Ripoti ya mauaji ya mwandishi Mwangosi

kwa tulio madongo kuinama tunaomba juhudi za kipekee tuweze kupata clip mapema kwenye mtandao
 
Wadau kipindi cha kuelezea kifo cha mwandishi wa channel ten kinatarajiwa kuonyeshwa mlimani tv j3 kuanzia saa 2.30 usiku usikose,naomba kuwasilisha.

Ile ya Ch 10 imeyoyo hatukuiona. Huku Ar hakuna Mlimani TV.
 
Mimi sijawahi kusikia kitu kinaitwa mlimani TV hebu waambie hao jamaa zako wakanunue airtime TBC ili tz yote tuone. Hiyo mlimani TV hata Nyololo sidhani kama inaonekana.
 
Huko mlimani TV anakotokea benson Bana?
Kama amehushwa kwa namna yoyote tutegemee maudhi kupindukia.
 
kwa sisi tuliopo mabondeni city mfanye mchakato na sisi tuweze kupata nyiuzi na kwa nini mtumie tv ambayo iko limitedi kwenye kavareji
 
Ripoti ya uchunguzi wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari mwakilishi wa kituo cha televisheni ya Channel Ten, mkoani Iringa, marehemu Daudi Mwangosi, uliofanywa na timu ya waandishi wa habari watatu kutoka Baraza la Habari (MCT) na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), itawekwa hadharani Oktoba 9, mwaka huu.

Azma hiyo ilitangazwa jana Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga, baada ya timu hiyo kukamilisha uchunguzi wake hivi karibuni.

Mukajanga alitangaza azma hiyo alipotakiwa na NIPASHE kueleza lini ripoti hiyo itatangazwa.

Akijibu swali hilo kwa njia ya maandishi, Mukajanga alisema kwa kifupi: “Jumanne Oktoba 9, 2012 Inshallah.”

Awali, NIPASHE ilizungumza na Katibu Mtendaji wa TEF, Neville Meena, ambaye alisema uchunguzi wa timu hiyo umeshakamilika na kwamba, ripoti yake imekabidhiwa kwa Bodi ya MCT.

Timu ya waandishi hao iliyoundwa Septemba 4, mwaka huu, iliongozwa na Meneja wa Utafiti na Machapisho wa MCT, John Mirenyi, wajumbe wakiwa ni Mhariri wa masuala ya siasa wa gazeti la Mwananchi, Hawra Shamte na Mkufunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Kitivo cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma, Simon Berege.

Timu hiyo ilipewa siku nane na ilianza kazi yake Septemba 6, mwaka huu, kubaini ukweli wa tukio hilo na kuweka kumbukumbu sahihi ya tukio hilo.

Wakati huo huo, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Senso, alikataa kuzungumzia timu ya jeshi hilo iliyoongozwa na Mkuu wake, Inspekta Jenerali (IGP), Said Mwema, umekwisha au nini kinaendelea, akisema hawaruhusiwi kufanya hivyo kwa kuwa liko mahakamani kisheria.

“…Waziri wa Mambo ya Ndani alishalisemea,” alisema Senso.

Mwangosi, ambaye alikuwa pia Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani humo (IPC), aliuawa kwa kupigwa na bomu lililosambaratisha mwili wake wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuwazuia kufungua tawi la chama hicho, katika Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi, mkoani humo, Septemba 3, mwaka huu.

Tayari askari polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), mwenye namba G2573, Pasificus Cleophace Simon (23), amefikishwa mahakamani akituhumiwa kwa mauaji ya Mwangosi.
 
Hizi ni stori tu, zamani zilikuwa zikiandikwa kwenye khanga, lakini sasa hata kwenye ma tshirt na madaladala zinaandikwa kila siku na hakuna kipya kinachotokea.
Hivi ziko wapi ripoti za mabomu ya Mbagala na Gongo la Mboto?
 
Ripoti imekamilika na imekabidhiwa, inakaa ofisini kwa zaidi ya siku tano kabla ya kutangazwa, Pasco tuambie mmeshanunuliwa?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom