Rose Kamili amemsafisha Dr. Wilbrod Slaa. Hongera Rose Kamili na wenzako mliofanikisha hilo

"Niliwahi kumsikia Dr. Slaa kwamba afadhali wamsingizie kwamba alikosana na baadhi ya maaskofu hapo angetetemeshwa kidogo na tuhuma hizo. Pia mlioangalia mdahalo kwenye TV siku mbili kabla ya uchaguzi wa 2010, Dr. Slaa alieleza wazi kwamba alipokuwa TEC, contena lilikuwa likija kwa kutumia jina la kanisa alikwua anaingilia na kwa kusaidian na Usalama wa Taifa walikuwa wanalipiga"


Nakubaliana na Theory hii ni ukweli ila kwenye Kipindi hicho cha runinga wakati huo Dr. hakufunguka kiviile kutokana na maadili yake na ukweli ni kwamba si kila kitu ni lazima kisemwe hadharani......
 
Hiyo ya kumtia ndani askofu kwa tuhuma za ufisadi kupitia mgongo wa kanisa ni kweli ila halikumtoa kwenye upadri bali lilimtoa kwenye cheo cha ukatibu wa tec.
Kilichomtoa upadri ni baada ya kuandika barua ya petition kwa pope kwasababu tayari alikuwa ana familia na kuijulisha hivyo rome.
 
Kabla ya July 2007 ni wachache sana walikuwa wakiithamini Habari ya sababu za Padri Wilbrod Slaa kuacha utumishi wake wa upadri. Binafsi hadi kufikia mwaka 2007 nilikuwa na theory kama tatu zote toka vyanzo Tofauti vikieleza ni sababu gani ilimfanya Dr. Slaa akaachana na shughuli za kanisa.

Theory ya kwanza niliyoisikia ilikuwa ni kwamba amempa mwanamke mimba na hivyo yeye mwenyewe akaamua kuachana na mambo ya misa akaomba kurudi uraiani ili akajenge familia yake. Theory hii mimi nilisikia katikati ya mwaka 2006.

Theory ya pili niliambiwa kuwa alipokuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu (TEC) alifanya ufisadi wa hali ya juu. Ufisadi wenyewe ni ule wa kula hela za ujio wa Pope John Paul II hapa nchini September 1990 na hivyo Kanisa likamuondoa. Theory hii niliisikia mwishoni mwa mwaka 2007 baada ya yeye kutangaza list ya mafisadi pale Mwembeyanga.

Theory ya tatu niliyoisikia huwa siisikii ikisemwa hadharani ni kwamba Dr. Wilbrod Slaa alikorofishana na askofu mmoja ambaye ninalihifadhi jina lake. Ugomvi haukuanza na huyo askofu. Bali ni kwamba huyo askofu alikuwa na ndugu yake pale TEC na huyo ndugu alikuwa ni mmoja wa wakuu wa kitengo cha misaada kiitwacho CARITAS.
Tatizo likawa kwamba yule jamaa wa CARITAS akawa anatumia jina la Kanisa na misaada ile kupitisha maslahi yake kama vile makontena. Padri Wilbrod Slaa kama Katibu wa TEC akagundua hilo na akachukua hatua za nidhamu kwa huyo jamaa.

Kumbe ambalo Padri Slaa hakujua ni kwamba yule jamaa hakuwa peke yake, alikuwa anashirikiana na askofu huyo ambaye jimbo lake liko kanda ya ziwa Victoria. Askofu yule akapata habari ya kusimamishwa yule staff wa CARITAS. Akamjia juu Padri Slaa.

Padri Slaa akakataa shinikizo la kumrudisha yule fisadi wa CARITAS na hivyo majibizano yakawa makali kati ya Slaa na yule askofu. Ikaonekana wazi kwamba kumbe yule askofu yuko team moja na yule jamaa wa CARITAS.

Kwa sababu mali za CARITAS ni zinasimamiwa na TEC basi hapa katibu wa TEC yaani Padri Slaa akaona huyu naye ni mtuhumiwa mwingine anayepaswa kuwajibika tena kwa ubishi wake. Hivyo, Padri Slaa akaamua Polisi wamweke ndani askofu yule kwa kushiriki ule ufisadi na yule jamaa wa CARITAS.

Kitendo cha askofu kuwekwa ndani kikawashtua na wakawasiliana haraka japo enzi hizo simu za mkononi hazikuwapo lakini Kanisa lina mawasiliano mengi tu wakati huo. Ndipo maaskofu wakati huo wakaingilia na askofu mwenzao akatoka rumande. Hivyo, askofu wa Kanisa Katoliki Tanzania akawa ameonja adha ya kuwekwa ndani kwa muda wa masaa! Rais wa TEC wakati huo akiwa Mrehemu Askofu Samba wa Musoma akaingilia kati na ikaamuriwa kwamba Padri Wilbrod Slaa amefanya utovu wa nidhamu kumweka askofu ndani. Na hili likamuudhi Dr. Slaa akaamua kuachana na utumishi ambako wengi kimakosa huita kuachana na upadri.

Hizi ndizo theory tatu nilizowahi kusikia kuhusiana na sababu za Dr. Slaa kuacha upadri. Narudia kueleza, theory zote hizi ninazijua tangu mwaka 2007.

Sasa tuje kuzichambua theory hizi. Theory ya kwanza imenichukua miaka mingi kuiamini kwani sikuwa namjua Rose Kamili kwani niliambiwa kwamba mwanamke mwenyewe ni mzungu wala si Rose Kamili. Sasa niliposikia kuwa Rose Kamili ni mke wa Dr. Slaa basi nikaanza kutoipa nafasi hiyo theory.

Theory ya pili ya kufisadi hela za Pope sikuwa na vigezo vya kuipinga. Lakini sikushangaa ilipoanza kutumiwa na wanasiasa mfano ni Stephen Wasira alivyoitumia kwenye kampeni ya uchaguzi mdogo huko Arumeru. Lakini hatimaye aliyekuwa Rais wa TEC hadi mwezi uliopita yaani Askofu Jude Thaddaeus wa Mwanza alikana hadharani kwamba Dr. Slaa hajawahi kutuhumiwa wizi wa hela za ujio wa Papa.

Theory ya tatu kwamba Dr. Slaa alimweka ndani askofu nimekuwa nikibishana na wenzangu wengi. Ukweli wanaoijua huwa tunatofautiana na handling ya issue hiyo lakini siyo event. Mtu mwingine kabisa ambaye nilidhani haijuia aliwahi kunieleza kwamba baada ya Dr. Slaa kumweka ndani yule askofu akalalamika kwa Askofu Anthony Mayala wa Mwanza. Mimi nimekuwa nikipinga na kuuliza iweje Dr. Slaa ashitakiwe kwa Askofu wa Mwanz wakati yeye hakuwa Padri wa Jimbo la Mwanza na alikuwa wa Jimbo la Mbulu?

Ninapowauliza hivyo wanakosa majibu. Lakini kukosa majibu maana yake ni kwamba tunakubaliana kwamba Dr. Slaa alimweka ndani yule askofu lakini tunatofautiana kujua hatua zilizofuata.

Utaona kwamba kama kulikuwa na juhudi ya wanasiasa kupeleleza habari za Dr. Slaa kule TEC basi hakika hii theory ya tatu hata kama wakiijua hawataweza kamwe kuitangaza. Kwa nini hawataweza? Kwa sababu Padri kumweka ndani askofu ni kweli unaweza kujenga hoja kwamba ni utovu wa nidhamu. Lakini kizazi cha sasa hakiishii hapo. Watu watauliza sababu ya kujua kwa nini askofu awekwe ndani.

Umati ukipogundua kwamba kumbe Dr. Slaa alimweka askofu kwa sababu ya ufisadi wa CARITAS basi maana yake ni kumpandisha chati zaidi kwamba kumbe Dr. Wilbrod Slaa alianza vita ya ufisadi tangu akiwa kanisani na mafisadi wa huko walimkoma.

Nimesema zote hizi tatu ni theory. Narudia tena kusema hii ya tatu sijawahi kuisikia kwenye vyombo vya habari ila ninaisikia tu kwa wachache sana wanaopenda kujishughulisha na mambo ya Kanisa Katoliki. Tunaijadili kwenye meseji zetu, kwenye vigenge vyetu na inaishia huko.

Lakini zile thoery mbili zimashamwagwa magazetini na wote mnajua.

Nilioongea hapo juu ni history sasa tuje kwenye hoja ya leo. Juzi, Rose Kamili anakuja na hoja mahakamani akisema kuwa alifunga ndoa na Dr. Wilbor Slaa June 18, 1987. Hapa maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba haijulikani kama iko siku Pope John Paul II atakuja kuitembelea Tanzania.

Sanasana kila nchi na kila jimbo mwaka huo walikuwa na mikikimikiki ya kuadhimisha mwaka wa Mama wa Yesu uliotangazwa na Papa huyu January ya mwaka huo.

Mnaopenda nyimbo za Bikira Maria mnakumbusha kipindi hiki ndipo zilitoka kwa wingi na zinavuma hadi leo. Ndiyo ilikuwa kazi kuu ya Kanisa wakati huo.

Sasa, kama Dr. Slaa alifunga ndoa ya kiserikali tarehe hiyo kwanza hapa unapaswa kujiuliza maswali mengi. Je, idara iliyofungisha ndoa hiyo haikujulishwa kwamba huyo mfunga ndoa ni padri wa Kanisa Katoliki? Binafsi ninajua kuwepo kwa mahusiano ya siri kwa mapadri na maaskofu dunian na wanawake lakini ndoa ya siri tena imesajiliwa hii ni habari niliyojifunza.

Tuendelee kuchambua. Pope John Paul II alipokelewa na Rais Ali Hassan Mwinyi pale airport September 01, 1990. Airport iko D'Salaam basi kikanisa askofu aliyemkaribisha alikuwa ni wa Jimbo la D'Salaam yaani Laurian Cardinal Rugambwa akiwa na Msaidizi wake (Coadjutor) aitwaye askofu Polycarp Pengo.
Katibu wa Baraza la Maaskofu aliyekuwaepo ni Padri Wilbrod Slaa.

Hii maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba Pope alikuja nchini ikiwa ni zaidi ya miaka mitatu huku Padri Wilbrod Slaa akiwa kweny endoa na Rose Kamili. Kumbe, wakati sisi tunajua kwamba Katibu wa TEC yuko kwenye jopo la kumkaribisha Pope mwenzetu Rose Kamili anaona kwamba mumewe wa ndoa anamkaribisha Pope tena ndoa yenye watoto wawili tayari.

Rose Kamili amewasilisha mahakamani maelezo kwamba kitendo cha Dr. Slaa kuzaa naye na kufunga ndoa June 18, 1987, kilimfanya aanze taratibu za kuondoka kwenye nafasi za upadri. Hapa Rose Kamili anatufunulia ukweli ambao hatukuujua. Ukweli uliotufanya tuogelee katika kila mtu na theory yake. Wasira alikuwa na theory moja wakati mimi nilikuwa na theory tatu nimezitaja hapo juu.

Kumbe wakati tunaona Padri Slaa anachacharika nchi nzima kuandaa ziara ya Pope basi leo ndiyo tumefunuliwa na kujulishwa kwamba hapohapo alikuwa na process nyingine ya kuanza kuachana na upadri.

Leo nimeona picha za wabunge wa CCM yaani Esther Bulaya, Sofia Simba wakimkubatia Rose Kamili bungeni leo. Siwezi kusema ni kumpongeza au kumfariji au ilikuwa ni issue nyingine. Lakini kama kuna watu nyuma ya Rose Kamili binafsi ninaona kwamba ni walewale ambao hawajui kwamba unapopambana na jambo linalohusisha Kanisa Katoliki basi inabidi ama tukuhurumie au tuone ulivyo na akili nyingi sana hapa duniani.

Kwani wengi hapa duniani ambao hujikuta wamegusa mambo yanayoguswa na Kanisa Katoliki wameishia kuumbuka kwa sababu ya ujinga wao kutojua mengi yanayohusiana nalo. Na wasipojirekebisha wataendelea kuumbuka tu.

Hili la Rose Kamili tayari ninauona ni ushindi kwa Dr. Slaa na kilio kwa wote waliomtafuta kwa scandal za tangu akiwa Kanisani.

Kwa sababu hadi dakika hii kuna wanaocheka wakidhani Dr. Slaa kaumbuka, lakini kwa kweli Rose Kamili katurahisishia kazi kubwa kutujulisha kwamba ni nini kilimfanya Padri Wilbrod Slaa aache upadri na aingine mtaani. Bahati nzuri Rose Kamili haongei bila ushahidi.

Sisi wengine wote na yote tuliyosema hayana ushahidi. Binafsi hadi sasa, niliamini zaidi theory ya kumweka ndani yule askofu kuliko theory zote. Lakini ukiniuliza ushahidi nitakwamba hadi siku yule askofu akisema au Dr. Slaa akisema au hata askofu yeyote akisema, kitu ninachoamini haitatokea.

Niliwahi kumsikia Dr. Slaa kwamba afadhali wamsingizie kwamba alikosana na baadhi ya maaskofu hapo angetetemeshwa kidogo na tuhuma hizo. Pia mlioangalia mdahalo kwenye TV siku mbili kabla ya uchaguzi wa 2010, Dr. Slaa alieleza wazi kwamba alipokuwa TEC, contena lilikuwa likija kwa kutumia jina la kanisa alikwua anaingilia na kwa kusaidian na Usalama wa Taifa walikuwa wanalipiga mnada.

Kwa mimi muumini wa theory ile niliona kana kwamba anautaja mgogoro ule lakini kwa jinsi ambavyo si rahisi kwa mtu baki kuulewa.

Hivyo, nahitimisha kwa kusema kwamba Rose Kamili amemsafisha Dr. Wilbrod Slaa hata kama kuna watu akili yao leo inashangilia kitendo cha Rose wakati akili zao hizohizo zilishangilia tuhuma za Stephen Wasira kule Arumeru kwamba Dr. Slaa alitimuliwa upadri kwa sababu ya kufisadi hela kwa ziara ya Pope John Paul II.

Hongera sana Rose Kamili. Kama kuna wenzio nyuma ya hili naomba uwafikishie hongera zangu kwao hata kama kila mtu katika Jamii Forum atanipinga kwa hili.

Mimi napenda kuamini kwamba kama kuna watu wawili - mmoja akisema "kuku" na mwingine akaisema "siyo kuku ni bata" - mimi mtu wa tatu niliyesikia siwezi, kwa kutegemea kauli hizo mbili, niseme aliyesema "kuku" kakosea. Hivyo, kwa Rose kusema alichosema na kwa vile hatujasikia akikisema tangu walipoachana na Dr Slaa na amekuja kukisema leo siwezi, kama ninataka kuwa neutral, kuamini kama ni kweli au si kweli. Mahali ambapo hatuna sababu ya kuamini kuwa ni kweli ni lazima tu'suspend judgement' ili kujiridhisa.

Mambo ya ndoa yana mambo mengi sana wakati mwingine unachokisikia siyo kile kilichofanyika. Nasema hivi kwa sababu nilishafanya utafiti kwa watu ambao ndoa zao zimevunjika nikajifunza mambo mengi. Niliongea na watu 400 uso kwa uso. Nilitumia miezi 2. Nilikuwa naanza asubihi hadi jioni. Habari nilizozipata ni "amazing". Kuna mfano mmoja niutumie bila kutaja wahusika na kwa kubadilisha mazingira. Ndoa x ilivunjika. Mume alidai sababu ilikuwa y. Mke alidai sababu ilikuwa z na watu waliowafahamu (ikiwa ni pamoja na ndugu) walidai sababu ilikuwa w. Hivyo, majibu yakawa matatu y, z na w. Sasa nani kati ya hao alisema ukweli au sababu zote tatu zilikuwa kweli?

Kuhusu 'theories' unazosema ni kwamba, hakuna maisha ambayo yana'attract speculations' kama maisha ya upadri na utawa. Na 'speculations' nyingi zinahusu fedha (wizi), pombe (ulevi) na wanawake/wanaume (uasherati). Kuna mfano mmoja wa padri x. Ilidaiwa kuwa ana lala kwa mke wa mtu na waumini wakasema wana ushahidi wa kuona kwa macho yao na wakasema wataenda kutoa ushahidi kwa askofu. Habari zikawa habari na kukaundwa kamati ya kwenda kuonana na askofu kuhusu jambo hilo baya.

Askofu aliposikia hivyo, ilibidi achukue hatua. Padri huyo alikuwa wa shirika na siyo wa jimbo. Mapadri wa shirika wanakuwa chini ya 'major superior' na si askofu. Mapadri wa jimbo ndio wako chini ya askofu. Sasa alichokifanya askofu ni kutoa taarifa kwa mkuu wa shirika la yule padri akisema hamtaki jimboni mwake akidai ndani ya siku mbili awe ameshaondoka parokiani.

