Risasi zarindima mtaa wa swahili

Inajulikana wazi kuwa Kova ana usongo na majambazi na aliahidi mwanzoni kuwa ama zao ama zake na ndio tunaona juhudi zake kuwa,kila wanapokutana face to face watamkamata japo mmoja.

Hata Zombe na Chicco walikuwa na usongo, ila basi tu ..
 
Da,
mjasiri haachi asili,
mi mkurya bwana... Kiswahili nilianza kujifunza siku nlipo ona gari kwa mara ya kwanza.
Kiingereza ndio usiseme....
Hadi leo najua yuwa my name is bujibuji
 
naanza kuziona gharama za kuua jkt watu hawawazi mbali tena zaidi ya kudhurumu vya wenzao tutegemee hali mbaya zaidi picha za eneo zipo michuzi
 
jamani hawa majambazi mbona hawaishi, sijui ni nani wa kulaumiwa na hili wimbi la majambazi
 
Mtaa wa swahili leo asubuhi ilikuwa patashika polisi wamepambana na majambazi ana kwa ana na inasemekana majambazi watatu wameuwawa na wengine watatu wamejeruhhiwa. kwa mwenye habari zaidi tuhabarishe
 
Habari kama hizi sio za kucomment kwani kila siku polisi wanaua watu kwa kisingizio cha ujambazi, inabidi tupate infor. za kutosha kwanza.
 
jamani hawa majambazi mbona hawaishi, sijui ni nani wa kulaumiwa na hili wimbi la majambazi

Hawaishi kwa sababu gani? Kila kukicha watanzania wengi zaidi wanatumbukia kwenye umaskini wa kutupwa. Pesa ambazo zingeboresha maisha yao zinaishia mikononi mwa watu wachache (mafisadi). Pengo la walionacho na wasionacho linazidi kuongezeka. Na wimbi la ujambazi halitamalizwa kwa polisi kupambana nao bali kwa usimamizi na mgawanyo mzuri wa raslimali za taifa.
 
hivi kwanini kunawaga na vitendo vya ujambazi mwingi mwaka mmoja kabla ya uchaguzi???
 
hivi kwanini kunawaga na vitendo vya ujambazi mwingi mwaka mmoja kabla ya uchaguzi???

Mkuu nashindwa kupinga kauli yako,lakini sidhani kama kuna uhusiano wowote kati ya ujambazi na uchaguzi.

Sidhani kama kampeni zinafadhiliwa na ujambazi wa kutumia silaha!
 
hivi kwanini kunawaga na vitendo vya ujambazi mwingi mwaka mmoja kabla ya uchaguzi???

Kapinga, sidhani kama ujambazi wa silaha unahusiana na mambo ya uchaguzi.... unless kama "EPA ya CCM 2010" imeamua kuchukua frontline battle this time around!!
 
Mungu aepushie mbali, sijui kwa jinsi tulivyo, pale Mbagala wakati wa lile sekeseke la milipuko ni silaha ngapi zilitoweka na sasa ziko katika mikono mibaya.
 
Hawaishi kwa sababu gani? Kila kukicha watanzania wengi zaidi wanatumbukia kwenye umaskini wa kutupwa. Pesa ambazo zingeboresha maisha yao zinaishia mikononi mwa watu wachache (mafisadi). Pengo la walionacho na wasionacho linazidi kuongezeka. Na wimbi la ujambazi halitamalizwa kwa polisi kupambana nao bali kwa usimamizi na mgawanyo mzuri wa raslimali za taifa.

Nakubaliana na wewe mia kwa mia kuwa ujambazi hauwezi kwisha as long as our national resources are not equitably distributed among the populace; haiwezekaniki kuwa rasilimali za nchi nzima zithibitiwe na wachache halafu uhalifu ukiwemo ujambazi upunguwe; kuwalinda hawa mafisadi wasiende lupango ndio kunazidisha umasikini wa raia na umasikini ndio unazaa uhalifu!! Muungwana atulie nyumbani kutatua haya matatizo.
 
Hapa hakuhitaji ushaihi maana ukitokeza pua umekula shaba,kulikuwa kama uwanja wa vita ,nakumbuka wakati Mkapa akimalizia majambazi wakiweka ile machine gun yenye utambi na miguu miwili mbele halafu anajila nayo katikati na wengine wakisanya hela kwenye maduka ,ile ilikuwa mwisho na wakiondoka ndio Zombe anatuma vijana wake kuulizia wapo wapi majambazi wakati huo majambazi yanakatisha Chalinze na kujichoma kwenye misitu waliyoizibiti.
 
Back
Top Bottom