Guyton
JF-Expert Member
- Jan 15, 2011
- 264
- 78
Natumaini hiki ulichosema hapo juu kimetoka kwenye mwitikio wa kihisia (emotional response) na siyo kutoka katika mwitikio wa kiakili (a rational response) kwani inasema mengi:
a. Umejuaje Waislamu "hawawataki"?
b. Waislamu gani hawawataki?
c. Kwanini ni Waislamu tu hawawataki?
d. Je ndani ya Chadema kuna muislamu yeyote?
e. Kama kuna muislamu japo hata mmoja - inaweza vipi kusemwa kuwa "waislamu hawawataki"?
f. Unafikiri Dr. Slaa akiondoka ndio Waislamu wataitaka hata kama haiwakilishi maslahi yao?
Nadhani ni hoja nyingine ambayo ni extremely prejudicial, biased and inherently offensive. Yaani, kukubalikwa kwa Chadema kunapimwa na kukubakika na Waislamu? Sasa wakimuondoa Dr. Slaa halafu waislamu wakakubali na Wakristu wakianza kukimbia wamuondoe huyo mtu mwingine ili wakubalike na "wakristu". Yaani, hatuna kanuni tena isipokuwa kufanya mambo kwa kujaribu kuridhishana tu?
Kuita majibu ya watu wengine wasiokubaliana nwewe kuwa ni "ujinga" ni kujaribu kulazimisha hoja pale ambao umeshindwa kusimamia hoja yako.
Nyerere aliposema nchi inakosa wasomi akumanisha watu weliofika chuo au maprofesa kama wengi walivyomuelewa vibaya, ila alimanisha people who can think critically like you, big up.