Ripoti ya Kifo cha Mwangosi

.
Bongo mtaji ni laptop na modem tu na wewe unaweza kuwa Bloger na mwandishi wa kujitegemea na ukashinda nyumbani kwa copy & paste tu.


ndicho walichofanya hawa waandishi wetu!!! kha!
 
Mara nyingi ripoti za kiuchunguzi zinakuwa kama na facts nyingi, nahisi kwa mtazamo wangu, wamejitahidi kueleza facts za tukio zima, all in all RIP Mwangosi!
 
Tumejazana tu hapa: There are currently 373 users browsing this thread. (67 members and 306 guests). lakini hakuna kitu kipya!! Bora wangekaa kimya tu kama na wenyewe ni waoga hivi.
 
CCM ni taifa kubwa hakuna CCM nyingine duniani ndio maana hakuna haja ya kuweka kirefu chake! hata mtoto alozaliwa leo anajua CCM inastand for what !
Kwa hiyo unamaanisha CCM ni scientific name siyo..approved by International Nomenclature Board..okay we endelea kupalilia maovu tu..
 
kuna hiki kipande tena....hapa chini kwenye red..ndani ya report sioni hao watoto wakitoa huo ushahidi muhimu!!

''Mashahidi walioshuhudia katika kijiji cha Nyololo, wakiwemo watoto
walikuwa vyanzo muhimu''

Tanzania inawasanii wengi sana. ndio maana uchumi bado haukui..
 
msilaumu sana, huo uchunguzi haukuwa wa KIPOLISI AU KIMAHAKAMA, It just like exploratory report or explanatory report.
Wamejitahidi sana japokuwa kwenye conclution na recomendation wamechemsha sana.
 
Tumejazana tu hapa: There are currently 373 users browsing this thread. (67 members and 306 guests). lakini hakuna kitu kipya!! Bora wangekaa kimya tu kama na wenyewe ni waoga hivi.

Mauaji yoyote yenye mkono wa ikulu, majibu ya uchunguzi wake yanakuwaga funika kombe tuu
 
"However, investigations by the MCT team could not establish if the killing of Mwangosi was pre-meditated". This statement nullify all of the stories in the Report. Na hii ndio tunasema ni matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi wa Tanzania


Naona ni makosa kwa ripoti kutoa conclusion kwamba "the killing of Mwangosi wa not pre-meditated" . Hii ni kwa kuzingatia yafuatayo;

- kwamba tayari kuna polisi alishamwambia Mwangosi kabla ya tukio kwamba kwa nini akaandike habari za Chadema zitakazoletea kifo chake
- kwamba tayari polisi walishaonyesha "collective enmity" dhidi ya waandishi wa habari, kuonyesha kulikuwa na namna ya mawasiliano na makubaliano baina yao kwamba waandishi wa habari wa Iringa washughulikiwe
- Kwamba jitihada za mkuu wa polisi wa Mafinga za kumuokoa Mwangosi hazikusidia kuonyesha polisi walikuwa wamedhamiria kumdhuru hata kumuua Mwangosi (intent to harm to the highest degree, possibly kill)
- Kwamba hakuna namna yeyote inayoonyesha kwamba waandishi wa habari walifanya jambo lililostahili polisi kutumia nguvu dhidi yao, kwani Mwangosi hakuwa akipigwa kwa kuwa labda alikuwa ana-resist arrest au katika kumshambulia polisi na hivyo kulazimisha polisi wajitetetee kwa kutumia nguvu.

Kwa ujumla basi, kuna kila aina ya circumstantial evidence kulikuwa na pre-meditated agression dhidi ya waandishi kwa ujumla, hata kama si specifically dhidi ya Mwangosi. Kama kulikuwa na pre-meditated agression dhidi ya waandishi, na Mwangosi alijulikana na polisi hao kwamba ni mwandishi, basi kulikuwa na pre-meditation ya agression dhidi ya Mwangosi.

Hivyo hii inapaswa kuwa kesi ya mauaji (first degree murder) na sio manslaughter.
 
Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu, leo nimekosa cha kusema.

Namuomba Mungu amlipe kila mtu kwa kadiri ya matendo yake, hii itokee hapa hapa duniani kabla hawajasahau walichowafanyia binadamu wenzao.
 
binafsi sijaona kama wamefanya uchunguzi, naona yale yale yaliyokuwa yanaripotiwa na vyombo vya habari ndio yaliyo katika ripoti hii. Muwe serious na neno uchunguzi jamani
 
Ni watu wangapi waliohojiwa? mfumo wa maswali ulikuaje? Je sample iliyotumika kuhoji ilikuaje? Je waliohoji walikua influenced na nini? je hawawezi kuwa biased? muda gani ulitumika kumhoji kila sample? umri wao na kazi zao? mahali pao pa kuishi na eneo la tukio! Source ya information kama TV inaweza ku-influence matokeo ya report yako kwa kiasi gani?
 
Hakika Polisi ndio walio muua Mwangosi
Poti sijakuelewa bado, ina maana uko hapa kusubiri tume ndio zikwambie ni nani alimuuwa Mwangosi? ina maana tangu siku ya kwanza hujui Mwangosi ameuliwa na nani? umenisikitisha sana halafu wewe una access na Internet vipi wale ndugu zako kijijini?

FFU.jpg


4.jpg
 
"Baada ya kuvunjwa kwa ghasia,Mwangosi alikimbilia walipo polisi na kitu kama bomu kikarushwa kundi la watu wanaokimbia na kumlipua Mwangosi"- Gazeti la Habari Leo

"Kilichosababishakifo ni kitu kilichorushwa na kundi la watu.Polisi wanachunguza"-
Gazeti la Mwananchi

"Hii ni amri na Polisi hairuhusiwi maswali zaidi kuhusu suala hili" RPC Kamuhanda

Hizi nukuu katika ripoti hii zimenikera sana sana. Magazeti ya ya Habari Leo na Mwananchi yamemsaliti mwandishi Mwangosi. Inasikitisha sana yalikuwa na maripota (waandishi) kwenye tukio hilo lakini yanatoka na nukuu zilizojaa utumbo kama huo as if ukweli haujulikani.

Kwa maneno mengine nukuu ya Kamuhanda inathibitisha aina ya Jeshi la Polisi tulilo nalo. Tuna kazi na safari ndefu sana kama mentality za polisi wetu ndiyo hizi za akina Kamuhanda.

Ripoti hii imeniuma sana, sina mengi ya kueleza. Real very sad. R.I.P Mwangosi
 
Ripoti imeweka bayana masuala mengi ya msingi.
Ni kazi waliyoifanya kufikia upeo waliofikia hivyo naamini itasaidia kwa sehemu kubwa kuujua ukweli na hata kuchukua hatua zaidi.

Uchunguzi umefanywa vizuri lakini hitimisho limechakachuliwa. KUtokana na ripoti yao ETI UCHUNGUZI UMEBAINISHA KUWA CHANZO CHA MAUAJI NI UHASAMA ULIOKUWEPO KATI YA POLISI NA WAANDISHI WA HABARI. Hili haliniingii akilini hata kidogo. LENGO NI KUPOTOSHA UKWELI KUWA POLISI WANATUMIWA KISIASA NA SI VINGINEVYO. Mtu makini atatambua kabisa kuwa taarifa za polisi zilizotolewa na Kamuhanda (pia msemaji wa polisi Advera Senso) ziliitaja CHADEMA kuwa ndicho kinahusika. Alidiriki kueleza vyombo vya habari kuwa Mwangosi aliuawa na kitu kizito kilichotoka upande wa wafuasi wa CHADEMA.

Uchunguzi wa kamati umeliona hili lakini haikulipa uzito kwa sababu zipi? Kauli za Tendwa zilzihirisha kuwa tayari kulikuwa na mkakati wa kusitisha mikutano ya CHADEMA kwa vitisho vya kukufuta. Kauli za Stephen Wasira kuwa CHADEMA itatoweka ndani ya mwaka mmoja pia ni ushahidi.

Mauaji ya Mwangosi si ya kwanza kutokea. Kwanini kamati haikujiuliza yaliyotokea Morogoro, Mbeya, Arusha na kwingineko? Ninaamini kwa nguvu zote kuwa wanakamati wametumiwa kunutralize uchunguzi wao kuwa walengwa walikuwa ni waandishi wa habari ili kuilinda CCM isionekane kuwa imehusika katika mbinu hizi chafu za kudhoofisha vyama vya upinzani. Ikumbukwe kuwa taarifa za polisi ktk mauaji ya Moro, Arusha na kwingineko pia ni zile zile za kutuhumu CHADEMA kuhusika na mauaji yote eti yamesababishwa na kurushwa kwa kitu kizito ambacho wanakifanyia uchunguzi (Sidanganyiki).

SIKUBALIANI KUWA MAUAJI YALITOKANA NA UHASAMA KATI YA POLISI NA WAAANDISHI WA HABARI, YALITOKANA NA HILA ZA CCM KATIKA KUHUJUMU HARAKATI ZA CHADEMA KAMA MAKADA WAKE (WASIRA, TENDWA) WALIVYOTHIBITISHA.
 
Nimeisoma kwa makini, neno kwa neno, hakika CHADEMA ni wa kulaumiwa, kwa sababu katika report hii sehemu kubwa ni ubishi wa CHADEMA ndio ulomuuwa Mwangosi, sijui CHADEMA mtamlipa nini mjane na watoto hawa YATIMA wa mwangosi, Namlaumu Joh Heche kwa yote haya yalotokea, tubu kwa Mola wako na waombee sana watoto wa MWangosi wapate malezi bora au sivyo sijui kizazi chako wewe kitakuwa vipi! NAWAPA POLE SANA FAIMIA YA MWANGOSI ... na MOLA AWAFARIJI WAKATI WOTE NA AWAKUZE WATOTO WENU KATIKA MAADILI MEMA YENYE UCHA MUNGU.

mkomatembo umekurupuka mkuu!!! soma tena hiyo ripoti
 
Hivi kwel jamani, kweli.....? au ndo usiache mbachao kwa msala upitaooo?
 
Usichanganye hii ni riport ya jukwaa la wahariri. Ile ya serikali bado nadhani, haijatolewa.
Hiyo ya serikali nayo imetolewa leo, lakini mambo mengi hayajawekwa hadharani na waziri Nchimbi, anajitetea kuwa wakianika yote itaingilia mwenendo wa kesi ya yule askari aliyeshtakiwa kwa mauaji
 
Swala hili liko mahakamani.Nina wasiwasi kuwa ripoti iliyotolewa itaathiri usikilizaji wa shauri hili kwa hasa katika swala zima la ushaidi na mashaidi, hasa kwa vile waliohojiwa na tume ya marehemu Mwagosi pengine siyo mashaidi katika kesi hiyo, na ripoti hii imetolewa wakati kesi haijaanza kusikilizwa.Tafadhali naomba wanasheria watupe ufafanuzi zaidi katika hili
 
Back
Top Bottom