Prisoner 46664
JF-Expert Member
- Dec 18, 2010
- 1,948
- 1,237
Mtoto wa aliyekuwa mbunge wa Bumbuli Bwana Shekukindo yuko kwenye hatua za awali za kujiandaa kulichukua jimbo hilo kwenye uchaguzi ujao wa 2015
Ronald Baraka Shelukindo ambaye ni maarufu kama afisa mwandamizi wa DSTV amesema kuwa anayo nia, uwezo na pia mitazamo mibadala kwa ajili ya jimbu hili.
Tatizo kubwa ambalo wachunguzi wa masuala ya siasa za Bumbuli wanasema linaweza kumkabili Ndugu Baraka ni kutojulikana jimboni ambako kijana January amejizatiti vilivyo kwenye ngazi zote.
Lakini hilo linaonekana haliwezi kumtatiza huyu kijana msomi na mcheshi bwana Baraka kwani tayari kashaanza michakato ya kuandaa mpago kambambe wa kuliendeleza jimbo la Bumbuli
Kwa maoni yangu nadhani vizuri kujitokeza lakini ninachouliza kama January anafanya kazi nzuri kwa nini Baraka Shelukindo asipewe ukuu wa wilaya ili wafanye kazi kama timu ya pamoja?
Imagine Baraka Shelukindo + January Makamba for Bumbuli
hamuoni kama ni dream team na wakaaachana na siasa za bufu za wazee wao?
Mkuu naona umejaribu kutumia akili kujipigia kampeni hapa..ila tatizo ni kuwa m.kwere huwa hasomi hizi thread..mwandikie barua ya maombi ya huo ukuu wa wilaya kabisa..kwani dstv vipi hakulipi??