Riziwan awavuruga UVCCM Dodoma na mamilioni

Malisa ni lowasa na lowasa ni antony mavunde na ndo mloyafanya haya mloyaandika hapa,msione watu ni wajinga.
 
Bangi za mchana zinakusumbuwa, labda ungesema hata wachawi ambao wako nje ya CCM ningekuelewa.
Kuwa mtoto wa Rais haimaanishi kuwa asishiriki siasa, huo ni uelewa finyu, kama yuko kwenye political platform na anashindana hiyo ndiyo siasa, hauwezi kumubagua kwenye siasa kisa yeye ni mtoto wa Rais, hakuna kitu kama hicho, mwenye Urais ni baba yake siyo yeye, kama kuna watu wanamuogopa na kufuata kila kitu anachokisema hata kama si cha msingi hilo ni tatizo lao siyo lake. Katika siasa hakuna cha kupewa kila kitu lazima uwekeze, kuwekeza siyo lazima rasilimali fedha hata rasilimali watu, hata kama hauna fedha kama kipaji unacho watu watakuona tu. Pambana, acha kulalamika.
 
Malisa ni lowasa na lowasa ni antony mavunde na ndo mloyafanya haya mloyaandika hapa,msione watu ni wajinga.

Naanza kuwa na wasiwasi na vijana walioko kwenye politics, napata hisia za kushiriki politics, maana wengi wao ni waoga wa kushindana, wanataka mwenzao asishiriki ili wapata mteremko, jamani pandeni mlima! hapo ndipo tutajua kweli mmekomaa na mnastahili kuwa viongozi wa siku za usoni, haiwezekana mfanye siasa za majungu then mseme mnastahili, Malisa na Mavunde kuna kipi ambacho ni tangible kama kipindi cha uongozi wenu? acheni siasa za rejareja. Pigeni mzigo, wanaume gani mnaona kivuli harafu mnakimbia! hamfai hata kuwa viongozi wa familia zenu.
 
Malisa bana,anaichezea uvccm kama kampuni ya baba ake,ngoja aendelee kumtumikia fisadi af ataishuhudia hukumu ya watanzania
 
Nyie ritz mnamsingizia mwenzenu alisema ana toyota vista na milioni 2 bank,hizo ametoa wapi?au ndo zile ambazo hutoka TRA mojakwamoja Ikulu bila kupitia Hazina?
 
mkuu unaonekana ni mpambanaji mzuri tatizo huko kwenu CCM.
Wapi wewe, kazidiwa kete huyu. Wacha kawaida yao (Takrima a.k.a Mlungula) uchukue nafasi yake. Ndo zao hizo.
Magamba ukiona wanalia rafu ujue mwenye kisu kikali anakula nyama. Yaani Mjanja ni yule mwenye nazo. Wakafie mbali !
 
Unahitaji vithibitisho gani.Ni jambo la ajabu kabisa kuona kijana anatumia wadhifa wa baba yakwe ku-dictate uongozi uliochaguliwa kihalali.UVCCM haiwezi kuamuliwa mambo yake na familia moja na wakae wakijua hilo halitafanikiwa.Watu wapo radhi hata kutumia nguvu na kuomba ushirikiano kwa vijana ambao wako nje ya chama
Well said Shigella.
 
Siyo dom tu,hata moro kafika kuna mshkaji jina lake limekatwa yani analaumu kinoma
 
Mtoto Rais Jakaya Kikwete, Riziwan, ambaye yupo Dodoma kuhudhuria vikao vya Kamati ya utekelezaji na Baraza kuu la vijana huko Dodoma amewavuruga vijana wenzake baada ya kuzidiwa hoja na vijana wengi nchi nzima kwenye vikao hivyo, sasa akaanza kutumia nguvu ya mamlaka/dola na mabilioni ya pesa ambayo amejitengenezea katika kipindi hiki cha Urais wa baba yake.

kwanza, anamtumia mtumishi wa UVCCM, Mzee Mipiko kubadilisha muhtasari/minutes za vikao vyote ili kuweza kulinda hoja zake ambazo alishindwa kwenye vikao. na kwasababu maamuzi ya UVCCM bado yanahitaji baraka za baba yake/ mwenyekiti wa chama, basi anataka kupeleka mapendekezo ambayo ni ya kulinda maslahi yake na Membe. bahati mbaya Katibu mkuu Shigela amekuwa makini sana na hata akamtonya Makamu Beno na muhtasari zote zikabadilishwa na zinaendelea kubadilishwa kutokana na mapendekezo ya vikao vya vijana.

pili, katika kujaribu kuanza kufanya kampeni ya watu kwenye uchaguzi nchi nzima na taifa, kwanza ni jambo ambalo linashangaza wengi, kwasababu anafanya kama vile Kikwete anautafuta Urais wa awamu ya tano au labda yeye angaombea. Kwakweli amejenga historia mpya ya familia za marais kwa nchi yetu ya Tanzania. Kwahiyo jana usiku aliwaita MAKATIBU WOTE wa MIKOA wa UVCCM na kuwapatia kila mmoja Tsh MILIONI MOJA, maana yake kama takribani MILIONI 30 jumla, na akwapa maelekezo na kuwatishia wengine kwamba wasipotii, ajira zao zitasitishwa. Haya nia matumizi mabaya sana ya madaraka na fedha za umma. Tunaomba tuikemee wote.

ni mtoto wa rais nyinyi vijana wa ccm mwacheni!mtapoteza madaraka! mimi nasema tena mwacheni kabisa anakijenga chama huyo nyinyi uvccm akiacha kufadhili nyny mtakufa
 
Back
Top Bottom