Rostam na Manji watoe maelezo vinginevyo watiwe pingu!

Hii nchi ni yetu sote, Mengi na mimi hatuna tofauti when it comes to maslahi ya taifa. Alilofanya Mengi ni jambo kubwa sana na tunatakiwa wote tujitoe kila mmoja kwa namna yake kuendeleza huu mpambano. 'Inatakiwa afanye action...' kwani yeye ni nani nchi hii? Nchi sio yake peke yake? Angekuwa yeye ni rais tungejua anafanya kazi tuliyomwajiri kufanya. Kumbe la, anajitolea tu! Tusipende kukaa na kumtegemea mtu mmoja tu ajitolee kwa ajili yetu. Na sisi tutoe michango yetu!

Tuambie hiyo action plan uliyo nayo!
 
Tuambie hiyo action plan uliyo nayo!

Kama ningekuwa na uwezo wa kumshauri Mengi ningemwambia kuwa tayari keshajilipua. Kwa hiyo hana cha kupoteza akisimama mbele ili tumfuate. Nadhani kwa sasa akiurdi nyuma atasababisha majeruhi zaidi. Kwa hiyo akubali kuwa Rajolina wetu ili sisi tumpe shavu kumalizia kazi.

Watu wanaomtuhumu Mengi kuwa siyo msafi wanaweza kuwa na hoja. Lakini wasilete za kuleta hapa. Tunaweza kumshughulikia Mengi baadaye ila kwa sasa naamini kazi yetu kubwa ni kumalizana na hawa mapapa! Tukiacha moto ukazimika hapa hatutaweza kuuwasha tena. Supu ya mbwa inanywewa bado ya moto, ikipoa hainyweki tena. Tunatakiwa kushikilia kamba hapa hapa! Mengi hebu kesho twende basi pale Mnazi Mmoja au Jangwani tuanze kazi ya kihistoria. Natamani hata ingekuwa leo jioni. Mzuka unapanda na presha pia. Finya hima Mangi!
 
Wakutiwa pingu kwanza ni MKAPA, ANNA MKAPA, IDDI SIMBA, KARAMAGI, MSABAHA, CHENGE, SUMAYE, LOWASSA. MZINDAKAYA, NEMROD MKONO, na MENGI, baada ya hapo ndio Wafuate ROSTAM na Wenzake.

FISADI Hana RANGI, Kama lazima wawe ni WEUPEEE Peke yao na WEUSI NDIO HASA MAFISADIIIIIII Sheria ianzie Juu na ni Msumeno ikate kote koteeeeee


Wewe lazima utakuiwa mtoto wa Rostam au wa Jeet Patel, maana watanzania tunalia na hawa majangiri wewe unawatetea !!!! uhwwwwwwwwwwwwwwwwwwwwwwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Pwani ya Kenya nisehemu moja wapo ilio na washairi au malenga wazuri, hebu basi nitupe kipande kimoja cha ushairi wa mmoja wa Mwana Kenya ili ushairi huu uwe ni zawadi kwa Mengi na Wapambe wake

DALILI YA MTU DUNI HUONWA VITENDO VYAKE
HATA ATIWE CHUPANI HUTOWA KIDOLE CHAKE
 
Pwani ya Kenya nisehemu moja wapo ilio na washairi au malenga wazuri, hebu basi nitupe kipande kimoja cha ushairi wa mmoja wa Mwana Kenya ili ushairi huu uwe ni zawadi kwa Mengi na Wapambe wake

DALILI YA MTU DUNI HUONWA VITENDO VYAKE
HATA ATIWE CHUPANI HUTOWA KIDOLE CHAKE

Ungetufafanulia maana yake ingetusaidia zaidi maana ushairi ni fasihi. Akina Mengi tuko wengi lijue hilo kabisa, wote wenye na uchungu na nchi hii, wapiga vita ufisadi.
 
Ukiacha madhaifu ya kawaida ya binadamu, mimi ninatamani sana kuwa mtoto wa Dr. Slaa au Mengi. Hawa ni wababa jasiri na shupavu, wanathubutu. Narudia tena, achana na mapungufu binafsi but are our parents, brothers and uncles who dare to peak out openly. Big up!!! Nataka hao mapapa waliotajwa jana wathubutu waende mahakamani!!! Zile kesi Kisutu za EPA zifutwe zote ibaki ya Jeet aunganishwe na mapapa wenzake. Period. Zikimalizika hizo, then zifuate za hao mapapa wadogo waliobaki then zifuate za vidagaa waliokwisha fikishwa mahakamani sasa tangu November 2008 (EPA, Richmond, na Matumizi mabaya ya Ofisi ya Serikali-kina Mramba).
 
We want our money and not killing anybody.

We can't get our möney back therefore is much better for them be killed in order not to steal again.
If our laws and rules can't try them so the best option is for we loyal citizen to try them by any means possible be by fire or knife
 
ukiacha madhaifu ya kawaida ya binadamu, mimi ninatamani sana kuwa mtoto wa dr. Slaa au mengi. Hawa ni wababa jasiri na shupavu, wanathubutu. Narudia tena, achana na mapungufu binafsi but are our parents, brothers and uncles who dare to peak out openly. Big up!!! Nataka hao mapapa waliotajwa jana wathubutu waende mahakamani!!! Zile kesi kisutu za epa zifutwe zote ibaki ya jeet aunganishwe na mapapa wenzake. Period. Zikimalizika hizo, then zifuate za hao mapapa wadogo waliobaki then zifuate za vidagaa waliokwisha fikishwa mahakamani sasa tangu november 2008 (epa, richmond, na matumizi mabaya ya ofisi ya serikali-kina mramba).


wazo zuri....sana but unless you want to blame your mum.,,you still have an opportunity to be yourself ....personality ..with reputation exceeding them....that starts today!!

Goodluck!!
 
mwanakijiji awali ya yote let me put my stand clear ktk haya mambo kwa ujumla inawezekana ningelipost haya ktk thread nyingine inayohusu nani kuongoza mapambano ya mafisadi but nimepost kwako specifically ili nijibu hili na kupitia hapa nikuombe usijetumbukia ktk vita iliyokosa muelekeo.

My stand ni kuwa falsafa nzima na nia ya mapambano ya mafisadi imepotea kabisa,sasa imekuwa ikitumika vita hii kwa maslahi binafsi ya watu either economic gain au political gain.

Nimekuwa msomaji mkubwa wa post zako,na makala zako katika tz daima na sometimes mwanahalisi i can see a brain in you,usije ukawa/tukaingia ktk vita iliyopoteza muelekeo.

Vita mafisadi imekuwa kama vita ya mwizi anawachomea wenzie kwa polisi ili yy aendelee kuiba na kuwaibia watu,jana nilipoona kauli ya mengi nikona aina ya unafiki ktk nchi hii mengi amehusishwa na kuikopa nbc na kuendesha mkakati wa kuimaliza lart iliyoundwa kukusanya madeni alikopa kupitia kampuni yake inayoitwa ( achwedu ltd ) ambayo alitumia kuchota pesa through import support na baadae kujenga hoja kuwa hakumuagiza gm wake kuchuka mkopo huo,huyu anaedai leo anaendesha vita ya mafisadi baada ya kuiweka under receivership achedu ltd ikawekwa chini ya lart ili iweze kuuzwa na asset zake through lart aliendesha mpango akiwa na kina iddi simba kuimaliza lart.

Mengi btn 1985 to 1995 ameshiriki ktk kui drain nbc,mbali ya hilo alichukwa mkopo mkubwa ambao hakulipa kuanzisha kampuni inayoitwa tanzania chemicals ltd ambayo iliitangaza muflis ikawekwa under lart lakini kabla hawajauza mali lart waz m alizwa,sasa huyu leo amenunua share ndani ya vikoba badala ya kufanya ununuzi wa share kwa njia za kawaida ili pesa anadai anawapa vikundi bure while fedha zile zinarudi ktk account ya vikoba na kwa taarifa amenunu 60% ya hisa za vikoba leo ana tumia hiyo pesa kutuo kama msaada kumbe ana rise capital ya vikoba kwa kudai anagawa bure kumbe ukiangalia marejesho ya wanachama wanarudisha pamoja na principle.

Vita hii ya ufisadi si vita takatifu watanzania tunadanganywa mchafu hawezi kusafisha uchafu,ni kama issue ya slaa anashiriki kupitisha poshao za wabunge anapokea hizo pesa akija nje kwa watanzania anatuambia posho za wabunge ni kubwa while ameshiriki kupitisha na bado anapokea,this is too much ifike mahali tusikubali mengi he is no clean na wenzie,ukiangalia mwakiembe si msafi ndie alimzuiya zitto asipeleke mswada bungeni wakuitaka serekali ipige marufuku magunia ya manila so that itumike ya katani ili ku promote zao hilo akamdanganya kwa hoja kuwa viwanda vyote vya katani ni vya mohamed enterprises,kumbe analinda maslahi yake kwani yy ana kampuni inayo import bags inaitwa tbc ltd.

Tukiwaangalia wote hawana nia njema na taifa hili hii wanayoita vita ya mafisadi haina genuinity yoyote it is just wanatumia a marketing psychology inayosema kuwa ( a threat to ur rival its ur opportunity either to grow or get rid of him ktk soko) hapa haman uhalisia its full ubinafsi.

Ndg zangu wana jf vita hii inahitaji sisi vijana hawa over 40 ndio waliotufikasha hapa umasikini anaodai mengi umetokana na mafisadi na yeye amechangia 80 to 90s mengi ameshiriki kufilisi bank zetu leo anatufumba macho,suluhisho wote wanyamaze tufanye national diolog na wanaotakiwa kushiriki ktk mdahalo huo ni watu wa umri usiozidi miaka 35, zaidi ya hapo wote ni wezi na ndio waliotufikisha hapa tutafute suluhisho letu wenyewe.
mawazo ya kipumbavu haina mfano,wewe kwa kutambua hilo hata kabla ya mengi kusema aliyosema jana, ulishawahi kuchukua hatua gani kukabiliana na tatizo hili??

vinginevyo nenda kasemee maneno haya uliyosema hayana nafas hapa!!!
 
