'Ripoti' ya Mziray na Mabadiliko ya Chadema kuelekea 2010

Kweli kama ripoti hii ina ukweli wowote basi Tanzania hatuna wapinzani wa kweli, wote wahuni. Nilikuwa nafikiria sana kuisupport CHADEMA (sijawahi kuwa na Chama maishani mwangu) baada ya kuona juhudi binafsi za watu kama Slaa na Zitto, lakini sasa naanza kufikiria mara mbili mbili. CHADEMA ovyo (according to this report), NCCR hawana mwelekeo, CUF hawaeleweki, Mtikila anakula na mafisadi, sasa nani yuko serious kuiondoa serikali ya mafisadi madarakani?! Duh! Hawa wakipewa nchi wataiweza kweli kama makao makuu yao tu ndio ovyo hivyo?! Si ndio tutakuwa tumewapa mafisadi part two, tena weneye njaa kali. KWA KAMA NDIO HIVI HAWA MAFISADI WA CCM WATATULA MPAKA WAVEMBEWE!
 
unaweza Kudanganya Watu Wachache Wakati Wote, Lakini Huwezi Kudanganya Watu Wote Wakati Wote (you Can Fool Some People Some Time But You Cant Fool All People All The Time), Mbowe Anapaswa Kujua Hilo.

Chadema Inatakiwa Kubadilika,vinginevyo Itazidi Kudidimia.sasa Hivi Watu Wanazungumzia Mtu Mmoja Mmoja Kama Dr.slaa,Zitto Kabwe Lakini Hawazungumzii Chadema Kama Chama Kwa Nini?.
Kwa Viongozi Wenye Maono Hili Tu Pekee Lingekuwa Somo Tosha Kuonyesha Kwamba Wananchi Bado Hawana Imani Na Chama.

Nilitegemea Baada Ya Matokeo Duni Ya Uchaguzi Mkuu Viongozi Walioshindwa Vibaya Watajiondoa Kupisha Wengine Wajenge Chama Na Kujenga Imani Kwa Wananchi.lakini Mhh!
 
Last edited:
Dada Asha, saidia wananchi wa Tanzania.

Je tume iliundwa? Je Mziray alikuwa kiongozi? Je ripoti hii iliwahi kutolewa? na Je kama sio hii hiyo tume ilitoa ripoti ya namna gani? Iko wapi? unaweza kuiweka hapa?

Je Madereva wanaotajwa wapo? Je upungufu wa komputa upo? Je wakurugenzi wanateuliwa? etc. etc. etc. etc....

Nijuavyo mimi

1. Hakuna tume iliyoundwa CHADEMA, mwaka 2007 paliundwa Kamati ndogo ya Kamati Kuu, Bwana Mziray alitaka iundwe Kamati kuchunguza ukabila tu CHADEMA, Mwenyekiti Mbowe akakubali na Kamati Kuu ikaongezea hizo hadidu rejea. Ikiwa ni sehemu ya kawaida ya kuboresha unafisi mahali popote.

2. Mziray kwa kuwa ndio mtoa hoja akateuliwa kuwa mwenyekiti, na wajumbe wengine ni kama ilivyotajwa.

3. Wakurugenzi hawateuliwi na Mwenyekiti, wanateuliwa na Kamati Kuu, soma katiba ya CHADEMA utaona. Lazima mapendekezo ya pelekwe na sekretariati au Viongozi wakuu lakini uteuzi unafanywa na Kamati Kuu. Soma kazi za Kamati kuu. ndio wakurugenzi wote walivyoteuliwa.

4. Upungufu wa kompyuta maanake yake nini? Mwaka 2006 niliwahi kupita makao makuu ya CHADEMA nikaona pana kompyuta. Sijawahi kwenda tena. Lakini wajumbe wetu waliokuja Zanzibar toka vikao DSM mwanzoni mwa mwaka huu wakati nikiwa Zanzibar waliteueleza kuwa makao makuu ya CHADEMA imepanuliwa. Sasa kuna ofisi kubwa mbili. Na kompyuta pia zimeongezeka. Sasa upungufu wa kompyuta sijui unaoelezwa hapo ni upi wa kiasi gani kwa kuwa hamna ufafanuzi.

5. Hilo la Maderava limeelezwa hapa na Mpaka Kieleweke kwa kutaja majina kabisa. Mimi nilisema maderava wako watano na mchagga ni mmoja tu kati yao. Yeye alisema wako sita na mchagga ni mmoja tu. Kwa hiyo kuna hoja ya pamoja kuwa dereva mchagga ni mmoja tu. Sasa hiyo ripoti imeamua kusema uwongo kabisa.

Mwanakijiji, mi naunga mkono kwa kweli. Mtafute Mziray na umuhoji maswali yafuatayo:

i. Je, ni ukweli kuwa ripoti ya Kamati yake ilikataliwa na Kamati Kuu kwa kura 28 za hapana dhidi ya kura tatu za NDIO na kupokolewa as no document na wajumbe kutoa hoja kuwa kamati yake ichukuliwe hatua? (Dr Slaa akihojiwa na citizen alisema hii ripoti ilikataliwa, na Zitto naye aliweka wazi pia kwenye gazeti mojawapo.
-Kwa taarifa nilizopewa mimi ni kuwa hii ripoti ilikataliwa kutokana na kutoa maelezo ya uwongo na yenye kulenga kuchochea mgawanyiko katika CHADEMA. Tundu Lissu aliita ripoti ya Kamati ya Kuratibu Majungu!. Wakati wajumbe wengine waliweka bayana kwamba ni Kamati imeandikiwa ripoti na CCM.

ii. Kwanini alikiri kwenye Kamati Kuu kuwa ripoti yake aliandika kwa kumhoji Amani Kaborou toka CCM? Je kwanini alikwenda kuwahoji CCM masuala ya ndani ya CHADEMA?

iii. Je, kwanini Katibu wa kamati ya Mziray mama Sophia khatau alipiga kura ya kuikataa ripoti ambayo yeye ni Katibu? Maana kura zilikuwa za wazi kabisa. Kwanini aliwasilisha kwenye kikao ripoti ambayo wajumbe wa kamati wala katibu hajasaini imesainiwa na yeye mwenyewe tu?

iv. Kama Kamati ilikuwa na wajumbe watano: Mmoja akafariki, Melecky ndugu yetu wa Zanzibar, Wakili Mbogoro hakushiriki kikao hata kimoja. Na Katibu wa Kamati ameikataa ripoti, Je, ripoti ya watu wawili ni ripoti ya Kamati?

Nitakuongezea maswali zaidi. Lakini naamini Dr Slaa, Zitto na Mnyika wakija hapa wataweka ufafanuzi zaidi

Asha
 
Chadema Inatakiwa Kubadilika,vinginevyo Itazidi Kudidimia.sasa Hivi Watu Wanazungumzia Mtu Mmoja Mmoja Kama Dr.slaa,Zitto Kabwe Lakini Hawazungumzii Chadema Kama Chama Kwa Nini?.
Kwa Viongozi Wenye Maono Hili Tu Pekee Lingekuwa Somo Tosha Kuonyesha Kwamba Wananchi Bado Hawana Imani Na Chama.

Nilitegemea Baada Ya Matokeo Duni Ya Uchaguzi Mkuu Viongozi Walioshindwa Vibaya Watajiondoa Kupisha Wengine Wajenge Chama Na Kujenga Imani Kwa Wananchi.lakini Mhh!

Utamaduni huu viongozi wengi wa Kiafrika hawana! Si tu waliokuwa madarakani wanataka kuendelea mpaka wanaposhindwa kutembea as if hakuna watu wengine wenye uwezo (Makamba, Kingunge, Mugabe, Kibaki...etc), lakini hata ambao wako vyama vya upinzani hawajifunzi kuwaachia watu wengine madaraka japo wameshaprove failure na hawana jipya (Seif, Mrema, Lipumba, na very soon Mbowe anawajoin). CHADEMA apewe Slaa, ameshaonyesha ni mtendaji mzuri mara elfu moja zaidi ya Mwenyekiti wake.
 
Dada Asha,

Tunashukuru sana kwa maelezo yako!!! Mwenye akili timamu anaelewa whatsup!!!

Maoni yangu bado ni yale yale jamii yetu imemomonyoka sana tunahitaji tujirekebishe.

CHADEMA ina goodwill kubwa kutoka kwa wananchi kutokana na juhudi binafsi za kina Zitto na Dr. Salaa, ni muhimu hizi juhudi zikisaidie Chama!

Kila kilichoelezwa kinawapa majibu waTanzania kwa nini CHADEMA haisongi mbele...
 
where is the problem? Mi Nadhani uchaguzi wa Chadema uko jirani tu na uko wazi kwa wana chadema.
Kwa kuwa wao ndio wenye uhuru wa kuchagua viongozi wawatakao tuwape muda na watakuja na kiongozi wanayemtaka.
Yaliyobaki naamini ni majungu tu ya watu wengi wanaojifanya wana uchungu na Chadema while ni wazandiki tu.
 
Nafikiri siku zote the best way to solve problem ni kukubali kwanza kama kuna tatizo. Kama tatizo hakuna then kamati iliundwa ya nini?! Ina maana iliundwa kumridhisha tu huyo Mziray huku wakijua hakuna tatizo? Japokuwa inawezekana kabisa matatizo yaliyoelezwa ni mengi kuliko yaliyopo, hii haiondoi ukweli kuwa kuna tatizo!
 
Wakati mwingine naamini kuna wasomi hapa, lakini saa kama hii ndio ninahoji uwezo wetu wa kupokea habari nzito na mwitikio wetu. Hofu yangu (iwe founded au la) ni kuwa tunaposoma habari hii reaction yetu inatoka kwenye vionjo vyetu na hisia zetu huku tukishaongozwa na preconceived ideas. Inakuwa vigumu kulihuku jambo kwa haki zote. Wengi tuliposoma habari hii nyuma ya mawazo yetu tumekuwa na "ukabila, wangwe, mbowe, n.k) badala ya kuihukumu ripoti hiyo na kutaka kujua mambo kadhaa kwanza.

a. Madai yanayotolewa ni mazito.
b. Ushahidi unaotajwa unaonekana ni mzito
c. Na mahitimisho yake kwa hakika ni mazito kabisa.

Lakini je hivyo ndivyo ilivyo.

a. Nashauri mtu aanze kurudia na kuisoma tena ripoti hiyo na kuiangalia kama mtu ambaye hajawahi kusikia habari za ukabila wa Chadema, au kusimamishwa kwa Wangwe. Yaani umpe mtu ambaye hajui mambo ya Chadema umuoneshe hiyo ripoti na umuombe aikosoe kwanza ili kuisimamisha kama shahidi. Hadi hivi sasa ripoti hiyo ukiileta mahakamani itachambuliwa kama mchele na kutupwa! Of course, kwa watu wengine, wanaona ripoti imevindicate their own preconceived positions.

Nitawapa mifano michache maana hata mimi baada ya kuisoma mara ya kwanza nilipatwa na mshangao wa madai mazito. Ni mpaka pale niliporudi pole pole ndipo nilipoweza kuona mapengo makubwa sana.

Mfano wa Kwanza: Hii Kamati ilitakiwa iwe ni kamati ya uchunguzi na utafiti kwa mujibu wa hadidu rejea. Swali la kwanza: Walitumia njia gani kufanya uchunguzi wao ili tuweze kujua mahitimisho waliyofikia ni sahihi. (Methodology). Ukiisoma hiyo ripoti unachoona ni kuwa imeandikwa kutoka kwenye kikao hadi kwenye mahitimisho kadhaa bila kusema katika kufanya utafiti wao walitumia njia gani. Walipowaita watu kuja kutoa ushahidi waliwaita kina nani, waliwaita katika mazingira gani, na watu hao walioitwa walikuwa kwa kiasi gani wako huru kusema ukweli au uongo? Na kwanini watu hao waliaminiwa na si wengine? Je kuna watu ambao hawakuitwa na wangekuwa na taarifa ya msingi?

Hilo hulioni kwenye ripoti hiyo?

Mfano wa Pili: Unapoandaa ripoti kama hii kuna mambo lazima uyatolee maana kwanza ili unapoyatumia mbeleni wasomaji wako wajue unazungumzia nini. Hebu angalia hapa:

Katika swala la uteuzi wa wakurugenzi waliohojiwa waliirifu kamati kuwa katika nafasi 8 za wakurugenzi, nne zinashikiliwa na watu wa mkoa mmoja wa Kilimanjaro (wachaga) kitu ambacho kamati katika uchunguzi wake imethibitisha.

Sasa mtu mmoja anaweza akasema "aha, unaona ni ukabila huo". Lakini mtu kama mimi nasema "So?" Ripoti ingetueleza kwanza kabisa kuwa kuna tatizo gani kwa watu wa mkoa mkoa au kabila moja kuwa katika ofisi au nafasi fulani. Na zaidi ya yote Ripoti hii ingelinganisha basi katika uongozi mzima wa Chadema kuna watumishi wangapi, ni wangapi wanatoka mkoa mmoja n.k Hivi ni wangapi wanatoka Dar hata kama si wote wa Zaramo? Tunalikubali hilo la ripoti kwa sababu tayari kumekuwa na kile ambacho nilikionesha huko nyuma "anti-chagga" sentiments. Ukiisoma hiyo ripoti utakutana na sentiments hizo: Hebu angalia:

kamati imegundua katika uchunguzi wake yupo mtu aliyependekezwa na kuajiriwa ndani ya chama kabla ya kuwa mwanachama (Bi Regina Mrema) ambaye ni Mchaga kabila analotoka Mwenyekiti wa chama, FREEMAN MBOWE.

Katika suala hili kamati imebaini utata katika ajira, moja ikiwa ni ya dereva na nyingine ikiwa ni ya Mkurugenzi. Kwa mujibu wa kumbukumbu ambazo kamati imeziona kuhusu ajira ya derevaBw. OLIVARI KARIA ambaye ni mchaga yafuatayo yalidhihiri

Kamati ilibaini kuna upendeleo wa kikabila katika ajira ya ukurugenzi kati ya HARBRON MWAKAGENDA na JOHN MREMA, ambaye ni mchaga kwa misingi ifuatayo

Badala yake JOHN MREMA aliyekuwa nyuma ya MWAKAGENDA akapendekezwa na kuingizwa katika payroll na hapo ikumbukwe Mheshimiwa KOMU na Mheshimiwa MREMA wanatoka mkoa mmoja (wachaga).

n.k

Sasa ukisoma habari ya huyo dereva Kamati yenyewe inasema hivi kwanza:

Inaonesha kama alipewa maelezo kwamba ili upate ajira ya udereva, lazima ulete kitu kidogo (rushwa/hongo) kwa muajiri, hivyo kitendo cha kupewa mkopo kabla ya kuajiriwa iliashiria kwamba ilikuwa ni kumuwezesha kifedha ili amudu kutoa kitu kigogo (rushwa) kwa maoni ya kamati.

sasa tungependa kuwauliza huyo jamaa aliajiriwa kwa sababu ni mchagga (kama wanavyotaka tuamini) au kwa sababu alitoa rushwa (kama wao wanavyoamini)? Watetezi wa ukabila watasema ni kwa sababu ni mchagga!

Naweza kuendelea kuivunja vunja hii ripoti kwa urahisi kama mabua! It is not even worthy my time. I was excited in the beginning lakini ninavyosoma, I find it to be a huge embarassment to anybody who has ever conducted an investigation into finding some truths on certain things. As a matter of fact, lilikuwa ni kosa kubwa sana kuwahusisha watu wa ndani ya Chadema kufanya utafiti wa ndani. Utafiti wa mambo kama haya ungefanywa na third party. Maana hata kwenye orodha ya majina ya wajumbe wa Kamati hatuambiwi wasifu wao ni nini hasa na kwanini waliqualify kuingia kwenye Kamati hiyo.

Hata hivyo nikiri kuwa kama lengo lao lilikuwa ni kugusa vionjo na hisia za watu basi wamefanikiwa na wanastahili pongezi. Lakini kama lilikuwa ni kushawishi akili basi kwa kutumia ushahidi wa kisomi (empirical evidence) wameshindwa vibaya sana.
 
where is the problem? Mi Nadhani uchaguzi wa Chadema uko jirani tu na uko wazi kwa wana chadema.
Kwa kuwa wao ndio wenye uhuru wa kuchagua viongozi wawatakao tuwape muda na watakuja na kiongozi wanayemtaka.
Yaliyobaki naamini ni majungu tu ya watu wengi wanaojifanya wana uchungu na Chadema while ni wazandiki tu.

