Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,173
- Thread starter
- #41
Hivi huku kama siyo kukiri basi nini?Alipotakiwa kueleza ni kwa sababu gani hasa jina lake limekuwa likitajwa katika sakata zima la sakata la Richmond, Rostam alisema jambo pekee analokiri kupata kulifanya ni kuwashawishi wamiliki wa kampuni ya Dowans Holdings SA iliyorithi mkataba wa Richmond kuja kuwekeza nchini katika sekta ya umeme.
Mimi nilishiriki katika kuwashawishi Dowans kuja nchini. Nitaendelea kushawishi wawekezaji waje nchini ili nchi iendelee, ajira ipatikane na kodi ziongezeke.
Juzi tu nimetoka Singapore, Malaysia na UAE (Falme za Kiarabu) kuwashawishi wawekezaji kuwekeza kwenye usafiri wa anga, alisema Rostam.