Risk Assessment and Management: CHADEMA nayo Imuondoe Dr. W. Slaa!

Waberoya lazima tuelewe kuwa unapopigania haki kati ya watu wasiotaka haki utapachikwa shutuma nyingi mno lakini uvumulivu unahitajika,sio ukishutumiwa tu unajivua gamba wakati huna gamba.Magamba yako ccm wamevua na wataendelea kuvua.
 
Miaka ya 1990's DP ya Mtikila, 1995+ NCCR ya Mrema, 2005+ Chadema. Kipindi chote hiki CCM wameendelea kuongoza. Kupendwa kwa ushabiki tusijidanganye. Kama kuna uchafu fatiki ya usafi ifanyike. Tusiwe wabishi Chadema ikitajwa na kushangilia CUF, CCM au NCCR vikipondwa.

Mchukiaufisadi,

Uko right na approach kama hii hakuna mtu wa kuikataa. Tumekuwa na ushabiki ambao nawezxa sema ni kama vile sisi na DINI zetu that hatujui what next after this life. We are tired with CCM at any cost. Kama tungekuwa na maisha ya kisiasa kama kule US kwa kweli wala tusingehangaika.

Progress ya CDM sio mbaya, kina mvuto na nasema hivyo tofauti na Wabe ambae huenda ana mapenzi mema na CDM yasio na busara lakini kitendo cha kuwa Active politics (kongamano la dodoma, movement za God, na pia move na huu mswaada wa katibu) zinaonyesha wapo kazini na kila siku wanasikika.

Lakini kuna makosa ambayo CDM wanayo (nakumbuka kuna hoja moja wa MKJJ) na slowly they are working on it na nina uhakika in next 2 years CDM will be a different part. Mimi ni just a member ambaye sina mawasiliano wala ukaribu na kiongozi yeyote. Labda kipind cha kampeni i did my part through district leaders. tuwape muda hasa ukuzingatia ruzuku ya 200ml per month na michango wa wanachama, na sas rasmi mali watu ndo tunawapaat. Yaani sifa anazozipata Godbless Lema u can understand tuna kiu fulani ambayo huenda akaptikana mtu akaisoma na kuitekeleza, the we will get there as a unique political party in TZ. Lakini hakuna anaezungumzia udini wala propaganda za CCM.

Asante sana
 
Waberoya

Kwa hiyo wewe kwa mtazamo wako ulitaka CDM imsimamishe mgombea urais mwenye sifa hizi;

1. Asiwe Mkristo, especially mkatoliki aliyewahi kusomea upadri ili kuwavuta waislamu
2. Asiwe anatokea kanda ya kaskazini kuondoa dhana ya uchaga (japo yeye mwenyewe si mchaga)

KISA??.....Propaganda za CCM!!!

Hizi ni siasa za ki-lofa kabisa!!

Kwa mtaji huu hata wewe mwenyewe inabidi ujivue gamba!!!
 
Tukikubali hoja ya Waberoya Wakristu waanze kuogopa kufikiria kushika nafasi ya uongozi. Hili ni pendekezo la hatari.
 
Conclusion zako kwenye post mbili zimenifanya nikuweke kwenye -ignore list, umeandika kama una uhakika kabisa! my God! namna hiyo unaweza kumgomnaisha mama yako na baba yako, ukimuona mama anaongea na mzee fulani utatoa conclusiona na kumweleza baba! childish, watu wanashindana kwa hoja na si kusingiziana vitu ambavyo personally unajua si kweli na kama unaamini umekosea!

poor MTM!


Kwa mkuwa hicho ndiyo kiwango chako cha kufikiria na kulinganisha masuala, ni dhahiri kwamba upeo wako unazidi kushuka siku hadi siku.

Kwa muktadha huo huo si ajabu ukamshauri baba yako amuache mama yako kwa kuwa jirani yake kaamua kuachana na mkewe!!

Yaani bora kumsikiliza tambwe hiza kuliko kusoma ushauri wako!!
 
Angalieni hoja za wana CDM-JF mpaka wanatia huruma, kichefuchefu tupu

SIJASEMA SEHEMU CDM INA GAMBA!! CDM haina tatizo lolote ila lisiasa kuna wakati huwa haueleweki unavyotaka ueleweke! nimetoa mifani ya salim na zuma, still you guys purposely mna -digress hoja!!

nwaonea huruma sijaona hoja , waislamu hawawatki BADALA YA KUWAAMBIA VIONGOZI WENU WAPIGANE NA HIYO HALI, MNABAKI KUTUMATUMA VIPOST VYA KISHABIKI..UJINGA HUO

HOJA ni kuwa CDM ifanye nini kujikwamua na hali hii kama mnaona is ok tuendelee!

Wabe,
Hivi unaweza kuishauri nini CCM endapo CDM watatumia ukristo wao makanisani kuiponda CCM kama chama cha KIISLAM? je utawaambia wasimsimamishe Vuai Nahodha siwecandidate wao wa 2015 kisa tu Muislam? au unataka kusema Wakristo ni wanafiki wasioweza kuyaona wafanyayo waislam na kuyajibu? Je unafikiri hiyo ulosema ndiyosolution Mkuu Wabe? Unaweza kujitokeza kunijibu haya?
Uliyoyasema yote ni SAWA ila si KWELI! Na yanapingana na fikra za wenye HEKIMA NA BUSARA NA wanazuoni.. Here i mean to solve the problems you need not to escape rather than face them.
 
Sasa tumuondoe nini?
  1. Uanachama(si mkatoliki pekee mwanachama)
  2. Ukatibu mkuu(Mangula ni mkatoliki)
  3. Ugombea Urais(uchaguzi umeisha na si lazima yeye agombee tena 2015)
 
Huyu Waberoya anayejifanya "kuzijali sana kura za waislamu" ndiye number one hater wa dini yao (alikiri yeye mwenyewe humu kuwa anauchukia uislamu).

Ana Inferiority complex mbaya, yuko very insecure. na hii yote ni matatizo ya kisaiokojia kwa sababu alikiri yeye mwenyewe humu JF kwamba mke wake ni mwislamu, sasa kwa wataalamu wa Saikolojia watafahamu kwamba chuki zake zimeanzia hapoooo, kwa kuwa ameshindwa kumfanya mke wake aamini katika kile anachokiamini yeye basi hasira zooote badala ya kuzihamishia kwa mke wake kwa sababu anampenda, basi anazihamishia katika dini ya mkewe, na ndiyo hasa huenda ikawa sababu ya kwa nini anachuki kali dhidi ya Uislamu.

Mimi ni Mwsilamu na ninaunga mkono sera za Chadema kwa sasa kwa hiyo hoja ya huyu Waberoya ya kwamba Waislamu hawaipendi Chadema ni Fallacy , lakini naamini kwa dhati kwamba lazima Slaa awaingage waislamu, na kuwashawishi kwa hoja kwamba yupo kwa maslahi ya Watanzania wote, na ninaamini kabisa kwamba Chadema ikiri kuna Tatizo la udini nchini na isaidie namna ya kulitatua, lakini pendekezo kama la huyu Waberoya, ni pendekezo mfu, si la maslahi kwa Wapenda mageuzi, na ni katika kile tunachokiita "Jaribu kupinga wengi kwa anti-hoja ili uonekane una akili"
 
Waberoya tumekusoma , tumekuelewa, wewe ni mujahidina uliyepewa jukumu la kupambisha moto hoja ya udini na mafisadi wa nchi hii. Hakuna ubishi kuwa muasisi wa hoja hii ni JK, na aliyeipigia debe kwa umma ni RA kupitia magazeti yake, na wewe Waberoya ndiyo unaindeleza hapa JF. Umejaribu kujificha lakini kwa kauli yako kuwa CDM haitakiwi na waislamu umejivua gamba na umesomeka vizuri. Labda nikuambie jambo moja Wabe, huwatendei haki Waislamu wenzako na Uislamu kwa ujumla kwa kuwaweka kwenye kapu la ujinga kuwa wanaweza kuwa vipaza sauti vya mafisadi.Wapo Waislamu wengi tu wenye akili zao timamu na wenye kuheshimika ambao wanamkubali Dr. Slaa na CDM kwa hoja wanazobeba za ukombozi wa Taifa letu toka mikononi mwa wakoloni weusi CCM. Nakushauri uwaombe radhi Waislamu kwa kuwadhalilisha, kama wewe umelipwa kufanya kazi hiyo endelea kwani ndiyo mradi uliochagua kujikimu lakini usiwhusishe Waislamu.
 
Huyu jamaa anaonekana ni mamluki anataka kutuharibia chama chetu, ametumwa mwogopen kama ukoma. kwa wale wakristo wanaelewa imeelezwa tujihadhari na wapinga kristo. Huyo nae ni wa type hiyo kama ckosei. but hii ni kwa mtazamo wangu.
 
ND. Wana JF,

Mimi naona hatujamuelewa mkuu Waberoya, anachotaka kusema hapa ni kwamba haikuwa kosa kumchagua Dr. Slaa kuwa mgombea, isipokuwa kwa bahati mbaya historia yake ya kuwa aliwahi kuwa padre kwa namna moja au nyingine kuna baadhi ya watu wameitumia vibaya either kwa makusudi ilikupotosha au kwa bahati mbaya kwa kutokujua ukweli wa mambo.

Waberoya anasema kuna baadhi ya watu na wenzetu waislam wameaminishwa kuwa huyu ni kibaraka wa wakristu na kanisa kwa ujumla,hivyo anajaribu kutuonyesha kwamba kama tunataka kuishinda propaganda hii ambayo ni dhairi inazidi kuinyongonyeza CHADEMA na inaweza kuwa kama ya cuf ambapo leo hii watu wengi wanaichukulia ni ya kislam kutokana na propaganda za CCM.

Mfano hai ni juzi chadema walipotangaza maandamano nchi nzima mmesikia kauli ya waislam na maazimio yao, wenyewe wanaamini eti maandamano hayo yana agenda ya kuingoa serikali ya JK kwa sababu ni muislam, kitu ambacho si kweli. Kiujumla waberoya ana hoja ya msingi labda jinsi alivyoiwakilisha ndio imeeleweka vibaya, I stand to be corrected
 
Ni mpenda watu, mkweli, ana uchungu na Taifa na katika watu watakaokumbukwa katika kizazi cha sasa Dr. Slaa hatasahaulika. Kikwete anaweza kusahauliwa tena haraka na jina la Slaa likachukua muda. Kwani yuko mioyoni mwa watu wengi.

Lakini katika hulka za binadamu au tabia tulizonazo kuna wakati mtu muhimu huwa tunampinga, tunampiga na hatuoni thamani yake mpaka pale anapokufa! Kuna wakati watu walio na upendo na mawazo mazuri , mawazo na nia zao nzuri zikachukuliwa au kupokelewa tofauti na baadhi ya makundi ya wat.

Chadema walipaswa kujua kuwa kuna position na situation za kisiasa ..ambazo mara nyingi hazina logic zinaweza kuinua chama au kukiua, Ni vile tukaona Salim A. Salim hatakiwi kuwa rais wa Tanzania na Kikwete akawekwa! Tumeona mpenda vidosho Jacob Zuma akipendwa ....bila sababu

Chadema ilifanya kosa kumteua Slaa kuwa mgombea urais, makosa haya kisiasa ni ya kawaida, kwani haujui adui yako anasema nini, japo swala la kupakwa uchafu wa udini kutokana na background ya Slaa lilikuwa wazi na hapa risk management ilitakiwa

Leo hii wote tunajua position na mchango wa Slaa katika taifa bila kujali dini wala kabila..

Lakini kwa bahati mbaya kwa sababu zilezile nilizozisema 'no logic' existence ya Slaa ndani ya chadema inaonekana kukiua chadema zaidi kuliko kukipaisha na hali hii inaendelea na ikitokea makundi ya wale wanaoipinga chadema yakafikia kuwa na umoja, basi mwisho wa chadema ndio utakuwa umefika..historia inaonyesha huwa hivyo

Chadema; wakati CCM inajivua gamba , na nyie ni wakati wa Slaa kuondoka na kukisafisha chama chenye tuhuma za udini na wanaowachukia hawafichi kabisa.Situation is worse and if you will not do something , I am afraid!

Huu ni ushauri tu, kuna technic nyingi zinaweza kufanyika,.....ila zenu hatujaziona bado

Just Imagine maandamo mliyoyatangaza tayari yamegubikwa na udini! tunaposema hivi ni kwa upendo tu.

Najua wengi wanaweza wakatukana kama kawaida yao, wengine tumejifunza kupambana kuwaondoa watu tongotongo na kusimamia ukweli--mapambano ya fikra hayako kuipinga CCM bali na blind followers, ukweli mara nyingi ambao kama ungefanyiwa kazi tusingekuwa hapa tulipo

Mkitaka kusubiri subirini tu, will recall this post one day

I wish you good Luck!

Wabe.

UNATAPA TAPA TU WEWE NDO HUNA LOGIC KABISAAAAAA! Kwani Slaa anatuhumiwa Ufisadi kama Chenge,Rostam na Edward Lowasa au Hujui Kwamba CCM Mnatakiwa Kuiheshimu na Kuishukuru CHADEMA na Dr.Slaa coz ndiye Kiongozi na CDM Ndo Chama vilivyoifanya CCM ijivue Gamba!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Kwanza Malizeni Uozo ndani ya CCM Kabla ya kuingilia ya Chadema,'Huwezi kuwa Mshauri wa ndoa ya mwenzio wakati yako bado ina migogoro"
 
Tukikubali hoja ya Waberoya Wakristu waanze kuogopa kufikiria kushika nafasi ya uongozi. Hili ni pendekezo la hatari.

MKJJ thanks for your contribution

Ndio maana nikaanza kwa kusema Risk assessment and managament, nashangaa Mods wamebadili title!

Mkuu issue ya Slaa imetokea sio kwa sababu ni mkristo! kwa sababu alikuwa padre!

Ok tunaweza kusema lolote lile, sijaona baya lolote la Slaa ila kwa wale mnaotegemea kutoa kura hawatampa kwa sababu ya background yake ya upadre! angekuwa mkristo kwenye ile position,tunayoyasikia leo yasingekuwepo.

Guys, nadhani mnasoma magazeti ya kiislamu, na manasikiliza redio za kiislamu they mean it.

Is this not supposed to be political games? kuwa aendelee kuwepo no matter what??

You will prove me right sonn, nina hakika na ninachokisema , deterioration ya chadema iko kwenye very high speed

Mimi nazungumzia upepo wa siasa na sio ushabiki tu.

Sijaona hoja bado

Propaganda ndoio zinaharibu vyama ndio siasa, how you deal with it?

MKJJ ukiwa kama great thinker unafikiri chadema wafanye nini kuondoa ili wingu baya? do nothing option is not an option here, we need their VOTES yet we pretend we will get them!!
 
SIJASEMA SEHEMU CDM INA GAMBA!! CDM haina tatizo lolote ila lisiasa kuna wakati huwa haueleweki unavyotaka ueleweke! nimetoa mifani ya salim na zuma, still you guys purposely mna -digress hoja!!

nwaonea huruma sijaona hoja , waislamu hawawatki BADALA YA KUWAAMBIA VIONGOZI WENU WAPIGANE NA HIYO HALI, MNABAKI KUTUMATUMA VIPOST VYA KISHABIKI..UJINGA HUO

HOJA ni kuwa CDM ifanye nini kujikwamua na hali hii kama mnaona is ok tuendelee!
na huwezi ku-predict nani mpya ataeleweka unavyotaka ueleweke!
 
Wapendwa waume na wake popote mlipo

Samahani kwa kumwaga huu upupu kwenye hili jamvi tukufu, samahani kwa kufikiria niliyofikiria bila kufikiria kwa umakini na kusema tu

Sikuwa na lengo baya na sitakuwa na lengo baya daima, ukisoma mawazo yangu nasikitika kwa lile MKJJ nalosema ni emotional response kuwa kuna tatizo la udini katika hiki chama

Samahani kwa kutoa wazo, ambalo si wazo baya kwangu mimi ni alert na kusema Kuhusu Slaa pengine ndiyo kosa langu

sasa ni hivi

KWENYE THREAD HII NANYOOOSHA MIKONO JUU KUWA NIMESHINDWA NA SITAKUWA NA HOJA YA KUELEWEKA

PLEASE GUYS I AM DONE IN THIS THREAD...MBELILE!

