Robert Novak dies:

Mwawado

JF-Expert Member
Nov 2, 2006
993
252
Mwandishi wa Habari wa siku nyingi Robert Novak amefariki Dunia asubuhi hii.Bob Novak alikuwa anasumbuliwa na Brain Cancer.Novak mwenye umri wa miaka 78 alifanya kazi na Kampuni ya Television CNN kwa miaka 25.Atakumbukwa zaidi kwa vipindi vyake vya Uchambuzi wa mambo ya siasa kama "The Capital Gang" na "Crossfire".

Mwaka 2003 Bob Novak aliingia katika matatizo na Vyombo vya Usalama baada ya kuweka wazi jina la Afisa wa Usalama ambaye alikwenda Africa kutafuta ushahidi wa ununuzi wa Uranium kwa ajili ya silaha za Nuklia,zilizothamiwa kuwepo Iraq.Jina la Afisa huyo lilitangazwa kuwa ni Valerie Plame Mke wa Mwanadiplomasia Wilson.Kutokana na sakata hilo Bob Novak aliwataja Richard Armitage (Deputy State Secretary) na karl Rove (Chief presidential Advisor) kuwa ndio waliomtajia jina la CIA agent huyo.

Pamoja na kufanya mambo yake mengi washington DC,Novak ni Conservative Columnist kwenye magazeti mengi Chicago,Ni Mzaliwa wa Jollie,Il.Mwenyezi mungu amlaze Mahali pema Peponi!
 




r-NOVAK-large.jpg


 
Back
Top Bottom