Ripoti ya Jopo la Wataalam wa UN juu silaha Haramu DRC

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Well... Tunashukuru vyanzo vyetu vya "kuaminika" once again.. we set the standard!

On Technicality?

Habari Leo

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kuacha siasa kwenye masuala yanayohusu maslahi ya Taifa.

Membe amesisitiza kuwa tuhuma kwamba Tanzania imeshiriki kusambaza silaha haramu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ni za uongo.

Kiongozi huyo ametoa changamoto kwa yeyote anafahamu kwamba Serikali ya Tanzania imeshiriki katika biashara hiyo kuweka hadharani ushahidi wake.

“Chadema iache kuleta siasa kwenye maslahi ya taifa. Serikali ya Tanzania haijahusika katika biashara haramu ya silaha Kongo, na madai hayo ni upuuzi, na Chadema ije na uthibitisho badala ya kung’ang’ania ripoti ya Umoja wa Mataifa ambayo tumesema ni ya uongo, na inataka kutudhalilisha,” amesema Membe.

Membe ametoa kauli hiyo mjini Havana baada ya kuulizwa na gazeti hili msimamo wake siku moja baada ya Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Chadema, John Mnyika kuwaeleza waandishi wa habari mjini Dar es Salaam kuwa Membe anapaswa kuomba radhi kwa kile ilichodai kuudanganya umma kuhusu taarifa hiyo ya UN.

Taarifa ya Wataalamu na wachunguzi wa UN imeituhumu Tanzania na baadhi ya nchi, ikidai zinahusika katika usambazaji wa silaha haramu kwa kikundi cha waasi cha FDLR cha Kongo kinachopigana dhidi ya raia wa Rwanda, mashariki mwa nchi hiyo ya Maziwa Makuu.

Membe akionekana dhahiri kukasirishwa na kauli ya Chadema, alisema hakuna mahali popote katika ripoti hiyo ya UN kunakothibitisha ushiriki wa Serikali ya Tanzania katika tuhuma hizo, lakini hilo pia haliondoi ukweli kuwa nchi inapaswa kuombwa radhi kwa kuchafuliwa jina lake katika medani ya kimataifa.

Amesema, hoja kwamba kumeonekana mawasiliano ya simu kati ya Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Francis Mndolwa na baadhi ya viongozi waasi, haina uzito kwa sababu haina uthibitisho kuwa mawasiliano yao yalihusu biashara ya kuuziana silaha haramu.

“Hoja kwamba namba ya simu ya Balozi Mndolwa imeonekana ikifanya mawasiliano na waasi haina uzito wowote, kwani hakuna uthibitisho kuwa mawasiliano yao yalikuwa ni kwa ajili ya kuuziana silaha,” amesema Membe anayefuatana na Rais Jakaya Kikwete ziarani hapa Cuba na kuongeza:

“Watoe uthibitisho wa kuuziana silaha, kwani hata mimi nimekuwa na mawasiliano na watu hao wa upinzani au wanaoitwa waasi, lakini si mawasiliano ya kuuziana silaha, yanaweza kuwa mawasiliano ya kupatanisha migogoro yao. Sasa tuje na uthibitisho, siyo tuhuma zisizo na ukweli.”

Alisema waliotoa tuhuma hizo wanapaswa kueleza jinsi Balozi Mndolwa na Watanzania wengine ambao simu zao zimeonekana kwenye ripoti hiyo ya UN, walivyoshiriki katika biashara hiyo haramu, na si kutoa tuhuma ambazo hazina uthibitisho zenye nia ya kuchafua jina zuri la Tanzania kimataifa.

“Chadema wasidandie ripoti, watoe uthibitisho wa Tanzania kushiriki katika biashara hiyo. Kuonekana kwa simu za Watanzania siyo uthibitisho, tunataka uthibitisho wa ushiriki wa Serikali ya Tanzania katika tuhuma hizo. Serikali inatoa changamoto kwa ye yote mwenye ushahidi wa ushiriki wake katika biashara hiyo autoe, vinginevyo hizo ni tuhuma zisizo na ukweli, ni upuuzi na tunadai kuombwa radhi,” amesema Membe.

Mnyika katika mkutano wake na wanahabari juzi alidai kuwa Membe alikurupuka katika kujibu tuhuma hizo alizodai chama hicho inaamini ni za kweli, kwa kuwa mifano ya vitendo hivyo na baadhi ya majina ya watu wakiwemo viongozi wa nchi yamo katika taarifa kuonesha kuwa walihusika.

Maoni yangu:

a. Kuna kitu hakiko sahihi katika mtiririko wa hoja za Bw. Membe. Kitu ambacho ni matumizi ya lugha ya kiufundi:

b. Sikutaka kurudia somo hili tena lakini CCTI inaandika barua ya wazi kwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na kujaribu kujibu baadhi ya changamoto zake. Inshallah, tutaweka barua hiyo muda si mrefu ujao.

c. Membe na serikali ya Tanzania wasichukulie jambo hili kiutani utani au kimzahamzaha. Kuna ushahidi mkubwa sana wa ushiriki wa maafisa wa Tanzania (aidha kama watu binafsi au vinginevyo) katika usafirishaji wa silaha katika eneo hili. Jambo hili siyo geni kwa wachunguzi wengi. Nendeni taratibu kina Membe... very careful.. mtamfungua sanduku la Pandora bure..
 
Attachments

  • Group_of_Experts_Report_DRC_november_2009.pdf
    524.5 KB · Views: 803
MMM, every time i try to let politiki za tanzania zinipite unakuja na vibomu vingine!!! anyway ngoja tuone halafu turejee ile ya meremeta halafu tumshukuru Mungu, maana wakuu wameshakataa katukatu

Naomba isiwe ninavyohisi ila tunaambiwa nyumba yako ikihifadhi vya wizi basi na wewe unahusika na wizi

Scary!!
 
Heshima kwako Mwanakijiji

Asante kwa nondo za uhakika,mungu akubariki
 
hii si ina connection na Victor Bout

jamaa last time nasikia alikamatwa Thailand and not sure yuko dunia gani

if anything he was a small fish kwenye hii game ya weapon dealings kama akina Adnan Kashogi na wale jamaa wanaoshinda kwenye zile Cafe za Haifa na Tel Aviv...wakipanga kuwaizia wa Iran all sorts of kits
 
ni taarifa kubwa, waacha niendelee kuisoma, lakini Membe na wenzake najua wataumbuka,maana hakujipa muda kutafiti, taarifa imefika, nasikia hata Cabinet haijakutana , mara kafyatuka na kuitusi UN....HII NI KITU AMBAYO LAZIMA IWE HANDLED KWA TAADHARI ILI KULINDA HADHI NA HESHIMA YA TANZANIA KAMA TAIFA.
acha niendelee kuisoma.
 
Mchezo huu ambao ni mauti kwa wenzetu wa DRC umewatajirisha wanasiasa wetu wengi tu. Membe akiwa ni mtu UwT wa miaka mingi hawezi kujifanya haujui. Labda angetoa kauli kama za Makamba kwamba mafisadi ni watu sio CCM. Na yeye angesema mchezo huu wanaufanya baadhi ya maofisa wetu waandamizi serikalini na sio serikali yenyewe.
 
mchezo huu ambao ni mauti kwa wenzetu wa drc umewatajirisha wanasiasa wetu wengi tu. Membe akiwa ni mtu uwt wa miaka mingi hawezi kujifanya haujui. Labda angetoa kauli kama za makamba kwamba mafisadi ni watu sio ccm. Na yeye angesema mchezo huu wanaufanya baadhi ya maofisa wetu waandamizi serikalini na sio serikali yenyewe.
so sad!!
 
tatizo ni pale hata masuala ya inteligensia yanapoanza kushughulikiwa kisiasa!!!
 
Mzee Mwanakijiji,

The Group concluded in its previous mandate that the principle source of arms and ammunition for the FDLR was the FARDC. However, in the course of the current mandate, the Group established that the FDLR received significant deliveries of weapons and ammunition in 2009 from outside the DRC, in particular equipment that has been smuggled into South Kivu across Lake Tanganyika from Tanzania. The Group has corroborated such information through several interviews with FDLR ex-combatants who personally witnessed such arms transfers, and from the Group's analysis of phone records of an individual who is in communication with both the FDLR and Tanzanian officials who the Group has confirmed as being part of an arms trafficking
network (see paragraphs 72 to 81).
Mbona paraghraphs hizo 72 hadi 81 sizioni mkuu wangu..
 
Watanzania nawaomba msi entatain atoms za namna hii kutoka UN.Wawachonganishe wao kwa masilahi yao ,watengeneze silaha wao na wawauzie wao harafu watusingizie sisi.

sisi kama nchi tuna airport na bandari kwa anjili ya biashara na huduma pia, kwa hiyo mzigo iliyo ya destination ktk nchi zingine sisi interest yetu kubwa ni kufanya biashara na si vinginevyo. Leo hii Uganda ikiagiza silaha na kupitia bandari ya dar es salaam harafu baadae hao Uganda wakaenda wakaivamia Kenya kwa silaha zilizopitia Dar na kusema eti TZ imeparticipate nafikiri ni argument za kipuuzi.

Hao UN watuletee uthibitisho kwamba serikali ya Tanzania ilikuwa ndo inanunua hizo silaha kwa mbadala wa hao waliowasaidia. kusema midege na minofu hio si argument na trafic ya mizigo na kuwa transit ktk nchi moja hadi nyingine hiyo si participation.
 
ni taarifa kubwa, waacha niendelee kuisoma, lakini Membe na wenzake najua wataumbuka,maana hakujipa muda kutafiti, taarifa imefika, nasikia hata Cabinet haijakutana , mara kafyatuka na kuitusi UN....HII NI KITU AMBAYO LAZIMA IWE HANDLED KWA TAADHARI ILI KULINDA HADHI NA HESHIMA YA TANZANIA KAMA TAIFA.
acha niendelee kuisoma.

Uko sahihi kabisa. Hata mimi baadaya kuisoma ripoti hiyo ni kama Waziri wetu kakurukupa. Ripoti hiyo inaonyesha wazi kilichofanyika ni magendo ya silaha ambayo hayakushirikisha serikali kwa aina yoyote. (Hivi majambazi yale ya kenya yaliyoshiriki wizi wa benki Mwanga serikali ya Kenya hakututaka tuiombe radhi?). Ni kitu ambacho serikali ilitakiwa kushirikiana na hiyo tume kuwahoji na kuwachukulia hatua wote waliohusika na taarifa hiyo. Kama ni raia wa nje kuwafukuza nchini. Hicho ndio kilichotakiwa kufanyika na sio kuilaumu instution kubwa namna ile ambayo Tanzania haijawahi kugombana nayo hata siku moja.
 
Watanzania nawaomba msi entatain atoms za namna hii kutoka UN.Wawachonganishe wao kwa masilahi yao ,watengeneze silaha wao na wawauzie wao harafu watusingizie sisi.

sisi kama nchi tuna airport na bandari kwa anjili ya biashara na huduma pia, kwa hiyo mzigo iliyo ya destination ktk nchi zingine sisi interest yetu kubwa ni kufanya biashara na si vinginevyo. Leo hii Uganda ikiagiza silaha na kupitia bandari ya dar es salaam harafu baadae hao Uganda wakaenda wakaivamia Kenya kwa silaha zilizopitia Dar na kusema eti TZ imeparticipate nafikiri ni argument za kipuuzi.

Hao UN watuletee uthibitisho kwamba serikali ya Tanzania ilikuwa ndo inanunua hizo silaha kwa mbadala wa hao waliowasaidia. kusema midege na minofu hio si argument na trafic ya mizigo na kuwa transit ktk nchi moja hadi nyingine hiyo si participation.

Mkamap hebu nisaidie kujua lile Dege lililokamatwa pale Mwanza na silaha halafu amri kutoka kwa wakuu wa nchi likaachiliwa lilikwenda wapi? na nani aliyetoa amri hiyo?
 
Watanzania nawaomba msi entatain atoms za namna hii kutoka UN.Wawachonganishe wao kwa masilahi yao ,watengeneze silaha wao na wawauzie wao harafu watusingizie sisi.

sisi kama nchi tuna airport na bandari kwa anjili ya biashara na huduma pia, kwa hiyo mzigo iliyo ya destination ktk nchi zingine sisi interest yetu kubwa ni kufanya biashara na si vinginevyo. Leo hii Uganda ikiagiza silaha na kupitia bandari ya dar es salaam harafu baadae hao Uganda wakaenda wakaivamia Kenya kwa silaha zilizopitia Dar na kusema eti TZ imeparticipate nafikiri ni argument za kipuuzi.

Hao UN watuletee uthibitisho kwamba serikali ya Tanzania ilikuwa ndo inanunua hizo silaha kwa mbadala wa hao waliowasaidia. kusema midege na minofu hio si argument na trafic ya mizigo na kuwa transit ktk nchi moja hadi nyingine hiyo si participation.

Mkamap tuahe unafiki mkuu,hapa facilitators wa matumizi ya silaha hizo nao hawawezi kuepuka responsibilities.Kama silaha zingekuwa zinapitia Mombasa kuja kwa guerilas say wa TZ ungesema Kenya wanafanya tu biashara na ni marafiki wazuri?Ujiulize pia je uhusiano wa TZ na DRC uko vipi?Je ni marafiki ama a hostile nation?Kwahiyo JK aendelee kumchekea Kabila huku akimwambia poa mshikaji ni biashara?Tanzania pamoja na amani iliyokuwepo,mambo kama haya yanaweza kuijeorpodize amani iliyopo kwasababu kama urafiki wenyewe ndo huo,kwanini na wao wasifanye the same against us?Kumbuka what goes around comes around.
 
Hebu kuweni wazalendo kidogo jamani, kama airport na bandari zetu zinatumika na sisi hatujui au kama watu wanahongwa zipite pia mtalaumu serikali??, YES mtalaumu

Lakini hiyo haina maana kuwa serikali inahusika.
 
Back
Top Bottom