Riz"One" mtoto wa Mzee wa Kaya

Status
Not open for further replies.
Wa Tanzania watu wa ajaabu sana,nina hakika wengi wanaondika hapa hawamjui huyu kijana kwa karibu ila wananukuu magazeti ya ajabu ajabu,sasa sikilizeni, mimi nimekuwa naye karibu sana katika matukio fulani fulani and this is my observation on him:Muungwana na malezi mema ana adabu kwa wakubwa zake na wadogo pia, hamwogopi mtu kwa jina au pesa zake.ana mwoogopa mungu,ni baba wa familia yake,amesoma hakubweteka na vyeo vya babake kwa maana sio kula kulala,kuwa mtoto wa Rais haina maana asijihusishe na maswala ya kijamii.
wivu unawasumbua acheni ufala

wewe ni mlamba miguu. ni mmoja kati ya wale wanaoneemeka na ofa zake ndio maana unatetea malezi yake na utu wema wake. kama ndugu zake tu wa karibu wanamtaja kuwa mtu mnafiki, wewe unajuaje kuhusu wema wake?
elimu gani unasemea? hiyo ya kufanyiwa mitihani?
huo ndio ufala ukisikia. Mbeleko unayotaka kumbebea, huiwezi
 
Namaki acha kutuchanganya sisi eti ana adabu kwa wakubwa na wadogo so kama ni mchafuzi asiambiwe??!! Huwezi kutumikia mabwana wawili yeye anafikiri ukubwa wa baba yake ni ukombozi wa maisha yake yana mwisho haya kwani baba yake atakuwa ikulu milele yote???Tutaonana mitaani tu halafu atajikuta kumbe yupo sawa tu na yeye yule huyu na wale...
 
Wa Tanzania watu wa ajaabu sana,nina hakika wengi wanaondika hapa hawamjui huyu kijana kwa karibu ila wananukuu magazeti ya ajabu ajabu,sasa sikilizeni, mimi nimekuwa naye karibu sana katika matukio fulani fulani and this is my observation on him:Muungwana na malezi mema ana adabu kwa wakubwa zake na wadogo pia, hamwogopi mtu kwa jina au pesa zake.ana mwoogopa mungu,ni baba wa familia yake,amesoma hakubweteka na vyeo vya babake kwa maana sio kula kulala,kuwa mtoto wa Rais haina maana asijihusishe na maswala ya kijamii.
wivu unawasumbua acheni ufala

Watanzania kwa mwendo huu hatutapata kuendelea, unakuta mtu anambeza Ridhwan eti tu kwa sababu ni mtoto wa Rais basi asishiriki katika kujenga nchi yake. binafsi sioni tatizo kama atafanya kitu kwa maslahi ya taifa. hapa hoja isiwe ni mtoto wa rais kwa hiyo akiona jambazi aogope kujitokeza kwa sababu tu ni mwana wa rais sio dunia ya kisasa inakokwenda.

Ridhwan ni msomi wa degree mbili na amesoma kwa fedha za watanzania ni lazima ashiriki kuijenga nchi yake kama njia ya kurejesha fadhila bila kujali ni mtoto wa rais. Ni vizuri tukamhukumu Ridhwan kwa tukio moja ama jingine lakini sio kumhukumu kwa kuwa ni mtoto wa Rais. Wapi kwenye katiba ya Tanzania palipozuia mtoto wa Rais kutoshiriki katika shughuli za nchi. Mbona watu mna uchungu wa kwamba Ridhwan atampotezea umaarufu baba yake kuliko Rais mwenyewe kwani Rais akianguka kwa sababu ya mwanaye inawakereketa nini? pilipili msioila yawawawashia nini au mna ajenda ya siri?

Mke wa Rais pia ni lazima ajitokeze kusaidia watanzania kwani wote wapo Ikulu kwa kodi zetu kwa nini mnataka wakae kimya hata pale mambo yanapoharibika nchini. Nani asiyejua kwamba kauli ya mtoto wa Rais katika mambo ya msingi ya nchi ina nguvu kuliko mimi na wewe?

Hebu angalia majuha, ni kosa gani hata kama Ridhwan akatoa taarifa ya uhamiaji/uraia kwamba baba kuna habari mpya kwamba Bashe sio raia naomba fuatilia. Huu ni uzalendo wa juu kwa mtoto wa Rais acheni kukimbilia tu kwamba kafanya hivyo kwa visasi. Hata hivyo nani ana uhakika kati yetu kwamba Ridhwan amefanya hivyo zaidi ya kusoma katika magazeti.

Ridhwan hata angefanya mambo ya sheria ambayo kasomea na anafanya hata sasa bado mtasema mtoto wa Rais katumia nafasi ya baba yake kushinda kesi au kuwashawishi majaji kushinda kesi.
 
Wa Tanzania watu wa ajaabu sana,nina hakika wengi wanaondika hapa hawamjui huyu kijana kwa karibu ila wananukuu magazeti ya ajabu ajabu,sasa sikilizeni, mimi nimekuwa naye karibu sana katika matukio fulani fulani and this is my observation on him:Muungwana na malezi mema ana adabu kwa wakubwa zake na wadogo pia, hamwogopi mtu kwa jina au pesa zake.ana mwoogopa mungu,ni baba wa familia yake,amesoma hakubweteka na vyeo vya babake kwa maana sio kula kulala,kuwa mtoto wa Rais haina maana asijihusishe na maswala ya kijamii.
wivu unawasumbua acheni ufala
Unajua yaliyomkuta pale Formerly known as faculty of law???
Walikula kichwa ila fitna ikatembea ndo akamaliza
 
Ngoja nimsaidie jibu ni [d], mi nilishawaambia hii familia ni limbukeni haikustahili hadhi iliyopewa kama familia yakiongozi mkuu wa taifa.

Angalia familia za marais waliotangulia ya Nyerere, Mwinyi na Mkapa mbali ya madudu yaliyofanywa na baba zao lakini watoto na familia hizo zilijua nini maana ya wazazi wao kuwa viongozi wakuu wa taifa. Wengine hata watoto wao hatuwajui si kwamba hawakuwa na uwezo wa kutumia madaraka ya baba zao, lakini kutokana na umuhimu na unyeti wa cheo hicho waliona si busara kuingiza mambo ya kifamilia ndani.

Nafikiri hii inatokana na mkuu wa familia anavyolichukulia jambo hilo, najua kabisa watoto wa Nyerere au Mkapa walivyokuwa wanapata ushauri toka kwa baba zao kwamba watenganishe kazi ya serikali (ikulu) na kazi za kifamilia yaani wazingatie masomo kwanza au wawe na shughuli zao tofauti kabisa.

Luteni unatoka nje ya hoja, ni makosa kumlinganisha Ridhwan na watoto wa Nyerere, Mwinyi na Mkapa. sio jambo la kawaidia kwamba watoto wa marais watakuwa na mfumo mmoja wa maisha. Wapo wataokapenda siasa na wengine mambo mengine, kama vile udaktari,uhandisi, ugavi, wachumi. Kwa mfano, Rose kamili mke wa Dr Slaa ameonekana kujitokeza sana katika siasa za nchi na tunaamini anafanya hivyo kwa maslahi ya wote, je leo Dr Slaa akiwa Rais ungependa mama huyo kuwa bubu au aache kabisa kumshauri mume wake kwa sababu tu ni mke wa Rais. kwa taaluma Ridhwan ni mwanasheria, Rais Kikwete aache kuomba ushauri wa kisheria kwa mwanaye kwa sababu zipi? Lakini pia watoto wa marais wanazidiana weredi sio vema kuwalinganisha watoto wa rais mmoja na mwingine. Mwalimu Nyerere alikuwa mjamaa mbona hivi sasa uchumi wetu ni wa soko huria hauoni kulinganisha nyakati kwa kufuata nafasi za viongozi ni fikra nyepesi?
 
I hope Riz"One" huwa anapitapita hapa... ukiona mtoto wa rais tena kiongozi wa umoja wa vijana wenye nguvu, mjumbe wa mkutano wa chama tawala, kada na kamanda wa vijana tena mwanasheria, zaidi pia ni mdau wa klabu kubwa zaidi tanzania anachorwa hivi ujue ana matatizo makubwa na kama ana akili timamu basi akae pembeni na kushika moja...

A GOOD LIFE IS A PRODUCT OF A HUMBLE BEGINNING, AND ITS DEFINITELY KWAMBA THEY BOY HAS LOST IT
UNLESS NI ILE SMEARING CAMPAIGN KAMA KAWA INAMHARIBIA DOGO

Ridhwan nimesoma naye sheria pale chuo Kikuu cha dar es salaam ni kijana mnyenyekevu sana na rafiki wa wanyonge na mtetezi wa haki. Tulipokuwa chuo kikuu Ridhwan alionekena kuwa na msimamo thabiti linapojitokeza jambo lenye kuathiri maslahi ya wengi.Ridhwan alikuwa anajituma katika masomo na kufanya vizuri kama ilivyo kwa mtoto yoyote wa maskini. Ridhwan hana papala bali ni mkweli na hilo pengine ndilo mwiba mchungu kwa baadhi ya watu. Mara kadhaa anasema alisomea sheria ili kuwakomboa watanzania wanyonge. tumpe support kijana huyu na tumsaidia kumshauri pale ambapo atateleza kama ilivyo kwa binadamu yoyoyte yule.
 
Wa Tanzania watu wa ajaabu sana,nina hakika wengi wanaondika hapa hawamjui huyu kijana kwa karibu ila wananukuu magazeti ya ajabu ajabu,sasa sikilizeni, mimi nimekuwa naye karibu sana katika matukio fulani fulani and this is my observation on him:Muungwana na malezi mema ana adabu kwa wakubwa zake na wadogo pia, hamwogopi mtu kwa jina au pesa zake.ana mwoogopa mungu,ni baba wa familia yake,amesoma hakubweteka na vyeo vya babake kwa maana sio kula kulala,kuwa mtoto wa Rais haina maana asijihusishe na maswala ya kijamii.
wivu unawasumbua acheni ufala

Namaki
  • profile.png
    View Profile
  • forum.png
    View Forum Posts
  • message.png
    Private Message
  • article.png
    View Articles
  • add.png
    Add as Contact
user-offline.png
Junior Member Join Date Mon Aug 2010
Posts 5
Thanks : 0
Thanked 0 Times in 0 Posts

Sina haja ya kushangaa! Huyu bila shaka ni Malaria Suguu!:confused2::confused2::confused2:
 
Ridhwan nimesoma naye sheria pale chuo Kikuu cha dar es salaam ni kijana mnyenyekevu sana na rafiki wa wanyonge na mtetezi wa haki. Tulipokuwa chuo kikuu Ridhwan alionekena kuwa na msimamo thabiti linapojitokeza jambo lenye kuathiri maslahi ya wengi.Ridhwan alikuwa anajituma katika masomo na kufanya vizuri kama ilivyo kwa mtoto yoyote wa maskini. Ridhwan hana papala bali ni mkweli na hilo pengine ndilo mwiba mchungu kwa baadhi ya watu. Mara kadhaa anasema alisomea sheria ili kuwakomboa watanzania wanyonge. tumpe support kijana huyu na tumsaidia kumshauri pale ambapo atateleza kama ilivyo kwa binadamu yoyoyte yule.

Sikubaliani na hizo red sana sana nashukuru kwamba umesoma naye. Unaweza kututhibitishia uwezo wake unaosema alifanya vizuri katika masomo? Ninachojua ni kilaza fulani tu. Unaweza kutuonyesha dalili hata moja ya dhamira ya kuwakomboa wanyonge? Tangu lini akawa mkweli huyu na ukweli ni kitu gani au unafiki wa kuvuruga hali ya hewa UVCCM na Yanga ndiyo ukweli? Ni mtizamo tu!!
 
Huyu mtoto ni hatari kuna member mmoja kasema anaweza kum cost baba yake, kachafua hali ya hewa UVCCM, kachafua Jangwani kawanyang'anya CCM fomu ya kutafuta wadhamini wa baba yake haya yote si haba katika duru za siasa.

Jamani tujiulize swali, Msauni alidanganya umri na kulazimika kujiuzuru nafasi yake ya uenyekiti wa UVCCM na Bashe anadaiwa kadanganya Uraia na hawa walikuwa viongozi wa UVCCM, je Rais angewapa kusimamia udhamini wasingedanganya? Kimsingi suala la kutafuta fomu sio la chama ni la mgombea binafsi na hii ni kanuni ya kuweka uwanja sawa na wa haki kwa wagombea. Kwa mfano, ndani ya CCM kungeweza kujitokeza wagombea wengi na kila mmoja anatafuta wadhamini hivyo sio haki kwa Rais aliyeko madarakani kuwatumia viongozi wa chama kumtafutia wadhamini kwani nafasi yake inaweza kuwanyima haki sawa wagombea wengine, kwa maana kwamba wanachama wa CCM wataelekeza nguvu yao zaidi kwa Rais anayemaliza muda wake kuliko wagombea wengine. Hapa ndipo umuhimu wa kila mgombea kutafuta watu wake linapojitokeza. Katiba ya CCM haizuii kumtumia mtoto au ndugu kutafuta wadhamini vivyo hivyo katiba za vyama vingine vya siasa isitoshe Ridhwan hakuwa peke yake alikuwa na vijana wengine 32. Wakati wa mchakato wa uchaguzi Rais naye ni mgombea kama wengine anajivua nafasi yake ili kutoa haki sawa.
 
Ridhwan nimesoma naye sheria pale chuo Kikuu cha dar es salaam ni kijana mnyenyekevu sana na rafiki wa wanyonge na mtetezi wa haki. Tulipokuwa chuo kikuu Ridhwan alionekena kuwa na msimamo thabiti linapojitokeza jambo lenye kuathiri maslahi ya wengi.Ridhwan alikuwa anajituma katika masomo na kufanya vizuri kama ilivyo kwa mtoto yoyote wa maskini. Ridhwan hana papala bali ni mkweli na hilo pengine ndilo mwiba mchungu kwa baadhi ya watu. Mara kadhaa anasema alisomea sheria ili kuwakomboa watanzania wanyonge. tumpe support kijana huyu na tumsaidia kumshauri pale ambapo atateleza kama ilivyo kwa binadamu yoyoyte yule.
Thanks mkuu..., ndio maana nikamalizia kwa kusema, "i hope ni smearing campaign tu!!!
 
Huyu siku hizi jina lake ni Uday Saddam Hussein al-Tikriti wa Bongo. Utafikiri ni copy ya yule mtoto wa Sadam kabisaaaaa

Haya ni matusi, administrator wafungie watu wa aina hii. Humu ndani weredi ni wengi ni bora zaidi kubishana kwa hoja. Kama hana la kuchangia kuhusu hoja hii ni bora kukaa kimya ni kama una chuki binafsi dhidi ya Ridhwan
 
Jamani tujiulize swali, Msauni alidanganya umri na kulazimika kujiuzuru nafasi yake ya uenyekiti wa UVCCM na Bashe anadaiwa kadanganya Uraia na hawa walikuwa viongozi wa UVCCM, je Rais angewapa kusimamia udhamini wasingedanganya? Kimsingi suala la kutafuta fomu sio la chama ni la mgombea binafsi na hii ni kanuni ya kuweka uwanja sawa na wa haki kwa wagombea. Kwa mfano, ndani ya CCM kungeweza kujitokeza wagombea wengi na kila mmoja anatafuta wadhamini hivyo sio haki kwa Rais aliyeko madarakani kuwatumia viongozi wa chama kumtafutia wadhamini kwani nafasi yake inaweza kuwanyima haki sawa wagombea wengine, kwa maana kwamba wanachama wa CCM wataelekeza nguvu yao zaidi kwa Rais anayemaliza muda wake kuliko wagombea wengine. Hapa ndipo umuhimu wa kila mgombea kutafuta watu wake linapojitokeza. Katiba ya CCM haizuii kumtumia mtoto au ndugu kutafuta wadhamini vivyo hivyo katiba za vyama vingine vya siasa isitoshe Ridhwan hakuwa peke yake alikuwa na vijana wengine 32. Wakati wa mchakato wa uchaguzi Rais naye ni mgombea kama wengine anajivua nafasi yake ili kutoa haki sawa.

Mkuu, kwani mwaka 2005 hii kanuni haikuwepo? Au 2005 walivunja kanuni leo 2010 ndo wamezinduka kuifuata? ...changanya na za kwako...
 
Huyu bwamdogo bora angebaki tu kwenye law firm ya kins Masha akaganga njaa siyo kujiingiza kwenye siasa ataishia kujichafua tu!
Na huko kwenye law firm ( kampuni ya sheria) mngemzulia jambo kwani huko ndo angekuwa sio mtoto wa Rais?
 
Haya ni matusi, administrator wafungie watu wa aina hii. Humu ndani weredi ni wengi ni bora zaidi kubishana kwa hoja. Kama hana la kuchangia kuhusu hoja hii ni bora kukaa kimya ni kama una chuki binafsi dhidi ya Ridhwan

Nashauri urudie tena na tena kusoma sheria za JF kabla ya kukilimbilia kwa admin. Mkuu uko hapa toka 2008 au sivyo?
 
Mkuu wa kaya anajaribu ku kompansate mapenzi aliyomnyima mtoto wake wakati wa utoto kwa kutumia ofisi yetu namba moja ya nchi.
Mapenzi yaliyokosekana utotoni hapatikani hata siku ya kuzikwa, mzee amechelewa anachofanya ni kujiongezea madhira na kuwpa watu cha kumsulubisha akiwa madarakani na vibaya mno atakapotoka ikulu. Kipofu toka lini akamuongoza kipofu mwenzake

Kuna bwana mmoja aliniambia kuwa hadi sasa Rais KIKWETE anasomesha watoto wake hapa tanzania tabia ambayo baadhi yetu tunadhani hawajali watoto ingawaje pia angewapeleka wote nje tusingekosa la kusema. kukosoa ni jadi yetu kuliko kutoa majibu mbadala

Naamini tabia hii ni mojawapo ya sababu zinazomfanya Domokaya kuona kwamba Rais hawajali watoto kwa kuwa nasikia Rais anataka watoto wake waishi maisha kama watanzania wengine na hili sio siri ndio maana watoto wanasoma nchini. Wapo wanaosema Rais KIKWETE hajaanza kushika madaraka leo wanaomjua tangu huko zamani wanasema maisha yao ni ya kawaida hadi sasa na ni wepesi wa kujichanganya na watanzania wengine?

kusema Mzee anarudisha mapenzi kwa Ridhwan aliyomnyima utotoni haina uzito ni mapenzi yapi unayotaka mzazi kutoa kwa mtoto wake zaidi ya kumpatia elimu ili aweze kujitegemea na huu ndio urithi mkubwa. Naamini Ridhwan hawezi kuganga njaa hata pale baba yake atakapotoka madarakani kwani ni msomi mzuri katika umri mdogo.
 
Luteni unatoka nje ya hoja, ni makosa kumlinganisha Ridhwan na watoto wa Nyerere, Mwinyi na Mkapa. sio jambo la kawaidia kwamba watoto wa marais watakuwa na mfumo mmoja wa maisha. Wapo wataokapenda siasa na wengine mambo mengine, kama vile udaktari,uhandisi, ugavi, wachumi. Kwa mfano, Rose kamili mke wa Dr Slaa ameonekana kujitokeza sana katika siasa za nchi na tunaamini anafanya hivyo kwa maslahi ya wote, je leo Dr Slaa akiwa Rais ungependa mama huyo kuwa bubu au aache kabisa kumshauri mume wake kwa sababu tu ni mke wa Rais. kwa taaluma Ridhwan ni mwanasheria, Rais Kikwete aache kuomba ushauri wa kisheria kwa mwanaye kwa sababu zipi? Lakini pia watoto wa marais wanazidiana weredi sio vema kuwalinganisha watoto wa rais mmoja na mwingine. Mwalimu Nyerere alikuwa mjamaa mbona hivi sasa uchumi wetu ni wa soko huria hauoni kulinganisha nyakati kwa kufuata nafasi za viongozi ni fikra nyepesi?

Kuna mtoto wa Mkapa ni TEJA, na kapigwa marufuku kuingia Marekani (USA). Mtoto wa JKN aliingia katika Siasa vile vile, na kunawakati alikuwa upinzani (nccr) si na aliongea maneno mabaya sana kuusu baba yake....je hayo ni malezi kutoka kwa ticha JKN?!
 
Jamani tujiulize swali, Msauni alidanganya umri na kulazimika kujiuzuru nafasi yake ya uenyekiti wa UVCCM na Bashe anadaiwa kadanganya Uraia na hawa walikuwa viongozi wa UVCCM, je Rais angewapa kusimamia udhamini wasingedanganya? Kimsingi suala la kutafuta fomu sio la chama ni la mgombea binafsi na hii ni kanuni ya kuweka uwanja sawa na wa haki kwa wagombea. Kwa mfano, ndani ya CCM kungeweza kujitokeza wagombea wengi na kila mmoja anatafuta wadhamini hivyo sio haki kwa Rais aliyeko madarakani kuwatumia viongozi wa chama kumtafutia wadhamini kwani nafasi yake inaweza kuwanyima haki sawa wagombea wengine, kwa maana kwamba wanachama wa CCM wataelekeza nguvu yao zaidi kwa Rais anayemaliza muda wake kuliko wagombea wengine. Hapa ndipo umuhimu wa kila mgombea kutafuta watu wake linapojitokeza. Katiba ya CCM haizuii kumtumia mtoto au ndugu kutafuta wadhamini vivyo hivyo katiba za vyama vingine vya siasa isitoshe Ridhwan hakuwa peke yake alikuwa na vijana wengine 32. Wakati wa mchakato wa uchaguzi Rais naye ni mgombea kama wengine anajivua nafasi yake ili kutoa haki sawa.

I can see a lost Puppy on the street!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom