Rostam ajipanga kuikimbia Tanzania; kutimkia Malaysia

Taarifa za ndani zinaonyesha kuwa

1. Fedha za Rostam zimekuwa zikipitia mabenki ya Marekani ..then uarabuni kwa jina lake na uthibitisho wa kila fedha alikoipata.
2. Lengo la kucheza na matawi ya benki zinazoendeshwa na policy za marekani hapa nchini ni kuzisafisha fedha zake
3. CCM haimo, haina chake, Nappe na rais ajaye watajua watakakokuwa wanakopa

kiuchumi YES, uchumi utatikisika. Lengo la kuchukua fedha kidogo kidogo linalenga kutotokea mtikisiko wa uchumi

Hiyo namba tatu mkuu umenivunja mbavu mkuu.....:lol:
 
Rostam hakuvunja benk kuiba mapesa aliyonayo bali alifanya biashara na alilipwa malipo halali. Wafanyakazi ndani ya bank na ndani ya mashirika yetu ya umma walimpa ushirikiano katika kufanya biashara zake na kufanikisha malipo. Sasa kama anaamua kufunga akaunti zake huo ni uamuzi wake kwani hizo ni pesa zake.
 
Aondoke. Lakini laiti tungelikuwa na Rais "Msafi" angelimtia hatiani mtu huyu, mali zake zingelikamatwa na kunadiwa kabla ya kutokomea Malaysia. Maskini Tanzaniaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!
mbona kama mnachekesha?? yaani rais huyu aliyeingia madarakani kwa pesa ya kagoda ageuke tena amkamate mwenye kagoda???
 
kumbe Nchi inaongozwa na watu wa kupita: wakisha chojoa raslimali zetu na kujua ka-nchi ketu kakoje IN and OUT wanaamua kusepa siyo!!! Haya bwana.
 
Wakuu, sidhani kama kuna mtu anatetea mafisadi ambao wakukwapua uchumi wetu..

Tunajadili hii habari ina ushahidi wa kujitosheleza mpaka tuamini kweli Rostam kafunga hizo account zake!

Muanzisha hii thread ingekuwa vizuri kama angeweka copy ya barua hiyo pamoja na kututajia jina la benki ya huko Malaysia.

JF kuna Great Thinkers sidhani kama wanaweza kujadili Gossip.
Na bado mwaka huu tutasikie mengi..................
 
watanzania watu wa hovyo sana..mtu anafunga akaunti zake kwa hiari yake nyie mnaazna kubweka bweka tu hapa..mbona nyie mkifunga akaunti zenu nmb hakuna anayewauliza ..
 
Rostam Aziz ameziandikia bank za CRDB na NMB ya kutaka kufunga account zake na kutaka kuhamisha fedha hizo katika nchi ya Malaysia, tukio hili lilifanya mameneja wa bank hizo kuomba muda wa kupitia na uhamuzi huo kabla ya kuruhusu kufungwa kwa akaunt hizo, kwani kutokana na kiasi kilichomo ndani ya akaunti hizo ni lazima wapate kibali ya kufunga na kuhamisha kutoka BOT.

Lakini wachambuzi wa mambo wanaliona ni tukio la bwana Rostam kuondoka nchini na kuelekea malaysia, hivyo basi kama Tanzania kuna chochote cha kumuuliza au tunataka kufahamu kutoka kwake ndio wakati muafaka sasa la sivyo zile tuhuma za wizi wa fedha za EPA kupitia Kagoda ndio ushahidi wake unapotea hivyo

Kuna watu bwana wako hatua tatu mbele ya matukio...wanaona mambo ambayo wengine inakuwa ngumu sana kuyaona.Anyway, that is life.....
By the way, familia yake kwani ipo nchini?
 
Mungu wangu! na ile mizee ya Igunga iliyokuwa inapiga mayowe na kugaragara alipojiuzuru itamfuta? Na nani atautengenezea tshirts za bure wakati wa Kampeni?Mungu atunusuru na dhahama hii
 
Kuna mzee mmoja ni maarufu sana siwezi kumtaja (ni mmoja wa maafisa wa Usalama wa Taifa) kwa usalama wangu maana natumia ID yangu orginal pamoja na Avatar ya picha yangu halisi..... alichoniambia kwamba Rostam Aziz ni Jasusi la CIA na yuko very protected, alikuja hapa kwa lengo maalum na kazi aliyoifanya ameshaimaliza na aliletwa na Marehemu Kambona....
siwezi endelea zaidi............

Dah huu ni uongo kabisa kijana,Rostam aziz kazaliwa Mwisi huko Igunga,kasoma shule ya msingi na moja ya baba zangu wadogo pae Mwamala nzega miaka hiyo,haya kaja lini toka America huo ushambenga unaitwa,
 
du kumbe rosti tamu tamu aziz ipo shilingi ehh mpaka benk wanampigia magoti
 
Wakuu, sidhani kama kuna mtu anatetea mafisadi ambao wakukwapua uchumi wetu..

Tunajadili hii habari ina ushahidi wa kujitosheleza mpaka tuamini kweli Rostam kafunga hizo account zake!

Muanzisha hii thread ingekuwa vizuri kama angeweka copy ya barua hiyo pamoja na kututajia jina la benki ya huko Malaysia.

JF kuna Great Thinkers sidhani kama wanaweza kujadili Gossip.

Kama hapo tu hauamini,je akiweka hiyo barua si utasema ni ya kutengenezwa? We unafikiri muanzisha sredi kakurupuka? Kwanin ujiulizi mbona hajaanzisha uzi wake huu juzi na kauleta leo?
 
Rostam Aziz ameziandikia bank za CRDB na NMB ya kutaka kufunga account zake na kutaka kuhamisha fedha hizo katika nchi ya Malaysia, tukio hili lilifanya mameneja wa bank hizo kuomba muda wa kupitia na uhamuzi huo kabla ya kuruhusu kufungwa kwa akaunt hizo, kwani kutokana na kiasi kilichomo ndani ya akaunti hizo ni lazima wapate kibali ya kufunga na kuhamisha kutoka BOT.

Lakini wachambuzi wa mambo wanaliona ni tukio la bwana Rostam kuondoka nchini na kuelekea malaysia, hivyo basi kama Tanzania kuna chochote cha kumuuliza au tunataka kufahamu kutoka kwake ndio wakati muafaka sasa la sivyo zile tuhuma za wizi wa fedha za EPA kupitia Kagoda ndio ushahidi wake unapotea hivyo
Kwani wizi wa EPA vipi alishamaliza kulipa, hata kama amelipa si lazima apelekwe mahakamani kujibu kesi ya wizi?????Dunia sasa ni kama kijiji hata kama atakimbilia Malaysia au kwenye visiwa vya Falkland bado serikali makini itamtafuta aje kujibu mashitaka ya wizi wa EPA period!!!!!

ni wakati wa vyombo vyetu vya udhibiti wa fedha kufanya kazi mimi nilizisikia habari hizi toka wiki iliyopita kutoka kwa mfanyakazi mmoja wa CRDB azikiwe . lakini cha kushangaza utakuta vyombo vyetu vya udhibiti vimelala mpaka akiondoka ndio vianze kupiga kelele za kumtafuta.

tulishuhudia kipindi cha meridian biao wakitoroka na fedha zetu huku BOT wakiwa wamelala na sasa rostam ndio anaondoka na mabilioni yetu na muda si muda tutaambia haonekani
 
wasiliana na mchungaji mtikila mzuri sana katika kufungua kesi za maslahi ya umma !!!
ni wakati wa vyombo vyetu vya udhibiti wa fedha kufanya kazi mimi nilizisikia habari hizi toka wiki iliyopita kutoka kwa mfanyakazi mmoja wa crdb azikiwe . Lakini cha kushangaza utakuta vyombo vyetu vya udhibiti vimelala mpaka akiondoka ndio vianze kupiga kelele za kumtafuta.

Tulishuhudia kipindi cha meridian biao wakitoroka na fedha zetu huku bot wakiwa wamelala na sasa rostam ndio anaondoka na mabilioni yetu na muda si muda tutaambia haonekani
 
Dah huu ni uongo kabisa kijana,Rostam aziz kazaliwa Mwisi huko Igunga,kasoma shule ya msingi na moja ya baba zangu wadogo pae Mwamala nzega miaka hiyo,haya kaja lini toka America huo ushambenga unaitwa,

Kwa fahamu zako za kutilia mashaka ukiambiwa JK, BM ni mawakala wa CIA utakataa. Ndivyo mlivyo nyinyi, lakini habari ndiyo hiyo,
 
Back
Top Bottom