Rostam Aziz kugeukia Waislamu, Kuibua wengine CHADEMA

jmushi1,
Kwa Hiyo Haya Yote Unayoiyasema Ni Kwa Sababu Wewe Mchagga Au?..
Maanake Nashindwa Kuelewa Kitu Kimoja Hapa.
Unaonyesha Utetezi Wako Kama Vile Ni Wa Kikabila Kukutea Dhana Chafu Zinazowaumbua Wachagga Lakini Inapofikia Kueleza Unatumia Utanzania Kama Vile Wachagga Tu Ndio Watanzania...kwa Maana Hiyo Nimeshindwa Kuelewa Huyo Mgagagigikoko Unayemzungumzia Ni Kabila Gani Ama Raia Gani?..
Mkuu Hili La Lugha Wala Sii Hoja Kabisa..
Wasomali Wote Wanaongea Lugha Moja Na Bado Wa Ukabila. Hao Wahutu Na Watusi Waongea Lugha Moja Na Bado Sii Kabila Moja..mimi Nadhani Ni Bora Sana Kuaacha Kubishana Na Huyu Jamaa Kuhusiana Na Hili Neno Kabila Maanake Mnatupoteza Wengi...

Nachokiona Mimi Toka Kwa Mgagagigikoko Kuhusiana Na Chadema, Ni Hali Ya Kawaida Kabisa Kwa Waafirka! Ndivyo Tulivyo - Hainipotezei Usingizi Wala Pumzi.

Chadema Ni Chama Cha Wachagga!..ni Lugha Ya Kawaida Kabisa Kwa Mtu Yeyote Aisetaka Majukumu. Haya Ndio Maneno Ya Majaluo Wakati Mau Mau Wanapigania Uhuru, Waliitwa Wao Ni Chama Cha Wakikuyu Kumbe Mjaluo Alikuiwa Mwoga Kuingia Vitani, Lakini Baada Ya Uhuru Kupatikana Kila Mmoja Anaweka Madai Kuwa Kenya Ni Yake!..
Ndiyo Anasema Kwa Vile Ni Mchagga Na Kaamua Kutumia Mushi Kutukuza Umangimweza Wake.
 
huyo Ni Obama Na Bibi Yake Huko Kenya!
Mimi Niko Hapa Kwenye Kampeni Yake Ya Obama For America Na Ninajifunza Mengi Na Ndio Maana Wewe Ni Ngedere Mdogo Sana Tu Inapokuja Kwenye Hoja..kwani Hata Mc Cain Kamasi Anatolewa.

Jifunze Na Demokrasia Ya Kuwa Na Diversity Ndani Ya Chama, Mjue Kufanya Siasa Za Engagement Na Si Isolation,discramination Na Kufukuza Watu Wa Makabila Mengi,
Naona Hujajifunza Kitu Toka Democratic Usingekuwa Mkabila Kiasi Hiki, Obama Amecahaguliwa Kwa Merit Licha Ya Rangi Yake Na Kabila Lake Au Jina Lake,
 
Siamini Mahita ni jambazi na kama Jambazi alijifunza au alifunzwa alipokuwa KILIMANJARO au LAGOS YA TANZANIA.

Mgagagigikoko,
'Amini usiamini Mahita ni jambazi. Magari yote yaliyokuwa yanaibiwa kulikuwa na mkono wake pale. Ashukuru tu kuwa Mwungwana na CCM waliamua kumfumbia macho.
 
Huu Ndio Ukabila Kwanini Hadi Ujue Kabila Yake? Haikutoshi Kuwa Mwanachadema Mwenzako? Inabidi Muwe Na Watu Wa Kutafsiri Mikutano Yenu Ili Muwa Acomodate Watu Kama Mkandara,kitila Na Mwanakijiji.

Ni lazima nijuwe kabila lake kwasababu yeye tayari anajuwa kabila langu.
Mjadala uwe fair!
 
mgagagigikoko,
'amini Usiamini Mahita Ni Jambazi. Magari Yote Yaliyokuwa Yanaibiwa Kulikuwa Na Mkono Wake Pale. Ashukuru Tu Kuwa Mwungwana Na Ccm Waliamua Kumfumbia Macho.

Alifunzwa Alipokuwa Lagos(kilimanjaro) Ya Tanzania? Maana Ukiishi Mji Wa Majambazi Na Wewe Unaweza Kuwa Jambazi.
 
Hao si ni ndugu za mke wake? What did you expect of a fisadi?

Huyu Mkapa alitumwa sikufichi!
Mpango mzima wa kuwasambaratisha wachagga ulikuwepo na kulisambaratisha Taifa kwani hata wachagga wenyewe ni wasafiri na wako everywhere kama wachina wenyewe..
Na wamemiksi na makabila mengi tu!
Kama mimi ni mchagga lakini asili ya baba original Mmasai na mama mchgga original mmeru!
Na hakuna MKOA WA TANZANIA USIOUKUWA NA MCHAGGA.
 
Mama nimeichukua hii toka web site ya Bunge

1391.jpg


First Name: Chacha
Middle Name: Zakayo
Last Name: Wangwe
Constituent: Tarime
Date of Birth: July 15, 1956

--------------------------------------------------------------------------------
EDUCATION
School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
University of Dar es Salaam Certificate (Edu.) 1978 1979 CERTIFICATE



Kuna mambo mawili ambayo Rostam Aziz anatofautiana na Chacha Wangwe. Na hayo mambo mawili ndiyo yamemfanya aanze kutafuta 'mashujaa' wengine kwa kuwa anajua kabisa kwamba Chacha ni mtu anayefaaa kutumika kwa muda tu, mkakati ukifikia hatua fulani atamweka pembeni.

Moja, ni hili la kughushi elimu yake kwenye taarifa za bunge. Rostam anafahamu kuwa Chacha Wangwe hana certificate ya UDSM. Chuo hicho wakati huo hakikuwa kikitoa certificates. Chacha Wangwe alitoroka nchi kwenda Kenya miaka ya 70 mwishoni baada ya kukumbwa na kashfa ya yeye na wenzake kuvunja sehemu ya kuhifadhia fedha pale UDSM na kuiba.

Pili, uamuzi wa Chacha kumtelekeza Mke wake wa Ndoa ambaye amezaa naye watoto 12 na ndiye aliyekuwa naye kwenye harakati kule Tarime katika shida zote na misukosuko ya kisiasa. Mara baada ya kushinda Ubunge Chacha Wangwe amemtelekeza na sasa anakaa Dar es salaam na Kimada mmoja Shombe Shombe nyumbani kwa Mama wa Kimada huyo mjane wa mmmoja wa waliokuwa viongozi waandamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, anakaa pale Mikocheni(Jina nalihifadhi kwa sasa). Chacha aliwaambia Rostam na Ballile kwamba wakati Kamati Kuu inajadili nidhamu yake na kutoonekana kwake Jimboni Tarime, Tundu Lissu alisimama na kutoa hoja kwamba yeye akienda Lissu akienda Tarime katika harakati za Madini wananchi wa Tarime wanamlaumu yeye Lissu kwamba amemtoa Chambiri ambaye alikuwa Mbunge expert wa Dar es saalaam haonekani Jimboni na kuwaletea expert mwingine Chacha Wangwe. Anasema pia Lissu akasema kuwa kilichomuuma zaidi ni Mke wa Chacha kumfuata na kumlaumu kwamba amevunja ndoa yake kwa kuwezesha Chacha kuwa Mbunge na kufanya ametelekeze. Hata hivyo, Chacha alijisifu kwa kina Ballile kuwa alimnyamazisha Lissu kwenye hoja hiyo kwa kumwambia kwamba yeye ana ubia gani na mkewe mpaka aingilie mambo yake ya ndani. Lakini kwa ujumla wote walimshauri Chacha arudi jimboni, chacha akakubaliana nao kuwa anarudi. Tatizo linalomkabili ni kuwa anataka arudi apokelewe kwa kishindo lakini uongozi wa CHADEMA Tarime umeshatoa tamko kuwa hawamuungi mkono. Hapo ndipo ulipowekwa ulimkakati niliodokeza jana wa kurejesha home base.

Sasa tusubiri tuone mambo yanavyoendelea, lakini ndio kwanza kazi imeanza sasa. Nitaendelea kuwajulisha mambo kadiri ninavyoyapata.

Toka wiki iliyopita Chacha amekacha vikao vya Bunge, yuko Dar es salaam. Kuna vikao vyake vingi vingi vya mikakati vinaendelea ikiwemo kupanga ziara ya kuzunguka mikoani kuwashambulia Mbowe na Dr Slaa.

PM
 
Kumbe Chadema Mna Wa/mbunge Anaefoji Vyeti? Nilikuwa Najua Ni Ccm Tu...kwakuwa Mnamuona Chacha Sasa Si Dili Mnaanza Kutoa Siri Zake...jamani...?

Pia Mambo Ya Mke Wa Chacha Nae Vipi?....naona Tunawakaribisha Akina Chinga ....
 
Mkuu PM,

Maneno yako mengi ni mazito sana, lakini inasikitisha sana kwamba mtu kama huyu mliweza kumpa umakamu wa mwenyekiti, tena miezi saba tu iliyopita that does not make a sense,

Haiwezekani kuwa Wangwe amefanya haya unayosema katika kipindi cha miezi saba tu, ni lazima amekuwa na hizi tabia siku zote, na hapa kwenye maneno yako mengi hakuna unapoonyesha Rostam kuhusika na kumpa Wangwe ubunge, au umakamu wa mwenyekiti wa Chadema,



Ahsante Wakuu!


Mkuu ES

Kwanza naona umeshanivika uanachama wa CHADEMA. Najua unajua mimi na wewe tuko hapa muda mrefu. Na hawa wanaCHADEMA wanakati wote wamekuwa wakiniita mimi ni CCM au mtumwa mwa mafisadi. Cha muhimu tu ni kwamba mimi ni mwanahabari. Ni kweli chombo ninachofanyia kazi kina mtaji pia wa mmoja wapo wa watuhumiwa wa ufisadi. Lakini mimi si fisadi wala si mwanachama wa CHADEMA. Mwafrika wa Kike anaujua zaidi ugomvi wangu na dogo Mnyika na wengineo.

Wangwe aliwaanza kuwaingiza mkenge CHADEMA kwa mara ya kwanza kwa kadiri ya habari nilizonazo wakati wa kamati ya Madini, pale alipokutana holiday inn na Mwanyika wa Barrick. Baadaye ndio akatoka na msimamo wa kukataa Zitto asiingie kwenye kamati ya madini na kusema kwamba Zitto ameshanunuliwa na CCM. Sasa wakati huo CHADEMA ikagawanyika kambi mbili. Wanaotaka aingie, Zitto, Mtei nk. Na wasiotaka- Chacha, Dr Slaa, Mnyika, Tundu Lissu nk. Sasa hii kambi ya pili, ya Chacha ilikuwa na kambi mbili ndani yake. Kulikuwa na Chacha mwenyewe, yeye Tatizo lake likiwa ni Zitto kwamba anatumika na CCM. Na kambi ya Dr Slaa, Tundu Lissu na Mnyika hawa walikuwa wanasema kwamba hawana na tatizo na Zitto as Zitto, wanatatizo na kamati yenyewe- muundo wake, motive, wakati wa kuundwa kwake, hadidu rejea na kutoshughulikiwa kwa maoni ya kamati za nyuma. Hawa walikuwa na hoja kuwa Zitto anatumika tu kuhalalisha udhaifu wa Kikwete na serikali yake na kwamba Kikwete hana nia njema. Ila kutokana na msimamo wa Chacha wangwe wakati huo tayari alishanza mawasiliano na Rostam, magazeti ya Mtanzania, Rai na Majira yakapotosha mjadala mzima. Mbowe akaitisha kamati kuu ambayo ilichukua uamuzi wa kati kati, Zitto aingie kwenye Kamati lakini tahadhari Zote za kina Dr Slaa, Tundu Lissu nk zizingatiwa.

Hapo ndipo Rostam akaona Chacha ni 'shujaa' mwafaka wa kumtumia. Chacha akaonyesha dhamira ya kugombea makamu mwenyekiti. Rostam akamuunga mkono. Kwa habari za uhakika ambazo nilizifuatilia kwa karibu Kampeni ya Chacha ilipewa fedha na Rostam Aziz na kuratibiwa na Kaborou, vikao vingi vikifanyika nyumbani kwake na kuhusisha viongozi wa Dar es salaam waliosimamishwa uongozi wa utovu wa nidhamu na wajumbe wa Baraza Kuu walikokuwa wakitumika na Kamati kuu. Kampeni zilifanyika kwa kutumia vipeperushi vyenye kuonyesha kwamba CHADEMA kuna ufisadi na kwamba yeye amelenga kuuondoa.Ndipo Kamati Kuu ilipotaka kuingilia Kati kama nilivyoeleza kwenye michango yangu hapo juu na mijadala ilivyokuwa kwa undani kwa kadiri ya recording ambayo Mzee Halimoja aliifanya. Mbowe, Dr Slaa, Zitto nk waliufahamu huu ukweli kabla, lakini waliamini kwenye busara za wajumbe kwa kuwa kumzuia Chacha angekuwa sawa na kumfagilia njia mpinzani wake Bwana Amour Arfi Mbunge wa Mpanda Kati, na hawakutaka kuwa na upande wowote. Chacha alitumia hoja kuwa wana upande wiki moja kabla ya uchaguzi kupitia habari za Mtanzania, Rai na Majira mpaka umma ukaamini kwamba wana upande. Kwa ajili ya kusimamia principle ndio maana mtakumbuka katika kikao hicho Dr Slaa na Zitto waliwasilisha kusudio la kujiuzulu nafasi zao kama suala la nidhamu halingejadiliwa. Suala likajadiliwa na chacha akapewa onyo lakini jina lake halikuchujwa, kamati kuu ikapeleka majina yote mawili kesho yake kwenye kikao cha baraza kuu bila kueleza kwa undani kulichotokea kwenye kamati kuu kwa kuhofia inngekuwa decampaigning kwa Chacha. Baraza kuu wajumbe kwa kutokujuwa hili na lile na kwa hasira yao kwa sekterariati kutokana na chuki ambazo Chacha alishapandikiza kupitia vipeperushi likampigia kura Chacha Wangwe. Kura nyingi za Arfi zilitokana na wajumbe wa Kamati Kuu ambao walijua undani wa mambo.

Hapa ndipo CHADEMA walipofikishwa, kutokana na Mikakati ya Bwana Rostam Azizi ambayo kwa kiasi Kikubwa imefunika ile ya Kila Lowassa, Karamagi, Chenge na Mkapa. Lakaini mambo mengi zaidi yataendelea kujitokeza. Kesho kutwa kuna kikao kingine kama Chacha hatasafiri kwenda Dodoma. Balille yuko mstari wa mbele katika kuratibu mkakati huu kwa sasa.

PM
 
Pm....muslims Are Not Cheap Like That...may Be They Have To Ask Bakwata As Government Department
 
Ukiona nimekupa "Thanks" ujue katika uliyoandika kuna ukweli mwingi. Wasioelewa wataelewa baadae. Hapa nimeamini wewe Paparazi kweli!
 
PM,

Nashukuru kuweka wazi wewe sio Chadema. maana ningekushangaa. Halafu hao hao Chadema wanakubali vipi kumweka kiongozi kihiyo kwenye umakamu mwenyekiti tena wa taifa?

Ufisadi sio wa CCM tu kumbe....

FairPlayer
 
Nilikuwa huko mikoani na niliporejea nimekuta jambo hili ni hot katika vyombo vya habari. Jana nilimwona Rostam ITV akitetea na kuchangia "mlungula wa shilingi milioni 7". Nilisikitika sana na jinsi alivyokuwa akishangiliwa na kulishangaa Kanisa kwa kumualika mtu ambaye integrity yake kwenye jamii ni questionable kwa sasa na haikushangaza alipotumia nafasi ilie kujaribu kujisafisha. Nilikusudia palepale (pengine kwa haraka na hasiri) moyoni kwamba sitanunua CD/Album ya hiyo kwaya!

Paparzai Muwazi, si jambo kla kushangaza kuwa Spika amekasirika kwa hilo maana habari nilizo nazo ni kuwa Spika Sita ni muumini wa Usharika huo wa KKKT Kinondoni na zaidi yeye alikuwa Mdhamini (Trustee) wa KKKT (sina hakika kama bado ni Trustee wa KKKT), kwa hiyo kwa Rostam kutinga MAdhabahuni ambapo Spika ni muumini na Mtu wa muhimu ni kutaka kumuonyesha Spika kuwa yeye Rostam ni gari kubwa na ni ule Mkakati wa "Mafisadi" kutaka kumwondoa Spika.

Wito wangu kwa Kanisa ni kuwa liwe makini sana maana Ufisadi unaanza kufunguliwa milango na kutumia Madhabahu kujisafisha ni sawa na kuukaribisha Ushetani mahali patakatifu. Siamini kama Kanisa halijui kuwa Rostam ndiye mmliki wa ile Kampuni ya Dowand/Richmond isipokuwa kuna watu na uongozi wa KAnisa pale KKKT Kinondoni ambao wanatumiwa au kutumika kimkakati kwa kutoa Jukwaa na Madhabahu kwa Watuhumiwa wa Ufisadi kujisafisha kwa rushwa ya Vijisenti. Kanisani ni vema likumbuke maadniko kuwa "kupenda pesa ni chanzo cha maovu yote" (1Tim. 6:10) Ole wako Kanisa!
 
Back
Top Bottom