Rostam ni mmiliki wa Dowans, Richmond - Selelii

Wa Ndima

JF-Expert Member
Aug 13, 2010
1,526
323
Akizunguma na Kituo cha Redio cha Zenji FM, 96.8 cha Zanzibar katika kipindi maarufu cha 'Mwangaza wa Habari', Selelii ameeleza kuwa aliambiwa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz anahusika na Kampuni ya Richmond na pia ni Mmiliki wa Kampuni ya Caspian, na hili kamati teule tuliambiwa na mwandishi wa habari aliyebobea, ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu bwana Salva Rweyemamu," alisisitiza Selelii.

"Ushahidi mwingine tulioambiwa kamati teule ya Bunge kwamba mmiliki wa Kampuni ya Richmond ndiye mmiliki wa Kampuni ya Caspian,ni mfanyakazi wake mwenyewe(Rostam),ambaye alithibitisha kwamba mawasiliano yote ya Dowans yalikuwa yakipitia katika kampuni ya Caspian", alithibisha Selelii.

"Mtu mwingine ambaye alituthibitishia kwamba Kampuni ya Richmond na Dowans ni kitu kile kile,ni mtoto wa mwanasheria maarufu sana nchini aliyekuwa akiitwa Mukaddas, ambaye ndiye aliyesaidia hata kupata nyumba ambayo walipanga, ambaye yeye ndiye alikuwa akilipia pango ya nyumba hiyo,kuanzia wakati wa Richmond na baadaye Dowans" alisema.
 
Mmh sema ww tukisema sisi tunawasingizia! Wakaangane wenyewe kwa wenyewe by 2015 watakuwa chumba cha mahututi, tuchukue nchi wenye nia ya kuiendeleza
 
Salva Rweyemamu kesho akiamka anatuma email kwenye vyombo vya habari kukanusha!
 
"Akizunguma na Kituo cha Redio cha Zenji FM, 96.8 cha Zanzibar katika kipindi maarufu cha ‘Mwangaza wa Habari', Selelii ameeleza kuwa aliambiwa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz anahusika na Kampuni ya Richmond na pia ni Mmiliki wa Kampuni ya Caspian, na hili kamati teule tuliambiwa na mwandishi wa habari aliyebobea, ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu bwana Salva Rweyemamu" alisisitiza Selelii.


Huyo kwenye Red jamani si ndo kawa mbele kwenye kukanusha hili jambo.......... mara kageuka loh shame up on him!!!!!
 
Seleli siku zote ni mpambanaji bungeni kutetea maslahi ya taifa. Sote tunamjua na tunamwamini anachokisema.

Bado wako wapambanaji wengi tu hapo nje hawajaongea hadharani juu ya mafisadi na ufisadi wao nchini. Subirini kidogo, mengi yataibuka zaidi na zaidi kama hayo maelezo juu ya Salva Rweyemamu anavyomg'ata na kumpuliza JK huko ikulu.
 
Hivi unahitaji kuambiwa na Seleli kwamba Dowans na Richmond ni kampuni hewa za Rostam ????????????????.
 
Issue sio kama RA anamiliki Dowans maana kila mtu anajua hilo.
Tatizo sheria zetu ziko loose kiasi kwamba mtu anamiliki kampuni lakini hakuna legal document inayomwonyesha kuwa ni mmiliki.

Kwa hili RA ataendelea kutupiga mabao ya kisigino
 
Haya sasa semeni mnataka nini tena,this is more than serious so let decide guys what we gona do with this Iranian jambazi
 
Kumbe mnajua RA ndiye mmiliki wa Dowans,sasa kelele mnazopiga dhidi ya viongozi wa nchi zinatoka wapi wakati RA si kiongozi wa TZ?
 
Kumbe mnajua RA ndiye mmiliki wa Dowans,sasa kelele mnazopiga dhidi ya viongozi wa nchi zinatoka wapi wakati RA si kiongozi wa TZ?

Rostam ni mwizi aliyetuibia AKIPITIA LANGO KUU na tena akisaidiwa na viongozi wa juu tuliowapa dhamana na kuwaamini kutulindia mali zetu na maslahi ya taifa. Hapo ndipo ugomvi unamojikita.
 
nadhani kwa hapa tulipofika na jambo hili sidhani kama haya aliyosema selelii ni habari mpya!.... jamani nadhani mnashindwa kukumbuka kuwa kwqnye kampeni za 2005 Rostam ndiye aliyekuwa akiongoza kampeni za mgombea urais wa CCM kama alivyofanya kinana safari hii. sasa mnadhani mtu kama huyo atafanywa nini?

bila shinikizo la nguvu la wananchi hiyo pesa italipwa tu!!!!!!.
 
Mmh sema ww tukisema sisi tunawasingizia! Wakaangane wenyewe kwa wenyewe by 2015 watakuwa chumba cha mahututi, tuchukue nchi wenye nia ya kuiendeleza
Wenye moyo tujiandae kuchukua nchi, chama cha kijani kwisha... watakaangana mpaka waive wote!!! :amen:
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom