Ripoti ya tume ya maadili ya Philip Mangula iko wapi?

Idimi,

Ungelitufanyia haki sana Watanzania kwa kutuwekea makala nzima ya huyu Mzee Mangula. Hii makala na uiweke hapa na ruhusa kwa waandishi wa habari, Blogs nk kuichukua na kuiweka nzimanzima kwenye magazeti yao ili muradi waweke credit kwa JF na member Idimi.

Umenifungua macho mambo mengi sana juu ya ujio wa huu uozo uliopo sasa Tanzania.

Kuna haja ya kubadili chama tawala ili tuone wengi wakifungwa. Kama katiba inatoa Imunite kwa Marais, kuna haja ya chama cha upinzani kitakachoshinda basi waziondoe ili kuanzia Mwinyi, Mkapa na wengine wote watakaokuja kumaliza Urais huko mbeleni washtakiwe kwa maswala yoote ambayo hayana uhusiano na maamuzi ya nchi kama Rais. Ufisadi upo nje ya katiba na Rais lazima ajibu.
Mhe Jasusi, uko sahihi kabisa, Mkapa aliachia uenyekiti wa sisiemu kabla ya muda kamili wa kuachia nafasi hiyo haujafika, akamuachia mwenyekiti wa sasa mhe. Kikwete, ambaye aliitumia nafasi hiyo effectively kuwaondoa wale asiowataka. Hope unakumbuka vizuri jinsi wanamtandao walivyovuruga uchaguzi wa mwaka 2007 katika ngazi zote, na vurugu zile hazijaisha, wanamtandao wanajipanga kwa uchaguzi mkuu wa chama mwakani. Wale wasioiva na JK (kutoka makundi ya Sumaye, Mwandosya na Salim) ndo wanataka kumvua uenyekiti, ili asiwe na nguvu katika chama, picha ndo kwanza inaanza. Kiini hasa cha kuvuana magamba ni juhudi za kutaka ku-deal na hao wanaotaka kumpoka hilo rungu. Anayeua kwa upanga hufa kwa upanga pia.
 
Kweli JF ni kisima cha data za ukweli - watu hawamungunyi data hata moja -- yaani ni true bin true kabisa - mi huwa nafikiri kumbe sisi Wa TZ si wasahaulifu na wazembe wa kufikiri bali tumepewa uvumilivu na mwenyezi mungu. Bila hili la uvumilivu huyu m kwere sasa hivi angekuwa asharudi chalinze kwenye kijiji chake alichojenga kupumzika.

CCM imekuwa ikibariki fitna kati ya makundi hasa wakati wa kugombea uongozi, na sasa dhambi hiyo hiyo inaanza kuwatafuna taratibu. Yaani niliishiwa nguvu lile zengwe alikopigwa nalo Salim A Salim na lile na Mzee Malecela yaani dakika za mwisho kabisa za nominations - kweli RA umewaambia ukweli wao na kutimua vumbi.
 
Idimi nimekuvulia kofia mkuu. Nimeridhika sana na taarifa ulizozileta hapa. Kwa bahati mbaya sana sikuweza kureact mapema kwenye hizi hoja kwa kuwa sikuwa na umeme kwa zaid ya wiki nzima. Ulikuwa unakuja usiku unaondoka asubuhi.
Ila Mangula atabaki kuwa shujaa daima, maana alikuwa ni kiona mbali cha nchi.

Mkuu habari hizi nzuri sana hebu endelea kutupa zaidi..mwaka huu tutasikia mengi sana..bado wanavuana magamba, kuna kambi rasmi ya upinzani ndani ya ccm(ccj), bado matatizo kibao na ahadi hewa za ccm...
Mkuu habari hizi nzuri sana hebu endelea kutupa zaidi..mwaka huu tutasikia mengi sana..bado wanavuana magamba, kuna kambi rasmi ya upinzani ndani ya ccm(ccj), bado matatizo kibao na ahadi hewa za ccm...

Idimi,

Ungelitufanyia haki sana Watanzania kwa kutuwekea makala nzima ya huyu Mzee Mangula. Hii makala na uiweke hapa na ruhusa kwa waandishi wa habari, Blogs nk kuichukua na kuiweka nzimanzima kwenye magazeti yao ili muradi waweke credit kwa JF na member Idimi.

Umenifungua macho mambo mengi sana juu ya ujio wa huu uozo uliopo sasa Tanzania.

Kuna haja ya kubadili chama tawala ili tuone wengi wakifungwa. Kama katiba inatoa Imunite kwa Marais, kuna haja ya chama cha upinzani kitakachoshinda basi waziondoe ili kuanzia Mwinyi, Mkapa na wengine wote watakaokuja kumaliza Urais huko mbeleni washtakiwe kwa maswala yoote ambayo hayana uhusiano na maamuzi ya nchi kama Rais. Ufisadi upo nje ya katiba na Rais lazima ajibu.

Msema Hovyo, The Emils na Sikonge,
Tumshukuru Mungu kwamba Watanzania ni wavumilivu sana, hatupendi kabisa vurugu za kisiasa (nadhani ni kwa kuangalia hali ya majirani zetu), otherwise tungekuwa tumeshashikishana adabu siku nyingi sana kwa madudu yanayoendelea katika siasa za Tanzania. Kuhusu JK na udhaifu wake, habari nzima ya alikotoka, alipo na anakokwenda, pitia thread hii hapa. Hapa JF hakuna kitu kinachopotea, tuko hapa kuweka mambo sawa kwa ajili ya kizazi hiki na kijacho.
Mangula, Sumaye, Salim, Mwandosya na Malecela ni sample ndogo tu ya waathirika wa siasa za majitaka na visasi, na topics zote hizo zipo hapa JF, tulishaandika sana, ila tutaendelea kukumbushana tu, kwa faida ya wote.

Kazi zaidi za mtandao wa Kikwete
Baada ya wanamtandao ku-deal na waliwaona kuwa ni wapinzani wakuu wao kisiasa katika ngazi ya taifa na kufanikiwa kushika dola, visasi viliendelea kwa wafuasi wao wakuu katika ngazi za mikoa, ngazi za wilaya na kata na katika jumuiya za chama. Ikumbukwe kwamba, kuna wakuu wa mikoa kadhaa ambao walishatangaza kabisa kutomuunga mkono Kikwete, kwa sababu walikuwa katika kambi nyingine, ikiwemo ya Sumaye, mmojawapo alikuwa ni mkuu wa mkoa wa Morogoro Musa Nkhangaa. Huyu alipewa tuhuma kwamba alishirikiana na Sumaye kupora wakulima mashamba kule Mvomero, tuhuma ambazo Sumaye anakana hadi kesho na hajafikishwa mahakamani. Baada ya JK kushika dola, huyu bwana Nkhangaa alikuwa wa kwanza kushikishwa adabu, akapokwa madaraka ya ukuu wa mkoa mchana kweupe! Mwathirika mwingine aliyekuwa kambi ya Sumaye ni Matheo Qaresi, huyu alikuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya, aliondolewa baada ya JK kushika dola na nafasi yake ikajazwa na mwanamtandao John Mwakipesile, aliyeukosa ubunge wa Kyela kwa kushindwa na Harrison Mwakyembe. Qaresi alipewa tuhuma za kuwapora mifugo wafugaji wa bonde la Usangu, lakini mpaka leo hajafikishwa katika vyombo vya dola kwa tuhuma hizi. Kuna wakuu wengine kadhaa wa mikoa walipitiwa na panga hili, nadhani wenzangu watajazia majina.
Kwa ngazi ya ukuu wa wilaya, nako hali haikuwa nzuri, wale wote waliokuwa against na mtandao walipitishiwa panga. Waathirika wachache ninaowakumbuka ni pamoja na Elias Maarugu (alikuwa Misenyi), Deusdedit Mtambalike (alikuwa Muleba), David Holela (alikuwa Babati),Mashimba Mashimba (alikuwa Kyela), Kanali Peter Madaha (alikuwa Nyamagana) na Gilbert Dololo (Kibaha) na wengine kadhaa ambao majina yao yamenitoka. Kumbuka mheshimiwa kanali Peter Madaha alishawahi mumjibu Lowassa "Dry", pindi alipokuwa ziarani Mwanza, kwa kumwambia Lowassa kwamba asimfundishe kazi. Hili lilimkasirisha sana EL, akaapa ku-deal naye. Nafasi zao hawa zikachukuliwa na wanamtandao akina Francis Issac, Betty Mkwasa, Kristofa Kangoye na wengine kadhaa.
Katika chama chake nako hakukuwa salama. Bwana Abiudi Maregesi alipokwa uenyekiti wa jumuiya ya wazazi, wakati wa uchaguzi mkuu wa chama. Huyu alikuwa amejitangaza kwamba ni meneja wa kampeni wa Sumaye, wakati wa kampeni za kuwania kuteuliwa na chama kugombea uraisi mwaka 2005. Hata katika mazingira ya kawaida, ingekuwa ngumu kwa JK kufanya kazi na mheshimiwa huyu, ambaye walikuwa na mitazamo kinzani. Katika jumuiya ya wanawake wa CCM, mwenyekiti wake mama Halima Mamuya akaundiwa zengwe kwamba kauza jengo la chama (Gogo Hotel) bila baraka za chama. Jengo hili ndipo ilipo Airtel, pale Morocco. Mama huyu alijitetea kwa kila hali kwamba uuzaji ulibarikiwa na chama na akaonesha na documents zote, lakini kwa kuwa wanamtandao walikuwa hawamtaki basi akapokwa cheo. Nafasi yake ikajazwa na mwanamtandao mheshimiwa Sofia Simba. Namna Simba alivyoingia madarakani kila mwana JF anajua. Kumbuka kwamba Lowasa naye aliuza kiwanja cha chama (UVCCM) pale nyuma ya jengo la vijana karibu na Fire hadi kuingia katika malumbano na Nape, na bado yuko madarakani hadi muda huu.Orodha ya visasi ni ndefu sana, kama nilivyosema, iligusa hadi ngazi ya kata. Kilichotokea UVCCM ya akina Yusufu Masauni, sidhani kama nina haja ya kuongelea, tumeandika mengi sana.

Ndugu wana JF, ukiangalia mlolongo mzima wa kazi ya visasi ya mtandao hapo juu unaona kwamba hawa jamaa wamejijengea uadui kuanzia ngazi za chini kabisa, katika serikali na katika chama, sasa inapotokea kutokuelewana tusishangae. Sio rahisi kwa mtu kama Mangula, Sumaye ama Malecela kutoa mawazo kwa JK juu ya kuboresha chama kwa sababu alishakwazana nao. Vurugu hizi tunazoziona UVCCM, UWT na kwenye jumuiya nyingine za chama si za kuisha leo wala kesho, magamba waliyoyaweka ni magumu sana, si rahisi kutoka, yakitoka yanatoka na chama. Uchaguzi wa ngazi ya chama mwakani utakuwa na maluwe luwe mengi sana, tutaona vioja vingi mno, zaidi ya tulivyoona mwaka 2007. Madhara ya kazi za mtandao ni beyond control, wamepanda miiba, sasa inawachoma wenyewe.
Hata juzi hapa wakati Rostam analalamikia siasa za majitaka, alikuwa kasahau kwamba yeye na wenzake ni waanzilishi wa siasa hizo, kwa kutumia magazeti ya Rai, Tanzania Leo na Mtanzania mwaka 2004/2005, wakiwatumia akina Muhingo Rweyemamu, Salvatory (Salva) Rweyemamu, Charles Charles, Manyerere Jackton, Prince Bagenda na waandishi wengine wanaochumia tumbo. What goes around comes around, ndicho kilichomkuta Rostam. Habari zaidi za visa vya mtandao zipo katika thread hii hapa.
Tuendelee na mjadala.



Nasikia Slaa ndio alishinda urais, laikini wabunge wa CDM walichaguliwa 22 tu kati ya 280.

Nduka, hilo sina uhakika nalo, lakini unaposikia kwamba Slaa aliongoza kwa kura za urais hadi katika wilaya ya Ludewa ambako hakufika kupiga kampeni, basi ujue lisemwalo lipo

Kweli JF ni kisima cha data za ukweli - watu hawamungunyi data hata moja -- yaani ni true bin true kabisa - mi huwa nafikiri kumbe sisi Wa TZ si wasahaulifu na wazembe wa kufikiri bali tumepewa uvumilivu na mwenyezi mungu. Bila hili la uvumilivu huyu m kwere sasa hivi angekuwa asharudi chalinze kwenye kijiji chake alichojenga kupumzika.

CCM imekuwa ikibariki fitna kati ya makundi hasa wakati wa kugombea uongozi, na sasa dhambi hiyo hiyo inaanza kuwatafuna taratibu. Yaani niliishiwa nguvu lile zengwe alikopigwa nalo Salim A Salim na lile na Mzee Malecela yaani dakika za mwisho kabisa za nominations - kweli RA umewaambia ukweli wao na kutimua vumbi.

Ndugu Fuso, hao wazee wawili nilioweka wino mweusi katika post yako, ukichanganya na Msuya, Mangula, Warioba, Butiku, Mzee Ruksa na wengine wachache wenye maono (namaanisha vision) ndio ambao wangetoa dira endelevu ya chama kwa miaka iyajo, lakini wamewekwa nje ya mfumo na maamuzi na wanamtandao, unadhani chama kitaelekea wapi? Think twice.
Nawasilisha
 
Idimi,

Nashukuru kwa shule nzito. Uliyoyasema yoote, nafikiri mwakani tutayaona yakishazaa matunda. Hatuna zaidi ya kusema tusubiri na tuombe Mungu yawe matunda mazuri. Ila kutokana na Wana mtandao kuzidi kushambuliwa na wao wenyewe kutengena, ninategemea kuwa kuna watu watamshambulia hadi Mwanyekiti wa Chama. Naogopa tusije tukapata Jacob Zuma wa Tanzania kwa kumuondoa mwenyekiti na hata kumshtaki na mwisho afukuzwe kwenye chama na kupoteza Urais.

Kama yeye aliwacheza wenzie kwa kujipanga miaka kadhaa nyuma, nina imani kuna wengine pia sasa hivi wanajipanga vizuri sana kulipiza kisasi. Ila visasi vyao vinaweza kuwa vikali sana. Muda wa Mtandao naona unakwisha kwani wote sasa hivi wana majeraha makubwa sana na mwamko wa Tanzania ni mkubwa. Sidhani kama Chenge au Lowassa wanaweza kugombea Urais. Kikwete ndiyo anamalizia miaka yake na sidhani kama kuna mtu mwenye akili sawasawa anaweza kuanza kujiweka upande wake maana itakuwa kukata tawi ulilokalia, upande wa majani.

Nina wasiwasi na maelezo yako kuhusu Mzee Ruksa. Huyu kasemwa sana kuwa ndiye yeye na Kawawa walimbemba Mwenyekiti wa sasa wa CCM hadi kufikia hapo alipo kwa kufunika mambo mengi kwenye hiyo mikutano mikubwa ya CCM. Sasa nashindwa kuelewa hadi leo kama alifanya hivyo kwa kumuandalia mwanae njia au alifanya hivyo kwa woga wa na yeye kushambuliwa na Mtandao? Tatizo la Mwinyi Jr ni hiyo milipuko mara mbili imetokea na yeye yupoyupo tu. Pia kwa hali ilivyo Tanzania, sijawahi hata kumsikia kasema kitu. Naona atakuwa anajiweka kama Nice Guy watu ambao kwa sasa naona hawatakiwi sana Tanzania.

Nashukuru kwa maelezo na sasa ni KUSUBIRI TU.
 
The late Morris Nyunyusa:eek:ur legendary drummer, whose composition has been adopted by TBC as news bulletin signature.

CDV6ljYVAAEbwrl.jpg
 
Back
Top Bottom