Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

IPP media website wameweka picha ya Mpakanjia na marehemu mkewe lakini cha ajabu hakuna story. Hiyo ndio media ya Bongoland, kuna mtu kapigwa stop kuiweka hiyo story lakini akasahau kuondoa picha. (Au makusudi) Kazi kwako.

http://www.ippmedia.com/
 
kichwamaji;62460
Nguvu ya PR machinery ya CHADEMA siwezi kuisemea kwani simo, nawe (kutokana na mtiririko wa hoja zako hapo juu) nadhani humo,
ni obsever kutoka nje.

Ni kweli simo kwenye CHADEMA na kwa sababu umekiri kuwa mimi no bserver than naweza kumonitor jinsi spin na propaganda machina zinavyofanya kazi ili kuwafikia walengwa.

Ninachotaka kukueleza hapa ni kwamba CHADEMA hawafanyi kazi peke yao, kuna mtandao mkubwa unaokerwa na usanii huu na unaojua kwa kina wapi muungwana na watu wanakosea, wapi wana nguvu na wapi wana udhaifu. Upo mtandao wa watu wanaoipenmda nchi hii na walio tayari kuwekeza nguvu na akili katika kuleta mabadaliko. Hilo nalijua fika, sihisi; na ningekushauri usiidharau nguvu hiyo.

Sijadharau nguvu hiyo hoja yako ndio maana nikasema kuwa network ya CHADEMA iko mpaka Ikulu lakini tatizo ni kuwa wengi katika mtandao wa CHADEMA hawako tayari ku risk career zao au biashara zao na mengineyo kwa kuwapa supporting documents au kuleak mambo ambayo kama ukifanyika uchunguzi then trail itawafikia na hivyo hawako tayari kuface the consequences za hatua hiyo. CCM wanawajua lakini as long as kila mmoja katulia na anapata tenda za hapa na pale au vipromotion vya hapa na pale then why bother them?

Pili, kauli ya Mbowe kuhusu serikali ya mkoloni haikuwa political suicide kam unavyodhani. Huu ni mwaka 2007 siyo 1970. Ni wananchi wangapi wanaoishi leo, wanaotegemewa, waliomuona mkoloni wakaumizwa naye kiasi cha kumuona Mbowe mbaya? Hawa anaowaaddress leo wanaishi katika mateso ambayo yanafanana na yale waliyosoma vitabuni kuhusu ukoloni. Wanaona watawala wanavyoishi kwa kutumbua na wao wanavyohangaika, na wana hasira zile zile tulizokuwa nazo dhidi ya mkoloni.

Maneno yako ni kweli this is 2007 na siyo 1970 lakini usisahau kuwa mpaka 1960 damu nyingi ilimwagika ndipo tukapata uhuru wetu. Je wale wanajeshi wetu watajisikiaje siku Mbowe anaapishwa Uwanja wa Taifa ili hali huko nyuma aliwahi kuwasifia waliotutawa? Narudia it might have not been a political suicide lakini itlikuwa ni Political gaffe ambayo aliitoa in a wrong place(Uwanja wa mashujaa). Kweli its almost 40 yrs atangu tumepata uhuru lakini huwezi kulaumi kila kitu wa serikali after all matatizo ya kuichumi ya Tanzania yanatokana na factors mbali mbali na nyingi ni external factors(thread yake itajitegemea)

Kumbe hujajiuliza kisa cha umma kuamka sana leo na kuunga mkono hoja ya Zitto?

Hilo ni tusi kubwa, Umma wa Tanzania uliamka tangu hajaja mkoloni na baada ya mkoloni na baada ya vyama vingi hivi umesahu watu walivopinga vya vingi? lakini serikali ya wakati ule iliamua kuwa ni bora kuwa na wapinzani kuliko kutokuwa nao. Watanzania waliamka hata kabla zito hajazaliwa.Unless unazungumzia mbunge ambaye ni charismatic then nakubali kuwa Zitto ni charismatic lakini siyo makini kutokana na sababu mbali mbali lakini zaidi anauza sana magazeti. Nakuhakikishia kuwa the only time he actually got passionate and detailed in a reply was when he was defending himself for not outlining policies! na hii ya "MABOMU" ndio imekuwa dstarction kubwa zaidi

Ni kwa sababu wananchi wanaona wanaishi maisha ya kitumwa wakatyi raslimali zao zinawatajirisha walio madarakani. Hisia zao zimejikita katika dhana ya chuki dhidi ya ukoloni mweusi, tena mbaya kuliko ule uliokuwapo - ambao hata hivyo wengi wa vijana wa leo hawakuuona. Hiyo ni political capital, sio suicide.

sasa naomba unifafanulie au nionyeshe kiongozi gani amejitajirika kwa wizi? je kuna ushahidi wowote wa kuback up hilo? Je kuna sehemu gani iliyoandikwa kwenye katika kuwa mwasiasa hatakiwi kuwa Tajiri? Freeman Mbowe anapesa nyingi tuuu je huyu naye ni Mkoloni mweusi? tumchukie Mbowe kwa sababu ni mfanyabiashara aliyefanikiwa?nadhani ni political bankrupt tukianza kuwachukia mawaziri au wanasiasa kwa sababu walifanikiwa kuwa na wepesi wa rizki.

Kusema Zitto anamu-outshine mkubwa wake ni dhana ya ki-CCM.
naomba unifafanulie unamaana gani dhana ya ki -CCM?

Katika CHADEMA wanatambua talent za watu na kuzikuza, wanajenga chama taasisi kwa nguvu ya kila mmoja, leo huyu kesho yule.
Na hilo ndilo tatizo la CHADEMA kwani talent pekee haitoshi.It takes more than talent to be a politician!

Katika suala hili, aliyefukuzwa na Bunge ni Zitto kwa kile alichokisimamia, lakini alikuwa anazungumza siyo kwa ajili ya CHADEMA ila kwa niaba ya upinzani.

No kilichomfukuza Zitto bungeni ni ubahili wa chama chake kushindwa kuwalipa researchers 2 ambao walitakiwa wadig deep on those issues za mikataba kabla hajaenda public. hii inaonyesha jinsi gani anavyoendekeza punch punch & judy politics ambazo hazina substance zozote kwani angekuwa makini na documents au source materials zake angeendelea kuwepo bungeni.Sikatai anaweza akawa ni potential politician but what Zitto is lacking is substance to back up his rhetoric.

Hamad Rashid ndiye kiongozi wa upinzani Bungeni, lakini halalamikii kuwa outshined kwa sababu hoja yao imekua. Bahati kwa CHADEMA ni kwamba hoja imesaidia kuwasha moto nchi nchi nzima na chama kinakua, hivyo njia inapatikana, na viongozi wanaitumia. Ukilitazama kwa macho ya ubinafsi, ndo utasema amemu-outshine mkubwa wake, Ni kweli kwamba kama angekuwa CCM wangeishamnyamazisha maana ndiyo system yao. Je, na sisi tujiruhusu kufikiri na kutenda kama CCM?

mheshimiwa, ukitaka kujua kuna matatizo katika opposition Tanzania basi mtazame MAALIM SEIF SHARIF HAMAD. I like and respect MAALIM, but in the eyes of the electorate, when it comes to winning elections - once a loser, always a loser, and making opposition leader would has been a disaster, a cracking addition to the shadow cabinet he'll make, but in terms of both party and opposition leadership, he is the past hivyo tumwache kwa sasa.

Suala la kuwa hoja imewasha moto nchi znima nadhani ni over statement. Sijaona evidence yoyote kuonyesha kuwa nchi nzima imewaka moto kwa sababu ya hoja ya Zitto Kabwe japo ni kweli watu wako curious kutaka kujua kuhusu mikataba lakini kosa zaidi ni kwa serkali kutoweka wazi na kwa lugha ambayo wananchi wanaelewa kuhusu mikataba ya madini. Usisahau kuwa both CHADEMA na CUF need to develop policies and must be prepared to attack the government's agenda and place it in constrast to their own. Na hiyo itakuwa the real test for Mr Freeman na Hamad. Na kama ningekuwa ni CCM then i only wish their were more like CHADEMA and CUF because you would keep us in office!

Tatu, kuhusu Dk. Slaa. Kumbe hujajua kinachoendelea. Hakupeleka tu internet sources bali alitumia hoja ya sources hizo kutaka serkali itoe majibu, halafu wenye sources wenyewe wakanza kufumuka.

Actually Spika alimuuliza source ya ile email na Dr Slaa akataja email address ya ilikotoka na ile video ya ule mjadala ilikuwepo humu na mwenyewe akakiri kuwa kwa sasa source siyo muhimu sana lakini kilichomuhimu ni contents za ile source sasa mheshimiwa unataka watu wajadili mambo tuu bila kuwekana sawa kuhusu sources? Once again sipo hapa kwa ajili ya kupinga kila kitu lakini so far hakuna hoja au official majibu (kwenye websites zao) toka kwa CHADEMA au CUF au WAPINZANI za kumcounter GAVANA wa benki kuu.Sasa kama siyo kuplay politics ni nini huko?Ubadhiribu ulikuwa unafanyiwa na bado unafanyiwa uchunguzi na PCB au TAKURU uchunguzi bado unaendelea lakini naona wengine hilo hawalitaki wanataka na whats Dr Slaa has done is is essentially a PR exercise based on positioning and I think it shows a lack of conviction ambayo niitegemea toka kwa mwanasiasa mkongwe kama yeye.

Lile likitabu limejaa documents ambazo hata kina EL wanashangaa amezipata wapi, na nyingine alikuwa hajawakabidhi anasubiri waruhusu hoja yake.

Actually no, kaipa serikali siku 24 na nadhani so far simebaki siku 20 so lets stay tuned na hayo "MABOMU" halafu hivi huu msamiati haukukumbushi kitu au mtu fulani??

He is very well informed, na wakubwa wanajua hilo, la sivyo ndiye wangeanza naye kabla ya Zitto. Ushahidi wa hili ninao lakini sio kwa ajili ya kumwaga hapa sasa hivi. Subiri tu siku zisogee utajua ninachosema.

He might be very well informed but he is'nt well sourced.Umekiri kuwa ushahidi unao sasa unaona ubaya gani ukaumwaga hapa kisha tujadiliane? hivi katika politics za leo bado kuna mambo ya Mrema kuwa ushahidi upo lakini sisemi? If huyo ZITTO is going to present substance then I welcome the opportunity for a proper debate because so far he's all about populist gimmicks.
 
Tatizo kubwa tulilonalo TZ na Africa kwa ujumla ni kwamba the so called wasomi, wengi wenu mnabwekea nje ya geti (ughaibuni) na hamko well informed na maisha ya wananchi wa kawaida wanao hangaikia mlo wa siku. Wengi wenu humu, mi nadhani its high time, muombe likizo muendee Kigoma, Buzirayombo, Shelui, Mpanda,Misungwi au Kasulu muone watu wanavyoishi na muache kutegemea internet na media za kitapeli za bongo. Njoo uone tunavyoishi huku na sio kutumia data za google kuangalia maisha ya watu ambao hawana uhakika wa aspirini. Huwezi pata picha sahihi kwa mtaji huo.

Jamaa hapo juu ameelezea safi kabisa, leo ni mwaka 2007 sio enzi za chama kushika hatamu, tatizo la wengi humu ni kuamini kwamba watanzania but tuko guided na sera za unyonge na ujamaa ndo maana wengi hamuishi kumnukuu Nyerere. Jmani fikra zinabadilika.

Mi personally nilimpigia kura JK, ila leo ukiniambia nikapige kura, I swear JK hawezi pata kura yangu na si mimi pekee yangu ni wengi humu kijijini kwetu! Kwa hiyo jua watu tunaamka taratibu. Kauli ya Mbowe, ingawa mimi si Chadema ila nakubaliana nayo Heri mkoloni mweupe kuliko mkoloni mweusi. Mi naamini aliyeko nje, anajitafutia Riziki kama mwana Adamu yeyote yule. Ila, tufike point tujue mageuzi ni jukumu LETU SOTE, Tanzania si ya Chadema wala CCM! Kwa nini inapokuja swala la kuilaumu CCM tuko pamoja, lakini likija swala la kutafuta njia mbadala ya haya matatizo, wote tunaelekeza shutuma kwa Chadema na CUF? huu ni ufinyu wa akili. Mara Zitto hana data, Slaa hana hiki, Seif hana hili, we jiulize we umefanya nini? atleast wao mchango wao umeonekana, wewe umefanya nini zaidi ya kukosoa tuu, tena kwenye internet ambayo mamilioni ya wapiga kura hawafiki? Kwa lugha nyingine mtu kama huyu ni irrelevant kwa harakati za kuikomboa Tanzania kwenye lindi la umaskini, maana huna link na walengwa.

Watu mnatoa hoja kwamba watu wanaendekeza njaa ndo maana hawatoki CCM, lakini mnasahau kwamba wenyewe mko ughaibuni, mnaogopa kurudi home kwa sababu mazingira yalipo hayawapi nafasi ya kuendeleza maslahi binafsi! What hypocricy?

Yaani watanzania tuichukulie TZ kama kampuni ambayo wote hapa ni shareholders not by any reason but by birth! Kwa hiyo kila mtu anajukumu la kutetea maslahi ya kampuni kwa sababu ni mwanahisa wa kudumu na hawezi kunyang`anywa hisa zake na mtu yeyote, kwa sababu alipata hizo hisa kwa sababu yeye ni mwanachama wa kampuni kwa kuzaliwa. I will be the last person to criticize Zitto au yeyote anayefanya kitu (hata kama kina mapungufu). Kila mtu aiulize nafsi yake. AMEFANYA NINI????

Nasema tena, nimekuwa MPIGA KURA wa CCM mda mrefu, ila nimegundua tunachezewa shere hapa. na hasira zangu nitazipeleka kwenye sanduku la kura 2010. Inshallah.
 
Ndugu yangu,

Umesema kweli. Nakubaliana nawe, kama nilivyoandika katika thread nyingine hapa hivi:

"Mimi nadhani kazi tuliyo nayo Watanzania ni kujitambua. Tukishajitambua, tutajitetea. Bila kujali itikadi za vyama, tutashiriki kuhimiza mabadiliko ama ya ndani au ya nje kwa ajili ya mustakabali wa nchi nzima. Uzima wetu ndio lengo letu.

Tusidhani kuna watu walizaliwa kuwapigania wengine. Kila anayeguswa ashiriki kwa namna inayolingana na uwezo wake. Kwa sababu hiyo, tusitarajie kwamba mabadiliko yataletwa na vyama vya upinzani. Wala hayataletwa na CCM hii. Kwa maoni yangu, mabadiliko ni muhimu sasa; au tuseme ni lazima. Lakini tukubali kuwa yataletwa na wananchi. Ndio sisi sote.

Hapa ndipo Mwalimu JK Nyerere alisema: "inawezekana, timiza wajibu wako;" kauli ambayo Rais Mstaafu Benjamin Mkapa amekuwa akiitumia mara kwa mara. Jiulize: wewe unashirikije? Au unadhani hayakuhusu?"
 
Ni kweli simo kwenye CHADEMA na kwa sababu umekiri kuwa mimi no bserver than naweza kumonitor jinsi spin na propaganda machina zinavyofanya kazi ili kuwafikia walengwa.Sijadharau nguvu hiyo hoja yako ndio maana nikasema kuwa network ya CHADEMA iko mpaka Ikulu lakini tatizo ni kuwa wengi katika mtandao wa CHADEMA hawako tayari ku risk career zao au biashara zao na mengineyo kwa kuwapa supporting documents au kuleak mambo ambayo kama ukifanyika uchunguzi then trail itawafikia na hivyo hawako tayari kuface the consequences za hatua hiyo. CCM wanawajua lakini as long as kila mmoja katulia na anapata tenda za hapa na pale au vipromotion vya hapa na pale then why bother them? Maneno yako ni kweli this is 2007 na siyo 1970 lakini usisahau kuwa mpaka 1960 damu nyingi ilimwagika ndipo tukapata uhuru wetu. Je wale wanajeshi wetu watajisikiaje siku Mbowe anaapishwa Uwanja wa Taifa ili hali huko nyuma aliwahi kuwasifia waliotutawa? Narudia it might have not been a political suicide lakini itlikuwa ni Political gaffe ambayo aliitoa in a wrong place(Uwanja wa mashujaa). Kweli its almost 40 yrs atangu tumepata uhuru lakini huwezi kulaumi kila kitu wa serikali after all matatizo ya kuichumi ya Tanzania yanatokana na factors mbali mbali na nyingi ni external factors(thread yake itajitegemea)Hilo ni tusi kubwa, Umma wa Tanzania uliamka tangu hajaja mkoloni na baada ya mkoloni na baada ya vyama vingi hivi umesahu watu walivopinga vya vingi? lakini serikali ya wakati ule iliamua kuwa ni bora kuwa na wapinzani kuliko kutokuwa nao. Watanzania waliamka hata kabla zito hajazaliwa.Unless unazungumzia mbunge ambaye ni charismatic then nakubali kuwa Zitto ni charismatic lakini siyo makini kutokana na sababu mbali mbali lakini zaidi anauza sana magazeti. Nakuhakikishia kuwa the only time he actually got passionate and detailed in a reply was when he was defending himself for not outlining policies! na hii ya "MABOMU" ndio imekuwa dstarction kubwa zaidi

Wewe kweli ndio umepotea..... Watu wanaongelea issue kubwa za maisha ya watanzania wewe unaitazama kwenye uuzaji wa magazeti?
Ama kweli kejeli za CCM na Rostam wao zitapita kipimo (normal) cha uvumilivu

sasa naomba unifafanulie au nionyeshe kiongozi gani amejitajirika kwa wizi? je kuna ushahidi wowote wa kuback up hilo? Je kuna sehemu gani iliyoandikwa kwenye katika kuwa mwasiasa hatakiwi kuwa Tajiri? Freeman Mbowe anapesa nyingi tuuu je huyu naye ni Mkoloni mweusi? tumchukie Mbowe kwa sababu ni mfanyabiashara aliyefanikiwa?nadhani ni political bankrupt tukianza kuwachukia mawaziri au wanasiasa kwa sababu walifanikiwa kuwa na wepesi wa rizki. naomba unifafanulie unamaana gani dhana ya ki -CCM?Na hilo ndilo tatizo la CHADEMA kwani talent pekee haitoshi.It takes more than talent to be a politician!

It's true it takes more than watu kama wewe wasiojua wanachosema I am glad wewe sio CHADEMA bali ni CCM maana watu kama wewe ni wengi sana huko CCM

No kilichomfukuza Zitto bungeni ni ubahili wa chama chake kushindwa kuwalipa researchers 2 ambao walitakiwa wadig deep on those issues za mikataba kabla hajaenda public. hii inaonyesha jinsi gani anavyoendekeza punch punch & judy politics ambazo hazina substance zozote kwani angekuwa makini na documents au source materials zake angeendelea kuwepo bungeni. Sikatai anaweza akawa ni potential politician but what Zitto is lacking is substance to back up his rhetoric.

Hakuna mfanya research yoyote ameruhusiwa kuona kilichoandikwa kwenye mikataba ya madini ya Tanzania. Mimi nimejaribu hata kumtumia mmoja wa watafiti maarufu hapa kiwanja ili kupretend kwamba tunafanya research ya madini Tanzania na serikali ya bongo walikataa kwamba sheria za biashara za kimataifa zinawazuia kuweka huo mkataba kwa public... hata wabunge wengi hawaruhusiwi kuiona hiyo mikataba... Hao researchers unaodai wangepata wapi data? sasa nimetambua kuwa unaongea kama RA

mheshimiwa, ukitaka kujua kuna matatizo katika opposition Tanzania basi mtazame MAALIM SEIF SHARIF HAMAD. I like and respect MAALIM, but in the eyes of the electorate, when it comes to winning elections - once a loser, always a loser, and making opposition leader would has been a disaster, a cracking addition to the shadow cabinet he'll make, but in terms of both party and opposition leadership, he is the past hivyo tumwache kwa sasa. Suala la kuwa hoja imewasha moto nchi znima nadhani ni over statement. Sijaona evidence yoyote kuonyesha kuwa nchi nzima imewaka moto kwa sababu ya hoja ya Zitto Kabwe japo ni kweli watu wako curious kutaka kujua kuhusu mikataba lakini kosa zaidi ni kwa serkali kutoweka wazi na kwa lugha ambayo wananchi wanaelewa kuhusu mikataba ya madini. Usisahau kuwa both CHADEMA na CUF need to develop policies and must be prepared to attack the government's agenda and place it in constrast to their own. Na hiyo itakuwa the real test for Mr Freeman na Hamad. Na kama ningekuwa ni CCM then i only wish their were more like CHADEMA and CUF because you would keep us in office! Actually Spika alimuuliza source ya ile email na Dr Slaa akataja email address ya ilikotoka na ile video ya ule mjadala ilikuwepo humu na mwenyewe akakiri kuwa kwa sasa source siyo muhimu sana lakini kilichomuhimu ni contents za ile source sasa mheshimiwa unataka watu wajadili mambo tuu bila kuwekana sawa kuhusu sources? Once again sipo hapa kwa ajili ya kupinga kila kitu lakini so far hakuna hoja au official majibu (kwenye websites zao) toka kwa CHADEMA au CUF au WAPINZANI za kumcounter GAVANA wa benki kuu.Sasa kama siyo kuplay politics ni nini huko?Ubadhiribu ulikuwa unafanyiwa na bado unafanyiwa uchunguzi na PCB au TAKURU uchunguzi bado unaendelea lakini naona wengine hilo hawalitaki wanataka na whats Dr Slaa has done is is essentially a PR exercise based on positioning and I think it shows a lack of conviction ambayo niitegemea toka kwa mwanasiasa mkongwe kama yeye.Actually no, kaipa serikali siku 24 na nadhani so far simebaki siku 20 so lets stay tuned na hayo "MABOMU" halafu hivi huu msamiati haukukumbushi kitu au mtu fulani??He might be very well informed but he is'nt well sourced.Umekiri kuwa ushahidi unao sasa unaona ubaya gani ukaumwaga hapa kisha tujadiliane? hivi katika politics za leo bado kuna mambo ya Mrema kuwa ushahidi upo lakini sisemi? If huyo ZITTO is going to present substance then I welcome the opportunity for a proper debate because so far he's all about populist gimmicks.

Wewe ndio unahitaji kufanya utafiti maana naona unatumia sana mtizamo wako wa kisiasa na chuki yako dhidi ya CHADEMA kuchambua mambo muhimu yanayohusu taifa letu. Tanzania njema ameanzisha mjadala kuhusu mkoloni wa kiirani anavyomiliki media na sasa anakuwa na influence kwenye serikali na wewe unaigeuza the whole issue kuwa anti-CHADEMA. Umelipwa kiasi gani na Rostam Aziz?
 
kichwamaji,masanja,ngurumo,
hivi kama wananchi wamebanwa kweli kimaisha na wanasikia maumivu mbona bado CCM inashinda ktk hizi chaguzi ndogo?

kwa mtizamo wangu watanzania bado hawajapigika kimaisha kiasi cha kuwafanya wafikirie kubadilisha watawala/chama.
 
Hao watanzania unaowasema ni akina nani? I thought its one man/woman one vote. Kwa hiyo unafikiria wanaoipigia kura CCM ni wakulima tuu? wenye njaa? Hapana ni wote wasomi kwa wakulima! Swala la wao kuamka, ni mpaka sisi tunaoandika humu twende kuwambia kwamba wana watu na sera mbadala wa kuwapigia kura ambao ni mimi na wewe wenye hii nafasi maana wao hawana hii nafasi

Hope umenipata. Sasa wewe kama alivyosema muungwana Ngurumo unadhani kuna aliyezaliwa kumpigania mwingine! Hakuna na haitatokea. Hatuwatendei haki wakulima wa nchi yetu pale tunapowalaumu kwamba ndo wanaipigia kura CCM tuu, as if the so called elites wanapigia upinzani. Kwani kama ni kuipigia CCM kura kwanza wakulima inabidi watucheke sisi maana sisi ndo wanafiki tunaofanya mambo ambayo tunajua madhara yake, wao atleast wanaweza singizia kwamba hawajui kusoma kiingereza kwa hiyo hiyo mikataba mibovu, BOT, IPTL hawavijui!!!!! Na sisi je? tutasingizia nini? Shame on us.
 
Wewe kweli ndio umepotea..... Watu wanaongelea issue kubwa za maisha ya watanzania wewe unaitazama kwenye uuzaji wa magazeti?
Naomba urejee nilishokiandika hapo juu...nimesema kuwa zaidi ya yote hayo pamoja na Zitto kuwa Charismatic pia ni media darling na hivyo magazeti mengi yanauzika kwa kuwa na heading za Zitto kama vile ilivyokuwa Mrema in the 90's. Na ni kweli media wamekuwa na field day tangu hii issue imetokea na wanauza sana magazeti kwa hilo sasa hilo nalo unabisha?

Ama kweli kejeli za CCM na Rostam wao zitapita kipimo (normal) cha uvumilivu
Naomba unipe mfano ni kejeli zipi unazozizungumzia?

It's true it takes more than watu kama wewe wasiojua wanachosema
Fair enough, you are entitled to have that view lakini sidhani kama personal attacks ni way forward au unasemaje?

I am glad wewe sio CHADEMA bali ni CCM maana watu kama wewe ni wengi sana huko CCM
Naomba unionyeshe wapi nimesema mimi ni CCM?

Hakuna mfanya research yoyote ameruhusiwa kuona kilichoandikwa kwenye mikataba ya madini ya Tanzania.Mimi nimejaribu hata kumtumia mmoja wa watafiti maarufu hapa kiwanja ili
kupretend kwamba tunafanya research ya madini Tanzania na serikali ya bongo walikataa kwamba sheria za biashara za kimataifa zinawazuia kuweka huo mkataba kwa public...

Kwanza hapo kuna mambo mawili la kwanza ni hilo la kusema kuwa hakuna resercher anayeruhusiwa kuuona mkataba wa madini. Naweza kusema si kweli kwani kuna baadhi ya documents ambazo zipo kwenye public domain, na pili umekiri kuwa ulikuwa unapretend kuwa mnafanya reserch huoni kama hiyo nayo itakuwa imekuharibia kabisa kwani umeonesha dishonesty na nia yako. Suala la pili ni kweli katika contract ya namna hiyo kuwa kunakuwa na vipengele ambavyo serikali na hiyo kampuni kutokana na usiri wa kibiashara walikuwa wamesign kuwa baadhi ya section zisiwe katika public domain .....umeendelea kwa kusema....

hata wabunge wengi hawaruhusiwi kuiona hiyo mikataba... Hao researchers unaodai wangepata wapi data? sasa nimetambua kuwa unaongea kama RA
Sijui hili la kusema kuwa wabunge wengi hawaruhusiwi kuona hiyo mikataba umeitoa wapi..je unaweza kutuonyesha ni kipengele kipi katisha sheria za bunge kinachosema kuwa wabunge wengi hawaruhusiwi kuuona hiyo mikataba? na unaposema kuwa "wabunge wengi" unamaana kuwa kuna wabunge wengine wanaruhusiwa na wengine hawaruhusiwi? hii umeipata wapi? .Hiyo ya kusema naongea kama R.A sitokujibu kwani ni irrelevant na sitoingia katika personal attcks na wewe bali nitajadiliana na wewe kihoja

Wewe ndio unahitaji kufanya utafiti maana naona unatumia sana mtizamo wako wa kisiasa na chuki yako dhidi ya CHADEMA kuchambua mambo muhimu yanayohusu taifa letu.
Unaweza kunionyesha ni wapi nimesema nawachukia CHADEMA? Hivi kuuliza kwa nini chama cha CHADEMA hawajatoa kuhusu FOREIGN POLICY yetu kuhusu Muungano wa Africa au kupeleka majeshi yetu Lebanon ni kukichukia CHADEMA?

Tanzania njema ameanzisha mjadala kuhusu mkoloni wa kiirani anavyomiliki media na sasa anakuwa na influence kwenye serikali na wewe unaigeuza the whole issue kuwa anti-CHADEMA. Umelipwa kiasi gani na Rostam Aziz?
Sijakuelewa unaposema Rostam ni mkoloni wa kiIran,je umetumia sources zipi ukafikia conclusion kuwa Rostam ni mkoloni wa Kiiran? Afterall hizi ni serious allegations na nadhani ingekuwa vizuri ukaclarufy hayo maneno yako hapo juu. Halafu kama ni influence katika serikali yetu mbona hujasema kitu jinsi serikali ya UK kupitia DFID walivyo na Influence katika serikali yetu na hivi leo kuna Kesi London ambayo imefunguliwa dhidi ya WAINGEREZA na inawaimplicate waingereza moja kwa moja...hilo mbona hatulisemi? Hivi Rostam kuwa na rangi ile imekuwa Nongwa? Je mwalimu alivyokuwa na P.A mzungu naye tusemeje alikuwa msaliti? hebu fafanua hoja yako
 
Sijui hili la kusema kuwa wabunge wengi hawaruhusiwi kuona hiyo mikataba umeitoa wapi..je unaweza kutuonyesha ni kipengele kipi katisha sheria za bunge kinachosema kuwa wabunge wengi hawaruhusiwi kuuona hiyo mikataba? na unaposema kuwa "wabunge wengi" unamaana kuwa kuna wabunge wengine wanaruhusiwa na wengine hawaruhusiwi? hii umeipata wapi?

Game hii ni kweli kwani wabunge mawaziri ndio huiona tu!, na kuwambia wengine kwamba ni siri ya serikali utadhani serikali ni malalika wengine toka mbinguni kumbe ni wabunge wale wale kwa kofia ya uwaziri!
 
Game Theory

The spinning is too much. I think you know I know and you know I know.
 
Sijakataa kuna documents nyingi tuu ambazo access wanazo ni mawaziri na wabunge tuuu. Mfano serikali kamaserikali nyingine yoyote ile haiwezi kuwa in public kuwa inatumia mbinu gani za kijeshi kujihami na maadui wa nje na ndani ya nchi.Sasa ndio maana nikamwomba huyo Mwafrica wa kike aje na Kipengele cha sheria kuback up ni wapi kumeandikwa kuwa baadhi ya wabunge wanaona hiyo mikataba na wengine hawaoni
 
Sijui hili la kusema kuwa wabunge wengi hawaruhusiwi kuona hiyo mikataba umeitoa wapi..je unaweza kutuonyesha ni kipengele kipi katisha sheria za bunge kinachosema kuwa wabunge wengi hawaruhusiwi kuuona hiyo mikataba? na unaposema kuwa "wabunge wengi" unamaana kuwa kuna wabunge wengine wanaruhusiwa na wengine hawaruhusiwi? hii umeipata wapi?

Game hii ni kweli kwani wabunge mawaziri ndio huiona tu!, na kuwambia wengine kwamba ni siri ya serikali utadhani serikali ni malalika wengine toka mbinguni kumbe ni wabunge wale wale kwa kofia ya uwaziri!

Mimi siku zote naamini katika kila jamii kunakua na kundi fulani la watu wanaorun the show hata hapa tanzania wako kundi fulani la watu wanao run the show na hawa sio CCM sio Serikali kutakuwa na kundi fulani la watu ambao serikali na CCM wanawasikiliza hawa wanachotaka na kadhalika

SIAJABU HAO UNAOHISI WANAJUA MIKATABA NA WENYEWE HAWAJUI WANAOJUA NI WATU WALIO KATIKA HICHI KIKUNDI CHA SIRI
 
..clashing of ideas!

..clashing of sides!

..clashing of interests!

..clashing of motives!

..clashing of cover ups!

..clashing of people!

..while Tanzania is being lost!
 
Naomba urejee nilishokiandika hapo juu...nimesema kuwa zaidi ya yote hayo pamoja na Zitto kuwa Charismatic pia ni media darling na hivyo magazeti mengi yanauzika kwa kuwa na heading za Zitto kama vile ilivyokuwa Mrema in the 90's. Na ni kweli media wamekuwa na field day tangu hii issue imetokea na wanauza sana magazeti kwa hilo sasa hilo nalo unabisha?

Tatizo la nchi na mikataba isiyo wazi huwezi kuliangalia katika mtizamo wa kuuza magazeti.... Akili yako na elimu yako vinatosha kukufanya uchunguze na ueleze vitu kwenye picha kubwa sio swala la kuuza magazet..... Britney Spears naye anauza sana magazeti hapa kiwanja kama ilivyo kwa Hilary Clinton, je kuna connection yoyote kati ya hawa wamama wawili?

Naomba unipe mfano ni kejeli zipi unazozizungumzia?

Una maana gani unaposema kuwa Zito anafanya populist gimick?
unaweza kuita hiyo statement kejeli au hoja?

Fair enough, you are entitled to have that view lakini sidhani kama personal attacks ni way forward au unasemaje?

Usianze kulia sasa kama mtoto mdogo!

Naomba unionyeshe wapi nimesema mimi ni CCM?

Prove otherwise kama wewe sio CCM

Kwanza hapo kuna mambo mawili la kwanza ni hilo la kusema kuwa hakuna resercher anayeruhusiwa kuuona mkataba wa madini. Naweza kusema si kweli kwani kuna baadhi ya documents ambazo zipo kwenye public domain, na pili umekiri kuwa ulikuwa unapretend kuwa mnafanya reserch huoni kama hiyo nayo itakuwa imekuharibia kabisa kwani umeonesha dishonesty na nia yako. Suala la pili ni kweli katika contract ya namna hiyo kuwa kunakuwa na vipengele ambavyo serikali na hiyo kampuni kutokana na usiri wa kibiashara walikuwa wamesign kuwa baadhi ya section zisiwe katika public domain .....umeendelea kwa kusema....Sijui hili la kusema kuwa wabunge wengi hawaruhusiwi kuona hiyo mikataba umeitoa wapi..je unaweza kutuonyesha ni kipengele kipi katisha sheria za bunge kinachosema kuwa wabunge wengi hawaruhusiwi kuuona hiyo mikataba? na unaposema kuwa "wabunge wengi" unamaana kuwa kuna wabunge wengine wanaruhusiwa na wengine hawaruhusiwi? hii umeipata wapi? .Hiyo ya kusema naongea kama R.A sitokujibu kwani ni irrelevant na sitoingia katika personal attcks na wewe bali nitajadiliana na wewe kihoja

Mbona unajimix... At one point unashauri watu kusoma recommended books za media na wewe mwenyewe hujui moja ya mbinu kubwa watu wa kwenye media wanatumia kupata info...

Kila siku media zinaumbua wauza madawa, tutes, wabakaji, wala rushwa nk kwa kupretend kuwa one of them ni mmoja wa wahusika na kisha watu wanaumbuliwa.

Nilipretend kuwa nafanya research lakini nilimtumia researcher maarufu sana hapa kiwanja. Jibu la serikali lilikuwa ni kwamba hiyo mikataba ya madini haiwezi kuwekwa public na wakasisitiza kuwa hata baadhi ya wabunge hawaruhusiwi kuiona.

Wewe endelea tu kutumia talking points za RA bila kufanya research yako mwenyewe....

Unaweza kunionyesha ni wapi nimesema nawachukia CHADEMA? Hivi kuuliza kwa nini chama cha CHADEMA hawajatoa kuhusu FOREIGN POLICY yetu kuhusu Muungano wa Africa au kupeleka majeshi yetu Lebanon ni kukichukia CHADEMA?

Unataka kulia sasa? CHADEMA wakisema kitu unadai kuwa hawako informed well.... na on the other side unataka watoe statement kwa kila kinachoendelea nchini... unachotaka hapa ni nini?

Sijakuelewa unaposema Rostam ni mkoloni wa kiIran,je umetumia sources zipi ukafikia conclusion kuwa Rostam ni mkoloni wa Kiiran? Afterall hizi ni serious allegations na nadhani ingekuwa vizuri ukaclarufy hayo maneno yako hapo juu.

Of course Rostam ni mkoloni na mwizi wa mali za nchi yetu... siku ukitoka kwenye payroll yake utarealize hili.

Halafu kama ni influence katika serikali yetu mbona hujasema kitu jinsi serikali ya UK kupitia DFID walivyo na Influence katika serikali yetu na hivi leo kuna Kesi London ambayo imefunguliwa dhidi ya WAINGEREZA na inawaimplicate waingereza moja kwa moja...hilo mbona hatulisemi? Hivi Rostam kuwa na rangi ile imekuwa Nongwa? Je mwalimu alivyokuwa na P.A mzungu naye tusemeje alikuwa msaliti? hebu fafanua hoja yako

Nani alikufundisha kuwa jambo baya linakuwa justified kwa tendo lingine baya? ......
 
Game Theory

The spinning is too much. I think you know I know and you know I know.

Hakuna serikali isiyo spin na ndio maana nikasema kuwa CHADEMA wakitaka wanaweza kuwa na department ya kucounter spin as long as haitoongozwa na JJ MNYIKA (ushauri wangu wa bure.

sasa haiwezekani ikawa wao ni watu wa kulalama tuu kuwa kuna spinning wakati wanayo nafasi ya kuwa na PR Dept ya ku counter mashambulizi ya CCM. Na hiyo yet inahitaji pesa, lakini la muhimu zaidi ni kuwa wanahitaji kujipanga vizuri na kuachana na politics za headline grabbing kwani hiyo haitowasaidia kushinda Uchaguzi
 
MWAFRIKA WA KIKE swahiba mwenye akili, nakuuliza suala njaa imekukabili, nusu ya mwezi hujala likaja kombe la wali, ukawekewa mahala hula ndipo ukanawa, au hunawa kisha ukala
 
Hakuna serikali isiyo spin na ndio maana nikasema kuwa CHADEMA wakitaka wanaweza kuwa na department ya kucounter spin as long as haitoongozwa na JJ MNYIKA (ushauri wangu wa bure.

sasa haiwezekani ikawa wao ni watu wa kulalama tuu kuwa kuna spinning wakati wanayo nafasi ya kuwa na PR Dept ya ku counter mashambulizi ya CCM. Na hiyo yet inahitaji pesa, lakini la muhimu zaidi ni kuwa wanahitaji kujipanga vizuri na kuachana na politics za headline grabbing kwani hiyo haitowasaidia kushinda Uchaguzi

BWANA GAME

HABARI ZA JIONI

NAKUNGA MKONO ASILIMIA 100 ZA ZAIDI KUHUSU MNYIKA KUTOKUPEWA NAFASI HUYU KIJANA NI DHAIFU MIMI NIMEMWONA MARA NYINGI HAPA UBUNGO MIMI NI MKAZI WA KIMARA KWAHIYO UBUNGO NI KWANGU PIA NIMEKUA NAMUULIZA MASWALI MARA NYINGI HAPA JAMBO HAJIBU , NIKAMPIGIA SIMU HAJIBU MPAKA SIKU NILIMWALIKA KATIKA DEBATE PALE UDSM AJE TUMUULIZE MASWALI MACHACHE YOTE HAYA HAJAJA KWAHIYO HUYU NDIO KIONGOZI GANI NA ALIKUA ANATAKA UBUNGO YETU ?

BORA KEENJA TUNAYEMJUA ANALALA BUNGENI NA HANA MPANGO WOWOTE NA UBUNGO
 
Hakuna serikali isiyo spin na ndio maana nikasema kuwa CHADEMA wakitaka wanaweza kuwa na department ya kucounter spin as long as haitoongozwa na JJ MNYIKA (ushauri wangu wa bure.

sasa haiwezekani ikawa wao ni watu wa kulalama tuu kuwa kuna spinning wakati wanayo nafasi ya kuwa na PR Dept ya ku counter mashambulizi ya CCM. Na hiyo yet inahitaji pesa, lakini la muhimu zaidi ni kuwa wanahitaji kujipanga vizuri na kuachana na politics za headline grabbing kwani hiyo haitowasaidia kushinda Uchaguzi

CHADEMA watahitaji watanzania wengi zaidi ya Mnyika ila wewe sio one of them maana katika moja ya postings zako huko nyuma kabla hujabadili jina hapa JF ulieleza kuwa unamission ya kummaliza mzee mwanakijiji. For now bora Mnyika kuliko wewe maaana angalau mnyika ataongea mambo ya nchi na sio kumaliza watanzania wenzake personally.
 
Tatizo la nchi na mikataba isiyo wazi huwezi kuliangalia katika mtizamo wa kuuza magazeti.... Akili yako na elimu yako vinatosha kukufanya uchunguze na ueleze vitu kwenye picha kubwa sio swala la kuuza magazet..... Britney Spears naye anauza sana magazeti hapa kiwanja kama ilivyo kwa Hilary Clinton, je kuna connection yoyote kati ya hawa wamama wawili?

Una maana gani unaposema kuwa Zito anafanya populist gimick?
unaweza kuita hiyo statement kejeli au hoja?

Usianze kulia sasa kama mtoto mdogo!

Prove otherwise kama wewe sio CCM

Mbona unajimix... At one point unashauri watu kusoma recommended books za media na wewe mwenyewe hujui moja ya mbinu kubwa watu wa kwenye media wanatumia kupata info...

Kila siku media zinaumbua wauza madawa, tutes, wabakaji, wala rushwa nk kwa kupretend kuwa one of them ni mmoja wa wahusika na kisha watu wanaumbuliwa.

Nilipretend kuwa nafanya research lakini nilimtumia researcher maarufu sana hapa kiwanja. Jibu la serikali lilikuwa ni kwamba hiyo mikataba ya madini haiwezi kuwekwa public na wakasisitiza kuwa hata baadhi ya wabunge hawaruhusiwi kuiona.

Wewe endelea tu kutumia talking points za RA bila kufanya research yako mwenyewe....

Unataka kulia sasa? CHADEMA wakisema kitu unadai kuwa hawako informed well.... na on the other side unataka watoe statement kwa kila kinachoendelea nchini... unachotaka hapa ni nini?

Of course Rostam ni mkoloni na mwizi wa mali za nchi yetu... siku ukitoka kwenye payroll yake utarealize hili.

Nani alikufundisha kuwa jambo baya linakuwa justified kwa tendo lingine baya? ......

MWAFRIKA WA KIKE

KUNA NJIA MBADALA YA KUPIGANA NA HAWA WALA NCHI YETU NAYENYEWE NI KWA NJIA YA MTANDAO , NIMEONA KATIKA MAJUKWAA YA FORUMS KAMA HIZI WENGINE WANACHANGANYA MADA KWA MAKUSUDI AU WENGINE NI MASHABIKI WA CHAMA KWAHIYO HAWAPENDI KUONA JAMAA ZAO WANAKOSOLEWA UKIKOSOA TU AU UKISEMA KITU SENSITIVE BASI ATATAFUTA NJIA YA KUJUANA NA WEWE , UKO WAPI JINA LAKO HALAFU ANAPELEKA KWA MHUSIKA HIYO NI MBAYA

SASA NJIA NZURI NI KUANZISHA BLOGU KWA MAJINA TOFAUTI AU KUFUNGUA FEED ZA EMAILS KWA MAJINA TOFAUTI KULE UNAWEKA EMAIL ZA WATANZANIA KIBAO UNAWATUMIA HABARI ZAKO NA BILA KUKUJUA WEWE NI NANI

KWA SASA NINA CONTACT ZA WATANZANIA KARIBU 3000 WALIO SEHEMU MBALI MBALI KWAHIYO NIKITUMA EMAIL YOYOTE NAKUA KAMA NIMEIAMBIA WILAYA MOJA YA TANZANIA KWAHIYO HUYU RASTAM NJIA YA KUMMLIZA NDIO HIYO KUTENGENEZA EMAILS NA KAMPENI KABAMBE

AHSANTE
 
Back
Top Bottom