Rostam acha siasa - Cheyo

Cheyo na mrema ni wazee waliochoka kimawazo jamani wanaJF tusipoteze muda kuwajadili hawa watu.................................
 
Cheyo nae sio msafi kiivo ni mnafiki kwani ni Mpinzani anaepingana na wapinzani wenzake na sio MBOGAMBOGA(Kijani) mie naona anasingizia kuongea ayo ili tupate kumwamini.Amsubiri Rais arudi aende akampe ushauri aache unafiki
 
Nakumbuka kuna wakati nyumba ya Cheyo iliuzwa kwenye mnada wa hadhara kwa kushindwa kurejesha mkopo wa benki, lakini baadaye alirejeshewa nyumba hiyo baada ya mtu mkubwa kuingilia kati: Maswali yangu, huyo mkuu aliyoingilia kati ni nani? Hivi kuna uhusiano wowote kati ya sakata hilo na uenyekiti wake wa hesabu za serikali?
 
Rostam kuacha siasa ni vigumu sana. Utajiri mkubwa alionao unatokana na siasa. Anajua kuitumia siasa ili ajiongezee mali, kwa hiyo kuacha kwake siasa ni sawa na kumwambia apate hasara katika biashara yake. Kwake yeye siasa ni biashara
 
Huyu jamaa ni mhujumu uchumi.. Anastahili kufungwa jela bila mjadala.

Angalia januari makamba anavyopigia debe mitambo ya dowans.. Hii ni aibu kubwa sana.. Ila nafurahi kuwa mahakama imesimamisha mijadala yote na tanesco.

Rostam akifungwa na jk naye afungwe pamoja na chenge na wote waliohusika kuhujumu uchumi.
 
NI HAPA KWE2 PEKEE AMBAPO MHE ANATUMIA NAFAC YAKE KISIASA KUHUJUMU TAIFA (ref RICHMOND- DOWANS) HALAFU WENYE NCHI ( WAATHIRIKA) WANAMPIGIA MAGOTI ETI AACHE SIASA! ! SHAME ON U ! VYOMBO VYA DOLA VIKO WP?
 
halafu huyu dogo rost-ham anadai kutumia ile mentality ya kuwa silence is stick to your enemy,bt what i belive ngoja tuone ataongea tu mana sauti ya wengi ikiongea atakuwa hana jipya tena.
 
Maelezo ya Mh. Cheyo yanaacha maswali mengi makubwa kuliko majibu.

1. Ni sheria gani Tz inayo kataza wafanyabiashara kuwa wanasiasa, maana nijuavyo mimi kuna wafanyabiashara kibao ambao mi wanasiasa kutoka vijijini hadi Taifani leo nchini Tz, tukianzia na yeye unless tumwombe Mh. Cheyo afafanue Mfanya Biashara ni nani kwa mujibu wa hiyo sheria ninayoisubiri au Kanuni ya Bunge. Aidha ni kwa nini wakati wa kutangaza nafasi za kugombea, sifa ya kuwa mfanya biashara na definition yake isiwekwe waziwazi kuwa ina m- disqualify mgombea? Je anajua kuwa hata kuwekeza katika kampuni fulani au kuwa na hisa au kuchukuwa mazao ya shamba lako na kuuza n.k pia ni kufanya biashara, vitu ambavyo Mawaziri, Wabunge , Madiwani wengi tu wako katika kundi hilo?

2. Anaonyesha kuwa watu (wengine) wana machungu na Rostam; je yeye Cheyo, naye ana hayo machungu (naomba kujua position yake)

3. Ukiendea kwenye media na kusema waziwazi kuwa ungekuwa wewe 'ingekuwa OUT'; sasa tunaomba Cheyo utamke waziwazi makosa ya Rostam na siyo kusingizia uchungu walionao watu wengine au kutunga kosa (maana sijaona sheria mimi ya kukataza kwa mwanasiasa na pia mfanya biashara).

Mtu haukumiwi kwa hisia tu za watu wengine na Cheyo kama kiongozi wa chama Kitaifa hawezi kusema tu 'OUT bila kuwa na uthibitisho fulani wa makosa ya Rostam. Na endapo hilo ndivyo, je pendekezo lake la 'Out' sijui kutoka katika Chama au katika uongozi linatosha? Kwa nini asiseme kuwa angekuwa yeye angemfikisha katika vyombo vya sheria?

Natamani ningekuwa mwandishi wa habari tumrejeshe Cheyo na kumpa nusu saa kwenye Conference ajibu hizi hoja zangu tatu waziwazi! Vinginevyo nitarudi hapa na kutoa tafsiri yangu ya kile alichokuwa anajaribu kukifanya!
 
Si kweli, kwa nafasi ambayo yeye alimteua (mweka hazina CCM) alimtoa tena kwa aibu kubwa, lakini ninyi wananchi mmemchagua kuwa mbunge wenu mlitaka afute ubunge wake? kwa nini mnaruka wajibu wenu? kwa vyeo vyote vya Rostam wananchi wakitaka wanaweza kumtoa.

Mkuu unachosema kina ukweli fulani. Lakini je ni kweli wana Igunga walimchagua Rostam? NI kweli JK alimfukuza RA uweka hazina, au "alimfukuza"? Yeye ndiye mfadhili mkuu wa chama na ndiye aliywapa pesa za kugombea ubunge, na ni mmoja wa wachangiaji wakubwa wa kampeni ya urais.

JK ana madaraka yote kikatiba (ya chama na ya jamhuri) ku-deal la RA problem.
 
Wacha wao wa enjoy na maisha yao
 

Attachments

  • baba andunje.jpg
    baba andunje.jpg
    55.9 KB · Views: 36
Rostam kwa kosa la kutudanganya watanzania kuwa huijui dowan na dowan mwenyewe akasema kuwa wewe ndio ulimfuata na akakupa nguvu ya kisheria kuwa mmiliki wake,Unatakiwa ujiuzulu na utuombe radhi watanzania.Pia jk nae alisema hajui lakini dowan na mwanahalisi walichapisha habari kuwa jk alionana na adawi huko uarabuni na adawi mwenyewe akakupongeza Je jk ni kweli ulikuwa humjui adawi au ulitudanganya watanzania.
 
Si kweli, kwa nafasi ambayo yeye alimteua (mweka hazina CCM) alimtoa tena kwa aibu kubwa, lakini ninyi wananchi mmemchagua kuwa mbunge wenu mlitaka afute ubunge wake? kwa nini mnaruka wajibu wenu? kwa vyeo vyote vya Rostam wananchi wakitaka wanaweza kumtoa.
JK alimpigia debe IGUNGA? Hiyo ndiyo ghalama ya demokrasia, wengi wape haijalishi ni akina nani na wanaupeo gani. kuna maeneo nchini kauli ya rais ni amri, kwa kumpigia debe wakamchagua hatushangai.
 
Mwenyekiti wa chama cha (UDP),John Cheyo ,amemtaka Raisi JK kufanya maamuzi magumu dhidi ya maswahiba wake ambao wanaliingizia taifa hasara katika masuala mbalimbali hasa tatizo la mgao wa umeme unaondelea nchini.Akizungumza na waandishi wa habari jana Cheyo alimtahadharisha Raisi jk kuweka urafiki kando na mfanya biashara na mbunge wa Igunga RA, kwani ameliletea taifa hasara kutokana na kuingia katika mikataba mibovu.
 
Anasema angekuwa yeye angemwambia "OUT"!..kwa maana kwamba aondoke kwenye chama mara moja!

....ahamie sisiemu akatoe suluhisho hilo! Kama wenye nae sisiemu wanamwogopa sembuse yeye Cheyo?
 
Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa ccm anatakiwa kuweka heshima ya chama hicho kwa kufanaya maamuzi mazito ikiwemo kumfukuza uanachama mbunge huyo."RA ni nani?kila mkataba yenye utata ya Richmond,EPA,Dowans yumo wapi tunalipeleka taifa na maisha ya wananchi wake,alisema Cheo.
 
cheyo hana influence yeyote kwa hiyo Jk HANA HAJA YA KUMJIBU.
Labda angeongea mtu influencial kama Dr. Slaa hapo ndio
 
Si kweli, kwa nafasi ambayo yeye alimteua (mweka hazina CCM) alimtoa tena kwa aibu kubwa, lakini ninyi wananchi mmemchagua kuwa mbunge wenu mlitaka afute ubunge wake? kwa nini mnaruka wajibu wenu? kwa vyeo vyote vya Rostam wananchi wakitaka wanaweza kumtoa.

RA ndiye aliyeomba kuacha uwqeka hazina kutokana na kutingwa na kazi na ndiye aliyempendekeza Amos Makala, na si kweli JK kuwa ndiyealiyemuondoa
 
Hivi Cheyo na Biashara zake za Ng'ombe, Ofisi yake ya pale Ubungo plaza na SIASA zinakaaje,mbona anamshauri RA aache SIASA afanye Biashara, Huyu Mzee HAYAWANI KWELI KWELI
nakupa tano huyu mzee mnafiki hana lolote la maana mambo yote mawili aliyoongea pumba tupu nafikiri wananchi wa bariadi hawana shida wanazopata kama wananchi wengine shida yao ni kumshauri rostam ajiuzulu na kuiponda chadema.nikikumbuka nyuma mtikila na mengi walivyojibiwa na rostam siku si nyingi huyu mzee ataanikwa na njaa zake.
 
Back
Top Bottom