Quinine, mwita, MKJJ, n.k please tukutane si nyingine

taxi17.jpg

 
CDM haiwezi kushauriwa CUF, CCM, UDP, NCCR pamoja na waberoya, maana wana chuki binafsi na CDM na Viongozi wake. wana chuki binafsi na waTZ masikini ambao wanahitaji ukombozi ukweli.
 
Sikutegemea graduate wa Umbwe Sekondari wanaweza kumwaga PUMBA kiasi hiki. Wow!
Sijasoma shule yoyote ya moshi, nimesoma Morogoro, Arusha na Tabora! nimeishi moshi na mzazi wangu mmoja ndiye aliyekuwa anfanya kazi umbwe, dont confuse! kama uliona nimeandika nimesoma umbwe basi ilikuwa changamsha baraza! Umbwe siyo tech na mimi nimesoma tech.

Tunayiyaandika humu huwa hatueleweki, nimesoma sociology,najiita injinia kwa sababu ya kusoma tech, siyo injinia wa ukweli

Try another toss!
 
Huyo ndiye Waberoya mkaazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam - kwake Chadema haina uongozi na ina wapenzi vipofu na wajinga. Kwa Waberoya, Chadema imeshazikwa kwa sababu Waislamu wameikataa na bila wao kamwe Chadema haiwezi kukamata dola milele. Huyo ndiye Waberoya ambaye amewahi kudai kuwa gumzo kubwa mitaani Mbagala inahusu kutokubalika kwa Chadema kwa wakaazi wake wengi. Ningeshtuka sana kama Waberoya angesema vinginevyo ! It is called an obscession !
 
Waberoya.....

Taratibu mkuu, wengine vichwa vyetu vimejaa maji....viko limited kwenye kutafsiri falsafa.

Hii thread yako lazima ina falsafa fulani hivi kwani kichwa yangu imepiga hola!!

Kama kichwa yangu haijapiga hola, nionavyo mimi unachoki-present kwenye argument yako ndicho haswa CCM wanachotaka wa-TZ wakiamini.

It'll present the darkest hour of this generation kwa the so called "wasomi" kuingia kwenye aina hii ya mitego ya kitoto - I mean, taking your (aka CCM's) udini argument at face value.

Kwa mtazamo wangu, kama argument yako haina falsafa nyuma yake, basi I can safely say you have swallowed it all from CCM....hook, line and sinker!
 
SIJASEMA SEHEMU CDM INA GAMBA!! CDM haina tatizo lolote ila lisiasa kuna wakati huwa haueleweki unavyotaka ueleweke! nimetoa mifani ya salim na zuma, still you guys purposely mna -digress hoja!!

nwaonea huruma sijaona hoja , waislamu hawawatki BADALA YA KUWAAMBIA VIONGOZI WENU WAPIGANE NA HIYO HALI, MNABAKI KUTUMATUMA VIPOST VYA KISHABIKI..UJINGA HUO

HOJA ni kuwa CDM ifanye nini kujikwamua na hali hii kama mnaona is ok tuendelee!

Webs, jionee huruma pia maana unataka kutuaminisha kuwa we ni nabii, kitu ambacho si kweli. Uwezo wako wa kuona na kuchambua mambo una ukomo pia kama wengine unaowaonea huruma. Je, unataka Dr. Slaa aondolewe CDM kwa sababu ya udini? Hv utamuweka nani ambaye hana dini? Kumbe wenye dini na wanyenyekevu hawaruhusiwi kujihusisha na siasa?

Hv kwa mawazo yako unadhani wanaoeneza propaganda ya udini CDM ukimwondoa Dr. Slaa watakosa hoja nyingine, mbona zipo nyingi tu? Ok, Zuma alikuwa Makamu wa Raisi kabla hajawa Raisi we unasema mpenda vidosho hawezi kuwa Rais? Kweli wa-South ni wajinga hawakuliona hilo? Waliompiga majungu Dr. Salim A. Salim ni CCM wenyewe na ilikuwa kwenye hatua za mwanzo sana, kama wangeruhusu jina lipite halafu wapige majungu kwenye free platform usingesema hayo sahv.

Anyway, sikuhukumu ila usiandike tu jaribu na kufikiria.
 
Back
Top Bottom