Rostam Aziz Kung'atuka!

TrueVoter

JF-Expert Member
Feb 13, 2008
2,141
1,704
Habari za kuaminika kutoka Igunga zinasema, katika hali ya kutatanisha mbunge wa Igunga bw. rostam aziz ambaye anafanya ziara jimboni kwake, amesikika akisema muda si mrefu atang'atuka kwenye siasa.

Akifanya mikutano ya hadhara katika sehemu mbali mbali za Igunga, amerudia ujumbe wa kung'atuka mara kwa mara. wengi wamejiuliza kwa nini anaongelea kung'atuka badala ya kuhimiza maendeleo!

Hata hivyo, katika sehemu nyingi, amepata mapokezi hafifu tofauti na zamani kabla ya tuhuma za ufisadi kumwandama! hali ilikuwa mbaya zaidi katika vijiji vya Ziba, Simbo na Nkinga ambapo wananchi walidiriki hata kumzomea mbali ya kubeba mabango yanayoeleza tuhuma zake!
 
Ebo! Angatuke? Fedha yetu aliyoiba amerudisha? Lazima anyeee debe na asituletee ujinga hapa!!
 
siasa ya bongo inavutia kweli kweli
Iba kisha jiuzulu ili kutoa nafasi kwa wengine waibe kisha watajiuzulu tehen generation inaendelea....
 
aking'atuka tu na sisi tunamtia majino kumng'ata ili alipe tokana na Ufisadi wa Hali ya juu.

hivi Bunge halijafikiria sheria ya kuponda mawe Mafisadi? mi ndio kilio changu maana hata kama watarudisha pesa, bado balaa litakuwa pale pale, tumeshaathirika na hilo haliwezi rudishwa nyuma.

CCM wanaoneana aibu, Mafisadi wanajiona wako juu ya Sheria na Mamlaka ya Utawala wa Tanzania yapo juu yao.

Ninekuwa najiuliza hili Swali kila siku, je tuna Rais ama Kibaraka wa Mafisadi?

JK aonyeshe Utanzania wake...Uzalendo wake si kwa Mafisadiali Wapiga Kura Wake!
 
Yale yale .Jamani huyu mtu ni hatari .Je kafanya nini Jimboni kwake ? Mukono kaiba kajenga mashule na barabara yeye je ?
 
Habari za kuaminika kutoka Igunga zinasema, katika hali ya kutatanisha mbunge wa Igunga bw. rostam aziz ambaye anafanya ziara jimboni kwake, amesikika akisema muda si mrefu atang'atuka kwenye siasa.

Akifanya mikutano ya hadhara katika sehemu mbali mbali za Igunga, amerudia ujumbe wa kung'atuka mara kwa mara. wengi wamejiuliza kwa nini anaongelea kung'atuka badala ya kuhimiza maendeleo!

Hata hivyo, katika sehemu nyingi, amepata mapokezi hafifu tofauti na zamani kabla ya tuhuma za ufisadi kumwandama! hali ilikuwa mbaya zaidi katika vijiji vya Ziba, Simbo na Nkinga ambapo wananchi walidiriki hata kumzomea mbali ya kubeba mabango yanayoeleza tuhuma zake!


Arudishe pesa zetu kwanza kabla ya kung'atuka. Sasa mafisadi wanaanza kuikimbia siasa maana kila fisadi alikuwa anataka kuingia kwenye siasa kwa kuwa huko ufisadi nje nje na kulikuwa hakuna hata wa kukunyanyulia kidole.
 
Hili nalimudu kama anang`atuka kweli na ameyazungumza katika jimbo lake nitawapa taarifa
 
kila fisadi anajiuzuru inabidi kuwe na sheria kila fisadi kabla ya kujiuzuru afilisiwe na adhabu ya kifungo segerea miaka 3 tu inatosha sana kuwanyoosha hawa viumbe wasio na huruma na na waTZ na nchi kwa ujumla,
 
Mwalimu ndio aling'atuka mwaka 1986 kama sikosei...Huyu Rostam ni wa kukamatwa mara moja.
Nitashangazwa sana kama hakuna mipango ya siri ya kuwaandalia jela nzuri nzuri kama ilivyokuwa kwa PABLO ESCOBAR huko Colombia kutokana na nguvu za kisiasa walizonazo ambazo kama wabunge wengine hawatafumbua macho...Basi hata wao wanaweza kuzipoteza kazi zao ama nchi kuingia kwenye mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.
 
wadungu inawezekana vipi kiongozi wa kisiasa wa kuwaongoza watanzania(waliteswa na mkono wa utumwa kwa miaka kenda na hatimae kuwa huru)akawa mtu mwene asili ya kiarabu,kihindi,kizungu?haikai akilini.
 
huyo alizaliwa na kukulia Igunga kitongoji cha Teheran, si muarabu wala mzungu, ruksa kuwa kiongozi wa taifa
 
wadungu Inawezekana Vipi Kiongozi Wa Kisiasa Wa Kuwaongoza Watanzania(waliteswa Na Mkono Wa Utumwa Kwa Miaka Kenda Na Hatimae Kuwa Huru)akawa Mtu Mwene Asili Ya Kiarabu,kihindi,kizungu?haikai Akilini.

Wasipowakamata Mafisadi...huko Ndio Tunakokwenda...mark Ma Words!
Utumwa Umesharudi!
Nani Ni Mtumwa Na Nani Ni Bwana Pia Iko Wazi Sasa!
Narudia Tena....kama Mafisadi Hawakamatwi Then Hii Nchi Ipigwe Panga!
 
huyo alizaliwa na kukulia Igunga kitongoji cha Teheran, si muarabu wala mzungu, ruksa kuwa kiongozi wa taifa

Wananchi wameshaanza kugawanyika na AMANI HII ITAPOTEA NDUGU ZANGU!
BUNGE LIWARUDISHE MAFIOSO MIKONONI MWA WANANCHI KWASABABU NDIO MIKONONI MWA MUNGU NA HAKI!
 
Mie nafikiri angejiuzulu badala ya kung'atuka. Naona kama anachelewa kujiuzulu. Asitake kubadilisha lugha hapa, kama wananchi wa jimbo lake wamemzomea basi hana nafasi tena hata kama angeamua kugombea tena. Ni vizuri ajiuzulu kabla hajatinga mahakamani. Ni soni kiongozi wa jamii kama mbunge kutinga mahakamani akiwa anashikilia hicho cheo. Pamoja na msemo wake huo watu bado tutam-deal tu mapaka arudishe pesa yetu.

Wananchi wa Bariadi nao wanahitaji kuiga mfano wa wananchi/wakazi wa Igunga. Tuendelee kuwazomea hawa mafisadi mpaka waachie ngazi huku tukiendelea kuwabana warudishe pesa yetu.
 
Asing'atuke!

Nina habari nzuri za kumfanya awe mtu mzuri. Nitumieni namba yake ya simu kwa PM, ili nimpigie.

./Mwana wa Haki
 
Awapishe wenzake naoo watoe mchango wao kwenye jimbo lake maana ilikuwa kama ni mali yake huwa anakosa upinzani kabisa...time will tell.
 
mtu kama Rostam ni mzuri wa kutafuta reactions za watu.
anasema anataka kung'atuka ili aone jamii itasemaje?
sidhani kama anataka kung'atuka tu bila sababu ya msingi, na hata kama atang'atuka basi jua ameshajua nchi haiwezi kumshtaki na anaweza kuwa hayupo kamwe tanzania wakati huo.
kung'atuka kunaweza kuwa his passport to freedom
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom