Ripoti ya Kifo cha Mwangosi

Kwani hawakuipitia vizuri hii ripoti (ya kiswahili) kabla ya kuiweka? Ripoti inasomwa na watu wengi, hivyo ilitakiwa walioiandaa waihariri vizuri kabla ya kuiachia.

Nilifikiri ni ripoti ya Nchimbi tuone nayo inasemaje.

RIP Mwangosi, kuna watu wanajiona wao ni miungu, wanahaki ya kutwaa maisha ya wenzao, na wanasahau kuwa pua zao zimeangalia chini na wanaishi kwa kubadilisha damu!
 
hii ndio ile kamati ya nchimbi au nimeuliza dumb question?nimeisoma yote,kamuhanda should be hanged
 
Asante sana mkuu.


Nimeridhika na maelezo ndani ya riport.

Kilichotokea ndicho kilichoripotiwa.

Suala la maamuzi ni kwa waziri kuturidhisha atachukuwa hatuagani, tusubili wale polisi sita ambao bado wanadunda na kamuhanda atafanywa nini.
 
Ni ripoti nyepesi mno.
Haikidhi kwa vigezo vyovyote uzito wa tukio na kilichomo katika taarifa, sana sana inaonyesha kiwango cha uandishi wa kuripoti badala ya kuhoji na kupata undani wa tukio. Baadhi ya mapungufu nilioyaona katika taarifa hii kwa muda mfupi wa kuipitia ni haya yafuatayo:-

1. Ripoti badala ya kujielekeza katika kiini cha tatizo inatoa taarifa na maelezo yale yale ambayo tayari yanafahamika. Hakuna uchunguzi wa kina kubaini chanzo, tukio lilivyokuwa, vielezo vya ushahidi?
2.Hadidu za rejea ni nyepesi mno na hazijibu maswai ya msingi:- Mfano, ilikuwaje akauwawa? Nani alitoa amri? Kwa nini?Mchakato mzima ulikuwaje?
3. Wahusika wakuu ambao wanahusishwa na mauaji haya, say Polisi, wamehojiwa?
4. Hojaji ziko wapi? Kina nani walihojiwa? Lini na wapi?
5. Mapendekezo ni ya jumla mno, hayalengi wahusika mbalimbali wa tukio hilo: Wanasiasa? Polisi? Waandishi wa habari? Wananchi?
6. Hatua zipi za kuchukua katika vipindi mbalimbali: Nini kifanyike sasa na kwa haraka? Baada ya muda mfupi? Mapendekezo gani yanatolewa kuzuia hali hii katika kipindi cha muda mrefu? Sera za utendaji? Usimamizi na
uendeshaji wa vyombo husika?
7. Wajumbe wa timu yenu wanakidhi mahitaji ya kazi mliyofanya? wana sifa na vigezo?

Kwa style hii, hakika mtaendelea kuburuzwa.

Labda kama mnayo nyingine, na hii ni kwa matumizi yenu ya ndani. Ni duni interms of quality, content, coverage, methodology, review, findings and recommendations and many others. Dont share it, improve it first.
 
"However, investigations by the MCT team could not establish if the killing of Mwangosi was pre-meditated". This statement nullify all of the stories in the Report. Na hii ndio tunasema ni matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi wa Tanzania
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Tanzania bwana! sasa kwanini report ni ya kiingereza?

Kuna attachments mbili; moja ya kiswahili na nyingine kiingereza.

Report imekaa vibaya kwa upande wa polisi na hasa RPC Kamuhunda.
 
nimepitia kwa haraka nimegundua in upendeleo kwa vyama vingine sijui kama wameliona hilo mfana kirefu cha chadema kimeelezewa vizuri ila cha ccm hamna ingawa neno ccm limetumiwa mara nyingi sana ndani ya ripoti yenyewe ina maana hili hawakuliona au ni makusudi mazima.
 
Wakuu ripoti ya Mwangosi (MCT) imeshatolewa.
Fungua atachmenti hapo chini.

Kamanda Ahasante sana.na nikwambie tu kwamba kwa ripoti hii Kamhanda hawezi kubaki hata chembe na nadhani hata wakati huu ambapo natuma hii Comment watakuwa wameshamuarest,bealive me n00b!!!!
 
nimepitia kwa haraka nimegundua in upendeleo kwa vyama vingine sijui kama wameliona hilo mfana kirefu cha chadema kimeelezewa vizuri ila cha ccm hamna ingawa neno ccm limetumiwa mara nyingi sana ndani ya ripoti yenyewe ina maana hili hawakuliona au ni makusudi mazima.

hahahhahaaaa,,,,wangeandika kirefu cha CCM.....??????
 
Nadhani. Ripoti ni ya kuelezea matukio yalotokea na it lacks analysis na tangible conclusion and way forward
Hii ni jinai, unataka wacoclude nini. Hapa ni wahusika kuakamatwa, lupango, mpaka kesi iishe. Na hizi kesi huwa hazina dhamana.
 
Nimeisoma kwa makini, neno kwa neno, hakika CHADEMA ni wa kulaumiwa, kwa sababu katika report hii sehemu kubwa ni ubishi wa CHADEMA ndio ulomuuwa Mwangosi, sijui CHADEMA mtamlipa nini mjane na watoto hawa YATIMA wa mwangosi, Namlaumu Joh Heche kwa yote haya yalotokea, tubu kwa Mola wako na waombee sana watoto wa MWangosi wapate malezi bora au sivyo sijui kizazi chako wewe kitakuwa vipi! NAWAPA POLE SANA FAIMIA YA MWANGOSI ... na MOLA AWAFARIJI WAKATI WOTE NA AWAKUZE WATOTO WENU KATIKA MAADILI MEMA YENYE UCHA MUNGU.
 
Naiona kuwa ni ripoti ambayo haikidhi, uzito wa suala lenyewe na kilichomo. Inaendeleza uandishi wa kuripoti badala ya kuhoji na kudadisi.

Kwa mapitio mafupi niliyofanya, haina jipya zaidi ya kurudia na kueleza kinachofahamika. Kimsingi inakosa masuala muhimu yafuatayo:-

1. Hadidu za rejea ni nyepesi na hazijielekezi katika kupata habari kuhusu chanzo cha tatizo, ilivyokuwa, nani walihusika na vielelezo kamilifu.
2. Hojaji na waliohojiwa ni kina nani? Wapi na lini?
3. Washukiwa wakuu wa tukio hili, say Polisi, wamehojiwa? Kina nani? wapi na lini?
4. Wadau wengine wakubwa, wanasiasa, wananchi, na wengineo taarifa hii imewadadisi kwa kiasi gani?
5. Mapendekezo: Yangewekwa kimpangilio badala ya kutolewa kwa jumla tu. Nini kifanyike sasa na kwa haraka? Nini kifanyike katika muda wa kati na mrefu? Mabadiliko ya kisera, kimuundo na kiuendeshaji ili kuzuia matukio ya jinsi hii katika siku zijazo?
6. Wadau husika wanaelezwa nini? Polisi? Wanasiasa? Wnanachi?
7. Nani alitoa amri na kwa nini?
8. Taarifa zipi hamkuzipata na kwa nini?
9. Mipaka yenu ya kiuchunguzi illishiwa wapi? Imekidhi malengo na matakwa ya mlichokusudia?
10. Wajumbe wa timu yenu, wana sifa na vigezo kwa kazi mliyofanya?

Na mengi mengine.

Iwapo taarifa hii ni ya ndani sawa, improve it first. Ni nyepesi, haikidhi na haina value for Money.
 
Back
Top Bottom