Padri akafunga mizigo yake kwenda shirikani kwao ili mkuu wa shirika aamue kifanyike nini. 'Most probably' ilikuwa kumrudisha kwao (nchi anakotoka). Habari zikawafikia watu wengi na hata yule mama. Maskini! Kumbe gari la padri lilikuwa linafanana na gari la mume wa yule mama, ambaye alikuwa akifanya kazi Afrika Kusini na akawa amekuja likizo kwa wakati huo. Na gari lake alikuwa akilipaki nje maana nyumba yao ilikuwa haina uzio ila ilikuwa kama mita 100 hivi kutoka barabara kuu.

Sasa waumini walipokuwa wanaona lile gari waliamini ni gari la yule padri. Kumbe haikuwa hivyo. Lilikuwa la mume wa yule mama. Baada ya ukweli kubainika wale waumini walijiona hawafai maana walitoa "ushahidi wa kudhania" - haukuwa na ukweli wowote ingawa wakati wanaongea na askofu walidai "wana ushahidi wa kuona kwa macho yao".

Mimi niseme, ukweli wa mambo ya Rose Kamili na Dr Slaa wanayajua wao kwa undani kuliko jinsi tunavyoweza ku'speculate'. Na kwa vile baadhi yetu 'speculations' ndizo zinazonoga kuliko ukweli, nawaomba tuendelee ku'speculate'!
 
Hiyo ya kumtia ndani askofu kwa tuhuma za ufisadi kupitia mgongo wa kanisa ni kweli ila halikumtoa kwenye upadri bali lilimtoa kwenye cheo cha ukatibu wa tec.
Kilichomtoa upadri ni baada ya kuandika barua ya petition kwa pope kwasababu tayari alikuwa ana familia na kuijulisha hivyo rome.

Mkuu naanza kukubaliana na nyinyi. Unajua wakati wa John Paul II kuomba petition uliaweza kutumia hata miaka minane kupata.

Na kuanzia mwaka 1980 hadi 1985, John Paul II alizuia kabisa haya mambo ya laicization.
 
Sasa, kama Dr. Slaa alifunga ndoa ya kiserikali tarehe hiyo kwanza hapa unapaswa kujiuliza maswali mengi. Je, idara iliyofungisha ndoa hiyo haikujulishwa kwamba huyo mfunga ndoa ni padri wa Kanisa Katoliki? Binafsi ninajua kuwepo kwa mahusiano ya siri kwa mapadri na maaskofu dunian na wanawake lakini ndoa ya siri tena imesajiliwa hii ni habari niliyojifunza.

Tuendelee kuchambua. Pope John Paul II alipokelewa na Rais Ali Hassan Mwinyi pale airport September 01, 1990. Airport iko D'Salaam basi kikanisa askofu aliyemkaribisha alikuwa ni wa Jimbo la D'Salaam yaani Laurian Cardinal Rugambwa akiwa na Msaidizi wake (Coadjutor) aitwaye askofu Polycarp Pengo.
Katibu wa Baraza la Maaskofu aliyekuwaepo ni Padri Wilbrod Slaa.

Hii maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba Pope alikuja nchini ikiwa ni zaidi ya miaka mitatu huku Padri Wilbrod Slaa akiwa kweny endoa na Rose Kamili. Kumbe, wakati sisi tunajua kwamba Katibu wa TEC yuko kwenye jopo la kumkaribisha Pope mwenzetu Rose Kamili anaona kwamba mumewe wa ndoa anamkaribisha Pope tena ndoa yenye watoto wawili tayari.


Huu ndio ukweli mwenyewe! Dr. Mwongo, Mzinzi na Si mwaminifu!
 
Hivi kusafisha au ndio umezidi KUPAKA TOPE tena lile tope la mikojo ya viboko katika mto! maana mie umenifngua na mengi,
1. ulidhani alizaa na mwanamke ndio akaacha upadre ...hapa ni UDHAIFU WA NAFSI mpaka akaacha upadre
2. Alichota pesa wakati wa ujio wa baba yenu mtakatifu ...hapa inaonesha jinsi alivo FISADI dah!
3. Aligombana na askofu mwenzie ... hapa inaonesha jinsi alivo hana msimamo

Kwa fikra zangu huyu hafai hata kidogo kuwa Rais anaweza KUTUGEUKA wakati wowote akatuuza sisi nchi nzima huyu! akiwa na shida anaweza kufanya ufisadi wa hali ya juu huyu , umesahahu jingine pia AMEIBA MKE WA WATU NA KUZINI NAE NA KUZAA NAE KITOTO CHA NJE ! what a president

Nchi yetu inaenda vibaya kwa kuwa na watu wengi wenye fikira kama zako. Kwako wewe ukisikia mtu anasema: "Jamani, mwizi... mwizi... mwizi...!" utachukua jiwe upige na kuua kwa kutegemea kauli uliyosikia bila kuuliza na kujiridhisha kama kweli ni huyo bwana ni mwizi au la. Kutaka kujiridhisha utaona unapoteza muda na unaona ni heri utende kitu ili uulize baadaye.

Mpika chipsi mmoja aliuliwa katika mazingira kama haya. Mwizi alikwapua simu kwa mama mmoja na kukimbia. Mama akapiga kelele na mpika chipsi alikuwa akifahamiana na huyo mama. Huyu bwana aliona aokoea jahazi kwa vile ni mtu wa mbiyo. Basi akamkimbilia yule mtuhumiwa. Yule jamaa alipoona huyu mpika chipsi anamkaribia ilibidi aitupe ile simu na kuendelea kulala mbele. Yule mpika chipsi akaiokota na kurudi huku akionesha kwa watu kuwa ameikoa. Alipofika karibu na yule mama, mama kwa furaha kubwa akalia: "Jamani simu yangu hii hapa! Nimeipata. Huyu hapa anayo!" Waliosikia walifikiri yule mpika chipsi ndiye mwizi. Wakapiga wakaua wakati mama hakuwa anamaanisha hivyo. Walipomaliza kuua baadaye watu waliokuwepo wakaanza kuelezea kilichotokea. Wewe ni mmoja wa watu ambaye ungekuwepo siku hiyo ungeshiriki kumwua mpika chipsi maana uwezo wako wa kufikiri ni sawa na watu wanaojichukulia sheria mkononi hata bila kujua kilichotokea ni nini!
 
Askofu aliposikia hivyo, ilibidi achukue hatua. Padri huyo alikuwa wa shirika na siyo wa jimbo. Mapadri wa shirika wanakuwa chini ya 'major superior' na si askofu. Mapadri wa jimbo ndio wako chini ya askofu. Sasa alichokifanya askofu ni kutoa taarifa kwa mkuu wa shirika la yule padri akisema hamtaki jimboni mwake akidai ndani ya siku mbili awe ameshaondoka parokiani

Mkuu Magobe,

Nakujua wewe ni msomaji mzuri wa magazeti. Mwaka 2008 Askofu Jude Thaddaeus Ruwa"Ichi wa Dodoma alikataa mchezo kama huo. Tuliona magazetini kwamba watu wa Parokia moja iitwayo Farkwa walikuja na kesi kama unayoeleza.

Kesi ile mimi niliiona magazetini. Watu wale walipofika kwa Askofu Jude Thaddaeus aliwaambia hawezi kuchukua hatua yoyote hadi wakamilishe ushahidi kamili yaani beyond reasonable doubt.

Huyo padri alikuwa ni "deocesan" yaani wa jimbo kama ulivyofafanua. Hakuwa "Religious" yaani wa shirika.

Hivyo, huyo askofu aliyemtimua alikosea na hakuna sababu za kumtetea kwa sababu ushahidi haukujitosheleza.

Matokeao kama ya askofu huyu ndiyo yanayofanya wengi wazushe kwamba Padri akituhumiwa Parokia fulani anahamishwa Jimbo au hata nchi.
 
Mama K, umetoa somo kwa wengi kulinda ndoa zao kabla hazijawaponyoka na kuibua mijadala ambayo vinginevyo isingekuwepo. Na tunakumbuka kule kwetu jimboni Hanang mlivyopigiana kampeni vizuri. Ukatuambia Slaa ni shemeji yetu, tumpe kura. Nae akakunadi kuwa mchapakazi makini mwenye busara.
 
Probelm ni kwamba kitabu kitakatifu hakijatoa ruksa ya DIVORCE and there is nobody to change that.
Kwa jinsi ninavyofahamu Kanisa (Katoliki) halitambui ndoa ya Kiserikali mpaka uwe umefungishwa ndoa hiyo kanisani. Kwa maana nyingine ni kwamba ndoa kati ya Rose na Wilbroad ni batili mbele ya RC.
 
La ajabu kumbe tayari kwa mujibu wa haya yasemwayo leo alishakutelekeza. Sasa ule uvumilivu na upendo wa siku zile umeacha wapi? nani mchonganishi? Nawe Dr. Slaa mzee wa hekima pamoja na ujuzi mwingi na sifa ya kufanya mambo kwa kukurupuka, tuthibitishieni kwa kuamua kumaliza jambo hili nje ya mahakama. Ki utu uzima. Maji yameshamwagika hayazoleki. Mapenzi yakihama moyoni kuyarejesha kazi. lakini, nani ajuae mtakutana wapi kila mmoja akihitaji msaada wa mwenzake? Na ni nani ajuae ukweli halisi wa kufikia kuruhusu mambo yafike yalipo zaidi yenu wawili? Basi malizeni
 
Devorce in ya Kisheria! Haihusiani na vitabu vitakatifu!

jana niliandika katika ule uzi mwingine ifahamike kuwa makanisa,wakuu wa wilaya na misikiti ni agents wa serikali kufungisha ndoa. Ni lazima waaply serikalini ili wapate kibali cha kufungisha ndoa pamoja na kununua vyeti vya ndoa. mfano sisi waluteri ukifunga ndoa hupewa cheti kingine cha ziada cha ndoa kinachotolewa na kanisa ambacho pamoja na mambo mengine huandikwa maneno "alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe".
 
Mkuu thanx kwa taarifa yako ya kina ila tafuta zaidi maana ys neno "theory". Kitaaluma hakuna theory kati ya hizo ulizozitaja.
 
nakupongeza kwa kuandika makala ndefu lkn tatizo ni kwamba MAKALA YAKO INAKINZANA NA KICHWA CHA HABARI. kwanza theory ni mbili. hii ya rose siyo theory. ilijulikana kwa muda mrefu sn! sikuelewi unapo sema rose kumshitaki slaa ni kumpa ushindi! ushindi upi!? naona kama ni kumuumbua na kumshushia heshima. elewa kuwa mambo mengi yameibuka kuhusu suala la rose. inasemekana baada ya idadi wa wabunge wa viti maalumu kutoka kilmanjaro , arusha na manyara kuwa kubwa, slaa alishauriwa asimuweke rose kwenye viti hivyo lkn hakusikia. rose kamili amekua diwani wa ccm kwa miaka 10.inasemekana slaa alimpa ubunge ili kumfanya akae kimya kuhusu uhusiano wake na mama ishumbisha (sp).

hii inaonesha kuwa slaa anaweza kutoa na kupokea hongo. jambo la pili ni kwamba mtu ambae ni padri tena katibu wa baraza la maaskofu, kuratibu ziara ya papa na kupeana nae mkono eyapoti, huku anajua kuwa na kimada rose, haipendezi. kama ni kweli kuwa alifunga ndoa ya serikali mwaka 1997, hali ya kua ni padri, basi hana uchamungu hata chembe. mimi ni muumini wa kawaida lkn siwezi kuoa mwanamke serikalini! slaa sidhani kama kashfa hizi zinampandisha chati. vilevile kumuiiba mke wa ishumbisha ni jambo la aibu. above all amezaa naye. ana watoto 2 na rose, huyu mtoto wa uzeeni wa nini? sina HAMU WITH THIS FOOLISH SLAA!
 
Hivi kusafisha au ndio umezidi KUPAKA TOPE tena lile tope la mikojo ya viboko katika mto! maana mie umenifngua na mengi,
1. ulidhani alizaa na mwanamke ndio akaacha upadre ...hapa ni UDHAIFU WA NAFSI mpaka akaacha upadre
2. Alichota pesa wakati wa ujio wa baba yenu mtakatifu ...hapa inaonesha jinsi alivo FISADI dah!
3. Aligombana na askofu mwenzie ... hapa inaonesha jinsi alivo hana msimamo

Kwa fikra zangu huyu hafai hata kidogo kuwa Rais anaweza KUTUGEUKA wakati wowote akatuuza sisi nchi nzima huyu! akiwa na shida anaweza kufanya ufisadi wa hali ya juu huyu , umesahahu jingine pia AMEIBA MKE WA WATU NA KUZINI NAE NA KUZAA NAE KITOTO CHA NJE ! what a president

UNA UTANI NA JAKAYA M. KIKWETE wewe, maana hata idadi ya wake mwenyewe haijui
 
Back
Top Bottom