Ripoti ya Richmond kutojadiliwa

Chama kimeshika hatamu, tumerudi kule kwenye party supremacy, Sitta amemuomba PM aliahirishe Bunge kunusuru uspika wake, maana mwisho wake ungeweza kuwa jana. Mbunge angesimama kutoa hoja ya kutokuwa na imani na spika, Spika angelazimika kutoka nje ili ijadiliwe, Makamba angesimama na kusema Rais anawaomba wale wenye mapenzi mema waunge mkono hoja. Spika Sitta would have been Kwishnehi!.
 
Chama kimeshika hatamu, tumerudi kule kwenye party supremacy, Sitta amemuomba PM aliahirishe Bunge kunusuru uspika wake, maana mwisho wake ungeweza kuwa jana. Mbunge angesimama kutoa hoja ya kutokuwa na imani na spika, Spika angelazimika kutoka nje ili ijadiliwe, Makamba angesimama na kusema Rais anawaomba wale wenye mapenzi mema waunge mkono hoja. Spika Sitta would have been Kwishnehi!.


sounds good but too short p/se come again mkulu, give us the inside story!

************
Amani yetu inatumika vibaya.
 
Tujikumbushe hayo ya Richmond....HIVI Watanzania ukweli uko wapi hapa?
 
Viporo vyashusha ‘hadhi’ ya Bunge
Imeandikwa na Na Waandishi Wetu; Tarehe: 8th November 2009 @ 23:59 Imesomwa na watu: 12; Jumla ya maoni: 0





KUPIGWA kalenda kwa baadhi ya hoja zilizokuwa zikitarajiwa kufikishwa na kujadiliwa katika vikao vya Mkutano wa 17 wa Bunge ulioahirishwa juzi, kumeufanya muhimili huo wa dola kuonekana kushuka ‘hadhi’ yake katika jamii.

Wakizungumza na Habari Leo Jumapili jana kwa nyakati tofauti, viongozi wa kisiasa na wabunge walihoji sababu za ratiba ya Bunge kutofuatwa na kukamilisha kilichowapeleka wawakilishi hao Dodoma kwa kutumia kodi za wananchi.

Baadhi ya hoja hizo ni pamoja na taarifa ya serikali ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu kashfa ya Richmond, ambayo yote yalishatekelezwa na kubakia kipengelea cha kumuwajibisha, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Dk. Edward Hoseah.

Awali katika mkutano wa 16 wa Bunge, serikali ilirudishiwa taarifa yake kwa kuwa ilikuwa haijawawajibisha baadhi ya watuhumiwa wa kashfa hiyo ambao ni watumishi wa serikali.

Watuhumiwa walioonekana kuwa kikwazo kwa Bunge kukubali taarifa ya serikali ya
Richmond katika mkutano huo wa 16 licha ya Dk. Hosea ni aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Arthur Mwakapugi ambao hata hivyo kabla ya kuanza kwa mkutano wa 17 wa Bunge, walistaafu.

Hata hivyo wakati wabunge wakitarajia kuwasilishwa kwa taarifa hiyo ya Serikali wiki hii, Dk. Hosea aliapa kuwa hatajiuzulu kama ambavyo wabunge hao walivyokuwa wakitarajia.

Aidha Dk. Hosea alitangaza rasmi kuwa Takukuru imeanza uchunguzi kwa wabunge kutokana na baadhi yao kutuhumiwa kupokea posho ya pili kutoka mashirika ya umma wanapokwenda kutekeleza wajibu wao wa kuyadhibiti ambao kimsingi kwa kazi hiyo, wabunge hao hulipwa posho na Bunge.

Ingawa baadhi ya wabunge walikerwa na uchunguzi huo na hasa kitendo cha wao kutakiwa kuhojiwa, Dk. Hosea alifika bungeni na kutetea na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Spika wa Bunge, Samuel Sitta ingawa ziara yake haikubadilisha msimamo wa wabunge kutaka awajibishwe.

Taarifa kutoka bungeni zinasema mpaka juzi asubuhi, wabunge wengi walikuwa wakitarajia kuwa angalau taarifa hiyo ya Richmond ingewasilishwa, lakini nao walipata mshangao kusikia kuwa bunge limeahirishwa na taarifa hiyo itawasilishwa katika mkutano ujao wa Bunge, Januari 26, mwakani.

Akizungumza kwa njia ya simu jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Philip Marmo, alisema Serikali haijakwepa suala la Richmond bali ratiba ya Bunge haikuruhusu suala hilo kujadiliwa.

“Taarifa kuhusu Richmond itatolewa…Serikali hajakwepa chochote imejiandaa kutoa taarifa kuhusu suala la Richmond, suala la mgodi wa Kiriwa na Shirika la Reli Tanzania (TRL) lakini ratiba ya Bunge haikuruhusu,” Marmo alisema kwa kifupi.

Pia Spika Sitta alisema kuwa tatizo lilikuwa muda kwani hata yeye alikuwa na nia kuwa swala hili liishe katika mkutano huu.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe alisema Bunge limekuwa kama kamati ya harusi kwa madai kuwa linafanyika bila kuwa na ratiba maalum pamoja na kushindwa kutekeleza kujadili maswala yaliyotarajiwa.

Mbowe alisema mambo yaliyofanyika bungeni ni ya aibu ambapo Watanzania wamefikia hatua ya kufedheheshwa kwa taasisi hiyo kufikia uamuzi usiozingatia maslahi ya taifa.

Naye Mbunge Mohamed Habib Juma Mnyaa wa Mkanyageni, Zanzibar (CUF) alisema taarifa inayosubiriwa inatokana na maazimio yaliyofikiwa na Bunge hivyo kitendo cha kuahirisha kutoa taarifa ya utekelezaji kinaweza kusababisha Bunge kudharaulika.

Kwa upande wa Mbunge wa Nzega, Lucas Selelii (CCM), amesema suala la Richmond limeshamchosha na anashangaa ni kwa nini serikali haitaki kulimaliza.

“Najiuliza kulikoni! Mbona Serikali haitoi taarifa? Kama kuna tatizo la kisheria au kikatiba ni vyema ikasema wazi ili sheria hiyo au kifungu cha katiba kinachokwamisha kiweze kurekebishwa na suala la Richmond litekelezwe ili kuweze kusonga mbele,” alisema Selelii
 
Dalili zinaonyesha kuwa mjadala wa kuhitimisha utekelezaji wa maagizo ya Bunge kuhusu Richmond utayeyuka kama ilivyokuwa kwa hotuba ya JK katika Bunge. Kuna mambo matano ambayo vigogo wa CCM wameyafanya na wanaendelea kuyafanya kuzika kabisa hitimisho la Richmond. Kwanza ni hatua ya NEC kumsulubu Sitta, pili ni kuundwa kwa kamati ya CCM kuzima harakati za baadhi ya wabunge wanaotaka kumalizwa kwa suala la Richmond na kitu cha tatu ni TAKUKURU kushupalia suala la posho, japo Richmond iliwashinda. Kitu cha nne ni matamushi ya mtumishi wa Bunge akizungumza na TBC1 kuwa mjadala wa Richmond hauna manufaa kwa taifa. Hiki ni kitu cha kushangaza kabisa. Taifa gani analozungumzia? kwa sababu wananchi tunataka huo mjadala ili kukata mizizi ya ufisadi wa Richmond. Huyu anafikiria kuhusu maslahi ya CCM halafu anasema ni ya taifa. Kitu cha tano ni kauli ya Mh. Sitta kuwa muda wa kujadili Richmond haukutosha. Inakuwaje masula mapya yapate muda wa kujadiliwa wakati ya zamani hayapati muda wa kujadiliwa? Danadana hii ya CCM kuhusu suala la Richmond inafanana kabisa na jishi mjadala wa hotuba ya JK ulivopigwa kalenda hadi ukaota mbawa.
 
Back
Top Bottom