Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,896
Ukisoma hali halisi inavyokwenda, jinsi viongozi na wenye dhamana ya kumtaja rasmi mmiliki halali wa Dowans, inaonyesha dalili ya kiwingu kinachowatia ububu huo. Angekuwa ni kigogo mdogo tu na kama angekuwa ni Rostam peke yake alishalipuliwa zamani kabisa.
Nakumbuka kulipokuwa na tatizo kubwa la umeme na kabla Ridhmond haijakubaliwa tenda hiyo Mheshimiwa Rais Kikwete alitamka rasmi kuwa matatizo ya umeme yatakuwa ni historia tu, na mara tukasikia Richmond hiyo ikaibuka.
Idara za usalama zinawajibika, idara za kuzuia rushwa zinawajibika, mkuu wa nchi anawajibika kwa vile masuala ya masuala hayo yasingefanyika bila hao kujua.
Mheshimiwa Hosea anasema hawezi tamka mmuliki halali labda akiitwa kwenye kikao cha kamati ya bunge. Nini anaogopa?
Kwenye kumbukumbu za Wikileaks Hosea huyo huyo anasema Rais Kikwete anakwamisha utekelezaji kwa kuwanusuru vigogo wasishtakiwe kwa matatizo haya ya bribe (backhander).
Ni dhahiri kuna woga kwa wahukika kumnyooshea kidole mhusika mkuu na hata kama ni mshiriki na mhusika mkuu ni mwingine. Uadilifu wa viongozi unatiashaka na ni doa.