Rose muhando aipasua ndoa ya alex msama

Status
Not open for further replies.

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
pix.gif

Na Mwandishi Wetu
Msanii nyota wa muziki wa Injili Bongo, Rose Muhando ‘anabeba’ mzigo wa lawama kufuatia kuwepo kwa mpasuko ndani ya ndoa ya Promota maarufu wa muziki huo nchini, Alex Msama na mtangazaji wa Kituo cha Redio cha WAPO FM, Laura Bonaventure, Risasi Mchanganyiko limesheheni data...

Chanzo cha habari hii kimepasha kuwa, ndoa hiyo ina ‘masiku kibao’ sasa ‘inapumulia mashine’ huku Rose akitajwa tajwa kuhusika na mgogoro wake.

Chanzo hicho kikaendelea kuweka ‘nje’ siri kuwa, chanzo cha kuwepo kwa ufa katika ndoa hiyo ni kufuatia mke wa Msama, Laura kuchezwa na machale kuhusu ukaribu kati ya mumewe na Rose Muhando kiasi cha kukosa amani kama siyo furaha.

Habari zinazidi kumwagika kwamba, hali hiyo ikashamiri, ikanawiri, ikafika mahali hisia za mwanamke huyo zikawa wazi na hivyo kuanza ‘kumsomea’ mashitaka mumewe akitaka maelezo kuhusu ukaribu huo.
Habari zaidi zinapasha kuwa, licha ya kujitetea bila ‘mwanasheria’, bado mke huyo akaweka ngumu kuelewa hali iliyosababisha kila mtu kuanza kuishi kivyake ndani ya nyumba.

“Hii hali ilifika mahali kila mmoja akawa kivyake ndani, Msama akashika hamsini zake, mkewe naye anakumbatia zilizobaki,” kilisema chanzo.
Kikaongeza: “Kubwa kuliko zote, kuna wakati Msama akipiga wimbo wowote wa Rose (Muhando), mkewe anazima redio au anapunguza sauti, moyo unamtuma kuwa, hisia zake zina ukweli.”

Habari zaidi zinasambaa kuwa, hata pale Msama anapokwenda Dodoma kwa shughuli za kikazi, mkewe hudhani ‘mista’ wake yupo ‘andapromisi’ na Rose hali ambayo imekuwa ikizidi kuvuruga ndoa hiyo.
Mambo yalipozidi kuwa mabaya, nyeti zinapasha, mke aliamua kuondoka nyumbani hapo na kwenda ‘kujichimbia’ sehemu moja jijini Dar es Salaam (Risasi linahifadhi jina kwa sasa).

UTETEZI WA WADAIWA
Kufuatia madai haya, Mwandishi Wetu alipiga ‘jaramba’ mpaka ofisini kwa Msama, Msama Promotion, Block 41, Kinondoni jijini Dar na kufanikiwa kuongea naye kwa kumpa ‘a e i o u’ ya ishu yake ambapo alipagawa kwa kuanza kutaka kujua ‘sosi’ wetu.

Alipokataliwa kutunza maadili, alisema mambo ya kifamilia yaachwe kwa wanafamilia, kwani ni jukumu lao kuweka sawa kwenye ‘korogesheni’ endapo mambo yataharibika.
“Mambo ya kifamilia yabaki kuwa hivyo, kama kuna tatizo linalomshirikisha Rose Muhando si kihivyo, hata wewe mkeo anaweza kukuuliza kuhusu mwanamke f’lani ukamwelewesha, akaelewa na mkaendelea na safari yenu ya maisha,” alisema Msama.

Risasi: Kwa hiyo ni kweli?
Msama: Nimeshakupa jibu kaka, mimi kwangu ni amani tu, hakuna wasiwasi wowote ule.
Aidha, Risasi likachanganya miguu kumsaka Laura, mke wa Msama lakini baadaye akapatika kwa njia ya simu ya kiganjani.

Kwa upande wake baada ya kupigwa ‘mashuti’ na Risasi alisema nyumbani kwake hakuna tatizo na wala hana kinyongo na Rose kisha papo hapo akamwomba Mwandishi amtwangie simu baada ya dakika tano, (eti) ana mgeni.
Mwandishi alizifuata sekunde kwa macho angavu hadi zilipotimu dakika tano, alipopigiwa tena, cha ajabu, akawa anakata simu.

Risasi halikuchoka, likamgeukia bingwa wa muziki wa Kwaito, Rose Muhando ambaye kwa ‘binafsi’ yake alisema tuhuma dhidi yake na Alex Msama ni maneno ya ‘wachovu’ wa kiimani, lakini akakiri kuwa karibu sana na Promota huyo kwa sababu za kikazi.

Alipobanwa kuhusu madai ya malalamiko ya Laura, Rose alisema anaapa kwa Mungu wake hakuna ‘malavidavi’ kati yake na Msama na Laura kwake ni wifi yake kwa kuwa Msama kwake ni kama kaka yake ingawa si wa damu moja.

KUMBUKUMBU ZA NYUMA
Mwaka 2007, gazeti moja (siyo la Global) liliwahi kuripoti kuwepo kwa uhusiano usiofaa kati ya Msama na Rose, wakati huo Promota huyo alikuwa kwenye vikao vya maandilizi ya harusi yake na Laura, lakini wenyewe waliruka ‘kimanga’.
 
Kweli udaku!

kutokana na nature ya kazi ya promoters na hawa wanamuziki, ni rahisi kufikiria hivyo, hili tatizo halimkumbi mke wa Msama tu bali wake wa mapromoter wengi sana. Kweli wapo promoters ambao huwa wanamaliza kabisa 'ku-promote' kila kila kitu.

Kinachotakiwa badala ya mwandishi kuleta habari hii ambayo ni damage kwa wahusika kama ni ya uongo ili wao wauze gazeti, wanatakiwa KUFANYA UCHUNGUZI, na kuwa na vithibitisho ambavyo ni havipingiki.

Hapa tutajadili lakini taarifa hii haina tofauti kabisa na vijiweni, kama haina uthibitisho then we have real to be careful

wahandishi wanaweza kabisa kufanya uchunguzi, aidha wavivu, hawana resources n.k

Please fanyeni uchunguzi, mbona kuna wachungaji na mashekh uchwara kibao wamewanasa magazetini?

tena kwa kuweka hii taarifa jamaa kama kweli kuna kitu kinaendelea ndio watafanya uchunguzi wao kuwa mgumu!
 
Kweli udaku!

kutokana na nature ya kazi ya promoters na hawa wanamuziki, ni rahisi kufikiria hivyo, hili tatizo halimkumbi mke wa Msama tu bali wake wa mapromoter wengi sana. Kweli wapo promoters ambao huwa wanamaliza kabisa 'ku-promote' kila kila kitu.

Kinachotakiwa badala ya mwandishi kuleta habari hii ambayo ni damage kwa wahusika kama ni ya uongo ili wao wauze gazeti, wanatakiwa KUFANYA UCHUNGUZI, na kuwa na vithibitisho ambavyo ni havipingiki.

Hapa tutajadili lakini taarifa hii haina tofauti kabisa na vijiweni, kama haina uthibitisho then we have real to be careful

wahandishi wanaweza kabisa kufanya uchunguzi, aidha wavivu, hawana resources n.k

Please fanyeni uchunguzi, mbona kuna wachungaji na mashekh uchwara kibao wamewanasa magazetini?

tena kwa kuweka hii taarifa jamaa kama kweli kuna kitu kinaendelea ndio watafanya uchunguzi wao kuwa mgumu!

Very right. Watu wanadhania kwamba waimbaji wa nyimbo za Injili na mapromoters wao hawana hisia miilini mwao. Kama hawako karibu wanawezaje kurahisi kufanikisha kazi zao? Sio kila walio karibu kikazi lazima wananihilii. Lakini pia wakinanihilii wanajua namna ya kujisafisha kwa Mungu wao na watu wao. Ni rahisi nyani kuliona nanihilii la mwenzake kwa kuwa la kwake halioni vyepesi. Kama tunaamini kwamba uimbaji wa nyimbo za Injili ni namna nyingine ya uhubiri, Mungu hakai kimya juu ya mtu wa namna hiyo kumtema kwa vile hapendi mtu vuguvugu - ambao si moto wala si baridi. Historia huonyesha kwamba wakifika kiwango hicho kazi zao hunyong'onyea na kuyeyuka kabisa kwa kuwa katika kujitetea kuhalalisha undava wao huingiziwa kiburi na majivuno, upako wa Roho Mtakatifu hupaa, wanabaki na skeleton na kuishia.
 
Sasa huyu mwandishi wetu anaeleza nini hapa? Kwanza amepewa ushirikiano na wahusika kwamba ndoa yao ina amani na wote wamekanusha habari hizo, bado anasema RM amesambaratisha ndoa? Huyu anafaa kushtakiwa anachafua hali ya hewa.

Chanzo hicho kikaendelea kuweka ‘nje' siri kuwa, chanzo cha kuwepo kwa ufa katika ndoa hiyo ni kufuatia mke wa Msama, Laura kuchezwa na machale kuhusu ukaribu kati ya mumewe na Rose Muhando kiasi cha kukosa amani kama siyo furaha
Kumbe ni hisia tu na wala hamna evidence. Promota na msanii ni kitu cha kawaida kuwa karibu na mwanamke kumuuliza mumewe kulikoni mbona u karibu na mama fulani ni kitu cha kaaida vilevile wala sio habari ya kupamba gazeti.
 
Hii habari ni ya kuvuruga ndoa za watu pamoja na kazi. Huyu mwandishi wa gazeti angejua ilivyo ngumu kumpata mume na mke mwema hasingethubutu kuweka hadharani habari ambazo zinaonekana wazi kuwa za kidaku. Angalieni akina Tiger Woods, Ashley Cole, John Terry, Wayne Bridge na madhara waliyoyapata kwa habari kama hizi
 
Udaku Plus + tatizo haya magazeti huwa yanatoa habari za ajabu ajabu tu ...kichwa cha habari hakinivutii kuendelea kusoma ....
 
Magazeti ya udaku yanauza sana kuliko yale yasiyo ya udaku.
Haya yana wateja sana mitaani.
 
Hivi ni gazeti la Shigongo lililoandika puuzi huu!!?
Huku ni kumuonea dada yetu Rose, mbona yeye Shiongo alichangia kifo cha Amina Chifupa kwa kumchafua na kumsimanga hata alipokuwa Hosptalini!
Kuuza gazeti kwa habari kama hiyo ni sawa na kutumia kitabu kitakatifu kupiga ramli!
 
Haya mambo ya udaku tukiyaendeleza humu yatatutoa umakini kwenye mambo muhimu na yenye maslahi kwetu na kwa nchi yetu.
A LUTA CONTINUA
Niliwahi kuuliza, je inafaa kuweka magazeti ya udaku hapa?, nikajibiwa kuwa hayafai, sasa leo tumewekewa na kuchangia hoja, nashauri tusiruhusu kuwekewa tena.
 
Nadhani tufikia mahali tuangalie ile sheria ya habari/magazeti vinginevyo huu mwanya wa magazeti ya udaku kuandika chochote tu unaweza kuigharimu sana jamii ya watanzania
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom