazima.

Hii serikali yenu imekurupuka tu kama wanavyokurupuka sehemu nyingine kama:-

Tabia yao ya kusimamisha magari yanayoenda mbagala asubuhi pale stesheni na kuyasimamisha magari hayo yanayotoka mbagala pale bandari na kuruhusu njia mbili kuanzia stesheni kupita BP hadi bandari, wakati walikuwa na uwezo wa kuvunja BD na kupanua hiyo njia kuliko kusimamisha abiria wa upande mmoja zaidi ya saa nzima bila kujali na wao wanaenda kazini vile vile.
 
kwa sababu wanaolengwa siyo wenye magari! As a matter of fact nadhani itachangia zaidi ongezeko la magari jijini Dar. Think about it.
commuter trains si kitu kibaya ukizingatia jinsi nchi zilizoendelea zinavyofanya utafiti, ujenzi na ukarabati wa reli zao, pia kuna evidence nyingi tu inayodhihirisha usefulness of such mode of transport. Tatizo kubwa kwetu ni gharama ya ujenzi (sijui mikopo itatoka wapi na itatumika vp), environmental impact (sidhani kama hii itaingia kwenye calculation zao) local expertise na pia ugawaji wa tenda. Kwa mfano ktk mji wa chicago kuna above ground rail inayofuata barabara za mjini. Yaani juu kwa juu ni treni, chini yake watu waendesha magari, hii reli pamoja na toll road nyingi inahamasisha watu kuacha gari nyumbani alafu kupanda treni. Ni vigumu kulinganisha effectiveness ya reli kwa kutumia mifano ya nchi ambazo ziko mbele yetu kimaendeleo, lakini huwa najiuliza kila siku "why not in tanzania?" hii imekaaje wadau?
 
kwahili serekali imejitahid, tuache kuwa na hisia hasi na ktk kila jambo linalofanywa na serekali. Wanastahili pongezi.
Nitaipongeza serikali kama watafikiri zaidi ya treni kwa sababu Dar yenyewe ina population zaidi ya mil5 na magari yasiyofika millioni moja lakini tuna msongamano mkubwa kiasi hiki.. Suluhu ya yote ni kuondoa makao makuu ya ofisi zote za serikali Dar na kuyahamishia Dodoma - Nusu ya msongamano itaondoka..
 
mbn bagamoyo road sioni route

Kuna kandarasi amepewa kutoka Morocco hadi Mwenge ila jinsi ya kupanua barabara imekuwa issue ya fidia. Kumbuka hiyo njia ni ya waheshimiwa sijui watasimama kupisha mabasi au vipi kwenye maungio ya barabara.
 
Kila jambo lazima liwe na mwanzo wake na huu ni mwanzo mzuri. Katika maendeleo ya nchi yoyote kuna mipango ya maendeleo ya vipindi tofauti. Muda mrefu, wa kati na muda mfupi. Mpango wa train ni wa muda mfupi na ni stopgap arrangement wakati ule wa mabasi yaendayo kasi ni wa muda wa kasi lakini kutakuwa na complementary effect. Wakati huo huo ipo mipango ya kutengenzea flyovers and bypasses lakini pia kuimarisha barabara za pembezoni ili ku- decongest hizi barabara kubwa. Ieleweke pia kwamba Lagos, jiji la watu karibu milioni 20 lina changamoto tofauti na Dar es Salaam na kila moja ina mikakati tofauti ya utekelezaji kutegemeana na ukubwa na chanzo cha matatizo.

Hata hivyo nakubaliana na wewe kwamba suala la vituo vya mabasi holela na magari ambayo ni vimeo ni mambo yanayohitaji kufanyiwa kazi. Lakini kukiwa na usafiri wa umma wenye heshima, staha na wa kuaminika kama nchi za wenzetu, ule ulevi wa kila mtu kuwa kwenye gari yake binafsi utapungua na hivyo kuondoa msongamano.

Nakubaliana na wewe kuwa kila jambo lazima liwe na mwanzo ila lazima uwe mwanzo mzuri. Usafiri wa mabasi unahitajika sana, wa treni unahitajika na bado watu wataendelea kununua magari binafsi kwa sababu mbali mbali na wala hakuna serikali itakayo zuia kwani ni chanzo cha mapato. Tatizo lipo kwenye mambo ambayo mimi naona yanaendela kuleta msongamano. Tuna hospitali 3 zinazoitwa za rufaa, kila siku ambulance zinatoka kwenye hizo hospitali kupeleka wagonjwa muhimbili, kipimo cha CT scan ni kama dola 300,000. hatujaviweka kwenye hizo hosp matokeo yake kila mtu atataka kwenda Muhimbili, ukita kuhamisha hati mpaka wizara ya ardhi, kila ofisi ipo ya serikali ipo Dar unatarajia nini? Vyuo karibu vyote vina matawi Dar unatarajia Dar haitakuwa na watu mil 20 ndani ya miaka 25 ijayo? Nido maana nasema macro approach inatakiwa hata kama ni mipango ya muda mfupi. Inasikitisha sana tunatumia fedha nyingi kujenga barabara kama Ubungo- Kimara na ndani ya miaka 10 inabidi kuvunja mradi mzima kana kwamba hatuwa na ufahamu kuwa huu mradi ulikuwepo kwenye mipango muda mrefu.
 
Back
Top Bottom