Ripoti ya Madaktari kuhusu chanzo cha kifo cha mchezaji wa Mbao FC

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,409
20,759
1.jpeg


Ripoti iliyotolewa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Dk. Thoma Rutta na kusomwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi inaeleza kuwa kusimama kwa moyo ghafla ndio chanzo cha kifo chipukizi wa Mbao FC ya Mwanza, Ismail Khalfan Mrisho.

Taarifa hiyo ilitolewa jana na kamanda huyo alipokuwa akizungumza kuelezea chanzo cha kifo cha mchezaji huyo kilichotokea Jumapili wakati wa mchezo wa Mbao FC dhidi ya Mwadui FC ikiwa ni ligi ya vijana katika uwaja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Daktari ametoa taarifa ya uchunguzi na kusema chanzo ni kusimama kwa moyo ghafla. Marehemu hakuwa na jeraha lolote, alisema Kamanda Ollomi.

Ismail Mrisho alizaliwa Mei 22, 1997 akiwa ni mtoto wa kwanza katika familia yao. Amesoma Shule ya Msingi Nyakabungo kuanzia mwaka 2006 hadi 2012. Mwana 2013 alijiunga na Sekondari ya Mwanza ambapo alihitimu mwaka 2016. Ismail alikuwa amepata ufadhili wa kwenda kusoma Chuo Kikuu cha Louisiana State nchini Marekani kuanzia mwakani.

Ismail lifikwa na mauti muda mfupi baada ya kugongana na mchezaji wa Mwadui, alipojaribu kusimama baada ya hapo alianguka tena ndipo alipokimbizwa hospitali mjini Bukoba lakini akafariki.

Kabla ya kukumbwa na mauti hayo, aliifungia timu yake ya Mbao goli la kuongoza ambapo mchezo ulimalizika kwa Mbao kupata ushindi wa 2-0.
 
Sawa riport hatupingi lakini kamati ya ufundi ya familia yake nayo inatakiwa itoe ripoti-naona kama kuna mkono wa mtu.
 
Ripoti sio exhaustive! kwanini moyo ulisimama kufanyakazi,wangeenda mbali ya hapo.hiyo ripoti waliyotoa ni too general hata layman anaweza kutoa.
 
Sawa riport hatupingi lakini kamati ya ufundi ya familia yake nayo inatakiwa itoe ripoti-naona kama kuna mkono wa mtu.
sasa hio ripoti y kuhusu mkono wa mtu na yenyew itapelekwa ikasomwe na RPC au hio inaenda wapi?
 
Ripoti sio exhaustive! kwanini moyo ulisimama kufanyakazi,wangeenda mbali ya hapo.hiyo ripoti waliyotoa ni too general hata layman anaweza kutoa.
ripoti inataka cause of death tu basi ambayo ndo hio iliotajwa
 
Ripoti sio exhaustive! kwanini moyo ulisimama kufanyakazi,wangeenda mbali ya hapo.hiyo ripoti waliyotoa ni too general hata layman anaweza kutoa.

Yaani nami niliposoma nikawaza hivyo hivyo. Au labda ripoti ya maandishi itakuwa na details lkn hawa waliotoa kwa public wameamua kutoenda mbali zaidi
 
Nianze kwa kutoa pole kwa wafiwa na timu nzima.

Lakini je daktari ameshindwa kwenda mbali zaidi kujua kwa nini moyo ulisimama ghafla?
Unaeza kuta kuna sababu ya msingi ambayo inaweza kuwaepusha wengine mfano kama kuna namna ya dawa za kuongeza nguvu zilitumika etc.
 
Sidhani kama madaktari wamefanya uchunguzi hapo....Hii report nahisi wame-refer hisia/makisio ya saili kadhaa za madaktari waliohojiwa kuhusu "nini hasa chanzo cha kifo"...
"Kusimama ghafla kwa moyo"...Mwe! mulijuaje wakati mutu keshakata roho-mna vifaa vya ku-rewind maisha ya mutu??
 
Hamna uhusiano was style yake ya ushangiliaji na kifo chake?
Nauliza ty
 
kilichomuua ni ile style ya ushangiliaji ili disturb mapafu akakosa hewa ikapelekea moyo kufeli madaktari gani hewa hawa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom