Rostam, Msabaha, Kikwete and Richmond - Yes I said it again!

Bado,

Analysis za Mwanakijiji... ni za kufikirika kumuweka ubaya RA kama muhusika... narudia... kumuweka mtu/taasisi kama fisadi au mwizi... u must have clear evidence without doubt? Hayo mambo ya kutumia logic etc. ni uzandiki tu kama magazeti yanavyofanya watanzania wasijadili mambo ya maendelea bali wajadili mambo ya uchawi.

Kasheshe... sijaspin kitu.

Ni lini Rostam alikanusha yeye kuhusika na Richmond? Siku ya Jumatano nitakuonesha kitu ambacho hakijaoneshwa na mtu yeyote kuhusu Kagoda na Rostam..!
Hili la evidence... mwanakijiji ana-spin tu! nothing new....

Evidence siyo lazima iwe ni kitu tu hata mazingira, na logic inatusaidia kutumia akili kuchambua vitu. Ndio maana wenzetu wanasema " it walks like a duck, it sounds like duck, and it looks like a duck then it a duck!" Mantiki inatusaiidia kuchambua ujanja wa maneno ya watu, unatusaidia kuona fallacies katika hoja. Hivyo kupuuza logic ni kwa hasara yako mwenyewe.

Kwa mara nyingine naungana na Kitila... kwamba vita ya ufisadi.. inaelekea kutushinda maana hatufuati mafisadi tunafuata victim wa mafisadi...

Yaani Rostam ni victim wa mafisadi? u must be kidding. Tafuta gazeti la Raia Mwema Mei 7 mwaka huu na wiki mbili kabla yake.
 
Mkuu FMES,
Hapa nakubaliana na wewe kabisaa.

Inawezekana JK alijua kuwepo kwa uhusiano wa Lowasa na RDC, kama biashara zake Lowassa, lakini ukiangalia kabisa tokea pale alipochemsha kuahidi umeme wa RDC kuwaka, inaelekea kabisa hakuwa mshiriki wa moja kwa moja. Kufahamu inawezekana lakini nafikiri Lowassa alimficha mwenzake details.



Mkuu MMJJ,
Hapa inabidi kuwa makini tusijepoteza mwelekeo.

Hadi hivi sasa hatuna kiunganishi chochote hata cha kimazingira mwenye nacho akiweke. Ni muhimu tupate data angalau kiduchu kuliko tukamzulia wakati anayo mengi tu yaliyo yake, EPA, Meremeta n.k.

tatizo ni kuwa kuna watu wanadhani JK ni safi, I don't.
 
Keil,

Ni kwa bahati mbaya watanzania tuna matatizo mengi sana... hebu angalia... Mh. Lowassa alithubutu kutaka kuvunja mkataba wa Richmond mara mbili, kila moja akiambiwa kwamba ukivunja taifa litapata hasara zaidi... na mshauri mkuu hapa ni Taasisi inayoitwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali chini ya Mh. Mwanyika. Baadaye hili lilisababisha waziri Mkuu kumwaga unga...

Sawa Mh. Lowassa alifuata ushauri wao akijua anashauri vizuri kwa manufaa ya taifa... juzi juzi serikali hiyo hiyo ikaweza kuona vifungu ambavyo wameamua kuvitumia kuvyunja mkataba ule ule ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliosema tusivunje....

Sasa angali Mwanasheria Mkuu wa Serikali Anakula Kuku hadi leo... wakati yeye ndio source ya matatizo yote...

Ambayo hawako direct na uvundo huo... ndio wanaathirika... Mh. Lowassa amejiuzulu, Mh. Rostam anasakamwa...

Ninyi watanzania muna matatizo gani... kwa nini hafuati kwenye matatizo munasumbuka na watu wengine?

Kasheshe kama Lowassa anajua alikuwa sahihi angesimamia msimamo wake. Kama Lowassa angejiuzulu wakati wa mchakato wa Richmond kwa kujikuta anapewa habari zisizo sahihi na kukataliwa kuvunja mkataba leo angekuwa shujaa. NI yeye aliyegwaya bungeni na kuamua kuachia ngazi badala ya kujitetea na matokeo yake ni kujaribu kujitetea kwenye TV.
 
Na hii issue ya AGOA hata Mbowe mwenyewe nilimpigia simu nikamuuliza...Na yeye sijui alipuuzia ama vipi...Lakini hakuona kama ni suala la kipaumbele...Sasa juzi tumesema hapa na yeye Kikwete at least kasikiliza kwani inawezekana na yeye alikuwa hapa!
Kwahiyo hiyo ni dalili nzuri kwani mara nyingi amekuwa akifuata kiaina ushauri wa hapa jf...!
Na sasa tunamuomba aufuate ushauri huu wa wazalendo kuhusiana na hizi kashfa za MAFISADI!
Kwani kama ni kweli anathamini michango yetu...Then NI MUHIMU SANA AKISIKILIZA USHAURI KWENYE HILI LA UFISADI PIA.
 
Keil,

Ni kwa bahati mbaya watanzania tuna matatizo mengi sana... hebu angalia... Mh. Lowassa alithubutu kutaka kuvunja mkataba wa Richmond mara mbili, kila moja akiambiwa kwamba ukivunja taifa litapata hasara zaidi... na mshauri mkuu hapa ni Taasisi inayoitwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali chini ya Mh. Mwanyika. Baadaye hili lilisababisha waziri Mkuu kumwaga unga...

Sawa Mh. Lowassa alifuata ushauri wao akijua anashauri vizuri kwa manufaa ya taifa... juzi juzi serikali hiyo hiyo ikaweza kuona vifungu ambavyo wameamua kuvitumia kuvyunja mkataba ule ule ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliosema tusivunje....

Sasa angali Mwanasheria Mkuu wa Serikali Anakula Kuku hadi leo... wakati yeye ndio source ya matatizo yote...

Ambayo hawako direct na uvundo huo... ndio wanaathirika... Mh. Lowassa amejiuzulu, Mh. Rostam anasakamwa...

Ninyi watanzania muna matatizo gani... kwa nini hafuati kwenye matatizo munasumbuka na watu wengine?
Kasheshe nalazimika kukutahadharisha kuhusu suala la Lowassa kutaka kuvunja mkataba mara mbili! Mwakyembe na wenzake walishaeleza kuwa ni kweli Lowassa alifanya hivyo mwezi wa tisa na kumi 2006 wakati mambo yameharibika! Mchakato wa kumpata Richmond ambao ulijaa mizengwe ulifanyika kati ya Februari na Juni, 2006 na Lowassa alihusika moja kwa moja kwenye hili. Ndo maana akina Mwakyembe wakamwambia: "pima mwenyewe uzito wa matokeo ya uchunguzi wetu na wajibu wako kikatiba ndani na nje ya Bunge". Lowassa akajipima, akaachia ngazi. Angekuwa hana tatizo, asingeachia ngazi haraka haraka hivyo, angeingia Bungeni na kujitetea kwa kuuchanachana ushahidi wa Kamati ya Dk. mwakyembe. Ni hilo tu Mkuu ulielewe.
 
Mimi nilisema hapa siku nyingi kuwa haingii hakilini subordinate afanye kitu ambacho hamjakubaliana na superior akae kimya kusubiri report ya bunge. JK anausika moja kwa moja na RDC na ndo maana EL amekasirika kiasi kikubwa kuona ametoswa wakati mwenye mzigo anatesa.

Mkakati wa EL kurudi utafunua mengi kama JK mwenyewe hakujitokeza na kusema jinsi gani haliusika kwani wananchi hawatamwelewa JK kuona anamwachia EL arudi bila maelezo ya kutosha.

Anayefikiri kuwa wananchi hawatauliza swala la RDC amekosea kwani wananchi hivi sasa wako makini mfano ni Masha kuulizwa ushiriki wake na Deep Green Finance na akaamua kusema ukweli kwa kuitosa serikali na kusema walielekezwa na serikali kuanzisha deep green na kuifirisi.

Kikwete anafaamu issue zote za RDC, EPA, Deep Green na mengineyo yanayoendelea kutokea hivi sasa na ndo maana hakuna hata fisadi mmoja atayepelekwa mahakamani.

Asante kwa mawazo yako. Lakini mpaka sasa hakuna ushaidi wa aina yoyote unaomuhusisha Jakaya na uchafu huu wa RDC na kama unao basi tuwekee hapa ili tuanze kumkomalia shingo.

Lowasa alishikwa na hasira kwa madai ya kutotendewa haki na tume ya Mwakyembe kwani hawakumwita kutaka maelezo yake katika suala zima la RDC na wala hana hasira na Jakaya.

Tafadahli tusipotoshe umma kwa vitu ambavyo havina ushaidi.
 
Asante kwa mawazo yako. Lakini mpaka sasa hakuna ushaidi wa aina yoyote unaomuhusisha Jakaya na uchafu huu wa RDC na kama unao basi tuwekee hapa ili tuanze kumkomalia shingo.

Lowasa alishikwa na hasira kwa madai ya kutotendewa haki na tume ya Mwakyembe kwani hawakumwita kutaka maelezo yake katika suala zima la RDC na wala hana hasira na Jakaya.

Tafadahli tusipotoshe umma kwa vitu ambavyo havina ushaidi.


Sidhani kuwa Msabaha alijibatiza ubangusilo kwa sababu ya Lowasa. Lowasa hakumteua - just thinking loud !!
 
Sidhani kuwa Msabaha alijibatiza ubangusilo kwa sababu ya Lowasa. Lowasa hakumteua - just thinking loud !!

Je, Dr. Msabaha aliposema nje ya kiapo kwamba Richmond ni mradi wa Bwana Mkubwa na Rafiki yake. Je, alimaanisha ni Bwana Mkubwa yupi? Maana JK, EL na RA wote ni marafiki. Is it JK + EL, or JK + RA or EL + RA? Just curious!
 
sema tu bado hatujafikia mahali pa confrontation kati ya Bunge na Rais. JK anahusika na Richmond na pasipo yeye Richmond wasingepata nafasi yote hiyo. Walimchangia katika kampeni yake na zile tenda walizopewa ikiwemo kwa Msabaha kupewa wizara ya madini ilikuwa ni malipo ya shughuli hizo. Kikwete anajua hilo, Gire anajua hilo, Msabaha anajua hilo na Rostam anajua hilo.
 
Je, Dr. Msabaha aliposema nje ya kiapo kwamba Richmond ni mradi wa Bwana Mkubwa na Rafiki yake. Je, alimaanisha ni Bwana Mkubwa yupi? Maana JK, EL na RA wote ni marafiki. Is it JK + EL, or JK + RA or EL + RA? Just curious!

Hilo swali Tume Teule ililijibu. Naomba kuwasilisha ripoti:

Ukurasa wa 38-39:

Lakini Mhe. Dk. Ibrahim Msabaha (Mb), baada ya mahojiano chini ya kiapo, akaiuma sikio Kamati Teule kuwa katika suala hilo yeye atakuwa kondoo wa kafara tu au, kwa maneno yake mwenyewe, “Bangusilo” kwa lugha ya Kizaramo. Maelezo hayo ya ziadaya Mhe. Waziri nje ya kiapo yalioana na maelezo aliyoyatoa Balozi Kazaura nje ya kiapo tarehe 30 Novemba, 2007 ambapo mara baada ya kumaliza mahojiano na Kamati Teule kwa kiapo, Balozi akatoa maelezo ya ziada kuwa Richmond ilikuwa mradi wa “Bwana Mkubwa” na “mshirika wake mkubwa kibiashara”, akimaanisha Mhe. Waziri Mkuu na Mhe. Rostam Aziz (Mb). Hii haikuwa mara ya kwanza kwa Balozi Kazaura kuuhusisha uteuzi wa Richmond Development Company LLC na mkono wa Waziri Mkuu. Mara ya kwanza ilikuwa Januari 2007 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Biashara...
 
hiyo "akimaanisha"... I think they got it real wrong..!ukiangalia what transpired since then.. Waziri Mkuu is not the "Bwana Mkubwa" referred to.
 
Ndio maana nilisema Bunge ni muhimu sana.

Hivyo ni wazi kuwa kama kina Rostam wana wasiwasi na Bunge..Then ni wazi wana lao jambo.

Maana juhudi za kujisafisha ni nyingi mno to the extent kwamba inatia shaka.

Kwani kama si USANII wangejibu mapigo na Lowassa asingejiuzulu.

Ile ilikuwa danganya toto na wao wanadhani kuwa kwa kusema mtu mbaya ni JK basi mambo yataisha.

JIBU NI NO!

WARUDI BUNGENI NA KAMA NI JK ITAJULIKANA.

Hao watu kama ingekuwa ni mahakamani na wana hatari ya kuswekwa ndani miaka mingi basi wangesema ukweli badala ya kwenda makanisani.

Lowassa na Rostam wamejiandaa kisiasa zaidi badala ya kihoja na kisheria na hapo ndio wasi wasi wangu mkubwa ulipo.

Na kwa mantiki hiyo basi...Narudia usemi wangu kuwa...JK mwenyewe tunampa benefit of doubt kabla hajaja washington.

Pia wakati anaandaa tripu yake na sisi tunaanda mambo yetu na hoja zetu za msingi.

Na kwasababu hoja ya madini itazungumziwa kabla ya tripu yake...Basi tunasikilizia.
 
hiyo "akimaanisha"... I think they got it real wrong..!ukiangalia what transpired since then.. Waziri Mkuu is not the "Bwana Mkubwa" referred to.

Hilo la waziri mkuu kutokuwa bwana mkubwa pia linaweza kuwa twist ya kisiasa kwani Lowassa ndiyo kauli yake hiyo pale alipodai alitoa ushauri ili Richmond ifutwe.

Sasa kama ni yeye alifacilitate Mkataba wa Richmond..Na baadaye kugundulika madhara yake...then alitakiwa kutowa ushauri ama kujiuzulu?

Mimi nafikiri alitakiwa ajiuzulu na si kusema eti alitowa ushauri.

Na ndio maana nasema hawa watu wakibanwa bungeni humo watasema kila kitu.

Kwasababu kama yeye ndiye aliyeushinikiza mkataba huo...Hakutakiwa atowe ushauri wa kuufuta mkataba..Bali alitakiwa kutowa amri.

Huwezi kuwa mtendaji mkuu wa serikali...ukaufanikisha mkataba mbovu na kuona madhara yake na bado kuyafumbia macho hadi utolewe nishai.
Angefuata mfano wa SOKOINE..HAKUFANYA HIVYO NA YEYE NI MMASAI FISADI!

Si wazalendo hawa ni MAFISADI.

Na sasa kwasababu wanajuwa wana influence...Basi wanaitumia hiyo opportunity kutuchezea akili na kutowa kauli ambazo zinamlenga JK.

Na kwasababu JK ni mshikaji wao..Wanajuwa atapiga kimya!

Kama wanaliheshimu bunge pamoja na wananchi...Basi watasema ukweli huko Bungeni.
 
hiyo "akimaanisha"... I think they got it real wrong..!ukiangalia what transpired since then.. Waziri Mkuu is not the "Bwana Mkubwa" referred to.

MMJJ, how did you know that they got it wrong? Didn't they have a reason to substitute Bwana Mkubwa for Lowassa and not JK??
 
...Ripoti imetolewa wote tumeiona, maneno yote ya Kikwete during hii deal yapo clear tena wazi, kuwa kila mara alikuwa akimhoji Msabaha mambo yanaendeleaje, sasa mkuu akisema hoja ambayo haikubaliani na mawazo yako basi imepikwa, imepikwa na nani? Kwa nini hoja zako hazijapikwa au huwa hazipoikwi? Mbona hili la kupika kupika habari unalielewa sana?

Hakuna kitu kama hicho kwenye ripoti.

Hakuna neno Kikwete kwenye ripoti, achilia mbali kwamba Kikwete kamwambia Msabaha kama dili/kampuni ya Richmond ni feki utakiona cha mtema kuni.

Umepata wapi hiyo taarifa?

Unasema hoja zangu mbona hazisemwi zimepikwa. Tofauti ni kwamba wewe umeleta ishu as a fact, not as an opinion.

Kikwete kamuonya Msabaha, umesikia wapi hilo?

Role ya Msabaha ipo kwenye ripoti, na Msabaha alihojiwa. Msabaha aka volunteer 'dataz' nje ya kiapo, akatapika anayoyajua. Kama aliwahi kuongea na Kikwete kuhusu richmond mara kwa mara, kama unavyodai, haya Tume ingeyagusia.

Hakuna maongezi ya Msabaha na Kikwete mle.

Umepata wapi habari za maongezi ya Msabaha na Kikwete?
 
Mwanakijiji,
Leo mkuu ameamkia wapi?... duh unatisha!...

Hata hivyo mkuu wangu naungana na wewe kati wa Watanzania wanaosema enough is enough!... KIkwete ni FISADI..
Unajua hapa nimepata mwanya wa kujieleza vizuri pamoja na kwamba nitaudhi wengi hasa kutokana na kuingiza hoja isiyohusiana na mada hii.

Wanabodi, hasa kwa wale ambao hawakunielewa ktk issue ya Mugabe na Morgan nadhani hapa ni mahala pazuri kwangu kuweka record yangu sawa.
Binafsi simpendi kabisa Mugabe kama kiongozi yaani kama leo akifa nitafanya maulidi lakini simkubali kabisa Morgan, ni MNAFIKI na mshenzi mwingine ambaye hafai hata kidogo kushika nafasi ya Urais..
Mtazamo wangu huo unafanana sana na Mkatazamo wa Mkapa na Kikwete!.. Simpendi kabisa Mkapa kama nisivyompenda Mugabe lakini kutompenda kwangu hakuna maana ninamuunga mkono Kikwete.
Kikwete hadi sasa hivi kaonyesha UNAFIKI mkubwa ambao hauna tofauti na hisia zangu kwa Morgan..Tofauti ni moja tu Morgan nimefahamu kabla yaa na Kikwete nimechelewa kufahamu! Kutokana na hisia hizo inanifanya nishindwe kujibu swali ikiwa mtu ataniuliza kati ya Mkapa na Kikwete nani bora kati yao!.. Jibu langu litakuwa:- Hawa wote ni washenzi na hawafai kuwa viongozi hata kidogo...
Hoja yangu hii ni nzito na inaweza kuwashtua wengi lakini jamani ndugu zangu kuna wakati inabidi tuyatoe yaliyotujaa rohoni!...
Mkapa aliuza NCHI na leo Kikwete Kauza ROHO za wananchi wake!..
Tanzania imebakia mitunga (Zombies), watu wanaishi kwa kudra za Mungu sijui ndio nguvu za roho mtakatifu au kitu gani..

Mkuu mwanakijiji nakuvulia kofia kwa hayo yote Uliyo yatanguliza, sii kazi ndogo kumhusisha rais moja kwa moja na Ufisadi ambao wengi wetu hasa mimi nilishindwa kusema. Hofu yangu kubwa ilikuwa kama nikimhusisha Kikwete then nani atachukua nguvu na sheria ya kuwaangusha hawa kina Lowassa, Rostam na wengineo...
Kikwete anaweza kujiuliza ikiwa hata mimi wananchi wanasema ni Fisadi sasa kuna faida gani kuwachukulia hatua hao wanaojengewa hoja ya UFISADI?..tena itakuwa mbaya zaidi kama hahusiki kabisa na ufisadi huu.
Zaidi ya hapo sikuwa na sababu nyingine kwani Kikwete niliyemtegemea wakati wa uchaguzi sii huyu hata kidogo!
 
Umepata wapi habari za maongezi ya Msabaha na Kikwete?

Ni maneno ya Msabaha ndani ya kikao kilichomlazimisha kujiuzulu wakati akijitetea, haya yote yamo kwenye mkanda wa video ndani ya bunge mkuu vipi hukuona kile kikao vipi? Halafu kuna mengi sana yanayoihusu hii deal ambayo ni facts lakini hayakuandikwa kwenye ripoti,

kwa mfanobaada tu ya kudungua kuwa kuna mchezo umefanyika, Rais alimwita Masha na kumtukana sana Ikulu kuhusiana na hii deal, kabala ya kumuhamisha wizara, Lowassa kabla aya kusomwa ripoti Dodoma aliwahi kwenda nyumbani kwa rais kujaribu kumshawishi kuwa hana makosa lakini Rais alimkatalia kabisa kumsikiliza na kumwambia aende Dodoma bungeni, kuna Mtoto wa Lowassa anayeitwa Fredrick ambaye anahusika sana na hii deal lakini sioni akitajwa kwenye ripoti ya Mwakyembe,

Kuna facts nyingi zinazo-miss kwenye ripoti ya Mwakyembe, ambazo zinanifanya niamini kuwa Rais hakuhusika kabisa na hii deal kwa sababu kama angehusika basi asingeyafanya haya yote ninayoyajua, lakini ninaamini kuwa alikuwa akijua yote yanayohusu BOT!
 
Back
Top Bottom