Rostam aanza kutikiswa

Hivi kuna haja ya kuendelea kumjadili huyu...........status yake wote tunaifahamu.............hashikiki kwa sasa....kumtoa huyu si rahisi lakini siku zake zinahesabika.......miaka mitano ijayo ikiisha chochote kinaweza kutokea huyu RA mwisho wake naona utakuwa mbaya sana kwa jinsi anavyoichezea nchi hii.
 
kila mtu ana haki ya kugombea iwapo tu atakuwa ametimiza masharti yaliyowekwa
 
Nimethibitishiwa na mtu wa umoja wa vijana kwamba yuko asilimia 100 kwamba Rostam hatagombea ubunge mwaka kesho.

Kama hii habari sio ukweli basi niumbueni mwakani. Kinachofanyika sasa ni RA kutafuta mtu wa kumrithi; ndio siasa za TZ hizo, wenye nchi kurithiana kazi utafikiri nchi yao wenyewe.

Tunapoteza muda bure kujadili hii thread maana Rostam sio mgombea mwakani.
 
i656_rostam2.jpg


  • Akutana na kigingi Igunga
ZAMA za mbunge wa Igunga, Rostam Aziz kushinda kinyang'anyiro cha ubunge bila kupingwa ndani ya chama chake, sasa zimefikia tamati, imefahamika.

Anayejitosa kumaliza himaya ya Rostam ni Deusdedit Mtambalike, mkuu wa wilaya wa zamani na mwanasiasa mwenye msimamo usioyumba.

Akizungumza na MwanaHALISI kwa njia ya simu kutoka Igunga, mwishoni mwa wiki, Mtambalike alithibitisha kujitosa katika kinyang'anyiro jimboni Igunga katika uchaguzi mkuu ujao.

Amesema, "Katika hili, hakuna mwenye uwezo wa kubadilisha msimamo wangu."

Akiongea kwa kujiamini, Mtambalike alisema, "Nagombea. Huyu bwana amezoea vya bure. Nataka hela zake zitumike vizuri," alisisitiza. Alisema tayari yupo Igunga kutekeleza kile alichokiita "Mkakati wa kuwaokoa wana-Ingunga."

Rostam aliingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 1994 katika uchaguzi mdogo uliotokana na kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Charles Kabeho.

Tokea wakati huo, Rostam amekuwa akijijengea utamaduni wa kupita bila kupingwa katika uchaguzi, ndani na nje ya chama chake.

Mtambile ambaye ni hasimu mkuu wa kundi la watuhumiwa ufisadi, amekuwa akitajwa kuwa ni mwiba mkubwa kwa Rostam, kutokana na kukubalika kwake ndani ya Igunga.

Mbali ya kuwa ni mwenyeji wa huko kwa asilimia mia moja, Mtambalike ana uwezo mkubwa wa kujieleza na kujenga hoja, ikiwamo kuzungumza kwa ufasaha lugha ya Kinyamwezi ambayo ni maarufu katika eneo hilo.

Akizungumza kwa kujiamini, Mtambalike alisema, "Mwaka 2000 nilitaka kugombea, akaniomba nimuachie. Akasema hatagombea tena katika uchaguzi wa mwaka 2005. Nikamkubalia," alisema.

Alisema, "Lakini ilipofika mwaka 2005, Rostam akawachezea wananchi wa Igunga baada ya kubadilika na kuamua kuchukua fomu za kuwania nafasi hii. Safari hii, nimekuja kufuta umungu mtu wa bwana huyu."

Anasema amejipima na ameona kuwa anazo sifa zote zinazohitajika na kwamba yeye ni zaidi ya Rostam. "Unazungumzia sifa za uongozi, mimi ninazo nyingi. Mimi ni mwadilifu na mwaminifu kwa taifa langu. Hii ni sifa kubwa ya kukabidhiwa jukumu hili," anasema.

Mtambalike anasema, tofuati na miaka ya nyuma, uchaguzi wa mwaka ujao, utakuwa mgumu kwa Rostam kutokana na wana-CCM wengi kuutamani ubunge wake.

"Safari hii, mambo hayatakuwa mazuri kwa ndugu yangu. Tuko wanachama wengi wa CCM tuliojitokeza kutaka nafasi hii," alisema.

Alipoulizwa amejiaandaa vipi kukabiliana na kigogo huyo aliyekwisha jigamba kuwa miongoni mwa "wafanyabiashara wakubwa," Mtambalike alijibu haraka, "Nimejiandaa vya kutosha. Sina fedha, lakini nina watu."

Alisema, "Hapa ndiyo nyumbani kwetu. Nimezaliwa hapa. Nimekulia hapa. Karibu wapigakura wote wananifahamu, nami nawajua na kuwaheshimu. Sasa unataka nijiandae na nini zaidi ya kuwa mwadilifu," alijigamba.

Alipong'ang'anizwa kwamba Rostam anajua iwapo yeye Mtambalike atagombea ubunge katika jimbo hilo alisema, "Bila shaka anajua."
Alipoulizwa Rostam anajuaje wakati yeye hajamwambia, Mtambalike alisema, "Nakwambia anajua. Anajua kwa sababu, wapambe wake wako hapa na wananiona napita vijijini kukutana na marafiki zangu kwa ajili ya kuweka mambo sawa."

"Nakwambia anajua, lakini hana la kufanya. Hapa ninapozungumza na wewe niko Igunga, tena vijijini kabisa nakutana na marafiki zangu. Watu wake wako hapa, wananiona na wengine nimewaambia hata mimi mwenyewe, kwamba katika uchaguzi ujao, hapa hapatatosha," alisema.

Taarifa kutoka Igunga zinasema, hali ya kisiasa ya Rostam imeanza kuwa ya mashaka katika siku za hivi karibuni, hasa baada ya Kanisa Katoliki kusambaza waraka unaotoa wito kwa wananchi kujadili wale wanaotaka kuwachagua kuwa viongozi wao.

Kutajwa kwa Rostam katika mahusiano mbalimbali ya biashara na mikataba yenye utata nchini, kunaweza kuzaa maoni toauti katika mijadala juu ya wanaotakiwa kuchaguliwa kuwa viongozi.

Rostam amewahi kunukuliwa akisema hatagombea tena ubunge wa Igunga, ingawa taarifa za hivi karibu zimesema amebadili msimamo wake huo na kwamba tayari ameweka makakati wa kutetea kiti chake.

Mtu mwingine anayetajwa kugombea ubunge Igunga, ni Peter Kafumu, Kamishna wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini.

BADO NAENDELEA KUSEMA CCM INAOKOLEKA KWA SASA huu ndio mwanzo na bado cha msingi ni fikra na mapinduzi ndani ya mioyo yetu.

Rostam ni binadamu kama wengine na anaweza kushindwa vile vile sababu yeye si Mungu.

Hongera Mtambalike kwa kuimarisha mapambano dhidi ya vita hii tuliyopo.
 
Haya ni makati ya siasa Mbovu za karne ya ujima..!! Baada ya Miaka 5 kuanzia sasa ,Hakuna mtanzania atakaye ruhusu ujinga wa serikali ya JK.
 
Nimethibitishiwa na mtu wa umoja wa vijana kwamba yuko asilimia 100 kwamba Rostam hatagombea ubunge mwaka kesho.

Kama hii habari sio ukweli basi niumbueni mwakani. Kinachofanyika sasa ni RA kutafuta mtu wa kumrithi; ndio siasa za TZ hizo, wenye nchi kurithiana kazi utafikiri nchi yao wenyewe.

Tunapoteza muda bure kujadili hii thread maana Rostam sio mgombea mwakani.

Tunakubaliana nawe kiasi fulani lakini ukweli wana Igunga kwa asilimia 100 wanafahamu kuwa Peter Kafumu ndie chaguo la RA ili baadaye amtumie kufanikisha malengo yake na RA atatumia nguvu yake yote kumnadi jamaa yule
 
Nadhani swala hapa sio RA kutikiswa bali ni wakati muafaka wa kufanya mabadiliko ili kupata mawazo mapya, kupata fikra mpya na kupata maono mapya yenye manufaa na faida kwa watanzania katika majimbo mengi ya ubunge. Hii nchi (pamoja na jimbo la Igunga) ni mali ya watanzania woote na kila mwenye sifa za kuchaguliwa anahaki ya kuchaguliwa. HAKUNA JIMBO LA UCHAGUZI LILILO MALI YA MTU FULANI.
 
ingekua igunga ni pemba hapo sawa maana wapemba uwape nini lakini ccm no bora wampe mbwa kura kuliko ccm bado watz tuna tatizo njaa zetu hatuiwezi akipewa fulana moja tu anasahau yote yatakayo pata ya miaka 5 ni viziwi vipofu mabubu
 
Rostam atashinda tu hilo halina ubishani ,kwanza huyu jamaa anajuwa kula na vipofu pili rangi yake ni kivutio kwa vipofu hao.amekuwa akiwajengea mambo mazuri na wengi wanafurahishwa na kazi yake Mungu amsaidie ashinde kipindi kijacho ili kuendeleza majukumu ya chama aliyopewa.
 
MMhm..
Labda wale wenye tamaa ya fedha... na hili ni la mtu binafsi zaidi na sio la kichama?
Maalim Seif kung'ang'ania uprez kwa miaka 15 sasa ana maana gani?

Hivi kibunago umemuona mtu mmoja tu ? hebu angalia hivi vizee katika bunge kuna wakati asatahafiru kusema ni kinya kuna wakati unahisi unataka kutapika ukiwangalia bado wamo tu mauti yatawakuta wakiwa ndani ya jumba la kuhubiri ubaya.lakini hawataki kupumzika na kucheza na vijukuu au kutupia hiyo pencheni yao mtu anamika 70 -85 anasubiri nini palipobki ni mauti tu hapo.
 
Rostam atashinda tu hilo halina ubishani ,kwanza huyu jamaa anajuwa kula na vipofu pili rangi yake ni kivutio kwa vipofu hao.amekuwa akiwajengea mambo mazuri na wengi wanafurahishwa na kazi yake Mungu amsaidie ashinde kipindi kijacho ili kuendeleza majukumu ya chama aliyopewa.


Duh !! babylon

Ndio umetuambia nini hapo labda uandike tena lol

Hivi kweli wewe ni mtanzania na unaeishi bongo? Na hata kama huishi bongo basi tueleze unajua anayo yafanya mshikaji wako RA ? ama unaishi planet nyingine. kama huishi bongo basi waonee huruma ndugu zako waliopo bongo maana ukiambiwa mikataba ambayo uncle wako ameifanya ungelia kuanzia leo mpaka x-mass

haya hebu tumwagie Data za ushabiki wako kwa fisadi
 
Duh !! babylon

Ndio umetuambia nini hapo labda uandike tena lol

Hivi kweli wewe ni mtanzania na unaeishi bongo? Na hata kama huishi bongo basi tueleze unajua anayo yafanya mshikaji wako RA ? ama unaishi planet nyingine. kama huishi bongo basi waonee huruma ndugu zako waliopo bongo maana ukiambiwa mikataba ambayo uncle wako ameifanya ungelia kuanzia leo mpaka x-mass

haya hebu tumwagie Data za ushabiki wako kwa fisadi

Huyu jamaa anatekeleza magizo ya wakubwa wa nchi sasa kumuhukumu peke yake ni kumuonea.kama ilivyo mkapa kuwa awachiwe na kupumzika kama alivyosema Rais Jk basi na jamaa achiwe afanye majukumu yake kwa wananchi waliomchaguwa ambao wengi wao wanamfurahia kwa msada wake anawapa.
 
swali lililopo mbele yetu? nani atamuidhinisha kugombea hicho kiti wakati RA ndio anachagua wagombea na kuwapitisha kwa kutumia pesa, labda Deusdedit Mtambalike aamue kugombea kwa tiketi ya vyama vya upinzani, ni matumaini yangu anaweza akashinda lakini sio kwa CCM hii iliyopo

Huyu ni njaa tu, angekuwa anataka kumuondoa rostam agombee kupitia CHADEMA
 
Hao kina mtambalike usikute wameshalipwa na huyo huyo RA ili ionekane wanamuandama kumbe ndo wanamsafishia njia ya kutoka salama. Sidhani kama RA anataka sana kuendelea kuwa ktk siasa hasa za bungeni so long kwa,mba yupo ktk CC ya chama dume inamtosha sana. Na kwa kuwa ameshaona aina ya ngoma ichezwayo anaweza akawa ameshatafuta wachezaji wake wa kulipwa wacheze ngoma kwa niaba yake.

Siasa za bongo unafiki mtupu. utakuta mtu anaongea mpaka povu linamtoka lakini moyoni ana lake jambo....

Mtambalike ninayemfahamu hawezi kuhongwa ni mtu mwenye msimamo.
 
Huyu Mtambalike ni mmoja kati ya wale watanzania wasanii na ambaye ametayarishwa na Rostam huyo huyo kuanza kupiga kelele. Wewe mtu mwenye nia thabiti na unayejua uwezo wako katika siasa na unataka kuingia kwenye siasa huwezi kuanza kwenda kuomba ruhusa kwa kiongozi aliyepo madarakani ili ugombee. Anasema alimwambia mwaka 2000 akasema amsubiri mpaka 2005 na yeye akakubali. Alikubali kivipi?? alipewa nini ili akubali?? alikuwa amejitayarisha kwa mwaka 2000? je 2005? je na mwaka kesho akiambiwa asubiri 2015?? huyu ni msanii wa ajabu na tumepoteza muda wetu kumjadili
 
Back
Top Bottom