Ripoti ya "ajabu" ya NAPE huko Houston...!

Bahati mbaya..,ndio nasema ni bahati mbaya sana kwa mahali kama JF, sehemu pekee katika social media ambapo watu wengi tunaoamini wanauelewa na ufahamu wa kutathmini na kufikiri kwa upana na umaridadi.,wanapokuwepo watu ambao akili zao na uwezo wao wa kufikiri hauzidi hata ule wa kidole cha "majivuno wa kusadikika"
 
Nyumbani ccm imegawika makundi makundi, magamba yamekwamia kiunoni, wewe unaenda kutatua migogoro Houston! Hayo si matumizi mabaya ya fedha? Au mnatuzuga umetumwa na mzee wa kuhemea ukatembeze bakuli? Angalia huko wanakuita duani! Safari ijayo sijuwi utatuambia unafuata nini make mgogoro alioushindwa jk wewe umeumaliza.
 
Nachelea kusema hao aliokutana nao sio watz ama ni watu wasiona uzalendo kwa nchi yao kwa waliowatz na wanaishi ughaibuni wanafahamu hali halisi ya ndugu, jamaa na marafiki zao wa huku tz sidhani wanaweza kupumbazwa na maneno ya Nape.
 
hivi watu nane si familia hiyo?
picha aliyopiga nape hapo sijui houston ilikuwa na watu nane.
swali?
unampongeza katibu mwenezi wa chama chenye wanachama 5000000 kwa ajili ya kusuluhisha ugomvi wa watu nane?
mgogoro ndani ya chama chake ili uishe unahitaji wenezi wangapi?
tuingie kwenye mahesabu kama katibu mwenezi mwenye uwezo kama ulivyomsifia ameweza kusuluhisha watu nane pamoja na yeye ili kusuluhisha wanachama milioni tano=5000000/8=625000.
mnahitaji makatibu wenezi wenye upeo mkubwa kama nape laki sita na ishirini na tano elfu ili migogoro ndani ya ccm iishe.

Hii imenoga zaidi,yaani kama tunatafuta post
ya kufungia mjadala hii ndiyo mwake! Brouha!ha!ha!
 
Mbona habari yako ni ya kiujumla kama kawaida ya habari zisizo na kichwa? Unasema alikwenda kutatua matatizo ya wana CCM Houston; Mbona hakuna picha kudhihirisha upatanishi? na Ijumaa Houston alikutana na viongozi wa upinzani wa CCM -- Jumamosi alikutana na jumuia ya Watanzania wapi alipata muda huo wa kuutatua mgogoro? Sasa kama umetatuliwa Viongozi ni kina nani sasa?

Upo USA jaribu kutupa in and out and the outcome --- hakuna cha kuficha...

IMG_3380.jpg

IMG_3382.jpg
 
Kwanini wategemee majibu ya NAPE wakati wao wenyewe wanaweza wakatembelea nchini, au kufanya tafiti ndogo tu za hali ya uchumi na kipato kwa Mtanzania?
Huenda kweli wengi walioko huko ni watoto wa zile familia bora...ambapo matatizo wanafanya kuyasikia kama simulizi katika kitabu cha NGANO ZA KALE.

Ndugu yangu nani kakwambia wanaweza kuja nchini, hao wengi wabeba maboksi wasiokuwa hata na makaratasi, hawawezi kurudi nyumbani, wakirudi ndio kimoja. Na kukaa marekani sio kigezo pekee cha kuwa na uelewa mpana, kama huna juhudi za kujielimisha unaweza ukawa marekani na uelewa wako ukawa kama mtu wa kutoka Sigimbi huko Newala. Sishangai kuwa Nape kawateka kiakili hawa jamaa, wengi upeo wao umemalizwa na kubeba maboksi.
 
Haya matatizo ya kutanguliza mbele hisia na kuweka nyuma ubongo sijui yataisha lini, yaani unajitengenezea karipoti kako kutokana na hisia zako halafu unategemea nini, machale kuncheza nkastuka!
 
Mbona habari yako ni ya kiujumla kama kawaida ya habari zisizo na kichwa? Unasema alikwenda kutatua matatizo ya wana CCM Houston; Mbona hakuna picha kudhihirisha upatanishi? na Ijumaa Houston alikutana na viongozi wa upinzani wa CCM -- Jumamosi alikutana na jumuia ya Watanzania wapi alipata muda huo wa kuutatua mgogoro? Sasa kama umetatuliwa Viongozi ni kina nani sasa?

Upo USA jaribu kutupa in and out and the outcome --- hakuna cha kuficha...

IMG_3380.jpg

IMG_3382.jpg
kaka napata shida kidogo katika kuelewa na kupima uwezo wako wa kujadili nje ya hisia zako..,nani kakwambia picha ni kielelezo cha suluhu ya mjadala.,unaulizia muda ama wakati..??? na mwisho je unaamini kuwa ili sehemu yenye mgogoro itulie ni lazima viongozi wabadilishwe..,sio kosa lako ni MWALIMU wako....!
 
Ni ajabu na inashangaza..,

Nape ameonyesha uwezo mkubwa wa kisiasa na uelewa wa siasa za kimataifa na mahusiano ya kidplomasia, pale alipofanikiwa kwa mara moja kumaliza mgogoro ambao ulidumu kwa muda mrefu baina ya watanzania waliopo jimbo la texas jijini houston, mgogoro ambao ulishindwa kumalizika hata pale ambapo Rais alifanya ziara nchini humo hivi karibuni.
Not so fast ndugu yangu. Kujulikana kuwa mgogoro umeisha itachukua muda kidogo... Umeshawahi kuisikia ile methali inasema kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa? kama kweli kulikuwa na mgogoro mkubwa kiasi hicho, si rahisi ukauisha kwa kasi hii unayoisimulia. Subira yavuta heri
 
Ni ajabu na inashangaza..,

Katika ziara ya Nape inayoendelea hivi sasa nchini marekani kumekuwa na matukio mbalimbali ambayo katika zama za sasa na upepo wa kisiasa ulivyo hasa ndani ya CCM ni sawa kuyaita matukio hayo kuwa ni ajabu na yasiyotegemewa hasa kwa mtu kama Nape kulingana na umri wake na hata nafasi yake. Miongoni mwa matukio hayo nitayataja baadhi, ambayo Nape ameonyesha uwezo mkubwa wa kisiasa na uelewa wa siasa za kimataifa na mahusiano ya kidplomasia, pale alipofanikiwa kwa mara moja kumaliza mgogoro ambao ulidumu kwa muda mrefu baina ya watanzania waliopo jimbo la texas jijini houston, mgogoro ambao ulishindwa kumalizika hata pale ambapo Rais alifanya ziara nchini humo hivi karibuni. Uwezo huu wa Nape kumaliza mgogoro mkubwa na tata kwa watanzania hao kwa muda mchache umeonekana ni wa ajabu kwani wengi walishindwa hapo kabla,alinukuliwa mmoja wa watanzania waishio jijini humo anayejulikana kwa jina la bwana Kittoga.

Nape pia alisisitiza kwa watanzania wa houston hasa wanaCCM kuwa lazima chama kisogezwe kwa wanachama kiutendaji na kimaamuzi na kusisitiza kuwa hilo ni agizo la Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM. Hivyo kuwataka wafungue matawi zaidi ili kuwafikia wengi zaidi kwa ukaribu na urahisi zaidi wa kufuatilia na kushughulikia shughuli za chama.

Lakini jambo lingine ambalo pia liliwashangaza wengi ni upeo binafsi wa Nape pale ilipofika wasaa wa maswali ya papo kwa hapo.,ambapo Nape alitumia muda mwingi wa mkutano wake katika hili ambapo watanzania hao wa houston walipata kuuliza juu ya hali halisi ya uchumi na maisha ya watanzania, ndipo Nape alipowaeleza kwa undani juu ya changamoto zinazoikabili serikali ya awamu ya nne na chama kama taasisi inayoisimamia serikali na pia kuelezea mafanikio yaliyopatikana chini ya CCM, kwa namna ya kipekee kabisa ya ufafanuzi na tafsiri sahihi ya matukio yanayoendelea Tanzania.

Na ilipofika wakati wa kuelezea juu ya falsafa ya chama inayotawala vichwa vya wengi nae Nape aliitolea maelezo, kuwa ni dhana iliyopotoswa sana kitafsiri hasa na wapinzani lakini aliwahakikishia kuwa hiyo ni falsafa ya mabadiliko makubwa katika chama yenye kulenga kubadili taswira mbaya ya chama na kukipa chama nguvu mpya kiutendaji na maamuzi na pia umaarufu zaidi na kukubalika hasa kwa vijana.

Alisisitiza kuwa "falsafa ya kujivua gamba na vita vya ufisadi ndani ya Tanzania ni vitu vinavyoenda sambamba,kwani zote vita dhidi ya matumizi mabaya ya rasilimali za nchi"

Aidha alimalizia kwa kuwataka Wana CCM kutumia matawi yao ya Chama kuwaunganisha Watanzania badala a kugeuka vijiwe vya majungu na kubaguana kwa vigezo vyovyote vile, huku akiwataka kuweka Utanzania wao kwanza kuliko itikadi na tofauti zao malimbali.

Nape anaendelea na ziara yake nchini Marekani yenye lengo la kukagua uhai wa chama, ambapo atatembelea Columbus-Ohio, New York na atamalizia Washington Dc, kabla ya kurejea nchini Tanzania wiki ya kwanza ya mwezi Novemba.
Aisee! Naona mtu anaamua kujifagilia mwenyewe hapa! Kuwakutanisha watu wa familia mbili ndio uzoefu wa diplomasia za kimataifa? Hapa la ajabu liko wapi? Kwa siasa hizi za kitapeli na propaganda za kitaahira, Tanzania bado tuna safari ndefu!
 
Hii ripoti ni upuuzi tu na upiga debe usio na maana! Maisha nyumbani ni magumu sana sukari 3000 leo, dolla ndo hiyo inaelekea 2000. ninyi wazee wa Texas mnasumbuliwa na njaa tu hamna lolote! pigeni box acheni upuuzi wenu. Kwanza sina hakika kama hata wewe unayeandika umehwahi kutembela nyumbani hivi karibuni! Njia ina miiba ukitoka hurudi hahahahahahahahahaa
 
Mbona habari yako ni ya kiujumla kama kawaida ya habari zisizo na kichwa? Unasema alikwenda kutatua matatizo ya wana CCM Houston; Mbona hakuna picha kudhihirisha upatanishi? na Ijumaa Houston alikutana na viongozi wa upinzani wa CCM -- Jumamosi alikutana na jumuia ya Watanzania wapi alipata muda huo wa kuutatua mgogoro? Sasa kama umetatuliwa Viongozi ni kina nani sasa?

Upo USA jaribu kutupa in and out and the outcome --- hakuna cha kuficha...

IMG_3380.jpg

IMG_3382.jpg

Naona baadhi ya watu wa Missouri kumbe wako Houston sasa.

Na huyo mmoja hapo katikati, si nilisikia alikuwa na kesi za mambo kama ya Mponjoli au mambo ya unga-unga? Au taarifa mbovu kama kawaida ya bongo?

Anyway, tukirudi kwa Nape wakati yeye anatalii huko wenzake wanakutana hapa na suala la uhai wake kama Mwenezi wa chama litagusiwa bila ajizi. Kuna watu wanakuja na agenda moja ya Nape na Chiligati waondoke. Watamsikiliza Mukama, ila nao watataka Mukama awasikilize. Mukama ana kazi.
 
Unamzungumzia nape yupi? huyu aliyekuwa anaongea matusi ya nguoni pale mwanza? au mwingine ? harafu si busara kumkejeri mwenyekiti unaposema nape kaonesha uwezo mkubwa kumshinda mwenyekiti, binafsi nahisi kizungu zungu kwa sababu huyo nape namfahamu kwa jinsi alivyo na akiri mbovu. sasa unaposifia kwamba hizo akiri ambazo mimi najua ni mbovu kwamba zimekuwa bora kuliko za mwenyekiti wake kwa hiyo kama nape anawezo mkubwa kuliko kikwete basi ikulu hakuna kitu , tunaenda kwa neema ya mungu
 
Inasikitisha!
Kama Watanzania hao waliridhika na majibu ya Nape, huku wakijua waziwazi hali halisi ya Mtanzania wa kawaida, BASI nashawishika kuzua shaka juu ya uzalendo wao, na huenda walifika Tanzania zamani mno!

Sina shaka kwamba hao waliomsikilkiza na kuridhika na majibu yake ni wale wasio na makaratasi, wanaishi huko kwa kuunga unga.

Mtu makini kabisa hawezi kuridhika na taarabu za nape hata siku moja, labda kama walimtangulizia maswali akaandaliwa majibu.
 
Ni ajabu na inashangaza..,

Katika ziara ya Nape inayoendelea hivi sasa nchini marekani kumekuwa na matukio mbalimbali ambayo katika zama za sasa na upepo wa kisiasa ulivyo hasa ndani ya CCM ni sawa kuyaita matukio hayo kuwa ni ajabu na yasiyotegemewa hasa kwa mtu kama Nape kulingana na umri wake na hata nafasi yake. Miongoni mwa matukio hayo nitayataja baadhi, ambayo Nape ameonyesha uwezo mkubwa wa kisiasa na uelewa wa siasa za kimataifa na mahusiano ya kidplomasia, pale alipofanikiwa kwa mara moja kumaliza mgogoro ambao ulidumu kwa muda mrefu baina ya watanzania waliopo jimbo la texas jijini houston, mgogoro ambao ulishindwa kumalizika hata pale ambapo Rais alifanya ziara nchini humo hivi karibuni. Uwezo huu wa Nape kumaliza mgogoro mkubwa na tata kwa watanzania hao kwa muda mchache umeonekana ni wa ajabu kwani wengi walishindwa hapo kabla,alinukuliwa mmoja wa watanzania waishio jijini humo anayejulikana kwa jina la bwana Kittoga.

Nape pia alisisitiza kwa watanzania wa houston hasa wanaCCM kuwa lazima chama kisogezwe kwa wanachama kiutendaji na kimaamuzi na kusisitiza kuwa hilo ni agizo la Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM. Hivyo kuwataka wafungue matawi zaidi ili kuwafikia wengi zaidi kwa ukaribu na urahisi zaidi wa kufuatilia na kushughulikia shughuli za chama.

Lakini jambo lingine ambalo pia liliwashangaza wengi ni upeo binafsi wa Nape pale ilipofika wasaa wa maswali ya papo kwa hapo.,ambapo Nape alitumia muda mwingi wa mkutano wake katika hili ambapo watanzania hao wa houston walipata kuuliza juu ya hali halisi ya uchumi na maisha ya watanzania, ndipo Nape alipowaeleza kwa undani juu ya changamoto zinazoikabili serikali ya awamu ya nne na chama kama taasisi inayoisimamia serikali na pia kuelezea mafanikio yaliyopatikana chini ya CCM, kwa namna ya kipekee kabisa ya ufafanuzi na tafsiri sahihi ya matukio yanayoendelea Tanzania.

Na ilipofika wakati wa kuelezea juu ya falsafa ya chama inayotawala vichwa vya wengi nae Nape aliitolea maelezo, kuwa ni dhana iliyopotoswa sana kitafsiri hasa na wapinzani lakini aliwahakikishia kuwa hiyo ni falsafa ya mabadiliko makubwa katika chama yenye kulenga kubadili taswira mbaya ya chama na kukipa chama nguvu mpya kiutendaji na maamuzi na pia umaarufu zaidi na kukubalika hasa kwa vijana.

Alisisitiza kuwa "falsafa ya kujivua gamba na vita vya ufisadi ndani ya Tanzania ni vitu vinavyoenda sambamba,kwani zote vita dhidi ya matumizi mabaya ya rasilimali za nchi"

Aidha alimalizia kwa kuwataka Wana CCM kutumia matawi yao ya Chama kuwaunganisha Watanzania badala a kugeuka vijiwe vya majungu na kubaguana kwa vigezo vyovyote vile, huku akiwataka kuweka Utanzania wao kwanza kuliko itikadi na tofauti zao malimbali.

Nape anaendelea na ziara yake nchini Marekani yenye lengo la kukagua uhai wa chama, ambapo atatembelea Columbus-Ohio, New York na atamalizia Washington Dc, kabla ya kurejea nchini Tanzania wiki ya kwanza ya mwezi Novemba.
Kama ni muhimu kuweka Utanzania kwanza, mambo ya kuanzisha Matawi ya Vyama vya siasa nje yanasaidia nini ??? Kuna matawi mangapi ya CDM, CUF, TLP, NCCR MAGEUZI, PPT-Maendeleo n.k.
 
Ni ajabu na inashangaza..,

Katika ziara ya Nape inayoendelea hivi sasa nchini marekani kumekuwa na matukio mbalimbali ambayo katika zama za sasa na upepo wa kisiasa ulivyo hasa ndani ya CCM ni sawa kuyaita matukio hayo kuwa ni ajabu na yasiyotegemewa hasa kwa mtu kama Nape kulingana na umri wake na hata nafasi yake. Miongoni mwa matukio hayo nitayataja baadhi, ambayo Nape ameonyesha uwezo mkubwa wa kisiasa na uelewa wa siasa za kimataifa na mahusiano ya kidplomasia, pale alipofanikiwa kwa mara moja kumaliza mgogoro ambao ulidumu kwa muda mrefu baina ya watanzania waliopo jimbo la texas jijini houston, mgogoro ambao ulishindwa kumalizika hata pale ambapo Rais alifanya ziara nchini humo hivi karibuni. Uwezo huu wa Nape kumaliza mgogoro mkubwa na tata kwa watanzania hao kwa muda mchache umeonekana ni wa ajabu kwani wengi walishindwa hapo kabla,alinukuliwa mmoja wa watanzania waishio jijini humo anayejulikana kwa jina la bwana Kittoga.

Nape pia alisisitiza kwa watanzania wa houston hasa wanaCCM kuwa lazima chama kisogezwe kwa wanachama kiutendaji na kimaamuzi na kusisitiza kuwa hilo ni agizo la Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM. Hivyo kuwataka wafungue matawi zaidi ili kuwafikia wengi zaidi kwa ukaribu na urahisi zaidi wa kufuatilia na kushughulikia shughuli za chama.

Lakini jambo lingine ambalo pia liliwashangaza wengi ni upeo binafsi wa Nape pale ilipofika wasaa wa maswali ya papo kwa hapo.,ambapo Nape alitumia muda mwingi wa mkutano wake katika hili ambapo watanzania hao wa houston walipata kuuliza juu ya hali halisi ya uchumi na maisha ya watanzania, ndipo Nape alipowaeleza kwa undani juu ya changamoto zinazoikabili serikali ya awamu ya nne na chama kama taasisi inayoisimamia serikali na pia kuelezea mafanikio yaliyopatikana chini ya CCM, kwa namna ya kipekee kabisa ya ufafanuzi na tafsiri sahihi ya matukio yanayoendelea Tanzania.

Na ilipofika wakati wa kuelezea juu ya falsafa ya chama inayotawala vichwa vya wengi nae Nape aliitolea maelezo, kuwa ni dhana iliyopotoswa sana kitafsiri hasa na wapinzani lakini aliwahakikishia kuwa hiyo ni falsafa ya mabadiliko makubwa katika chama yenye kulenga kubadili taswira mbaya ya chama na kukipa chama nguvu mpya kiutendaji na maamuzi na pia umaarufu zaidi na kukubalika hasa kwa vijana.

Alisisitiza kuwa "falsafa ya kujivua gamba na vita vya ufisadi ndani ya Tanzania ni vitu vinavyoenda sambamba,kwani zote vita dhidi ya matumizi mabaya ya rasilimali za nchi"

Aidha alimalizia kwa kuwataka Wana CCM kutumia matawi yao ya Chama kuwaunganisha Watanzania badala a kugeuka vijiwe vya majungu na kubaguana kwa vigezo vyovyote vile, huku akiwataka kuweka Utanzania wao kwanza kuliko itikadi na tofauti zao malimbali.

Nape anaendelea na ziara yake nchini Marekani yenye lengo la kukagua uhai wa chama, ambapo atatembelea Columbus-Ohio, New York na atamalizia Washington Dc, kabla ya kurejea nchini Tanzania wiki ya kwanza ya mwezi Novemba
.

MAELEZO HAYA YOTE NI UONGO WA KUTUNGA.. MTU MZIMA MWONGO.. MAREKANI UNAYOONGELEA NI IPI.. TANDALE?.. UONGO MKUBWA HUU.. Halafu we Nape Unapata wapi Ujasiri wa Kutunga Uongo na kuumwaga JF this way..Kesho tunaamka na wewe Utuelezee nani kaandika Upupu Huu.. kwanini watanzania wa Migodini uwaaibishe.. that much you are.. nakwambia Kesho jamaa wanakusaka uingie mji wa watu, watu wanabondeka na maisha, kisha unawanyea kwa kutaka sifa zako..Ugomvi gani uliokuwepo na Umeutatua nini.. na hapanakukana thread hii.. Yaani kwmba wewe ni mbabe kuliko mzee?, Kitoga Yupi.. Kitoga huyu anaejifanya protokali ya viongozi.. si huyu tapeli ambaye anaishi kwa kumangamanga. si huyu kila pull ya greenvisa yumo na anatupwa nje. sasa habari za Kiherehere mmoja anauzia jina?.
 
Nape ni NURU na TAA ya matumaini yaliopotea CCM kwa siku nyingi.Anawanyima usingizi wapinzani wake na anazidi kuwatimulia vumbi, ushahidi ni Igunga.viva nape viva ccm viva kikwete.

Umesema vyema... Nape ni nuru na taa ya matumaini yaliyopotea CCM, sio Tanzania.... ni CCM!!!

at least ume-qualify statement yako....

As far as I am concerned, Nape is significant to CCM, and not Tanzania

Am I right?
 
Hapa jf unatakiwa uandike habari za mbowe,slaa,lema,ndesa kina lisu na kina halima mdee.ukiandika za kina nape unachefua watu kaka..learn the behaviours of jf b4 hujaingia kichwakichwa.
 
Wote waliopo huko hawajui maisha halisi ya mtanzania wa kawaida huku vijijini. Nape anapoteza tu muda huko wakati chama huku kina mgogoro mkubwa sana!
 
Back
Top Bottom