Last edited by a moderator:
Tutawaleta watu wengine kwa nafasi zao; hoja zangu ni kwa watu hawa wawili kwanza Rostam na Manji. Tayari kuna kazi ambayo nimeiandaa ya Mkapa na wengine. So, focus! Rostam na Manji watoe maelezo juu ya mambo hayo niliyoyataja vinginevyo watiwe pingu!
 
pole mwanakijiji kumgusa rostam usokwa uso, naona amekuvaa na kukutukana vilivyo. ila mwisho wao upo, na unakuja tena haraka sana. watz tumechoka nao, tumechoka, tumechoka jamani.
 
pole mwanakijiji kumgusa rostam usokwa uso, naona amekuvaa na kukutukana vilivyo. ila mwisho wao upo, na unakuja tena haraka sana. watz tumechoka nao, tumechoka, tumechoka jamani.

Hili kundi la watu wachache haliwezi kutuchagulia viongozi na kutuamulia hatima ya taifa. Na kuna mtu mmoja ambaye anastahili kubeba lawama za kulea uzembe huu na mtu huyo si JK.. tumempigia kelele hashtuki, tumemuamsha haamki, na tumemuimbia nyimbo na hataki kucheza.. badala yake wanaendelea kugusana kwa kukimbizana kama wanacheza "kidali po"!
 
mimi nafikiri mtu anayewabeba kina Rostam na Manji nai JK. wewe mwanakijiji umesema si Jk, ninani sasa? JK hata kina Jeetu na patel amewapeleka lukapu kwa kuwatoa muhanga tu. mbona nasikia amechukua milioni kadhaa kwa sumaiya kwaajili ccm? JK hana ujanja, hana nguvu kwa hawa watu wawili. pingu hazitiwi hapo, hao watu wawili wamewaweka viongozi wetu mkonini, jk yuko kwenye kiganja cha mkono tena mkono mchafu.
 
Ila Mengi hata kama ana mapungufu..ni shupavu!

Hivi ktk Tz ukiwa na Riasi Mengi na Waziri Mkuu Slaa! Sii tunngeenda mbele kwa kasi zaidi?

Yaani kuwa na raisi mtu Progressive at the same time akiwa mzalendo, na pia jasiri wa kutenda!
 
"Rostam na Manji watoe maelezo vinginevyo watiwe pingu!"
Niliposoma tu hiki kichwa cha habari nilitamani mtoa kauli hii angekuwa ni mtu mzito serekalini au hata Raisi mwenyewe, that would have got me really excited! Hili ni agizo/amri/ an order! Lakini nagundua ni Mwanakijiji!- who the hell is he? Utafanya nini wasipotoa maelezo? Una nini cha kuwafanya hao wasiotaka kuwatia pingu? Absolutely nothing!
 
Mi kwa maoni yangu wananchi wajichukulie sheria mkononi kama wanavyowachoma vibaka moto kwa wizi wa elfu moja.Hawa jamaa wametufikisha hapa tulipo ni zaidi ya vibaka wanaokwapua vihela vyetu.Hawa watu wakipita mitaani ni kuwarushia mawe wachomwe moto kwa matairi ya magari yao ya kifahari.Ni wezi na serikali (hasa CCM) wanajua hilo.

Tuungane watanzania tuwateketeze hawa mafisadi

Nani atamfunga paka kengele shingoni??
 
Mmoja atoe maelezo ya kuhusika kwake na wizi wa EPA na Dowans (kabla sijaamua kujitolea kumsaidia kurahisisha kutiwa pingu kwake ) na tena aeleze kwanini ya Al-Adawi walibuni hii mbinu ya kufungua kampuni ya Dowans kwenye Free Trade Zone kule Costa Rica mahali ambapo hawana ofisi wala jengo na kampuni hiyo iko mfukoni mwa mwanasheria asiyejuliikana na haionekani kwenye taasisi zinazoandikisha biashara na wale kwenye orodha ya makampuni yaliyopo kwenye hiyo trade zone! na mwingine ajitolee kutoa maelezo kwanini alisema fedha alizorudisha za Kagoda ni za baba yake marehemu wakati jina lake na jina la baba yake hayaonekani kwenye nakala za Kagoda.

Vinginevyo, time is up!

Nani wa kuwatia pingu Baba!!! :( wakati wao ndiyo wala nchi na wanajua kutokana na 'michango' ya mabilioni waliotubia Watanzania kwa CCM na katika kinyang'anyiro cha mgombea wa CCM 2005 hakuna wa kuwagusa. Wameshapata ujeuri sasa kwamba wanaogopwa na hakuna atakayethubutu kuwagusa. Tutapiga kelele, tutafoka lakini kamwe hawa mapapa wa mafisadi hawataguswa ng'o :( Tusimsahau na yule 'wakala' wa awamu ya tatu wa rada, ndege ya Rais, magari na helicopters za jeshi ambaye alitoroka nchini katika mazingira ya kutatanisha pamoja na kuwa tayari polisi na TAKUKURU walishaanza kumuhoji, papa fisadi Vethalani.
 
Back
Top Bottom