Rombo kama Loliondo!

Wizara ya afya wanashindwa kutupa idadi ya watu waliokunya dawa wakapona?hivi hao wanafunzi wanaosoma pcb,pcm,wakisikia ya loliondo watakuwa hamu ya kuwa madaktari
 
Hapa nahisi kuna mkono wa watu fulani ili tusahau Dowans na ugumu wa maisha..
 
ni wajinga tu walao ujinga
kwani mwelevu hutafuta zaidi hekima
kwa kuwa ndiyo chakula chake

mtu hawezi kushindwa kuwa mjusi Tanzania
harafu akawe mamba Uingereza
hapo kila na akili kichwani mwake
 
Njaa inaupeleka ukiristo pabaya- kuna. Ukiristo umekuwa tatizo kwani wanatapeli watu kwa mgongo wa maono. Mf. DECI walidai kuoteshwa wakaibia watu. Kina kakobe, mzee wa upako, mwingira wote hawa wanawaibia waumini wao kila siku kwa kisingizio cha unabii/utume. Sasa wamezuka wengine kina babu wa loliondo na sasa nabii james wa rombo. Huu ni msiba mkubwa, wakiristo amkeni na utafuteni ukweli wa dini.

Nakupinga kwa hilo. Ukristo umetokana na Kristo mwenyewe na wala hauwezi kuwekwa pabaya na manabii wa uwongo. (Kumbuka jiwe kuu la pembeni). Watakaowekwa pabaya ni hawa ambao wanajifanya ni wake wakati Kristo walio wake wote anawajua. Nachelea kuwaita hawa ulowasema manabii wa uwongo maana bado nimekatazwa kuhukumu. Hakimu wa Haki na Ukweli ni mmoja tu. Labda jiulize, dunia imefaidika nini na uwepo wako duniani? Au ukitoka leo hasara yake itakuwaje?

Hao wote watapita lakini neno lake kristo (ambalo ndilo chimbuko la ukristo litasimama).
 
Ni siku za mwisho? Hili ndilo swali lililoanza kuumiza vichwa vya watu baada ya kijana mmoja kuibuka wilayani Rombo, mkoani Kilimanjaro na kudai ameoteshwa dawa ya ajabu na Bikira Maria inayotibu magonjwa sugu ukiwamo Ukimwi.Kama ilivyo kwa mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambikile Mwasapile wa Loliondo ambaye amejizolea umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi, kijana huyo naye amekuwa akitoa tiba kwa sh500.

Kwa imani ya waumini wa Kanisa Katoliki Duniani, Bikira Maria ni mama wa Yesu ambaye anaaminiwa na waumini wa Kanisa hilo na hata katika sala jina lake ndilo linalotumika zaidi huku wakiamini kuwa Yesu ni mtoto wa Mungu.Habari za uhakika kutoka eneo la Customs katika mji mdogo wa Tarakea, mpakani mwa Kenya na Tanzania, zilimtaja kijana huyo ambaye sasa anajiita Nabii, kuwa ni Hilary James Kitwai (28), kutoka wilayani Babati.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu kutoka Tarakea, Kitwai alisisitiza kuwa dawa hiyo ameoteshwa na Bikira Maria na Yesu na kwamba inatibu Ukimwi, Saratani, Kisukari, Shinikizo la Damu, Figo, Pumu na maradhi ya maumivu.
"Walinitokea kwenye ndoto wakanionyesha huo mti na waliniambia kwa sasa tuko wawili tu Tanzania, lakini huyo mwenzangu simfahamu. Mimi natoza Sh500 lakini katika hiyo pesa yangu na familia yangu ni Sh300 tu,"alidai.

Kitwai ambaye amekuwa gumzo katika mji wa Tarakea, alisema anakabiliwa na changamoto kubwa katika kuwahudumia wenye mahitaji kwa kuwa hana msaada na kuomba serikali imsaidie kumpatia wahudumu.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka wilayani Rombo, tayari vyombo vya ulinzi na usalama vimemzuia kwa muda, kijana huyo kutoa tiba inayofanana na ya mchungaji Mwasapile na kuitisha sampuli za mizizi anayoitumia.

Kijana huyo ambaye ni fundi baiskeli kwa miaka mingi katika eneo hilo, aliibuka Jumatatu wiki hii na kuanza kutoa tiba kwa kutumia kikombe na tayari watu takribani 100 kutoka Kenya na Tanzania wamekunywa dawa yake.

"Anadai kuwa ameoteshwa na Bikira Maria na alielekezwa huo mti ambao una utomvu na kuanzia juzi (Jumatatu),watu kama 100 hivi walishakunywa dawa hiyo ambayo wenyeji wanadai mti wake ni sumu,"kilidai chanzo chetu.Ofisa Mtendaji wa Kata ya Tarakea, Motamburu, Kimario, alilithibitishia Mwananchi kuwapo kwa kijana huyo.

Kimario alisema yeye binafsi, Ofisa Afya na Ofisa Usalama wa Taifa, walifika nyumbani kwa kijana huyo juzi na kumfanyia mahojiano."Tulimhoji akasema alitokewa na Bikira Maria na Yesu ambao walimwonyesha mti huo ambao upo katika Mto Tarakea na walimwambia yupo mmoja tayari anayetibu maradhi sugu na kwamba yeye atakuwa wa pili,"alisema mtendaji.

Kwa mujibu wa mtendaji huyo, kijana huyo aliwaeleza kuwa baada ya Babu wa Loliondo na Yeye, bado atatokea mtu wa tatu ambaye naye ataoteshwa dawa za kutibu maradhi hayo na baada ya hapo Yesu mwenyewe atakuja duniani.

"Tulimuuliza kama ameshatoa dawa hiyo kwa watu mbalimbali akasema alianza kutoa Jumapili na watu kama 20 hivi walikunywa na alitupa vipande vya miti viwili vya dawa hiyo na tumevikabidhi kwa uongozi wa juu,"alisema Kimario.

Kwa mujibu wa Kimario aliyekuwa akimkariri kijana huyo, alisema 'nabii' huyo ameamua kutoendelea kutoa tiba hiyo hadi hapo serikali itakaporidhia na kwamba kwa sasa anamuomba Mungu ampe maono zaidi juu ya dawa hiyo.

Wananchi walioongea na Mwananchi baada ya kuzagaa kwa taarifa hizo, wameitahadharisha serikali kuwa makini na watu wanaojiita ni manabii vinginevyo wananchi wanaweza kukumbwa na maafa ya kunywa sumu bila kujua.

Wananchi hao wameitaka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kuwajibika kikamilifu kwa kuzuia matumizi ya dawa ambazo hazijathibitishwa kutokuwa na madhara.Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, Anthony Tesha ambaye pamoja na kukiri kusikia habari hizo lakini alisema anaviachia vyombo husika kufuatilia jambo hilo.
 
Hebu thibitisheni hiyo habari fasta fasta kwani loliondo ni mbali sana hapo Tarakea is just a stone throw away from Dar ni gari moja tu unachukua Meridian ama dar express saa nane tisa umeshatia timu...TFDA fanyeni fasta bana... Sa tufanyeje wananchi kama serikali yetu imeamua kutupeleka kwenye mambo ya imani unadhani what to do?
 
Ingekuwa amri yangu ningefunga makanisa yote, ambayo ndo chanzo cha ujinga huu. Yamekuwa magenge ya wenye njaa kila siku wakitafuta mbinu mpya za kuibia watu. Mf. DECI lilikuwa zao la kanisa.,kina kakobe, mwingira,mzee upako-wote ni wezi wanaotumia miujiza ya kichawi ya nigeria.
 
Haya sasa....mtasikia mengi,tetesi za vita,njaa,matetemeko huo ni mwanzo wa utungu,na watu wengi watatumia jina langu kuponya na kuwadanganya hata walio wateule....Wana JF mimi sishangai haya yanayoendelea hapa kwetu..na kwa hakika nategemea mengi zaidi....ni wakati wa kila mtu kumuuliza Mungu yaliyo kweli ni yapi......
 
kwa nini itokee tu tanzania? na siyo sehemu nyingie ya dunia? kama ni tanzania kwanini iwe kaskazitu tu?
 
hii imenistua kidogo coz pale tarakea ndio home town kabisa
nimewasiliana na watu kule wameniambia kijana malaria ilikua imepanda kumkichwa.
amechukuliwa jana jioni na ameshikiliwa na polisi kwa mahojiano.

Hee kumbe we homeboy!! wapi kikelelwa, kimanyatu, kasirwa, mbomai, nduweni,etc etc...nimeongea na jmaa hawamkubali kabisa. Lakini kumbuka nabii hatambuliki kwao. Hata babu wa loliondo alikuwa akilalamika kwamba alishawaambia wenyeji wachukue dawa wakawa wanampuuza!!
 
Ina bidi watanzania tuwe macho na hawa jamaa, kweli ni muujuzi lakini yatupasa pia kumomba Mungu ili atupe uhakika wa manabii hawa kama kweli wametumwa na Mungu awu ni wasanii, kwani kama Mungu anawezakukuotesha dawa ashindwi kuonyesha na watenda kazi wenzako
 
Back
Top Bottom