Elections 2010 Rostam na Kikwete Dhidi ya Dokta Slaa

CCM imetuletea duara jeuri la umaskini.

HATUA YA KWANZA: CCM Imetuletea umaskini
HATUA YA PILI: Kutokana na umaskini huo, tuna njaa kali sana
HATUA YA TATU: Kutokana na njaa hiyo tuko tayari kuuza chochote tulicho nacho ili tupambane na njaa
HATUA YA NNE: kutokana na hali hiyo ya kuuza chochote, tuko tayari kuuza haki yetu ya kuchagua viongozi
HATUA YA TANO: Kwa hali hiyo hapo juu, wakati wa uchaguzi Rosatamua anakuja kununua kura zetu kuichagua CCM
HATUA YA SITA: Kwa kuuichagua tena CCM inabidi tukaanze tena hapo juu kwenye hatua ya kwanza.
 
Hayo ni maneno ya uswailini na mitaani, atoroke nchi kwa kumuogopa nani? na alishasema kama kuna mtu ana ushahidi aende mahakamani, sasa nyie mnae sema pembeni munaogopa kufika mahakamani?? basi watumeni wale ambao hawaogopi kufika mahakamani, kina nyangumi....
 
Rostam SI Mtanzania. SI raia. Lakini wanaondolewa raia kama Hussein Bashe, wanawekwa mamluki toka Rwanda!

Hiyo ndiyo CCM "mnayoililia"? Yaani kwa sasa, rangi ya njano na kijani INATIA KICHEFUCHEFU!

Heri enzi za TANU, alipokuwapo Mwalimu. Tulimpenda, alitupenda. Tulimheshimu, akatuheshimu. Tulimwogopa pia, lakini aliongoza kwa haki, HAKUPENDA MAJUNGU! Kama kulikuwapo na viongozi wanaolumbana, mnaitwa wote Ikulu, kujieleza. Papo kwa papo! Hakutaka UZANDIKI!

Kwa JK? Thubutu! Labda jogoo aote meno!
 
Hao wanaozungumzia miaka 50 ya utawala wa CCM kuimaliza nchi halafu kuwa vigeugeu kugeuka kuanza kumsifia Nyerere aliyekula miaka zaidi ya 25 kati ya hiyo 50 inayotajwa ndiyo wanaoshangaza kweli. Wakati wa Nyerere nyie mnaojifanya vidomodomo mngekuwa mnanyea kwenye makopo sasa hivi. Acheni kupenda visivyopendeka! Eti hakupenda majungu? Alikuwa baba wa majungu, nenda kawaulize waakina Babu na Kassim Hanga... Alituheshimu my rear... Mtu alikuwa anakaa kwenye redio masaa mawili mpaka matatu anazungumza yeye pekee yake bila ya kuulizwa maswali. Tena hayo mazungumzo yamejaa vicheko vya kejeli. Kiongozi gani umemsikia anahutubia wananchi wake kupitia redio ya Taifa halafu anakuwa anachekacheka kwenye hiyo hotuba? Acheni hizo...
 
Tuache maneno tufanye vitendo nchi inaangamia kwa kuwaweka hawa wahuni waliopo CCM ya leo. Wako wapi wazee wetu kina Sokoine,Kawawa, Nyerere jamani amkeni huko mlipo mtuombee maana Taifa letu linaangamizwa na hawa wahuni. Eeh mwananchi Mtanzania mkombozi wetu kashafika sasa tumia kura yako vizuri CHAGUA Dk.WILBROAD SLAA chagua CHADEMA hii ya sasa maana ndio itakayo ponya majeraha yanayoiumiza Taifa letu. EEh Mola Utusaidie
 
mimi ni malembeka shija mwana nzali na sio rostam ila watu wanazidisha maneno na ndio kazi yetu watanzania tuliyobaki nayo!mimi napita sana igunga na nimeanza kupita since 91 na ve seen alot of change taking place so i dont see why people bluff
 
Maharagande alikilalamikia CHADEMA akisema kimekuwa kikitumia lugha za kashfa dhidi ya wagombea wengine bila kujali ni wa CUF au chama kingine.
Alibainisha kuwa kitendo cha mgombea urais wa CHADEMA, Dk. Wilibrod Slaa kuzungumzia posho, mishahara na mafao ya wabunge kuwa ni makubwa na kutumia ajenda hiyo kwenye kampeni ni usaliti.
Alisema Dk. Slaa ni sehemu ya viongozi waliopitisha mafao hayo kwa kuwa alikuwa Naibu Kiongozi wa Upinzani pamoja na Mbunge wa CUF, Hamad Rashid Mohamed na kwamba Dk. Slaa mwenyewe alichukua mafao na mishahara hiyo ya wabunge anayodai ni mikubwa.

Source: Raia Mwema

Hakuna jipya hapa...!
Yatarudiwa hayahaya weeee....posho za bunge...posho za bunge....mishaharaaa!!!!
Nothing alse!
Shame on you Dubo-thing!
 
Wakuu najua wanachama wengi wa JF siku hizi wameacha kusoma magazeti ya RA. Hivyo nimeona niwaletee mada hii ambayo imetoka kwenye gazeti lake la leo, RAI, ili vichwa viweze kijadili. Habari yenyewe ina kichwa kisemacho "Ndoa kati ya Dk Slaa na Chadema yafichuka". Katika habari hiyo ambayo imewekwa kwenye ukurasa wa mbele kabisa ina dondoo zifuatazo:

:lol: Ni baada ya chama chake kumtaka agombee urais wa Tanzania
:lol: Yeye alitoa sharti alipwe mshahara wa sh milioni 12 kwa mwezi
:lol: Chadema ilipokubali ikamwahidi pia mafao sawa na ya wabunge
:lol: Ni kwa kipindi cha miaka atakachokuwa nje ya Bunge
:lol: Atakuwa ni katibu mkuu wa kwanza kulipwa mshahara mkubwa.

Nimejaribu kuisoma kwa undani zaidi hii habari kwa uelewa wangu nikaona kuwa wanachajaribu kusema kwenye hii habari ni kuwa Dk Slaa anapingana na Ilani ya chama chake ambayo ameanza kuitangaza kwenye kampeni zake, ya kupunguza mishahara ya wabunge na viongozi wengine wa serikali. Na kwa mtazamo mwingine inaonekana Dk Slaa ni mbinafsi mwenye kujali maslahi yake zaidi kuliko maslahi ya wengine, Je akiingia madarakani atatimiza kweli anayohubiri?

Nimeileta mada hii kwenu ili tuweze kujadili:
1) Ukweli wa suala hili
2) Kama ni ya kweli, Je Dk Slaa ni Mbinafsi
3) Nini Impact ya habari hii kwenye uchaguzi mkuu 2010

Nawasilisha
 
Ndiyo maana tunamtaka dr.slaa aje aondoe uchafu huu wa kimtandao wa kikwete,rostamu,lowasa na vimelea vyao tumew3achoka yaani nchi inatawaliwa na watu wasiozidi kumi tu...........
Rostam kaja kufanya biashara watu km hawa ni bora tuweke mipaka wasiingie kutuchafulia serikali na nchi yetu tuwaruhusu tu kwa nia njema waendelee na biashara na sio haya mambo ya kuwaingiza serikalini mpaka wanawaweka viongozi wetu mfukoni kiasi hiki..........
 
Nimegundua uzalendo ni kitu muhimu sana na ukiwa si mzalendo u can do anything inhuman bse hauna uchungu na nchi yako.
Kutokuwa na uchungu ni kwa sababu unako kwenu ambako unaweza kukimbilia
 
kuna maneno nikiyasema,nitaambiwa ni MHAINI....ngoja wakati muafaka ufike..
 
hakuna jipya hapa...!
yatarudiwa hayahaya weeee....posho za bunge...posho za bunge....mishaharaaa!!!!
nothing alse!
shame on you dubo-thing!

ni kweli huu ni usaliti mtupu, mbona wewe paka jimmy unafanya selective information processing, kwani unataka sisi sote tuone mambo kwa mtazamo wako tuu????? Shame on you too!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Tatizo mafisadi papa na mafisadi nyangumi sasa wameungana; JK alikuwa anaondoka ila sasa wameshapozana; hujuma zao za kibishara zimerekebishwa; hapo ndio namuonaga Mengi kama kibaraka asiyejua anakokwenda; these differences could make something

Haya Mr Ephraim Kibonde na Mgosi Makamba tunaomba your comment on this!!:A S 8:
 
hawa akina rweyemamu ni masikini wa kipato na akili na njaa zao ndo zinazofanya watumiwe ila hawataweza na huyo rostam ni mwizi mkubwa asiejua ni nani hatuhitaji kupelekwa darasani kwa hilo
 
Back
Top Bottom