Rostam ajipanga kuikimbia Tanzania; kutimkia Malaysia

Anyang'anywe passport mapema kabla na apandishwe kizimbani kujibu tuhuma kama anazo.
 
Shamba la bibi hili. Mwacheni achume mpaka achoke, sisi wa TZ kazi yetu ni kupiga kelele...
 
Aende yeye mwenyewe kama alivyokuja TZ, fedha zetu asiruhusiwe kwenda nazo!!
 
Inawezekana kabisa kuwa pesa aliyonayo ni nyingi kiasi kwamba benki hizo zilikuwa zinategemea pesa hizo katika mzunguko mzima wa biashara ndio maana wanataka kwanza wakae wajue cha kufanya.
Ningekuwa na uwezo nikazitaifisha pesa zote na kumuacha aende zake tu maana ni tishio kwa maendeleo ya nchi na wananchi wake.
 
Teh teh teh teh teh tumwombe msamaha maana akiondo anaondoka na robo tatu ya pesa zote nchini. Lol !
 
Du, CRDB Bank PLC ilifungua account ya yale makampuni yaliyohamishiwa pesa iliyokwapuliwa kwenye akaunti ya EPA kule BOT!

Nasikia aliyedhamini ufunguzi wa akaunti hizo ni Yusufu Manji.
 
Tuseme ukweli kwa mtu makini kama Rostam hilo angelistukia leo? kwamba agizo la BOT lilivyotoka naye akaanza pilika za kufunga akaunti zake..sikubali kirahisi.Kwa sababu yeye mwenyewe ana makampuni kadhaa yanayo-operate hapa nchini na inawezekana kabisa anazo fedha kiasi kidogo (kwa viwango vyake) kwa ajili ya kuendeleza shughuli zake - hawezi kuzihamisha.

Hawezi kuwa amestuka leo,kama ni kuzihamisha tayari alishazihamisha siku nyingi kama alivyohamisha hisa za Vodacom kwenda South africa.Tusisahau alipokuwa anaongea na waandishi wa habari 2010 kumjibu Mengi kuhusu tuhuma za kuwa na account nje ya nchi - alisemaje? "Nampa changamoto Mengi aseme na yeye kama hana akaunti nje ya nchi"
 
Kuna mzee mmoja ni maarufu sana siwezi kumtaja (ni mmoja wa maafisa wa Usalama wa Taifa) kwa usalama wangu maana natumia ID yangu orginal pamoja na Avatar ya picha yangu halisi..... alichoniambia kwamba Rostam Aziz ni Jasusi la CIA na yuko very protected, alikuja hapa kwa lengo maalum na kazi aliyoifanya ameshaimaliza na aliletwa na Marehemu Kambona....
siwezi endelea zaidi............
 
Rostam Aziz ameziandikia bank za CRDB na NMB ya kutaka kufunga account zake na kutaka kuhamisha fedha hizo katika nchi ya Malaysia, tukio hili lilifanya mameneja wa bank hizo kuomba muda wa kupitia na uhamuzi huo kabla ya kuruhusu kufungwa kwa akaunt hizo, kwani kutokana na kiasi kilichomo ndani ya akaunti hizo ni lazima wapate kibali ya kufunga na kuhamisha kutoka BOT.

Lakini wachambuzi wa mambo wanaliona ni tukio la bwana Rostam kuondoka nchini na kuelekea malaysia, hivyo basi kama Tanzania kuna chochote cha kumuuliza au tunataka kufahamu kutoka kwake ndio wakati muafaka sasa la sivyo zile tuhuma za wizi wa fedha za EPA kupitia Kagoda ndio ushahidi wake unapotea hivyo

Mkuu, JF sio sehemu ya porojo wala kijiwe cha mbege! Kwa hiyo unapoleta data zako humu JF kwa Great Thinkers lazima uwe na facts za kutosha.

Sio kuokota maneno mitaani na kwenye magazeti ya udaku ndio ushahidi wako..

Ebu weka hiyo barua ya Rostam Aziz, humu JF tuione ndio tujadili zaidi ya hapo tutakuwa tunajadili umbeya!
 
yaani jamaa na mchuzi mpaka benki zinajishauri? huyu jamaa kweli ametushika...
 
Rostam Aziz ameziandikia bank za CRDB na NMB ya kutaka kufunga account zake na kutaka kuhamisha fedha hizo katika nchi ya Malaysia, tukio hili lilifanya mameneja wa bank hizo kuomba muda wa kupitia na uhamuzi huo kabla ya kuruhusu kufungwa kwa akaunt hizo, kwani kutokana na kiasi kilichomo ndani ya akaunti hizo ni lazima wapate kibali ya kufunga na kuhamisha kutoka BOT.

Lakini wachambuzi wa mambo wanaliona ni tukio la bwana Rostam kuondoka nchini na kuelekea malaysia, hivyo basi kama Tanzania kuna chochote cha kumuuliza au tunataka kufahamu kutoka kwake ndio wakati muafaka sasa la sivyo zile tuhuma za wizi wa fedha za EPA kupitia Kagoda ndio ushahidi wake unapotea hivyo

sema yote kuwa

1. theluthi ya fedha zilizoko uko benki ni za Rostam
2. kuwa akine kimei walifunga safari kumfuata ughaibuni kumuomba abadilishe uamuzi wake akakataa
3. alichowasadia ni kuwa atazitoa fedha kwa awamu
4. anai-ondoa na kampuni yake ya caspian ambayo makao yakemakuu ni uarabuni
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom