Rostam: Tajiri anayedhulumu walalahoi?

chaArusha

Member
Mar 24, 2011
88
31
Mimi ni mwajiriwa wa Rostam Aziz katika kampuni yake ya New Habari.

Huyu jamaa ni tajiri sana, ana kampuni nyingi, lakini nafikiri anapata utajiri wake pamoja na kudhulumu. Hivi ninavyoandika, wafanyakazi wote wa kampuni hiyo wanakatwa malipo ya PPF lakini hajapelekwi.

Kuna idadi kubwa ya wafanyakazi wameacha au kufukuzwa tokea aingie Hussein Bashe, lakini wakienda PPF, hakuna hata senti tano iliyoingizwa tokea 2008 ingawa wanakatwa kila mwezi. Pia, wafanyakazi hao hawajalipwa mishahara ya miezi ya Agosti, Septemba na Oktoba hadi wengine wameacha kazi wanadai mishahara.

Hivi hakuna wa kumwajibisha huyu fisadi alipe haki za watu?
 
Aiseee poleni sana ... fuatilieni hili swala kisheria.. inabidi mmoja wenu ajitoe mhanga liwalo na liwe ...
 
Kuna idadi kubwa ya wafanyakazi wameacha au kufukuzwa tokea aingie Hussein Bashe, lakini wakienda PPF, hakuna hata senti tano iliyoingizwa tokea 2008 ingawa wanakatwa kila mwezi. Pia, wafanyakazi hao hawajalipwa mishahara ya miezi ya Agosti, Septemba na Oktoba hadi wengine wameacha kazi wanadai mishahara.

Hivi hakuna wa kumwajibisha huyu fisadi alipe haki za watu?

Tafadhali leta ushahidi wa hili ulisemalo. Ni tuhuma nzito sana, na kama ni umbea tafadhali muombe msamaha Rostam ASAP
 
Pia, wafanyakazi hao hawajalipwa mishahara ya miezi ya Agosti, Septemba na Oktoba hadi wengine wameacha kazi wanadai mishahara. Hivi hakuna wa kumwajibisha huyu fisadi alipe haki za watu?

Jumla ya mishahara yenu kwa hiyo miezi ni shillingi ngapi na nyie mmezalisha shillingi ngapi? Msitegemee kuwa achukue pesa za "deal" zake nyingine aje kukulipeni mishahara; andikeni habari zinazouzika ili magazeti yenu yanunuliwe muwezi kujilipa mishahara
 
nadhani kama ni habari cooparatiom ile inayotoa magazeti ya mtanzania jamaa atakuwa anaendesha biashara kwa hasara maana magazeti yake hayauziki. ila kuhusu kutowasilisha michango yenu ppf kama ushahidi unao strong lete tafadhali
 
si ni vijigazeti vilivyojipanga kuwasifu Rostam, Chenge na Lowasa, na kuaandaa mkakati wa kuchukua nchi huku kesi zao za rada, richmond na EPA zikikaliwa na wenyewe kuendeleza libeneke la kula kilichombele yao kama kiwavi jeshi, sasa vita ya Urais Mkuu kaisha iua baada ya kumkwapua Kamanda wao Makamba na Kumweka Mtu wa Jazba Ndugu Nape sasa wanashindwa kubadilisha habari za kuwasafisha mabosi wao, kama wameshindwa na mkuu ndio anawakacha kukutana nao si maji yako shingoni, hela za kutorokea ulaya atatatoa wapi kama si kuzipeleka Iran zikatunze maana baada ya kesi tutamkuputisha kila alichonacho na kumpa masaa 24 awe ameondoka nchini akipenda aondoke na maswahibwa wake EL, CH na kale kajamaa ka Arusha.
 
nadhani kama ni habari cooparatiom ile inayotoa magazeti ya mtanzania jamaa atakuwa anaendesha biashara kwa hasara maana magazeti yake hayauziki. ila kuhusu kutowasilisha michango yenu ppf kama ushahidi unao strong lete tafadhali
Ushahidi upo mkuu, watu wameenda hadi huko PPF wanaambiwa hakuna michango iliyoingizwa.
 
Mkuu pole sana kwa hilo, lakini hakuna asiyemjua huyu jamaa ni fisadi zaidi ya fisadi, lakini nchi yetu inaendeshwa kwa sheria na katiba, kuna vyombo vyingi sana vya sheria hapa Tz, unaonaje kama sheri ikachuku mkondo wake?

Nendeni mahakamani bana.
 
Hiyo miezi ulioitaja ya mwaka gani? Kwani sijui ni mTanzania yupi aliekwisha lipwa mshahara wa August September na October 2011, au nyie hulipwa in advance?
 
Jumla ya mishahara yenu kwa hiyo miezi ni shillingi ngapi na nyie mmezalisha shillingi ngapi? Msitegemee kuwa achukue pesa za "deal" zake nyingine aje kukulipeni mishahara; andikeni habari zinazouzika ili magazeti yenu yanunuliwe muwezi kujilipa mishahara

hili ndo neno!
 
Hiyo miezi ulioitaja ya mwaka gani? Kwani sijui ni mTanzania yupi aliekwisha lipwa mshahara wa August September na October 2011, au nyie hulipwa in advance?

dada yangu, ni wewe au ntu ingine?
nimezoea kuona always upo against
 
Hiyo miezi ulioitaja ya mwaka gani? Kwani sijui ni mTanzania yupi aliekwisha lipwa mshahara wa August September na October 2011, au nyie hulipwa in advance?

Matatizo mengine ni ya kujitakia. Chanzo cha matatizo haya ni magazeti ya kampuni hiyo kudoda mtaani kutokana na kuwa na habari za kipuuzi za kusifia mafisadi na kuwaandama wale ambao mmiliki anaona kwamba ana bifu nao. Waandishi na wahariri wa magazeti haya walikuwa wanatumika kutekeleza matakwa ya mmiliki na wakati huohuo kujichimbia kaburi machoni mwa wateja. Sasa ndiyo mnashtuka kwamba hata mishahara sasa ni tatizo na ndiyo sasa mnalalamika. Mmechuma janga, kaleni na wa kwenu. Watu mliowaumiza kwa vitendo vyenu vya kuwatungia uongo na kusifia vitendo vya kidhalimu ni wengi na waote hao wamekuwa wakilia na nyie na sasa matokeo mnayaona.
 
Forget,this guy is above the law.
Mimi ni mwajiriwa wa Rostam Aziz katika kampuni yake ya New Habari.

Huyu jamaa ni tajiri sana, ana kampuni nyingi, lakini nafikiri anapata utajiri wake pamoja na kudhulumu. Hivi ninavyoandika, wafanyakazi wote wa kampuni hiyo wanakatwa malipo ya PPF lakini hajapelekwi.

Kuna idadi kubwa ya wafanyakazi wameacha au kufukuzwa tokea aingie Hussein Bashe, lakini wakienda PPF, hakuna hata senti tano iliyoingizwa tokea 2008 ingawa wanakatwa kila mwezi. Pia, wafanyakazi hao hawajalipwa mishahara ya miezi ya Agosti, Septemba na Oktoba hadi wengine wameacha kazi wanadai mishahara.

Hivi hakuna wa kumwajibisha huyu fisadi alipe haki za watu?
 
Hiyo miezi ulioitaja ya mwaka gani? Kwani sijui ni mTanzania yupi aliekwisha lipwa mshahara wa August September na October 2011, au nyie hulipwa in advance?
You must be enjoying your life as it is...You can crack very funny jokes. Keep it up.
Warning: Be aware of the mass who are disgranted
 
kwa kuanza kumuwajibisha anza wewekumfungulia mashtaka mahakamani kuhusu malipo ya PPF yako,utakuwa mwanzo mzuri
 
Wafanyakazi wa kampuni hii wanafanyiwa dhuluma nyingi sana na taratibu tutaendelea kuyasikia mengi.
 
Back
Top Bottom