Anyway, my political knowledge could be somehow limited, but I'm not aware how transparent and democratic that will be. Na hii inaanzia katika kuteua/kuchagua hao wagombea ndani ya vikao vya chama, maana kama sijakosea nimewahi kuona hapa JF kwamba moja ya sababu ya ugomvi wa Wangwe na Mbowe ni kwamba Wangwe alionyesha nia ya kuwania uenyekiti.
 
Mwanakijiji Bwana...

Nakuaminia, kwa hiyo unataka tujadili uandishi wa report "kwa hawajasoma research methodology"

Kwi kwi kwi... kweli vita yako ya kubadili mitazamo...ni ngumu,,, kwa kuwa kuna mabadiliko unayoyalazimisha yawe hivyo unavyotaka wewe!

Unatakiwa kujua kwamba kama chama makao makuu kina udhaifu, na waidhaifu wanatajwa mpaka wasemaji ambao katiba haiwatambui kama "John Mnyika" hivyo wewe ulitegemea Mziray yeye atakuwa mzuri atatoa ripoti nzuri kama ya Mwanakiji?ji...

Issue ni kwamba regardless ya mtiririko wa ripoti, yanayoandikwa yapo... kinachotakiwa ni nini kifanyike... simple....

Sasa kama unalinganisha na ushahidi wa kesi ya jinai... then for sure... mzee wangu uzee unaanza kukuletea shida...

Nilikuwa najianda ku-staafu kuandika hapa JF, lakini kwa kweli mzee wangu... hizi spinning sio nzuri hata kidogo!!!

Nani asiyejua kwamba Mnyika alikuwa anakurupuka kuweka misimamo ya CHADEMA pasipo na vikao wala kuwa na mandate ya msemaji wa CHAMA.

Nani asiyejua kwamba CHADEMA hivi sasa inashikiliwa na juhudi binafsi za kina Zitto na Dr. Slaaa... are you saying hii inahitaji report writting skills...

Acha ndugu watanzania wanaona munayo-spin hapa!!!
 
UKWELI WA MOSHI UNAOFUKA NDANI YA CHADEMA

Ripoti ya Kamati Ndogo ya Kamati Kuu iliyoteuliwa katika kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA iliyokutana katika ukumbi wa Haidery Plaza Dar es salaam kati ya Julai 31 na Agosti 1, 2007. Taarifa hii imejumuisha matokeo ya uchunguzi, maoni na mapendekezo ya wana-kamati. Kamati hiyo ndogo inajulikana kwa jina la kamati ya Mziray.

Ripoti hii ya utafiti wa kamati ya Mziray ndiyo ilikataliwa na FREEMAN MBOWE lakini pia haikiwahi kuwekwa wazi kwa watanzania, hususan mashabiki, wapenzi na wapiga kura wa CHADEMA.

KAMATI ILIANZA VIKAO VYAKE AGOSTI 16, 2007 SAA 4.15 ASUBUHI NA KUKAMILISHA KAZI ZAKE DESEMBA 16, 2007 KWA AWAMU MBILI NA VIKAO VILIFANYIKA KATIKA UKUMBI WA TCD.

WAJUMBE WA KAMATI NA MUUNDO WAKE

Bw. MECKY MZIRAY – MWENYEKITI
Bi. SOPHIA KATAU – KATIBU
Bw. PHILIP SHELEMBI – MJUMBE
Bw. MUHSIN MELEK – MJUMBE
Bw. EDSON MBOGORO – MJUMBE

Bw. EDSON MBOGORO hakuweza kuhudhuria vikao vyote vya Kamati kwa udhuru.

1.0 HADIDU REJEA ZA KAMATI

Kamati ilipewa hadidu za rejea zifuatazo:

i) Kuchunguza tuhuma za kuwepo ubaguzi ndani ya makao makuu ya chama.
ii) Kuchunguza tatizo la mawasiliano ndani ya chama hususan makao makuu.
iii) Kuchunguza kiini cha viongozi hususan wa juu kujiondoa katika chama.
iv) Kuboresha maslahi ya watendaji makao makuu ili kupunguza wimbi la kuondokewa na viongozi ndani ya chama.

2.0 MATATIZO NA MAFANIKIO

Kutokana na uvyeti wa masuala yaliyojitokeza wakati wa mahojiano kamati ilibaini muda iliyopewa kukamilisha kazi zake haukuwa wa kutosha. Jumla ya wanachama 42 walijitokeza na kuhojiwa na kamati, kati yao wapo wajumbe wa secretarieti ya chama.

Kamati inashauri swala la uteuzi wa wabunge wa viti maalum katika siku za usoni uwepo umakini wa hali ya juu katika uteuzi wa viti hivyo kwa kuzingatia matakwa ya katiba ya chama na pia uwepo utaratibu wa ukomo wa vipindi vya mbele vya kuwa mbunge wa viti maalum.

3.0 Uteuzi wa nafasi za Wakurugenzi

Katika swala la uteuzi wa wakurugenzi waliohojiwa waliirifu kamati kuwa katika nafasi 8 za wakurugenzi, nne zinashikiliwa na watu wa mkoa mmoja wa Kilimanjaro (wachaga) kitu ambacho kamati katika uchunguzi wake imethibitisha.

Katika hili kamati inatoa maoni na mapendekezo kwamba nafasi zote za kazi katika chama zitangazwe ndani ya chama katika ngazi zote. Hii itasaidia kuweka wigo mpana katika uwiano wa kikabila, dini na jinsia miongoni mwa watendaji na kukifanya chama kuwa na sura ya kitaifa.

Pia kwa kufanya hivyo tutaweza kuwa na uhakika wa muombaji wa nafasi ya uongozi kama ni mwanachama mwenzetu, maana kamati imegundua katika uchunguzi wake yupo mtu aliyependekezwa na kuajiriwa ndani ya chama kabla ya kuwa mwanachama (Bi Regina Mrema) ambaye ni Mchaga kabila analotoka Mwenyekiti wa chama, FREEMAN MBOWE.

4.0 Upendeleo katika ajira ndani ya chama

Katika suala hili kamati imebaini utata katika ajira, moja ikiwa ni ya dereva na nyingine ikiwa ni ya Mkurugenzi. Kwa mujibu wa kumbukumbu ambazo kamati imeziona kuhusu ajira ya derevaBw. OLIVARI KARIA ambaye ni mchaga yafuatayo yalidhihiri:-

Barua ya maombi ya kazi iliandikwa Septemba 25, 2005 na maombi yake ya kazi yalipokelewa Julai 13, 2006 na kushughulikiwa na Bw. A. KOMU ambaye pia ni mchaga kwa kuandika ajibiwe kama nafasi ikitikea ataitwa.

Aprili 20, 2006 aliandika barua ya kumuarifu kwamba ameingizwa katika orodha ya wafanyakazi wa kujitolea. Ilipofika Machi 28, 2006 aliomba mkopo wa sh. Laki moja na nusu na kukubaliwa kwa makato ya sh. 20,000 kwa mwezi ina maana alipewa hata kabla hajaajiriwa rasmi.

Inaonesha kama alipewa maelezo kwamba ili upate ajira ya udereva, lazima ulete kitu kidogo (rushwa/hongo) kwa muajiri, hivyo kitendo cha kupewa mkopo kabla ya kuajiriwa iliashiria kwamba ilikuwa ni kumuwezesha kifedha ili amudu kutoa kitu kigogo (rushwa) kwa maoni ya kamati.

Kamati ilibaini kwamba kabla ya OLIVARI KARIA kuajiriwa, palikuwa tayari na Bw. PELA NGUNANGWA ambaye alikuwa akifanya kazi ya kujitolea kama dereva tangu 2005 na alikwisha tuma maombi ya ajira ya udereva tangu 2005 kabla ya OLIVARI KARIA kutuma maombi yake.

Kamati ilishindwa kuelewa ni kwa nini awe OLIVARI KARIA aliyeajiriwa wakati tayari kulikuwa na dereva ambaye alikuwa akijitolea kwa kipindi kirefu na baadaye kuachishwa kwa maelezo kwamba chama hakihitaji dereva. Lakini baada ya mwezi mmoja OLIVARI KARIA akaajiriwa kwa kazi hiyo.

Pili, kamati ilishindwa kupata kigezo maalum kilichomsukuma Mheshimiwa ANTHONY KOMU, apendekeze ajira ya OLIVARI KARIA badala ya dereva aliyejitolea kufanya kazi kwa kipindi kirefu. Hapa ndio harufu ya upendeleo katika ajira kwa kigezo cha ukabila (uchaga) inapata nguvu.

5.0 UTEUZI WA NAFASI ZA WAKURUGENZI WA IDARA ZA
CHAMA

Kuhusu ajira za wakurugenzi, Kamati ilipokea maelezo kutoka kwa wahojiwa mbalimbali wakiwemo wahusika na katika uchunguzi wake, kamati ilibaini kuna upendeleo wa kikabila katika ajira ya ukurugenzi kati ya HARBRON MWAKAGENDA na JOHN MREMA, ambaye ni mchaga kwa misingi ifuatayo:-

MWAKAGENDA alikuwa na sifa za kuwa Mkurugenzi kwa vigezo vilivyowekwa na chama.
MWAKAGENDA alikitumikia chama kwa muda mrefu kabla ya MREMA.

Kwa mujibu wa maelezo ya ANTONY KOMU mbele ya kamati hii, alieleza kwamba yeye ndiye anayependekeza kwa sekretarieti ajira na hatimaye kuingizwa kwenye payroll (Orodha ya watumishi wanaolipwa mshahara) kama mtumishi.

Kamati ilishindwa kuelewa ilikuwaje kwa miaka zaidi ya mitatu KOMU alishindwa kupendekeza kwa sekretarieti ajira na hatimaye kuingizwa katika payroll Mheshimiwa MWAKAGENDA. Badala yake JOHN MREMA aliyekuwa nyuma ya MWAKAGENDA akapendekezwa na kuingizwa katika payroll na hapo ikumbukwe Mheshimiwa KOMU na Mheshimiwa MREMA wanatoka mkoa mmoja (wachaga).

Hii pia imesababisha Mheshimiwa MWAKAGENDA kuondoka makao makuu na kwa maelezo yake mwenyewe MWAKAGENDA alisema kuwa alikwisha omba kuingizwa katika ajira ya ukurugenzi na kuwekwa kwenye payroll kabla ya MREMA.

Katika hayo mawili kamati inatoa maoni na mapendekezo yafuatayo:

Katibu Mkuu achukuliwe hatua za kiutawala dhidi ya matukio hayo mawili kwa wahusika na taarifa iletwe kwenye kamati kuu.

Kamati inapendekeza kwamba kurugenzi ya fedha na utawala zitenganishwe. Na kuwa kurugenzi mbili zinazojitegemea. Pendekezo hili linalenga kupunguza nguvu na majukumu ya Mkurugenzi wa Fedha na Utawala.

Kamati inapendekeza kwamba kama itaonekana gharama kutenganisha kurugenzi hizo, basi kurugenzi ya Fedha iunganishwe na kurugenzi ya Rasillimali.

6.0 UBAGUZI WA DINI

Katika suala la ubaguzi wa dini, kamati ilipokea maelezo toka kwa wahojiwa mbalimbali, lakini kamati ilibaini kwamba moja lilijitokeza ni katika nafasi za kurugenzi.
Kamati ilipokea maelezo na kuthibitisha kwamba, kati ya wakurugenzi nane waliopo sasa hivi, ni mkurugenzi mmoja tu Mheshimiwa ZITTO KABWE ndio muislamu.

Zilitolewa hoja mbele ya kamati kuonesha kwamba kuna ugumu wa kupata watendaji kwa kigezo cha uwiano wa dini, hoja ambayo ilijibiwa kwamba Tanzania visiwani kuna waislamu wengi lakini hakuna mkurugenzi anayetoka huko.

Hivyo, kamati ilibaini kwamba dhana ya ubaguzi wa kidini inatokana na uwiano usio sawa wa watendaji hususan wakurugenzi katika makao makuu.

Katika hili kamati inatoa maoni na kupendekeza kwamba uanzishwe utaratibu wa kutangaza nafasi zote za watendaji katika ngazi zote ndani ya chama na kutumwa mikoani, ambako wanachama wenye sifa zinazotakiwa, watapata fursa ya kuomba kazi hizo na hivyo kuwa na wigo mpana wa kuweza kuweka uwiano wa kidini kikabila na kijinsia katika kurugenzi za chama na ajira nyinginezo.

Mtindo uliopo sasa ambao kamati imeubaini wa kuangalia zaidi vijana wanaotoka vyuo vikuu haufai kuendelea kutumika.

Kamati ilishangazwa sana na maelezo yaliyotolewa na mkurugenzi wa vijana (JOHN MNYIKA) kwamba yeye ndiye anayewatafuta kwa kuwashawishi vijana wanaomaliza vyuo vikuu wajiunge na chama ili wapate ajira ndani ya chama.

7.0 UBAGUZI WA ELIMU

Kamati imeridhia kwamba, dhana ya ubaguzi kwa kigezo cha elimu inatengenezwa na mazingira yaliyopo kwa watendaji makao makuu. Mfano, sifa ya mkurugenzi ndani ya chama ni elimu ya chuo kikuu.

Kamati inaona kwamba, pamoja na umuhimu wa kuwa na watendaji wenye elimu ya juu, hasa kutoka chuo kikuu inawezekana kwa sababu hiyo kwa mtu ambaye hakuweza kufika elimu ya chuo kikuu akaona anabaguliwa kielimu.

Chama kinahitaji watendaji wanaoweza kutekeleza majukumu yao kwa hali ya juu hata kama hakufika ngazi ya elimu ya chuo kikuu.

Katika hali hiyo kamati inatoa maoni na kupendekeza kwamba pawepo na utaratibu wa kutathmini uwezo wa maafisa wa chama ngazi zote pale itakapodhihirika yupo ofisa mwenye uwezo wa kumudu ngazi ya ukurugenzi apandishwe cheo hata kama hana elimu ya chuo kikuu.

Hii itaongeza tija na changamoto kwa watendaji wa ngazi zote na kuondoa dhana ya kubaguliwa kwa kigezo cha kukosa elimu.

8.0 KIINI NA SABABU ZINAZOFANYA VIONGOZI WETU WAJIONDOE KATIKA CHAMA.

Katika hili kamati ilipata maelezo kutoka kwa wahojiwa waliofika mbele ya kamati pamoja na wahusika.

Kutokana na yaliyojitokeza katika mahojiano hayo, kiini kilichosababisha viongozi kujiondoa katika chama ni staili inayotumiwa na viongozi wa ngazi za juu.

Kamati ilibaini viongozi wetu wa ngazi za juu ni wazito kumkabili mtu na kumwambia ukweli badala yake wanakuwa wasengenyaji na kuwindana.

Kwa mfano, kamati ilibaini kwamba aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Mhe. AKWILOMBE alikuwa na matatizo na udhaifu mkubwa kiutendaji kwa maana kwamba, mahudhurio yake yalikuwa hafifu na hakuwa mwaminifu katika masuala ya fedha.

Lakini kamati haikupata ushahidi wowote kwamba Mheshimiwa huyo aliwahi kuripotiwa katika kamati kuu kutokana na udhaifu wake huo. Isipokuwa viongozi wa ngazi ya juu walikuwa wakimsengenya tu kwa watu mbalimbali juu ya udhaifu wake.

Hii ndio tabia ya kusengenyana na kuwindana ambayo inazaa majungu ambayo baadaye humfikia mhusika na hatimaye kujiona anatengwa na kubaguliwa na viongozi wenzake.

Uchunguzi wa kamati ulibaini chanzo cha Naibu katibu Mkuu, AKWILOMBE kuhama chama ni pale alipohisi kwamba anabaguliwa na kutengwa na viongozi wenzake.

Kwa upande wa Dkt. Kabourou kamati ilibaini kwamba kulikuwa na uhusiano wa mashaka kati yake yeye na Mwenyekiti wa chama taifa Mheshimiwa MBOWE.

Kwa maelezo ya mheshimiwa Kabourou, ni kwamba yeye akiwa Katibu Mkuu wa chama, Mheshimiwa MBOWE akiwa ni Mbunge wa Hai, aliongoza kampeni za kumuondoa Ukatibu Mkuu kwa maelezo kwamba yeye na Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Makani wameshindwa kutekeleza majukumu ya kukiongoza chama na chama kufikia kudhoofika.

Mheshimiwa KABOUROU kwa kauli yake mwenyewe alimtuhumu Mheshimiwa MBOWE kuwa alitoa shilingi milioni mbili (2,000,000/-) kwa kamati iliyokuwa ikikutana Legho Hotel kupanga mkakati ya kumuondoa. Hicho kilipelekea uhusiano wa mashaka kati ya Mwenyekiti na Makamu wake wakati wote hadi alipohamia kwenda CCM.

Katika hili kamati inapendekeza kwamba viongozi wetu wawe na ujasiri wa kumkabili kiongozi yeyote anayeonesha kwa maneno na vitendo vyake kwamba anapotosha chama na sio kumjadili pembeni au kumsengenya ama kufanya hila za kumuengua.
9.0 TATIZO LA MAWASILIANO NDANI YA CHAMA

Katika swala hili kamati imehoji na kuthibitishwa na wahojiwa wote kwamba mtiririko wa mawasiliano Makao Makuu ni mbovu sana na kamati nayo imethibitisha kuwa mawasiliano ni mabovu na hayana mtiririko wa kiitifaki.

Kwa mfano, Mwenyekiti anamshirikisha vipi Makamu katika utendaji wa kazi tumebaini kwa waliohojiwa kuwa Mwenyekiti huteua baadhi ya watendaji kufanya nao kazi au kuwapa maagizo ya ofisi.

Mwenyekiti anapokuwa safarini hufanya mawasiliano na Bw. JOHN MNYIKA badala ya kuwasiliana na Makamu Mwenyekiti kama mtendaji wa shughuli za chama.

Hoja hiyo ipo kwa Katibu Mkuu anapokuwa nje ya ofisi hufanya mawasiliano nje ya mtiririko wa kiitifaki na hata kumruka aliyemuachia ofisi. Hii inasababisha dharau na kutojenga heshima kwa anayekaimu nafasi yake kwa mantiki hiyo kamati imeona ni vyema itifaki ifuatwe, mtiririko wa majukumu uende sambamba na nafasi aliyo kiungozi.

Swala la watendaji nalo kamati imeona kuwa hakuna mtiririko wa mawasiliano. Watendaji hufanya uamuzi kulingana na jinsi wanavyomfahamu mkurugenzi fulani.

Kwa mfano tabia ya Bw. MSAFIRI kufanya matengenezo ya magari imelalamikiwa na madereva wote kuwa hawana nafasi ya kueleza matatizo ya magari kwa utawala badala yake yeye (MSAFIRI) ndiye husimamia kazi hizo kama nani?

Kwa upande wa wakurugenzi, hufanya safari za chama mikoani na wanapofika huko hawawasiliani na uongozi wa wilaya na huamua kufanya kazi hizo peke yao na hili linapelekea kushindwa kufanya kazi za chama kwa mafanikio.

Mheshimiwa JOHN MNYIKA ametajwa mara zote kuwa hufanya kazi za kurugenzi nyingine bila taarifa kwa mfano anapotoa taarifa kwa vyombo vya habari wakati Mkurugenzi wa habari yupo makao makuu.

Kamati hii imebaini mawasiliano mabovu kati ya makao makuu bara na visiwani, mara nyingi sekretarieti imekuwa ikikutana Dar es salaam lakini haimshirikishi Naibu Katibu Mkuu kutoka Zanzibar katika vikao vyake.

Kamati hii imebaini dharau za watendaji wa makao makuu kushindwa kuwapokea na kuwakaribisha wajumbe wa kamati kuu na baraza kuu na wageni wengine kama wanavyostahili

Kamati imebaini kuwa ofisi za makao makuu zinatumiwa na wageni wa watendaji kwa shughuli binafsi za wageni wao binafsi. Na hata kutumia vitendea kazi mfano kompyuta za chama kwa shughuli binafsi.

Pia palitolewa malalamiko kuwa ofisi ya Katibu Mkuu inatumiwa na watendaji isivyostahili kwa mfano watendaji huingia ndani ya ofisi hiyo ambapo wanatuhumiwa kufanya maongezi binafsi na marafiki zao wa kike.

Kamati ilibaini kwamba ofisi za chama makao makuu muda wote zinakuwa hazifungwi kitendo ambacho kinahatarisha usalama wa vifaa na nyaraka za chama na uvujaji wa siri za chama.

Kamati imebaini kwamba maazimio mengi ya kamati kuu hayatekelezwi ipasavyo na sekretarieti ya chama, kwa mfano kamati Kuu iliagiza kurugenzi ya wanawake na vijana zipatiwe fedha kwa ajili ya utendaji wake, lakini hadi sasa secretarieti haijatekeleza kimamilifu agizo hilo.

Pia ikumbukwe kwamba ni muda mrefu kamati kuu iliagiza ruzuku za mikoa kupelekwa mikoani lakini secretarieti imekawia kutekeleza agizo hilo.

Kamati imebaini mambo mawili yanayosababisha secretarieti kupata nguvu ya kutotekeleza maagizo ya kamati kuu kama yafuatavyo:-

Kitendo cha Mwenyekiti kuhudhuria baadhi ya mikutano ya secretarieti
Kitendo cha wajumbe wa secretarieti kuhudhuria na kushiriki mijadala ya vikao vya kamati Kuu.

Katika hili kamati imeona wajumbe wa secretarieti kuhudhuria vikao vya kamati kuu ni sawa na kuwadhalilisha wajumbe wa kamati.

Mapendekezo na maoni ya kamati katika swala la mawasiliano

Makabidhiano ya ofisi yafuate mtiririko wa kiitifaki
Mawasiliano yote ya kiutendaji na kiutawala yasipelekwe moja kwa moja kwa wakurugenzi na maafisa wa chama isipokuwa kupitia kwa Katibu Mkuu.
Nafasi ya Naibu katibu Mkuu (ZNZ) anapokuwa ofisi ya makao makuu Dar es salaam ifafanuliwe.
Ofisi za Makao Makuu ziwe zinafungwa pale ambapo wahusika hawazitumii.
Kitengo cha ulinzi na usalama makao makuu ya chama kiimarishwe kwa kupata maofisa wenye utaalam wa kutosha katika masuala ya usalama na utambuzi.
Wageni wote binafsi wa watendaji wawe na mahali maalum pa mazungumzo.
Kuwe na mikutano ya mara kwa mara baina ya watendaji wa makao makuu ili waweze kufahamiana na kujenga mahusiano ya karibu miongoni mwao. Katika hili kamati inapendekeza kuanzishwa kwa tawi la chama makao makuu haraka.
Wajumbe wa secretarieti waondolewe kuwa wajumbe wa kamati kuu.

10.0 KUBORESHA MASLAHI YA WATENDAJI MAKAO MAKUU

Katika swala la uboreshaji wa maslahi ya watendaji wa makao makuu
kamati ilizingatia mambo mawili yafuatayo.

Uboreshwaji wa maslahi ya watumishi makao makuu.
Uboreshwaji wa vitendea kazi makao makuu.

Kamati ililitizama hili la kuboresha maslahi ya watendaji na kubaini kwamba wengi wa waliohojiwa na kamati walipendekeza kiasi cha posho kiongezwe

Kamati ilizingatia kwamba wengi wa waliotoa mawazo hayo walikuwa ni wajumbe wa secretarieti ambao walikuwa na mgongano wa kimaslahi katika swala hili.

Hivyo kamati inapendekeza posho wanayolipwa watendaji isiongezwe (ibaki kama ilivyo), katika hili kamati imezingatia zaidi hali halisi ya utendaji kazi makao makuu na hali ya mapato na matumizi ya chama.

Kamati iliangalia swala la vitendea kazi katika makao makuu ya chama na kubaini mapungufu yafuatayo.

Upungufu mkubwa wa vyumba vya ofisi kwa watendaji
uchache wa kompyuta
usimamizi mbovu wa matengenezo ya magari
mtandao (Internet) wa chama kutokuwa na mawasiliano ya uhakika.

Mapendekezo na maoni ya kamati

Watumishi wa ngazi zote waajiriwe kwa mikataba ya miaka miwili ili waweze kupata kiinua gongo wanapomaliza muda wao wa mkataba.

Watumishi wataoajiliwa kwa mikataba waingizwe kwenye mifuko ya jamii kwa mfano NSSF ili waweze kupata huduma na mafao yanayotolewa na mifuko hiyo.

Kuwepo na muda wa kuingia na kutoka kazini unaotambulika na inapotokea kazi za ziada baada ya muda unaotambulika wa kazi kuwe na utaratibu wa kumlipa mtumishi malipo ya ziada au posho maalam.

Kuwepo na utaratibu wa kutathmini utendaji wa kila mtumishi ili ithibitike kuwa kile anachokifanya kwa chama kina tija kiasi gani na kinalingana na thamani ya malipo anayolipwa na chama.

Kamati ilitia shaka juu ya utendaji wa wakurugenzi na maafisa wa chama baada ya kuona wakurugenzi na maafisa wote wa chama ni wakazi wa Dar es salaam. Lakini cha kustaajabisha mkoani Dar es salaam, si kwamba hakuna ofisi ya mkoa tu, bali hata uongozi wa mkoa una matatizo ya msingi hivyo kamati ina mashaka na uwajibikaji wa wakurugenzi na maafisa wa vitengo kama vya organization , vijana na wanawake.

Chama kichukue hatua za dharura kukabiliana na tatizo la upungufu wa vyumba vya ofisi kwa watendaji na kwa kuanzia kamati inapendekeza kila kurugenzi iwe na ofisi yake.

Katika hili kamati inapendekeza kuwa kutokana na uharaka na gharama, chama kinunue makontena mawili ya futi 40 ambayo yatatengenezwa na kufanywa kuwa ofisi.

Kamati inapendekeza kwamba kutokana na uhaba wa kompyuta ambacho ni kitendea kazi muhimu katika ulimwengu wa sasa, chama kinunue kompyuta moja kwa kila kurugenzi.

Chama kitoe zabuni kwa mtu au kampuni kwa vigezo vya sifa na uwezo kwa ajili ya kufanyia matengenezo magari ya chama.

Kamati inapendekeza hatua za haraka zichukuliwe kuhakiki mawasiliano ya Internet ili yaboreshwe katika ofisi ya chama makao makuu.

Kamati inapendekeza kuwepo kwa uwiano kati ya watumishi na kazi zilizopo, na kwa hali ilivyo sasa kamati inapendekeza watumishi wapunguzwe makao makuu.

Paparazi Muwazi na Ukweli kuhusu kinachoitwa Mgogoro wa CHADEMA:

Hapa alianza na Igunga-

https://www.jamiiforums.com/showthread.php?p=228844#post228844

Halafu akasema:

https://www.jamiiforums.com/showthread.php?p=229412#post229412

Halafu akaanza kuizungumza ripoti ya Mziray:

https://www.jamiiforums.com/showthread.php?p=238055#post238055

Halafu akalipua Bomu la Rostam na Chacha Wangwe na ripoti ya Mziray:

https://www.jamiiforums.com/showthread.php?p=240809#post240809

Halafu akaendelea:

https://www.jamiiforums.com/showthread.php?p=240964#post240964

Aendelea kuanika Mengine:

https://www.jamiiforums.com/showthread.php?p=240969#post240969

Akaanika kosa la kisiasa la Mbowe kuhusu Ripoti ya Mziray:

https://www.jamiiforums.com/showthread.php?p=240992#post240992

Akaendelea kueleza mengine:

https://www.jamiiforums.com/showthread.php?p=241031#post241031

Akadokeza tofauti ya Chacha na Rostam:

https://www.jamiiforums.com/showthread.php?p=241580#post241580

Akaweka bayana kuhusu Zitto, Rostam na uchaguzi wa kumchagua Chacha Wangwe mwaka 2007:

https://www.jamiiforums.com/showthread.php?p=241602#post241602

Azungumzia mikakati mingine:

https://www.jamiiforums.com/showthread.php?p=241636#post241636

Aendelea kubainisha:

https://www.jamiiforums.com/showthread.php?p=244499#post244499

Azungumzia kwa kina asili ya taarifa ya Mziray na Mkakati wa kutaka viongozi wa CHADEMA wajiuzulu:

https://www.jamiiforums.com/showthread.php?p=244687#post244687

Azidi kuanika Mkakati wa kutaka viongozi wa CHADEMA wajiuzulu kwa kutumia ripoti ya Mziray, na Mkakati wa Rostam wa kuchafua Dr Slaa kwa kutumia ripoti hii, aeleza Ballile anavyoratibu:

https://www.jamiiforums.com/showthread.php?p=244704#post244704

Aanika mikakati mingine zaidi:

https://www.jamiiforums.com/showthread.php?p=245983#post245983

Azidi kudokeza yanayoendelea:

https://www.jamiiforums.com/showthread.php?p=246090#post246090

Ataja suala la Benki Statement za Mwanahalisi(hii ni kabla ya polisi kusema kwamba suala hili linahusiana na NBC:

https://www.jamiiforums.com/showthread.php?p=250000#post250000

Kwa kweli nimesoma hizo thread zote alizoandika toka mjadala uanze, naona zinaeleza mengi sana

Asha
 
Mwanakijiji Bwana...

Nakuaminia, kwa hiyo unataka tujadili uandishi wa report "kwa hawajasoma research methodology"

Kwi kwi kwi... kweli vita yako ya kubadili mitazamo...ni ngumu,,, kwa kuwa kuna mabadiliko unayoyalazimisha yawe hivyo!

Unatakiwa kujua kwamba kama chama makao makuu kina udhaifu, na waidhaifu wanatajwa mpaka wasemaji ambao katibu haiwatambui kama "John Mnyika" hivyo wewe ulitegemea mziray yeye atakuwa mzuri atatoa ripoti nzuri kama ya Mwanakijiji...

Issue ni kwamba regardless ya mtiririko wa ripoti, yanayoandikwa yapo... kinachotakiwa ni nini kifanyike... simple....

Sasa kama unalinganisha na ushahidi wa kesi ya jinai... then for sure... mzee wangu uzee unaanza kukuletea shida...

Hivi Katiba haimtambui Mkurugenzi wa Vijana wa CHADEMA kama msemaji mkuu wa vijana wa CHADEMA? Hivi matamko ambayo amekuwa akiyatoa si ya vijana?

Hivi CHADEMA si ina utaratibu wa Makaimu Katibu wakuu wakati Katibu Mkuu na Manaibu wake hawapo? Sasa Kimesera na Mnyika si ndio ambao wanakaimu mara kwa mara na kutoa matamko kwa niaba ya chama chetu na hawa wote wawili ni wakurugenzi ambao wana mamlaka kabisa ya kutoa matamko ya kiutendaji?

Hebu tuonyeshe tamko moja tu ambalo limetolewa na kiongozi wa CHADEMA ambae hana mamlaka ya kutoa tamko alilolitoa.

Asha
 
Dada Asha,

Usipate shida, mchawi murudi mezani, muredi kwenye chama chetu mujisahihishe...
 
Mwanakijiji Bwana...

Nakuaminia, kwa hiyo unataka tujadili uandishi wa report "kwa hawajasoma research methodology"

Kwi kwi kwi... kweli vita yako ya kubadili mitazamo...ni ngumu,,, kwa kuwa kuna mabadiliko unayoyalazimisha yawe hivyo!

Unatakiwa kujua kwamba kama chama makao makuu kina udhaifu, na waidhaifu wanatajwa mpaka wasemaji ambao katibu haiwatambui kama "John Mnyika" hivyo wewe ulitegemea mziray yeye atakuwa mzuri atatoa ripoti nzuri kama ya Mwanakijiji...

Issue ni kwamba regardless ya mtiririko wa ripoti, yanayoandikwa yapo... kinachotakiwa ni nini kifanyike... simple....

Sasa kama unalinganisha na ushahidi wa kesi ya jinai... then for sure... mzee wangu uzee unaanza kukuletea shida...

Kasheshe pamoja na madhaifu yote ya CCM lakini wao wanapoandika ripoti ya jambo ndugu yangu wanafanya kisomi. Hata kama hatupendi wanachokisema lakini wanajitahidi kwa kiwango kikubwa angalau kujenga ripoti yao kisomi. Sasa wewe unasema yanayosemwa yapo! sasa kama yapo kwanini kuyachunguza?

Je yawezekana walipokuwa wanafanya uchunguzi wao tayari walikuwa wanatafuta kuthibitisha kitu ambacho wao wenyewe wanakijua? Imesemwa hapo juu kuwa uchunguzi ulianzishwa baada ya Mziray kutoa hoja ya kuanzishwa uchunguzi wa ukabila (yaani tayari alishakuwa na mawazo hayo) halafu huyo huyo mnampa uenyekiti wa kutafuta kama kuna ukabila, sasa amekuja na kuonesha ukabila inashangaza!?

Tunaweza si wote wasomi kama wengine, lakini hata kwa elimu yangu ya vidudu siwezi kukumbatia ripoti ya namna hiyo. Na hapa simlaumu Mziray na timu yake nalaumu uongozi wa Chadema kwa kuunda kamati mbovu kama hii isiyo na uwezo wa kufanya uchunguzi huru. Kama kuna sababu ya mtu yeyote kujiuzulu ni hii ya kushindwa kuendesha uchunguzi huru.

Ndio maana hata EPA walioweza kutuonesha ukweli na umetulazimu kuamini walikuwa ni Deloitte and Touche na baadaye Ernst and Young! Binafsi ningeheshimu sana findings of a credible, unbiased, and neutral team of investigations. This is a "sham" investigation. It is a pure as that. Unaweza vipi kwenda kuchunguza kitu ambacho unajua tayari kipo? Have you ever heard of something called "self-fulfliling prophecy"? My friend Pundit is a master of explaining that.
 
.[/U]

3.0 Uteuzi wa nafasi za Wakurugenzi

Katika swala la uteuzi wa wakurugenzi waliohojiwa waliirifu kamati kuwa katika nafasi 8 za wakurugenzi, nne zinashikiliwa na watu wa mkoa mmoja wa Kilimanjaro (wachaga) kitu ambacho kamati katika uchunguzi wake imethibitisha.

Katika hili kamati inatoa maoni na mapendekezo kwamba nafasi zote za kazi katika chama zitangazwe ndani ya chama katika ngazi zote. Hii itasaidia kuweka wigo mpana katika uwiano wa kikabila, dini na jinsia miongoni mwa watendaji na kukifanya chama kuwa na sura ya kitaifa.

Pia kwa kufanya hivyo tutaweza kuwa na uhakika wa muombaji wa nafasi ya uongozi kama ni mwanachama mwenzetu, maana kamati imegundua katika uchunguzi wake yupo mtu aliyependekezwa na kuajiriwa ndani ya chama kabla ya kuwa mwanachama (Bi Regina Mrema) ambaye ni Mchaga kabila analotoka Mwenyekiti wa chama, FREEMAN MBOWE.
[/B]

Yani huu ni uwongo aisee. Kamati imethibitisha kitu ambacho hakipo!

1. CHADEMA haina wakurugenzi wanne wachagga. Kusema kwamba kuna wakurugenzi wanne wachagga ni uongo. Ndio maana Kamati Kuu ikaikataa taarifa kwa kuwa kamati kuu ndio iliyoteua wakurugenzi inajua hakuna wakurugenzi wanne wachagga.

2. Kusema kwamba kuna mtu anaitwa Regina Mrema makao makuu ya CHADEMA na ni mchagga ni uwongo wa mchana. Nimeshaeleza wazi kwamba kuna dada mlemavu anaitwa Regia Mtema, ambaye hata namba yake alinipatia na ni mtu wa asili ya Morogoro. Hata hata mzazi mmoja mchagga au mtu wa kilimanjaro.

Swali la kujiuliza, ni kwa nini Kamati ya Mziray, ama tuseme Mziray mwenyewe kwa kuwa hata katibu wa kamati alipiga kura ya kuikataa ripoti. Ni kwanini akaandika ripoti ya uwongo, na ni kwanini ripoti hiyo ikaandikwa na gazeti la Mtanzania kabla hata ya kuwasilishwa kwa kamati kuu Dodoma?

Ni kwanini ripoti hiyo ambayo inajulikana kabisa ni ya uwongo inasambazwa kwa nguvu zote hizi? Kupitia makala za magazeti nk

Je, huu sio mkakati mahususi wa kuichafua CHADEMA na viongozi wake katika kipindi hiki cha vita dhidi ya ufisadi ili watanzania wapoteze imani nao?

Je, hii haifanani na ule waraka kuhusu Mbowe, waraka kuhusu Zitto, na Waraka kuhusu Dr Slaa ambayo ilisambazwa kwa kasi mwaka jana mara baada ya CHADEMA kuanza kuibua kwa nguvu ufisadi lakini ikaja kubainika kuwa tuhuma na shutuma zote zilikuwa za uongo?

Kwa kweli naelekea kukubaliana na Paparazi Muwazi, hapa kuna jambo.

Kwa kweli nimeamini chama changu ni safi ukilinganisha na vyama vingine, kama pamoja na mkakati wote hizo ndio hoja zinazotolewa kuichafua CHADEMA na viongozi wake basi hii ni taasisi ni safi sana. Imagine kama CCM ndio ingepandikiziwa watu wa kuanika kila kilichomo hali ingekuwaje. Au taasisi nyingine.

Hii ina nipa nguvu zaidi ya kuipenda CHADEMA kwa kweli, chama cha demokrasia na maendeleo.

Hofu yangu ni kama huu ufafanuzi unaotolewa humu kuvunja vunja haya majungu hautolewi kwenye vyombo vya habari wakati ambapo ripoti hii gazeti la Rai na Majira wameichapa neno kwa neno.

Wakati umefika sasa wa kina Mwanakijiji, Kitila Mkumbo, Ansebert Ngurumo, Mpayukaji, Kibanda, Happiness Katabazi na wengineo kuandika kwa kina haya yanayoanikwa humu kama wachambuzi huru baada ya kupima pande zote mbili.

Pengine wakina Mbowe, Dr Slaa, Zitto, Tundu Lissu, Mnyika, Baregu wanaacha kuandika makala kwa kuwa wakiandika wao wataonekana tu wanajitetea baada ya Kamati Kuu kumsimamisha Chacha Wangwe. Ni wakati wa watu huru kabisa kuandika kwa kina kuchambua hali hii.

Ama sivyo chama mbadala cha Tanzania. CHADEMA kilichomstari wa mbele kwenye vita dhidi ya ufisadi na kutetetea rasilimali za taifa kitavikwa sifa ya ukabila na ubadhirifu. Hali ikifika hapo, nchi itakuwa mashakani.

Asha

Asha
 
Kasheshe pamoja na madhaifu yote ya CCM lakini wao wanapoandika ripoti ya jambo ndugu yangu wanafanya kisomi. Hata kama hatupendi wanachokisema lakini wanajitahidi kwa kiwango kikubwa angalau kujenga ripoti yao kisomi. Sasa wewe unasema yanayosemwa yapo! sasa kama yapo kwanini kuyachunguza?

Je yawezekana walipokuwa wanafanya uchunguzi wao tayari walikuwa wanatafuta kuthibitisha kitu ambacho wao wenyewe wanakijua? Imesemwa hapo juu kuwa uchunguzi ulianzishwa baada ya Mziray kutoa hoja ya kuanzishwa uchunguzi wa ukabila (yaani tayari alishakuwa na mawazo hayo) halafu huyo huyo mnampa uenyekiti wa kutafuta kama kuna ukabila, sasa amekuja na kuonesha ukabila inashangaza!?

Tunaweza si wote wasomi kama wengine, lakini hata kwa elimu yangu ya vidudu siwezi kukumbatia ripoti ya namna hiyo. Na hapa simlaumu Mziray na timu yake nalaumu uongozi wa Chadema kwa kuunda kamati mbovu kama hii isiyo na uwezo wa kufanya uchunguzi huru. Kama kuna sababu ya mtu yeyote kujiuzulu ni hii ya kushindwa kuendesha uchunguzi huru.

Ndio maana hata EPA walioweza kutuonesha ukweli na umetulazimu kuamini walikuwa ni Deloitte and Touche na baadaye Ernst and Young! Binafsi ningeheshimu sana findings of a credible, unbiased, and neutral team of investigations. This is a "sham" investigation. It is a pure as that. Unaweza vipi kwenda kuchunguza kitu ambacho unajua tayari kipo? Have you ever heard of something called "self-fulfliling prophecy"? My friend Pundit is a master of explaining that.

Mwanakijiji, kweli kabisa.

Lakini tujiulize, ni kwa nini Katibu wa Kamati ambaye ndio akapeswa kuwajibika kwa taarifa kuwa mbovu aliikataa taarifa? Huyu inabidi umuhoji

Lakini wakalaumiwa zaidi hapo ni Wakili Mbogoro kwa kutokushiriki kabisa. Huyu naye umuhoji.

Ila naambiwa Kamati Kuu ilitaka iirudishe taarifa bila kuijadili kwa kamati ikafanye kazi tena kutokana na kuleta kazi mbovu, na wengine walitaka kamati ivunjwe iundwe nyingine. Lakini wengi waliona kwamba kama ripoti ya kamati ikiachwa bila kujalidiliwa wakati ilishaanza kusambazwa mitaani basi itaonekana kwamba Kamati Kuu na wakina Mbowe wameigopa ripoti. Basi ndio maana wakakubaliana kuwa pamoja na kuwa ripoti hiyo haikufuata utaratibu kama ambavyo Paparazi Muwazi ameeleza basi ijadiliwe tu ili kama ina hoja zizingatie lakini kama haina hoja ikataliwe. Ikabainika kwamba ripoti ilijaa uzandiki. Hayo yote uyasemayo inaelekea yalijadiliwa.

