Rostam atingisha mkutano wa hadhara igunga

Hili la kugawa pipi limenikuna na kunikumbusha kampuni ya Caspian walipomaliza project ya kujenga bwawa pale Geita Gold Mine RA alitayarisha asante kwa wafanyakazi wote, amini usiamini mwanaume yule aligawa pipi machungwa mbili mbili kwa kila mfanyakazi, anayebisha afuatilie kwa wafanyakazi waliokuwepo, jamaa nuksi kwelikweli
icon6.gif

Aisee, this is good kumbe Caspian wanamaliza miradi on time na wanaamua kupongezana kwa namna ambayo wanaifurahia wao. Mimi sikuwepo lakini nina uhakika hawakufurahia kwa pipi mbili tu. Lazima kulikuwa na mengine ambayo kama wewe ulihudhuria lakini unaamua kutoyasema una lako!

Anayefanya kazi na asile. Na anayefanya kazi vizuri ale na kupongezwa.
 
Wakazi wa Igunga wanapenda PIPI, nadhani ndiyo maana ni miongoni mwa wilaya zilizo nyuma kimaendeleo. Waliofika Tabora na kwenye wilaya zake wanaijua INAVYOTIA HURUMA utadhani imelaaniwa ila leo nimegundua ni kwa ajili ya HIZO PIPI.

Wajameni nilishasema tangu zamani kuwa Tabora tuna ka-Uarabu sana na dawa ni moja tu yaani VIBOKO. Watu kama hawa inabidi kuwatembeza kijeshi hadi wanaanza kuwa wanafikiria. Yaani unamwambia achimbe shimo, akikataa unamlima bakora, akichimba unamlima tena, akiuliza kwa nini unamwambia, mbona hakuuliza hilo shimo la nini? Hii itafanya wawe wachapa kazi ila pia wanatumia ubongo kabla ya kufanya jambo lolote.


- Waache wafu wazikane wenyewe huko Igunga na kiongozi wao, maana kama hizi habari ni za kweli basi sikio la kufa hilo!

William.

Weee Mgogo wee, HESHIMA kwa Wazee wako Wanyamwezi. Tukija tena Dodoma safari hii na Mirambo wetu, tutakutandikeni hadi ugonjwa wa macho uishe. Yaani wewe bila aibu kabisa unatuambia wazee wako UKWELI? Hujui ukweli UNAUMA???
 
- Mkulu Sikonge, na nyinyi mmezidi jamani hata baada ya utumwa kuisha bado mnaulilia tu kama Lipumba na waarabu wa Oman, ahhggrr inatia kinyaa hommie!

FMEs!

Heshima Mbele FMES.

Now you are talking, yote yanayoongelewa kiini chake ni ubaxxxi. Endeleeni wakuu iko siku mtagundua otherwise.

Hata George W. Bush katika vitu anavyo-regret ni vita ya Iraq Mkuu.
 
Mkuu you took the word from my mouth? yeye ni nani?

Ukistaajabu ya Mussa.., ama kweli pesa za bure bure zinalevya, inafikia mahali mtu anajisahu na kuona wanadamu wenzie wote kama vikaragosi vyake! Kwahiyo anawakemea wabunge wenzake wasitembee na Mengi?
Yaani ana mamlaka hadi ya kuchagulia wenzie nani uongee naye, nani utembee naye makubwa haya nye!

Yeye si ndiye aliyewachagulia mpaka Rais....sasa wabunge kwake si kazi ndogo mfano akisema uchaguzi ujao sitaki fulani awepo na asishinde kura za maoni an ikawa kama atakvyo. Lakini ni wana CCM wenyewe na baaadhi ya wananchi ndio wanalea na kuwapa vichwa watu kama hawa. Si ulisikia wazee wa Yanga juu ya Yusuf Manji kuwa msisakame mfadhili wao.
 
Ndugu zangu, Rostam amewazidi ujanja na hizi kelele zenu hazina faida yeyote, kwani hizi skendo zimeanza leo bongo, zamazile tulikua tunayajadili vijiweni na sasa kwenye mtandao. Wajanja wanakula tu. Rostam ni mwizi lakini ni rafiki ya Rais ya Tanzania, uchaguzi unakaribia na pesa zitahitajika kuwahonga watanzania kwenye uchaguzi ili wizi wale wale tuwachague tena. hizi kelele zetu ndio zinawapa akili na mbinu mpya ya kuiba tena. Watanzania ni asili yetu kupiga kelele bila kuchukua action. Mbona hakuna hata walio andamana ili Rais (AKA sindibadi) alitatue hili swala? Wazungu wanasema If you cant beat them, join them. Nendeni mkamuombe dili Rostam kuliko hizi kelele.
 
Kwani kosa hasa la Rostam ni nini? Kaiba? Kama kaiba, basi kaiba nini? Kaua? Kama kaua, kaua nani? Mpaka sasa mimi sijaona kosa la mtu huyu, mchukueni wenyewe mkamhukumu kwa sheria yenu. Leteni mashitaka halali kama mnataka hukumu. Kila siku RA, RA, RA, he, hakuna mambo ya kitaifa ya kufanya zaidi ya kuandika RA na Mengi? Mengi kataja mafisadi papa, mambo yapo mahakamani, mengine ya RA yapo PCCB, sisi tuchape kazi, tuache kupiga domo. Ohoo, Watanzania! Tutumie nguvu hizi kuwasaidia wa Mbagala etc.
 
ndugu, nafikiri ni mapema mno kuwalaaumu watu wa Igunga na Tabora kwa jumla. History ni mwalimu mzuri saana, natumaini mnakumbuka kabla ya kuanguka Shaushesho wa Rumani, siku tatu kabla kulikuwa na congress ya chama chake. Alipita kwenye uchaguzi kwa kishindo watu wote wakishangilia mpaka wanalia, siku tatu baadae hutaamini yaliyotokea. Kwangu mimi, wa Tabora, Arusha hata Shinyanga naamini kabisa hawako nyuma ya hawa mafisadi. Kufika kwenye mkutano haina maana unamshangilia, wakati mwingine unakuja usikie na upande mwingine kuna nini ili ukweli uujue, ukikaa nyumbani utajua nini? Cha kujiuliza, si tuliambiwa serikali imetoa onyo kwa RA na RM? sasa tusikie kama serikali ina ubavu wa kumtia msukusuku RA.
Kingine, pamoja na maovu yote ya RM, hivi na yeye anatafuta nini? na yeye anatakiwa pia kujibu hoja za RA kama ambavyo RA anatakiwa ajibu hoja za RM. Kwangu mimi naona pia hasira tumeelekeza mno kwa RA, lakini ukweli usiozibika hili soo lote majibu muhimu anayo mtu ambaye sote hatutaki kuandamana kushinikiza atupe ukweli, huyu mtu si mwingine ni MH MKAPA.
 
Kama kweli watu wa IGUNGA wameyafanya haya kwa RA, pamoja na kelele na shutuma zote anazolaumiwa huyu mtu, basi nadhani tumelogwa. Na ndipo ule usemi wa mwanafalsafa wa JF unapokuwa na nguvu ".. Miafrika ndivyo tulivyo..."

Wangapi huko Igunga wanasoma magazeti? Kama Dar kwenyewe unakuta Watanzania wanatolea macho magazeti kwenye vibanda vya wauzaji huku wakiwa hawana uwezo wa kuyanunua, unategemea nini kutoka kwa watu wa Igunga!

Ukiwa nje ya nchi unadhani kwamba nyumbani mambo yamebadilika sana, lakini ukweli unabaki palepale, Watanzania wengi bado ni mbumbumbu na wala wengi wao hata huo msamiati unaoitwa UFISADI hata hawajui maana yake!

Safari bado ni ndefu, lakini hakuna kukata tamaa! Pengine kina Martin Luther King Jr wangekata tamaa, Obama asingekuwa rais wa dunia leo hii!
 
Leo mheshimiwa Rostam kapokelewa kwa shangwe kubwa na msululu mrefu wa wapiga kura wake kwenye uwanja wa samora mjini Igunga,baskeli pikipiki pamoja na maelfu ya wakazi walijumuika kwenye mapokezi hayo....kisha aliwahitubia akichanganya lugha ya kisukuma na kiswahili pamoja na mambo mengine ya maendeleo aliwataka wananchi wake wayapuuze maneno ya kejeli yanayotolewa na Mengi dhidi yake.aidha alitoa tahadhari kwa wabunge wa mkoa wa tabora wanaopenda kuongozana na Mengi kwenye ziara zake za mkoa wa tabora na kuwa kamwe hawatvumiliwa tena jambo ambalo lilishangiliwa kwa nguvu kubwa

Hii sasa ukisikia hali halisi ya kwenye ground ndiyo hii. Wafanye wawe fukara halafu tumia hela uliyowaibia kuwafanya wakuone shujaa.

Hapa kilichopo ni kwamba kila mtu anaangalia atanufaika vipi?, mfano sisi tunapiga vita ufisadi sana tu, haya inatokea mali za umma haziibiwi then what next?, kama watu hao ambao ni custodiam watakuwa wanaangalia hazina hawana plan yoyote au hawajui wafanye nini nazo?, je mwananchi wa Igunga atanufaika vipi?, second scenario mtu anaiba mali ya umma na kwenda kuwapa wapiga kura masikini 0.1% ya hizo angalau wananunua chumvi na magodoro unatajia wananchi hao watamuonaje Fisadi huyu?. Ni lazima watamwona mkombozi wao.

Sisi hapa JF tuendelee kufanya analysis lakini on ground mambo ni tofauti sana unless na sisi tuingie on ground kuwa elimisha wananchi kuhusu tunayoyajua hapa. Internet cafe saa 1 ni shs 2,000 tena ukiclick unasubiri 10 minutes page ifunguke unataji Mtanzania ambaye kwake hata Shs 500 hajui aanzie wapi atakuwa na muda wa kufuatilia?, Ni dhahiri kuwa akina RA, EL, Chenge et al watakuwa mashujaa tu majimboni kwani wanajua kucheza na Simba mwenye njaa.
 
Kama ni kweli amepokelewa hivyo lazima tujiulize na kuwatazama hao walioandaa hiyo 'hafla'. Katiza enzi hizi za maisha magumu na taabu nyingi kwa mtu mwenye pesa kama yeye ni rahisi kuvuta kundi fulani la watu, wakala wakanywa na kushangingilia. ndo maisha yalivyo. Hata misiba mingi inapata watu maeneo ya vijijini kulingana na uwezo wa familia iliyofiwa. Issue hapa ni kula tu. Kazi bado tunayo.
 
well said ....naomba kibao cha Les MWENGE ...vijana wa CTU arusha ,dansi lao hata muungwana JK akiwa capt alikuwa akilicheza....

kibao- KILA MNDU AVE NA KWAO.

Waswahili wanasema mcheza kwao huunzwa.....hata wasipomtunza bado familia yake haiwezi kumtupa...,familia inaanzia nyumbani ,mtaa,kijiji,eneo,mkoa,kanda,taifa etc....kama unaishi vema na familia yako hata ukiwa katili namna gani ....watakutetea hadi damu ya mwishi,ndivo maisha yalivyo~~~! hii ni ishara kuwa rostam anaishi vema na familia yake ya wana tabora!.....if mengi want to convince tabora to turn him down will be a wrong war strategy....hasa pale inapokuwa tayari wapo kwenye total warfare....tayari kuna tension,ingekuwa tofauti zao hazijawa wazi.....ingekuwa mbinu yake ya kutumia kina seleeli etc..ingesaidia...kumpata mgombea wa kumuondoa rostam bila watu kustuka ......

pia lingine ni kuwa mzee mengi inaonekana anazidiwa ujanja na rostam hasa pale inapoonekana wazi kuwa rostam na wenzake wana wafuasi wanaomzunguka mengi.....cant you imagine mengi alijuwa kuwa mbunge aziza suleyman yuko upande wake na akampa baiskeli 300 na pesa ...na days after aziza huyo huyo anaongozana na rostam kwenye ziara........watu wanamlia mzee mengi pesa bila yeye kujijua...huku wenzake wanajiimarisha kibiashara na kimkakati!!


Si dhani kama Mengi alitoa baiskel 300 kwa Aziza Suleyman kwa matumizi yake binafsi , bali kwa matumizi ya wananchi wenye shida kama mimi..!!

Unapokosa Elimu kichwani mara nyingi ni tatizo kubwa sana..! Sitegemei kwa mtu mwenye upeo mkubwa wa kujua na kufikiria mambo kukubaliana na kushangilia mtu mwenye kulinyonya taifa lake..! Na kama atakuwepo basi atakuwa ni MTUMWA !!!

Wanakimbilia vijijini wakijua fika kwamba mtanzania aliepo kule hata sabuni ya kuogea hajui inafanana vipi !!!


Anae support ujinga wa jinsi hii ninashaka nae sana :rolleyes:!!!
 
well said ...

pia lingine ni kuwa mzee mengi inaonekana anazidiwa ujanja na rostam hasa pale inapoonekana wazi kuwa rostam na wenzake wana wafuasi wanaomzunguka mengi.....


KWA MAONI YAKO WEWE ANAEZIDIWA UJANJA NI MENGI AU WANANCHI WA TABORA :confused: !!!!

AM SO SAD !!!
 
Rostam apokewa `kitemi` kwao Igunga

[FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Na Mwandishi Wetu, Igunga

WANANCHI wa Jimbo la Igunga, Tabora, wametuma salamu maalumu kwa mahasimu wa kisiasa na kibiashara wa Mbunge wao, Rostam Azizi, kwa kumpatia mapokezi makubwa.zito.

Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita, wakati Mbunge huyo alipotembelea jimbo hilo, na kupata mapokezi mazito yaliyowakusanya watembea kwa miguu wa rika zote, waendesha baiskeli, pikipiki, Bajaj, mikokoteni na magari makubwa na madogo.

Katika mapokezi hayo yaliyoanzia takriban kilomita tano kabla ya kuingia mjini Igunga, ambayo hajawahi kuyapata Mbunge huyo tangu achaguliwe kwa mara ya kwanza 1994, baadhi ya wananchi wa mji wa Igunga na vitongoji vyake walisema mapokezi hayo wameyafanya ili kutuma salamu kwa mahasimu wa kisiasa wa Mbunge wao, pamoja na kumpongeza kwa ujasiri aliouonyesha katika kujibu mapigo.

"Tulikuwa na shauku ya kumuona moja kwa moja ili tumpongeze kwa ujasiri aliouonyesha wakati akimjibu yule anayetaka kuwasemea Watanzania kwa kutumia magazeti, redio na televisheni zake na kuwatukana watu, wakati hajawahi kuchaguliwa na wananchi kuwa hata mjumbe wa nyumba 10, wala mwenyekiti wa kitongoji," alisikika akisema kijana mmoja mwendesha baiskeli.

Rostam alifanya ziara ya siku moja jimboni Igunga Ijumaa iliyopita, ziara ambayo pamoja na mambo mengine, ililenga kuhani misiba iliyotokea jimboni humo na kuwapa pole wagonjwa wenye maradhi mbalimbali katika kijiji cha Mwisi, ambako ndiko alikozaliwa pamoja na kijiji jirani cha Ndembesi ambako kuna wajomba zake.

Maandamano hayo ya mapokezi kwa Rostam baada ya kuingia mjini Igunga, yalielekea moja kwa moja katika ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), na baadae yeye na wajumbe wenzake wa Halmashauri ya Wilaya, waliendelea na kikao cha ndani, ambacho kilifunguliwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Tabora, Asha Kimengule.

Aidha, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja, Mbunge wa Urambo Mashariki, ambaye pia ni Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya, na Mbunge wa Viti Maalumu na pia Mumbe wa NEC Taifa, Azuza Sleyum, walihudhuria kikao hicho kama wageni waalikwa.

Akijibu mapokezi hayo, katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya kumbukumbu ya Sokoine jioni mara tu baada ya kikao hicho cha halmashauri ya wilaya, mbunge huyo alisema baada ya majibu yake kwa mmoja wa mahasimu hao, kwa sasa hana ‘time' (muda) nao tena na wala hawamnyimi usingizi.

"Sisi watu wa Igunga tunapendana na tunaishi kama ndugu wa baba na mama mmoja. Hatuna tabia ya kutuhumiana wala kuhukumiana. Watu kama hawa ni ‘kuwabebye', nashukuru nanyi kuniambia hapa kwamba ‘mmewabenye," alisema Rostam na kufuatiwa na makofi na vigelele kutoka kwa mama waliohudhuria.

‘Kubedye' ni neno la Kisukuma na Kinyamwezi, lenye maana ya kuwadharau. Kwamba wananchi wa Igunga, wamewadharau mahasimu wa Mbunge huyo.

Akizungumzia mahasimu wake hao bila kuwataja majina, Mbunge huyo alisema kipo kikundi cha watu wachache walioko Dar es Salaam na Dodoma, ambao wameamua kuchafua rekodi nzuri za watu. Alisema tayari watu hao wamepenya hadi ndani ya Mkoa wa Tabora kwa lengo la kuwafitinisha wabunge wa Mkoa huo ili wasielewane.

"Hawa ni mahasimu wa kisiasa na wengine ni mahasimu wa kibiashara. Hawa ni watu wanaotapatapa, wana agenda zao za kisiasa nje ya utaratibu wa chama na wengine wana chuki zao binafsi za kibiashara, mimi kama mjumbe wa NEC ninayewakilisha Mkoa wa Tabora, nitaendelea kushirikiana na wabunge wote wa mkoa huu kuleta maendeleo katika majimbo yote ya mkoa wetu," alisema Rostam.

Akiwakumbusha wananchi wake baadhi ya mambo waliyoshirikiana kuyatekeleza kwa ajili ya maendeleo yao, Rostam alisema Igunga ndio wilaya pekee nchini, si tu yenye zahanati katika kila kijiji, bali iliyoweka utaratibu wa bima ya afya kwa kila kaya, gari moja la wagonjwa lenye redio ya upepo (radio call) katika kila tarafa, pamoja na zahanati zisizokaukiwa dawa.

Alisema, Igunga ya 1994 wakati anapata ubunge, ilikuwa na shule za sekondari tatu, lakini leo ina sekondari 29, sawa na sekondari moja katika kila kata. Aidha, alisema aliikuta wilaya hiyo ikiwa haina umeme, lakini leo karibu vijiji vyote vimefikiwa na umeme, na vinapata mawasiliano ya simu kupitia mitandao yote ya simu nchini.

"Tuna kiwanda kikubwa cha kisasa na cha mfano hapa Igunga cha kuzalisha mafuta ya pamba, na mwakani kitaanza kusokota nyuzi za pamba.

"Tuna mabwawa 40 ya maji kwa ajili ya kilimo na mifugo yetu, kuna mradi mkubwa umeanza wa kuweka mtandao wa maji safi na salama hapa mjini na katika vijiji vyote vya wilaya hii, najua tuna safari bado ya kuelekea kwenye maisha bora, lakini nawahakikishieni Igunga tunapaa ikilinganishwa na wilaya nyingine nchini."

Kabla ya Mbunge huyo kupewa jukwaa, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mgeja na Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Kapuya, walipewa fursa ya kuwasalimia wananchi wa Igunga.

Katika salamu zake, Mgeja alisema Igunga anayoijua ya mwaka 1994 kabla ya Rostam kuwa Mbunge si Igunga hii ya sasa baada ya kushikwa na Mbunge huyo.

Alisema wote wanaomchokonoa Mbunge wao, wamejawa na wivu wa maendeleo, kwa hiyo akawataka wananchi hao kuendelea kumuunga mkono Mbunge wao ili awaletee maendeleo zaidi.

Kwa upande wake, Profesa Kapuya katika salamu zake alizoziwasilisha kwa kutumia zaidi methali na hadithi za kale, alisema wahenga wa zamani, ingawa hawakuwa wamesoma wala kulijua darasa, waliweza kutoa maono ambayo hadi leo yanaendelea kutuongoza.

Alitolea mfano wa methali isemayo; "Asiyekujua hakuthamini' na ile ya ‘Ukiona vinaelea vimeundwa.' "Ndugu zangu, asiyekujua, anaweza akakupuuza, akakutukana na kukukejeli. Lakini, kwa unayemjua sivyo, nyie na sisi Urambo ndio tunaojua kwamba Rostam ni lulu kwetu, tusiipoteze," alisema Kapuya.
[/FONT]​
 
Mie nawashangaa watu hapa jamvini hamjui mnabishana na nani
KWA TAARIFA YENU MNAYEBISHANA NAE NI HUYU HUYO PAPA
Kwa macho yangu nimeoina kwenye laptop yake anawajibia hoja zenu JF busy kucheki updates

HALO HALO IDUMU JF HAWALALI KUCHUNGULIA DEVELOPING ISSUE


Hata kama sio yeye papa ni wapambe wake wale wa gazeti fisadi la MTANZANIA. Kuna mmoja kasema alikuwa katikati ya mkutano, ndio hao wamelipiwa kila kitu na mkuu wao wa kazi. JF TUWE MAKINI NA MABISHANO KUNA WATU WANATUCHOTA AKILI.
 
- Waache wafu wazikane wenyewe huko Igunga na kiongozi wao, maana kama hizi habari ni za kweli basi sikio la kufa hilo!

William.

Mkuu,
Kwa sisi tunaotembelea Tanzania nzima tunajua mengi.Huko Igunga kunamaendeleo mengi sana ukilinganisha na Jimboni kwa Akina Kilango na wenzake.
 
Wajameni nilishasema tangu zamani kuwa Tabora tuna ka-Uarabu sana na dawa ni moja tu yaani VIBOKO. Watu kama hawa inabidi kuwatembeza kijeshi hadi wanaanza kuwa wanafikiria. Yaani unamwambia achimbe shimo, akikataa unamlima bakora, akichimba unamlima tena, akiuliza kwa nini unamwambia, mbona hakuuliza hilo shimo la nini? Hii itafanya wawe wachapa kazi ila pia wanatumia ubongo kabla ya kufanya jambo lolote.




Weee Mgogo wee, HESHIMA kwa Wazee wako Wanyamwezi. Tukija tena Dodoma safari hii na Mirambo wetu, tutakutandikeni hadi ugonjwa wa macho uishe. Yaani wewe bila aibu kabisa unatuambia wazee wako UKWELI? Hujui ukweli UNAUMA???

Hongera sana Sikonge

Post zako,kweli zinanikosha roho yangu.

Wewe ni mtu muhimu sana kwenye JF.
 
Back
Top Bottom