Rostam ajipanga kuikimbia Tanzania; kutimkia Malaysia

Naomba tutafakari hii saga katika context ya "dual citizenship" ambayo Membe amekuwa anaipigia debe sana. In theory dual citizenship ni kitu kizuri maana tunaambiwa kuwa watu walio nje ya nchi wataweza kuwekeza nyumbani. Sijui wako wangapi na kati yao nani anafanya kazi kubwa kubwa na nani anabeba mabox! Ila wasiwasi wangu kwenye issue ya dual citizenship ni kwamba unapokuwa na nchi/serekali legelege watu watahamisha 'capital' kurahisi kabisa kwa sababu wana uraia wa nchi nyingine.

Swali langu kwanini Rostam amechagua Malaysia? Kwa nini isiwe China, Uswisi, Cambodia, Urusi au hata Kosovo? Why Malaysia?

Hizo nchi nyingine akifanya ufilauni kama huu wa huku tanzania ndani ya minute wanamnyonga!!!!
 
waziri wa mambo ya ndani fungia pass za kusafiria za huyo MANG'ATI, halafu ndo mengine yaweze kuendelea juu yake,yani aondoke na mpunga wa watz?
 
Mkuu, JF sio sehemu ya porojo wala kijiwe cha mbege! Kwa hiyo unapoleta data zako humu JF kwa Great Thinkers lazima uwe na facts za kutosha.

Sio kuokota maneno mitaani na kwenye magazeti ya udaku ndio ushahidi wako..

Ebu weka hiyo barua ya Rostam Aziz, humu JF tuione ndio tujadili zaidi ya hapo tutakuwa tunajadili umbeya!

Get a life man, for real!!!
 
Now you are talking!
Lakini mkuu, hii move inaweza ikawa swala la kuhamisha sehemu ya fedha za CCM kwenda nje ya nchi.
These guys are clever...............share za Voda hizo mkuu!
sema yote kuwa

1. theluthi ya fedha zilizoko uko benki ni za Rostam
2. kuwa akine kimei walifunga safari kumfuata ughaibuni kumuomba abadilishe uamuzi wake akakataa
3. alichowasadia ni kuwa atazitoa fedha kwa awamu
4. anai-ondoa na kampuni yake ya caspian ambayo makao yakemakuu ni uarabuni
 
Naomba tutafakari hii saga katika context ya "dual citizenship" ambayo Membe amekuwa anaipigia debe sana. In theory dual citizenship ni kitu kizuri maana tunaambiwa kuwa watu walio nje ya nchi wataweza kuwekeza nyumbani. Sijui wako wangapi na kati yao nani anafanya kazi kubwa kubwa na nani anabeba mabox! Ila wasiwasi wangu kwenye issue ya dual citizenship ni kwamba unapokuwa na nchi/serekali legelege watu watahamisha 'capital' kurahisi kabisa kwa sababu wana uraia wa nchi nyingine.

Swali langu kwanini Rostam amechagua Malaysia? Kwa nini isiwe China, Uswisi, Cambodia, Urusi au hata Kosovo? Why Malaysia?

FJM,umenena!,na swali hilohilo ndilo ninajiuliza mimi pia.halafu naongezea kuuliza Hivi MALAYSIA si ndio inakotoka ile kampuni inayotufilisi ya IPTLmalaysia pta?
Na ikumbukwe kuwa kampuni ile iliingia mkataba wa kuzalisha umeme nchini enzi hizo waziri wa wizara husika akiwa ni Jakaya mrisho kikwete?
 
Wanaanza kuondoka mmoja mmoja kabla ya uchaguzi wa ccm maana baada ya hapo hali itakua mbaya sana kwa mafisadi..

nani kakwambia uchaguzi wa CCM utawaondoa wezi,mafisadi na matapeli ktk chama chenu? hao wataondoka siku CCM ikiondolewa madarakani,kwasasa hawawezi ondoka na chama hakina uwezo wa kuwaondoa,wapo ktk shamba la bibi!
 
Nani ana ubavu katika watawala wa Tanzania kumgusa Rostam.Huyu bwana ni bosi wao katika kila nyanja.Na kuhusu kuhama kwake kama ni kweli,it is understable.Huyu mtu alikuja Tanzania kimasilahi,kama masilahi hayapo tena akae afanye nini.Wajinga ni sisi tulioshindwa kubaini mapema kwamba si mwenzetu.
Rostam Aziz ameziandikia bank za CRDB na NMB ya kutaka kufunga account zake na kutaka kuhamisha fedha hizo katika nchi ya Malaysia, tukio hili lilifanya mameneja wa bank hizo kuomba muda wa kupitia na uhamuzi huo kabla ya kuruhusu kufungwa kwa akaunt hizo, kwani kutokana na kiasi kilichomo ndani ya akaunti hizo ni lazima wapate kibali ya kufunga na kuhamisha kutoka BOT.

Lakini wachambuzi wa mambo wanaliona ni tukio la bwana Rostam kuondoka nchini na kuelekea malaysia, hivyo basi kama Tanzania kuna chochote cha kumuuliza au tunataka kufahamu kutoka kwake ndio wakati muafaka sasa la sivyo zile tuhuma za wizi wa fedha za EPA kupitia Kagoda ndio ushahidi wake unapotea hivyo
 
Buriani Rostam, kalale mahala pema motoni huko Malaysia.
TUMEIBIWA KIASI CHA KUTOSHA, TUMENYONYWA KIASI CHA KUTOSHA NA TUMETAPELIWA KIASI CHA KUTOSHA
Unyonge wa mkulu ndio umetufanya tuibiwe, tunyonywe na tutapeliwe na mafisadi.
 
Rostam Aziz ameziandikia bank za CRDB na NMB ya kutaka kufunga account zake na kutaka kuhamisha fedha hizo katika nchi ya Malaysia, tukio hili lilifanya mameneja wa bank hizo kuomba muda wa kupitia na uhamuzi huo kabla ya kuruhusu kufungwa kwa akaunt hizo, kwani kutokana na kiasi kilichomo ndani ya akaunti hizo ni lazima wapate kibali ya kufunga na kuhamisha kutoka BOT.

Lakini wachambuzi wa mambo wanaliona ni tukio la bwana Rostam kuondoka nchini na kuelekea malaysia, hivyo basi kama Tanzania kuna chochote cha kumuuliza au tunataka kufahamu kutoka kwake ndio wakati muafaka sasa la sivyo zile tuhuma za wizi wa fedha za EPA kupitia Kagoda ndio ushahidi wake unapotea hivyo
Tulowapa jukumu wameshindwa na sasa jamaa kamaliza kazi iliyomleta hana budi kukusanya masurufu yote aliyotuibia/kutunyang'anya na kwenda nayo huko anakoona kunafaa kuzitunza nasie tutakapopata akili ya kuzidai hatutaweza kuzifikia.. kweli viongozi wa Tanzania vilaza
 
Dr Harry Mwakyembe aliwahi kuwaambia watanzania siku moja kwenye ukumbi wa Maelezo, na kilichotokea pale ni wale waandishi uchwala waliokuwa wametumwa na mtu asiyekuwa na uchungu wa nchi hii (Rostam) wakawa wanamuuliza maswali ya kejeli mwakyembe kisa njaa zao ambazo kila nikiwaona njiani wanaona aibu na hili la rostam kuondoka ni aibu ya pili kwao kwa kumlinda na kalamu zao mtu mchafu na mwizi na mwenye miguu mitatu huko nje kama alivyosema mwakyembe.

sasa leo yanatimia je hao waandishi mtaandoka na nyie kisa mliajiliwa na mtanzania au mtafia hapa na huyo mwakyembe?

kuna siku itafika watu kama nyie tutawapiga bastola maana ndio mliandika uongo na hamkusema kweli kuwa rostam ana passport tatu ingali mkijua
 
Rostam aziz, moja ya watu hatari kwa taifa, aliechangia kuyumbisha nchi na serikali, the masterminder of dubious deals crime, forgery and dirty money, anajiandaa kutoroka na mabililion ya watanzania. Wazalendo mko wap? I cant wait!
 
Rostam Aziz ameziandikia bank za CRDB na NMB ya kutaka kufunga account zake na kutaka kuhamisha fedha hizo katika nchi ya Malaysia, tukio hili lilifanya mameneja wa bank hizo kuomba muda wa kupitia na uhamuzi huo kabla ya kuruhusu kufungwa kwa akaunt hizo, kwani kutokana na kiasi kilichomo ndani ya akaunti hizo ni lazima wapate kibali ya kufunga na kuhamisha kutoka BOT.

Lakini wachambuzi wa mambo wanaliona ni tukio la bwana Rostam kuondoka nchini na kuelekea malaysia, hivyo basi kama Tanzania kuna chochote cha kumuuliza au tunataka kufahamu kutoka kwake ndio wakati muafaka sasa la sivyo zile tuhuma za wizi wa fedha za EPA kupitia Kagoda ndio ushahidi wake unapotea hivyo

Nina mashaka na hii habari, imepatikana wapi?, we unavyomjua rostam ni mtu wa kutaka kufunga accounti yenye fedha nyingi?, ameshindwa kuhamisha zote akabakiza laki ya kufia humo mpaka account iwe domant?, hakuna ukweli hapa labda sio Rostam Aziz ni Rostam mwingine! kasome vizuri barua na ikibidi weka copy hapa ndio utanishawishi!
 
Aondoke. Lakini laiti tungelikuwa na Rais "Msafi" angelimtia hatiani mtu huyu, mali zake zingelikamatwa na kunadiwa kabla ya kutokomea Malaysia. Maskini Tanzaniaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!

Yaani namkumbuka Hayati baba wa Taifa - J. K. Nyerere.

Kwanza huyu hata hii kauli asingeliitoa kwani tayari kanyanganywa Passsport na kila kitu ili asiondoke.

Lakini hapa tena usishangae akafanyiwa sherehe kubwa tu IKULU kumuaga rasmi.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Alipokuja Tanzania alikuwa na Pesa kiasi gani? na amefanya biashara gani mpaka ameweza kuwa na hizo pesa? Je Amelipa kodi zote ki halali.
 
Nina mashaka na hii habari, imepatikana wapi?, we unavyomjua rostam ni mtu wa kutaka kufunga accounti yenye fedha nyingi?, ameshindwa kuhamisha zote akabakiza laki ya kufia humo mpaka account iwe domant?, hakuna ukweli hapa labda sio Rostam Aziz ni Rostam mwingine! kasome vizuri barua na ikibidi weka copy hapa ndio utanishawishi!
mkuu ni kweli waweza kuwa na mashaka na habari hii lakini mwishoni itakuwa hii hii na ku-reflect ukweli huu kwa >95%.

Kikubwa hapa ni muda tu nao utatwambia kila kitu
 
Yote haya ameyasababisha Jk mwenyewe kwa kuyabeba majizi ya rasilimali zetu,inauma sana kwa kweli jinsi wanavyotuibia pesa zetulakn huu mpango upo chini ya mkulu hili lipo wazi
 
Back
Top Bottom