Asha
 
Yani huu ni uwongo aisee. Kamati imethibitisha kitu ambacho hakipo!

1. CHADEMA haina wakurugenzi wanne wachagga. Kusema kwamba kuna wakurugenzi wanne wachagga ni uongo. Ndio maana Kamati Kuu ikaikataa taarifa kwa kuwa kamati kuu ndio iliyoteua wakurugenzi inajua hakuna wakurugenzi wanne wachagga.

2. Kusema kwamba kuna mtu anaitwa Regina Mrema makao makuu ya CHADEMA na ni mchagga ni uwongo wa mchana. Nimeshaeleza wazi kwamba kuna dada mlemavu anaitwa Regia Mtema, ambaye hata namba yake alinipatia na ni mtu wa asili ya Morogoro. Hata hata mzazi mmoja mchagga au mtu wa kilimanjaro.

Swali la kujiuliza, ni kwa nini Kamati ya Mziray, ama tuseme Mziray mwenyewe kwa kuwa hata katibu wa kamati alipiga kura ya kuikataa ripoti. Ni kwanini akaandika ripoti ya uwongo, na ni kwanini ripoti hiyo ikaandikwa na gazeti la Mtanzania kabla hata ya kuwasilishwa kwa kamati kuu Dodoma?

Ni kwanini ripoti hiyo ambayo inajulikana kabisa ni ya uwongo inasambazwa kwa nguvu zote hizi? Kupitia makala za magazeti nk

Je, huu sio mkakati mahususi wa kuichafua CHADEMA na viongozi wake katika kipindi hiki cha vita dhidi ya ufisadi ili watanzania wapoteze imani nao?

Je, hii haifanani na ule waraka kuhusu Mbowe, waraka kuhusu Zitto, na Waraka kuhusu Dr Slaa ambayo ilisambazwa kwa kasi mwaka jana mara baada ya CHADEMA kuanza kuibua kwa nguvu ufisadi lakini ikaja kubainika kuwa tuhuma na shutuma zote zilikuwa za uongo?

Kwa kweli naelekea kukubaliana na Paparazi Muwazi, hapa kuna jambo.

Kwa kweli nimeamini chama changu ni safi ukilinganisha na vyama vingine, kama pamoja na mkakati wote hizo ndio hoja zinazotolewa kuichafua CHADEMA na viongozi wake basi hii ni taasisi ni safi sana. Imagine kama CCM ndio ingepandikiziwa watu wa kuanika kila kilichomo hali ingekuwaje. Au taasisi nyingine.

Hii ina nipa nguvu zaidi ya kuipenda CHADEMA kwa kweli, chama cha demokrasia na maendeleo.

Hofu yangu ni kama huu ufafanuzi unaotolewa humu kuvunja vunja haya majungu hautolewi kwenye vyombo vya habari wakati ambapo ripoti hii gazeti la Rai na Majira wameichapa neno kwa neno.

Wakati umefika sasa wa kina Mwanakijiji, Kitila Mkumbo, Ansebert Ngurumo, Mpayukaji, Kibanda, Happiness Katabazi na wengineo kuandika kwa kina haya yanayoanikwa humu kama wachambuzi huru baada ya kupima pande zote mbili.
Pengine wakina Mbowe, Dr Slaa, Zitto, Tundu Lissu, Mnyika, Baregu wanaacha kuandika makala kwa kuwa wakiandika wao wataonekana tu wanajitetea baada ya Kamati Kuu kumsimamisha Chacha Wangwe. Ni wakati wa watu huru kabisa kuandika kwa kina kuchambua hali hii.

Ama sivyo chama mbadala cha Tanzania. CHADEMA kilichomstari wa mbele kwenye vita dhidi ya ufisadi na kutetetea rasilimali za taifa kitavikwa sifa ya ukabila na ubadhirifu. Hali ikifika hapo, nchi itakuwa mashakani.

Asha

Asha

How far are you sure kwamba hawa ni wachambuzi huru?
 
Dada Asha,

Tunashukuru sana kwa maelezo yako!!! Mwenye akili timamu anaelewa whatsup!!!

Maoni yangu bado ni yale yale jamii yetu imemomonyoka sana tunahitaji tujirekebishe.

CHADEMA ina goodwill kubwa kutoka kwa wananchi kutokana na juhudi binafsi za kina Zitto na Dr. Salaa, ni muhimu hizi juhudi zikisaidie Chama!

Kila kilichoelezwa kinawapa majibu waTanzania kwa nini CHADEMA haisongi mbele...

Wewe jamaa umesahau kabisa kuwa Dr Slaa ni Katibu Mkuu wa CHADEMA na Zitto Kabwe ni naibu wake na wote ni wabunge wa chama hicho. Nyuma yao ni wakurugenzi wa chama hicho ambao ndio wanapika hoja mbalimbali na kuandaa matukio ya kisiasa unayoyafagilia. Tatizo lenu ni kuwa mnafikiria kiCCM sana maana wao ndio waliosema Mafisadi wakuu serikalini, vigogo wa juu wa chama chao ufisadi ni wao tu, hauna uhusiano wowote na chama. Wakati ambapo fedha zenyewe zimeenda zingine kwenye kampeni zao. Mafaniko ya Dr Slaa, Zitto nk ni kutokana na kuwa na taasisi nzuri ya CHADEMA. Sasa kinachofanywa sasa na Mafisadi ni kuibomoa CHADEMA kama taasisi ili Dr Slaa na Zitto na wengine wabaki kama individuals waweze kuwamaliza tu kirahisi!. Mnachokifanya cha kuita mafanikio wa Dr Slaa na Zitto ni yake binafsi ni kutaka kuivua CHADEMA mafanikio ili isionekane mbadala wa CCM. Huu ni mkakati wa kutaka Chama Cha Mafisadi kiaendelee kudumu madarakani. Ni mkakati wa kumchafua kwa kila njia Mwenyekiti Mbowe, wakati mchango wake katika kuijenga CHADEMA mwaka 2004 na hasa kupitia kugombea kwake urais mwaka 2005 unajulikana wazi. Huu ni mkakati wa kukikandamiza chama cha CHADEMA kionekane si kitu ila kuna watu wachache ndani yake ambao wanafanya kazi wenyewe. Hizi ni akili za watu wasiojua kuwa chama cha siasa ni wanachama hivyo mafanikio ya CHADEMA ni matokeo ya kina Mbogoro Songea, Mnyika Ubungo, Ngaiza Muleba Kaskazini nk. Kila mmoja kwa nafasi yake.

Hebu tuelezeni, matatizo ya taasisi inayoitwa CHADEMA ni yapi hasa? Ina tatizo la malengo yake? Ina tatizo la Muungo wake? Ina tatizo ya Viongozi wake? Wakina nani,be speficic!

Asha
 
How far are you sure kwamba hawa ni wachambuzi huru?

Wao si viongozi wa CHADEMA wala si wajumbe wa Kamati Kuu iliyomsimamisha Wangwe. Ni watanzania walioko ya uongozi wa chama. Mmoja tu ndiye mwanachama wa CHADEMA, Kitila Mkumbo. Wengine ni waandishi tu.

Asha

Halafu mbona mnanichangia wengi jamani: peasant, kasheshe nk wote against Asha, leo tutakesha hapa!

Lakini mi natoa hoja nyingi nyie hata hamzijibu hoja badala yake mnahamisha mjadala. Sasa hapa nimejibu hoja kwa kina wewe unazua lingine kabisa la uchambuzi huru wa wakina mwanakijiji, au umeshindwa kuzichambua hoja zangu na kuzipinga?
 
Chadema kunani paleeee...........au ni annex ya CCM??sielewi..naona ukabila ukabila.....tuu kwenye nafasi zote zenye ulaji...hivi Tz tuna chama pinzani kwelii ambacho kikipewa uraisi kesho kinaweza kutuongoza.......kwelii nina mashaka..sana na ubinafsi....

Ukabila uko wapi hasa? au uzushi tu na uzandiki!

Asha
 
Back
Top Bottom