Rostam Aishtaki Mwanahalisi

Hapa ni pazuri nafikiri tunaelekea kwenye ushindi watanzania tumechoka kumlipa FISADI pesa kila siku.

Mwahalisi kuguswa ni kugusa watanzania.

Sijui kama huyo Rostam amekurupuka maana ukiangalia toleo analo lilalamikia ni la muda mrefu huenda amekaa na wanasheria na majaji na washauri kibao kuona jinsi watakavyo weza kulishitaki gazeti hilo!
Pia inasekemekana Mwakeyembe hua analiandikia gazeti hilo na pia alivujisha baadhi ya siri ya tume kwenye gazeti hilo kabla ya kuwasilisha bungeni!
Sidhani huyo Rostam atakuwa punguani kiasi hicho pamoja na ufisadi wake anajua anacho kifanya!
HIVI SIMBA MWENYE NJAA AMEKWENDA KUWINDA NYAMA AMEANZA KULA GHAFLA UNAMCHUKULIA NYAMA KUTOKA KINYWANI MWAKE!UNATEGEMEA NINI!!!


Waswahili walisema mwenyezi mungu akupe nini? Hapa tumekaa mkao wa kula tu, ngoja mambo yaanze ameyataka mwenyewe.
 
Tutasikia Mengi Na Mazito Maana Kule Sasa Ndio Mbichi Na Mbifu Zitajulikana.....tujue Uhusiano Wake Na Rdc Na Dowans Na Kwa Nini Yeye Huwa Mbelembele Kwenda Hazina /bot Kuchukua Malipo Ya Dowans ............etc....
 
Anajikaanga kwa mafuta (fedha) yake mwenyewe. Ila kuna uwezakano akiona mambo yanaenda sivyo akafuta kesi..... lets wait and see...
 
Kutapatapa huku ni LAANA ya maelfu ya Watanzania walioathirika na wengine kupoteza maisha kutokana na vitendo vyao vya kifisadi. Tutasikia na kuona mengi mwaka huu.
 
A wakeup call for Journalists to adhere to responsible and accountable journalism...

I believe in innocent until proven guilt and since RA has opted for court, we will get chance to hear evidences from both sides.

Only time will tell.
 
Okay! now he is talking, sasa cha muhimu hapa ni kwa Mwanahalisi kwenda naye kwenye sheria, ili ukweli usemwe wazi ninasema haitakuja tena nafasi kama hii, kama ikibidi tuwasaidie wenzetu wa huko gazeti la Mwanahalisi kwa hali na mali, ili hii ishu ifike mahakamani ili nyani akomwe mchana,

Wakuu wa Mwanahalisi, hapa tuko ukurasa mmoja wakuu huyu Patel ni kukutana naye mahakamani tu na apewe ukweli wa uovu wake, upo mwingi sana, labda tuanze kuwasogezea ushahidi pole pole,

wananchi hatuwezi kutishiwa nyau na mafisadi...!

KAKA? Hapa nakuunga mkono kabisa, ni muhimu kuanza kuwasogezea ushahidi polepole maana tukiwaacha mwanahalisi wakawa watoto wakiwa tutakuwa tunajimaliza na kuifanya vita hii kuwa ngumu na MAFISADI wataendelea kutamba.
 
ushindi mwingine wanukia JF tuwape sapoti ya nguvu Mwanahalisi & co fisadi litajikaanga tu
 
Ni kweli, hapa tunatishiwa nyau!

Ukweli ni kwamba MwanaHalisi walinukukuu (na kutoa tathimi yao) taarifa ya Kamati Teule ya Bunge kuhusu Kashfa ya Richmond, iliyoongozwa na Mhe. Harrison Mwakyembe, Mbunge wa Kyela.

Bunge limeona kwamba alichotaka kukisema Rostam bungeni hakikuwa na uzito wala mantiki. Sasa mfa maji huyu anatapatapa, anaamua kwenda kuwazuia MwanaHalisi kuandika, jambo ambalo ni kazi yao.

Kipengele cha pili cha mashtaka yake ni kuweka "temporary injunction" kwa MwanaHalisi wasiendelee kuandika habari za Rostam wakati kesi ya msingi iko mahakamani. Huu ni ufisadi.

Kwanza, zuio hilo linakwenda kinyume na Katiba; Haki ya Kufanya Kazi na Haki ya Kutoa Maoni. Sidhani kwamba nahitaji kunukuu vifungu husika vya katiba.

Wanasheria wa MwanaHalisi (kama mnasoma hapa) tumieni strategy hii kwa upande wa utetezi ili zuio hilo litupiliwe mbali. Ukweli lazima uandikwe, ujulikane. Na MwanaHalisi wasizuiwe kufanya kazi yao.

./Mwana wa Haki
 
Kama kawaida nimeridhishwa sana na harakati zinazofanywa na JF kwa ujumla katika kupambana na MAFISADI na mafanikio tumeyaona. Kishajiweka hadharani tuanze kazi.
 
RA anakosea kushtaki magazeti anatakiwa awashitaki JF na wanachama wake wote maana ndiyo source of information zote zilizo ktk magazeti. Anatakiwa aseme hivi JF wanilipe billioni 3 pia front page iwe na thread 50 zinazoniomba radhi like "Tunakuomba radhi RA" by Ufunuo.
 
Mahakamani ndipo mwanahalisi watakapo jitetea na kusema habari zingine tumezipata Jambo forums ndipo Jaji atakapo sema waleteeni jambo forums mahakamani!!
 
Actually, mimi ninamsupport Rostam kwenye hili. Media Tanzania imejaa ma rottweiler journalists na sidhani kuna ubaya mtu ukiona umekashifiwa ukashitaki

Sasa kama Rostam ni fisadi au la so far hakuna ushahidi wowote ambao umewekwa mbele ya vyombo vya sheria ambao umeconclude kuwa ni mla rushwa etec

As much as ninazo doubts zangu juu ya Rostam i wouldnt like it kuona anahukumiwa na vyombo vya habari badala ya mahakama huru

Najua ni unpopular opinion humu JF lakini nimoeona bora nichukue msimamo tofauti nanyi

Maana kama ndio hivyo basi JK naye ni mla rushwa au tuseme ashitakiwe kwani impression ni kuwa anaweza kuwa guilty by association. Sasa ushahidi uko mbele ya mahakama gani?



 
Asalamu alaykum.

Mimi naona Rostam anataka kujimaliza sasa na lengo lake ni kutaka yale yanayoanikwa magazetini yasianikwe lakini sio mwanahalisi peke yake wanaoandika mambo ya Richmond na uovu wa rushwa ni magazeti mengi tu sasa atawashitaki wahariri wote? au atashitaki makampuni yote ya magazeti pamoja na wamiliki?
Naona anachukua tabia za Amani Karume kulishitaki gazeti la Dira na akalifunga kwa kuwa linaandika uovu wake na familia yake wanavyojikusanyia mali.

matokeo yake gazeti limefungwa kesi wameihukumu wanavyotaka wakishirikiana na huyo fatuma karume wao gazeti limefungwa na hayo mambo hayaandikiki tena maana hakuna gazeti mbadala zanzibar watu wanategemea magazeti ya huko bara. any way wache tuone atakavyojimaliza huyo bwana hindi.
 
Actually, mimi ninamsupport Rostam kwenye hili. Media Tanzania imejaa ma rottweiler journalists na sidhani kuna ubaya mtu ukiona umekashifiwa ukashitaki

Lakini hizi media hazijaanza haya mambo juzi, sasa tumeshuhudia kwa mwaka wa pili mfululizo habari za namna hii hii .. na pale tunapotaka kudharau taarifa hizo (za media) .. ndipo tunaposhtuka na kukuta tumeshalizwa!

Yeye kama raia wa kawaida ana haki ya kwenda Mahakamani kuombwa kusafishwa, lakini kwa mtazamo wangu "it's too late"!Ameshachafuka sana! Na ninavyojua "Hali Halisi Publishers" siku zote wamekuwa wakiombea kupelekwa mahakamani ili wakamwage kila "kitu"! Na sasa RA amejitoa muhanga!!

RA ni mvivu wa kusoma, na hafahamu mambo kiundani! Ni kama yule "mwingine" aliyesema kuwa kwenye hii "ripoti" wameweka magazeti ya "udaku" alipoombwa kuthibitisha akashindwa! mwisho wa siku ikagundulika hakuisoma ile ripoti bali alikurupuka tu!
 
Huku ndiko ukweli utapatikana. Hata hivyo nina hofu na muhimili wa sheria wa nchi yetu, mara nyingi sana wanaopata haki (hata kama kikweli haiwastahili) ni wale wenye uwezo wa kutoa pesa, kifupi mahakama zetu zimeharibika na watendaji wachache sana wanasimamia kikamilifu haki za wanyonge. Nafikiri unawakumbuka kina Lugakingira na Mwalusanya, kama kesi hii itashikwa na jaji makini na anayeangalia haki hakika RA ataumbuka na hivyo kufanya umma utambue maovu yanayofanya na wale wote walioaminiwa madaraka.

RA hajakashifiwa kama anavyotaka kutuaminisha, anachotafuta kitajulikana, tusubiri.
Hata hivyo nimpongeze kwai amekuwa ni fisadi wa kwanza kwenda mahakamani kuwashitaki wapiga filimbi, wenzake walitishia wakaona maji marefu wakatulia na sasa yeye kayavaa, labda anategemea atapata ushahidi mzuri toka kwa SR


UKIPENDA KATAA, LAKINI INAWEZEKANA SISIMIZI KUMUUA TEMBO
 
Sijui kama huyo Rostam amekurupuka maana ukiangalia toleo analo lilalamikia ni la muda mrefu huenda amekaa na wanasheria na majaji na washauri kibao kuona jinsi watakavyo weza kulishitaki gazeti hilo!
Pia inasekemekana Mwakeyembe hua analiandikia gazeti hilo na pia alivujisha baadhi ya siri ya tume kwenye gazeti hilo kabla ya kuwasilisha bungeni!
Sidhani huyo Rostam atakuwa punguani kiasi hicho pamoja na ufisadi wake anajua anacho kifanya!
HIVI SIMBA MWENYE NJAA AMEKWENDA KUWINDA NYAMA AMEANZA KULA GHAFLA UNAMCHUKULIA NYAMA KUTOKA KINYWANI MWAKE!UNATEGEMEA NINI!!!

Usije ukakimbia hapa maana hukawii kuingia mitini wewe na dogo Kada .Pia ua kakosea na wame muingiza mkenge maana wamechoka naye .Toleo moja tuta mwambia mwanasheria wa Mwana Halisi afumue mambo kibao .Yaani dots ziwe connected then tuanze kumnyama Mnyama .
 
Hawa mafisadi wa bongo ndio mikwara yao kila anayetuhumiwa lazima ajifanye anataka kwenda mahakamani baadae issue ikichachamaa tunaona mtu mzima "chali" miguu juu. Si unamuona mzee wa vijisenti, Balali na yule mgosi wa hazina "kijivu mgonjwa" alijifanya anam-consult lawyer wake kiko wapi katulia nae anasubiri muda wake wa kuonana na pilato....Let this gabachori aende huko kortini then asikie kitu ya moto... Hapendwi mtu hapa!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom