Rombo kama Loliondo!

Hii ni neema kwa Wakatoliki wote kwani Mungu hapendelei ametoa babu Loliondo kwa walutheri. Na sisi wakatoliki tumshukru Mwenyezi Mungu kwa kutufunulia dawa huko Rombo. Tumsifu Yesu Kristu.
 
Mhhh jamaa ameamua kuipiku KKKT!!! Maana kaona kwa nini KKKT iwike na hali kuna RC???? Kwa mtaji huu bado tutasikia pia wengine wakitokea FGBC, SDA na hata BAKWATA na BARAZA KUU bila kuwasahau BAMITA: Ama kweli bongo tambarare!!!!!!!!!!
 
Rombo kama Loliondo Send to a friend Thursday, 17 March 2011 20:25 0diggsdigg

Daniel Mjema, Moshi

Ni siku za mwisho? Hili ndilo swali lililoanza kuumiza vichwa vya watu baada ya kijana mmoja kuibuka wilayani Rombo, mkoani Kilimanjaro na kudai ameoteshwa dawa ya ajabu na Bikira Maria inayotibu magonjwa sugu ukiwamo Ukimwi.Kama ilivyo kwa mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambikile Mwasapile wa Loliondo ambaye amejizolea umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi, kijana huyo naye amekuwa akitoa tiba kwa sh500.

Kwa imani ya waumini wa Kanisa Katoliki Duniani, Bikira Maria ni mama wa Yesu ambaye anaaminiwa na waumini wa Kanisa hilo na hata katika sala jina lake ndilo linalotumika zaidi huku wakiamini kuwa Yesu ni mtoto wa Mungu.Habari za uhakika kutoka eneo la Customs katika mji mdogo wa Tarakea, mpakani mwa Kenya na Tanzania, zilimtaja kijana huyo ambaye sasa anajiita Nabii, kuwa ni Hilary James Kitwai (28), kutoka wilayani Babati.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu kutoka Tarakea, Kitwai alisisitiza kuwa dawa hiyo ameoteshwa na Bikira Maria na Yesu na kwamba inatibu Ukimwi, Saratani, Kisukari, Shinikizo la Damu, Figo, Pumu na maradhi ya maumivu.
"Walinitokea kwenye ndoto wakanionyesha huo mti na waliniambia kwa sasa tuko wawili tu Tanzania, lakini huyo mwenzangu simfahamu. Mimi natoza Sh500 lakini katika hiyo pesa yangu na familia yangu ni Sh300 tu,"alidai.

Kitwai ambaye amekuwa gumzo katika mji wa Tarakea, alisema anakabiliwa na changamoto kubwa katika kuwahudumia wenye mahitaji kwa kuwa hana msaada na kuomba serikali imsaidie kumpatia wahudumu.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka wilayani Rombo, tayari vyombo vya ulinzi na usalama vimemzuia kwa muda, kijana huyo kutoa tiba inayofanana na ya mchungaji Mwasapile na kuitisha sampuli za mizizi anayoitumia.

Kijana huyo ambaye ni fundi baiskeli kwa miaka mingi katika eneo hilo, aliibuka Jumatatu wiki hii na kuanza kutoa tiba kwa kutumia kikombe na tayari watu takribani 100 kutoka Kenya na Tanzania wamekunywa dawa yake.

"Anadai kuwa ameoteshwa na Bikira Maria na alielekezwa huo mti ambao una utomvu na kuanzia juzi (Jumatatu),watu kama 100 hivi walishakunywa dawa hiyo ambayo wenyeji wanadai mti wake ni sumu,"kilidai chanzo chetu.Ofisa Mtendaji wa Kata ya Tarakea, Motamburu, Kimario, alilithibitishia Mwananchi kuwapo kwa kijana huyo.

Kimario alisema yeye binafsi, Ofisa Afya na Ofisa Usalama wa Taifa, walifika nyumbani kwa kijana huyo juzi na kumfanyia mahojiano."Tulimhoji akasema alitokewa na Bikira Maria na Yesu ambao walimwonyesha mti huo ambao upo katika Mto Tarakea na walimwambia yupo mmoja tayari anayetibu maradhi sugu na kwamba yeye atakuwa wa pili,"alisema mtendaji.

Kwa mujibu wa mtendaji huyo, kijana huyo aliwaeleza kuwa baada ya Babu wa Loliondo na Yeye, bado atatokea mtu wa tatu ambaye naye ataoteshwa dawa za kutibu maradhi hayo na baada ya hapo Yesu mwenyewe atakuja duniani.

"Tulimuuliza kama ameshatoa dawa hiyo kwa watu mbalimbali akasema alianza kutoa Jumapili na watu kama 20 hivi walikunywa na alitupa vipande vya miti viwili vya dawa hiyo na tumevikabidhi kwa uongozi wa juu,"alisema Kimario.

Kwa mujibu wa Kimario aliyekuwa akimkariri kijana huyo, alisema 'nabii' huyo ameamua kutoendelea kutoa tiba hiyo hadi hapo serikali itakaporidhia na kwamba kwa sasa anamuomba Mungu ampe maono zaidi juu ya dawa hiyo.

Wananchi walioongea na Mwananchi baada ya kuzagaa kwa taarifa hizo, wameitahadharisha serikali kuwa makini na watu wanaojiita ni manabii vinginevyo wananchi wanaweza kukumbwa na maafa ya kunywa sumu bila kujua.

Wananchi hao wameitaka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kuwajibika kikamilifu kwa kuzuia matumizi ya dawa ambazo hazijathibitishwa kutokuwa na madhara.Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, Anthony Tesha ambaye pamoja na kukiri kusikia habari hizo lakini alisema anaviachia vyombo husika kufuatilia jambo hilo.

source:Rombo kama Loliondo
 
hii imenistua kidogo coz pale tarakea ndio home town kabisa
nimewasiliana na watu kule wameniambia kijana malaria ilikua imepanda kumkichwa.
amechukuliwa jana jioni na ameshikiliwa na polisi kwa mahojiano.
Nchi ya mazingaombwe hii! Mtu ambaye malaria imepanda kichwani amechukuliwa na polisi na anahojiwa!!!
 
duh! Tanzania taifa lililokosa matumaini kwa umaskini wa mtu mmoja mmoja. Naogopa kuishuhudia ile siku ambayo dawa hizi zitaanza kuonyesha side effects. Hili biological bom linalotengezwa nafikiri soon litaripuka.
 
Duh hizi sanaa sasa!baada ya kuona ufundi wa baiskeli haumtoi,bora atoke kwa style ya 'babu',teh teh teh!
 
Ndugu zangu katika jf mie nimeamua kusalimisha maisha yangu kwa yesu christo ili awe bwana na mwokozi wa maisha yangu. Wewe je? Unataka kitokee kitugani ili uweze kutambua mambo haya!. Tumuombe mungu atupe utambuzi wa hayo mambo kwakuwa kwa akili zetu hatuwezi ila kwa msaada wake tutaweza
 
Dogo hatuwezi kumhukumu,lakini ukiangalia kimazingira utagundua msoto wa maisha umemfanya agundue opportunity ya kuponea,tatizo hasije kuua watu.
 
Kweli maisha yametuchapa wabongo.... huyu kaona biashara ya makenika wa baiskeli haulipi sasa kaamua kuwa msanii :embarassed2:!!!!
 
tatizo ukisema ukweli watu wanapandisha hasira lkn sijui itakuaje ikigundulika kuwa babu naye malaria ipo kichwani.Yaani tanzania yetu ina mambo ya aibu sijapata kuona.yaani siamini nahisi nina illucinate.kama kweli watu wanapona serikali inishindwa nini kuchukua japo watu kumi tu waliodhihirika kuwa ni wagonjwa wakapewa hiyo dawa kisha wakapimwa tena tuone kama wamepona au la.Hivi jaman hiyo cocktail anayotoa babu kama inaside ifects mbaya tutamlaumu nani hasa ukizingatia kila mtanzania anataka anywe hicho kikombe.eeeh mungu kwani ubongo wa watanzania uliuumba kwa material gani maana mambo yetu ni zaidi ya ze comedy ya joti na mpoki.mi hicho kikombe hata kwa bunduki sinywi na hizi mvua tusubiri mlipuko wa kipindu pindu,na hivyo vikombe kumi vinavyonywewa na midomo zaidi ya malaki sijui vinasafishwaje tusubiri mlipuko wa TB na fungus za midomo.
 
Hivi kwanini watanzania mmekuwa rahisi kudanganywa kiasi hiki, kwa mwendo huo mtaendelea kunyweshwa sumu huku mnajiona, tusubiri side effect ya hizo sumu, nachelea tunaweza kupoteza watu wengi wakiwemo viongozi wa nchi.
hii kitu ingetokea ulaya lazima hawa wanaojiita manabii wangepelekwa kupimwa akili zao kwanza.
 
Huyu wa Rombo ni maniac muongo mkubwa msimfuate hana lolote.

tapeli kabisa huyu achaneni naye
 
Dogo hatuwezi kumhukumu,lakini ukiangalia kimazingira utagundua msoto wa maisha umemfanya agundue opportunity ya kuponea,tatizo hasije kuua watu.
Hivi kiswahili cha hasije badala ya asije, taharifa badala ya taarifa, hameacha badala ya ameacha nk. mbona kinazidi kushamiri hapa JF, mnakera ebo!
 
Ukikubali ukweli huu, utakuwa huru.

1. Mtu akifa hawezi kabisa kuwasiliana na walio hai

Mungu aliwambia Adam na Eva Ukikubali ukweli huu, utakuwa huru.

1. Mtu akifa hawezi kabisa kuwasiliana na walio hai

Mungu aliwambia Adam na Eva mkila tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya mtakufa hakika, Mwanzo 2. Shetani akamwambia Eva, mkila hamtakufa hakika Mwanzo 3.

2. Waliokufa hawajui neno lolote, kumbukumbu lao limetoweka, Mhubiri 9:5.

3. Habari ya Bikira Maria na watakatifu wengine kuenndelea kuwa hai, inapingana na maandiko. Hilo ni moja ya mafundisho ya uongo yalioingizwa kanisani na Wakatoliki, Wakolosai 2:8, Daniel 7:25,

4. Uongo huo umefungua njia kwa ibada za wafu na kupitia wafu, na shetani na mapepo yamekuwa yakijitokeza katika sura ya marehemu, nakuwakeuza watu kumwelekea Mungu. Ndio maana utasikia Nyerere kanitokea, sijui Bikira Maria au mtakatifu flani, huu ni uongo. Pepo alimtokea Sauli katika Sura ya Samwel, wakati Samweli aliisha kufa, Samwel 28.

5. Ukifahamu hili utakuwa huru, hakuna ataykudanganya kwamba kaoteshwa dawa na Bikira Maria. Labda Pepo Mchafu. Hakuna ushahidi wowote wa kimaandiko wa kupalizwa kwa Maria. Hakuna cha pagatory, soma uelewe upate kuwa huru. 2 Wathesalonike 2:7-12. Hakuna maombezi kupitia wafu aka watakatifu, ni kupitia Yesu tu!! 2 Timotheo 2: 5

6. Biblia haijipingi, andiko lolote linalozungumzia kuishi baada ya kifo, humaanisha kuishi baada ya kuja kwa Yesu ambaye atawafufua watakatifu na watamlaki mawinguni. Ukisikia yesu amekanyaga ardhi hii, usijisumbue, huyo ni yesu feki, cosmic Christ, Yesu wa kweli hatagusa ardhi, bali tutamlaki mawinguni.

7. Sikashifu dini wala imani ya mtu. Anayekashfu ni yule, anayepindisha maandiko na kuwasingizia watu waliolala mauti kuwa wamewatokea.mkila tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya mtakufa hakika, Mwanzo 2. Shetani akamwambia Eva, mkila hamtakufa hakika Mwanzo 3.

2. Waliokufa hawajui neno lolote, kumbukumbu lao limetoweka, Mhubiri 9:5.

3. Habari ya Bikira Maria na watakatifu wengine kuenndelea kuwa hai, inapingana na maandiko. Hilo ni moja ya mafundisho ya uongo yalioingizwa kanisani na Wakatoliki, Wakolosai 2:8, Daniel 7:25,

4. Uongo huo umefungua njia kwa ibada za wafu na kupitia wafu, na shetani na mapepo yamekuwa yakijitokeza katika sura ya marehemu, nakuwakeuza watu kumwelekea Mungu. Ndio maana utasikia Nyerere kanitokea, sijui Bikira Maria au mtakatifu flani, huu ni uongo. Pepo alimtokea Sauli katika Sura ya Samwel, wakati Samweli aliisha kufa, Samwel 28.

5. Ukifahamu hili utakuwa huru, hakuna ataykudanganya kwamba kaoteshwa dawa na Bikira Maria. Labda Pepo Mchafu. Hakuna ushahidi wowote wa kimaandiko wa kupalizwa kwa Maria. Hakuna cha pagatory, soma uelewe upate kuwa huru. 2 Wathesalonike 2:7-12. Hakuna maombezi kupitia wafu aka watakatifu, ni kupitia Yesu tu!! 2 Timotheo 2: 5

6. Biblia haijipingi, andiko lolote linalozungumzia kuishi baada ya kifo, humaanisha kuishi baada ya kuja kwa Yesu ambaye atawafufua watakatifu na watamlaki mawinguni. Ukisikia yesu amekanyaga ardhi hii, usijisumbue, huyo ni yesu feki, cosmic Christ, Yesu wa kweli hatagusa ardhi, bali tutamlaki mawinguni.

7. Sikashifu dini wala imani ya mtu. Anayekashfu ni yule, anayepindisha maandiko na kuwasingizia watu waliolala mauti kuwa wamewatokea.
 
Back
Top Bottom