Ripoti: Uchumi unakua, umasikini unaongezeka

Ndg Mabadilikosasa, Watu hawataki uwape mfano wa Lowasa kwasababu ni sawa na kuruka mkoj.. na kukany@# #@5!. Tolea mifano ya Dr Mwakyembe na Dr Magufuli. Ukitamka Lowasa watakuona kama umetomwa kuchokoza, kupima upepo au kumsafisha fisadi.

Lakini hoja yako ni marudio tu ilishazungumzwa sana. Dr Slaa aliimba hadi kulia alipoona umasikini wa watu na nyumba zao huko Dodoma. Je uliwahi kufuatilia hotuba zake hizo?
 
Kwa siku mbili zilizopita na leo asubuhi hii tumeshuhudia wabunge wetu wakiendelea na kikao huku vijembe vikielekezwa kwa chadema. Spika na Naibu spika wameonekana kuwa wababe wakiwalinda wabunge wanaoongea hoja ambazo hazina tija kwa hatma ya watanzania.Watanzania tumebaki yatima baada ya wawakilishi wetu kuwa ni wawakilishi wa chama chao (CCM) badala ya wawakilishi wetu. La kushangaza hata baadhi ya vyama vya upinzani sasa wanaiwakilisha CCM bungeni badala ya wananchi wao.

Huku wabunge wa CCM, CUF na NCCR wakitumia muda wanaolipwa kwa kodi zetu wakiwadhihaki wenzao, tunazidi kuumia na ugumu wa maisha. Muda wa mgawo wa umeme umeongezwa toka mara 3 hadi tano kwa wiki. Bei za bidhaa zinaongezeka bila kukicha, watoto wetu wanazidi kufeli mitihani ambalo linachangiwa kwa sehemu kubwa na mgomo baridi wa walimu ulioanza mwaka jana. Pia tatizo linaloonekana wazi kuwa haliepukiki mwaka huu. Tatizo la njaa.

Nyingi ya Kamati za kudumu za Bunge sasa zinaongozwa na watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi au wafuasi wao wa karibu. Watu hawa ndo wanaotuhumiwa kuzihujumu sekta za madini na umeme na barabara.

Kama halii hii itaendelea (na ninaamini itaendelea hivyo), Bunge halitaweza kusimamia maslahi ya wananchi serikalini. Napendekeza wana jamvi tuache sasa ya Dodoma tuanze kujadili njia mbadala ya kushughulikia matatizo mengi yanayolikabili taifa hili.

Kwa ufupi sana ni kwamba bunge la Tanzania ni kupoteza fedha na rasilimali zetu, kwani kwa kiasi kikubwa halina manufaa yoyote kwa mwananchi wa kawaida. Tunaweza kuishi hata bila kuwepo hilo bunge. Wabunge karibia wote (CCM na upinzani) wapo pale kwanza kutetea maslahi yao, next maslahi ya vyama vyao. I think is high time something ought to be done.Wananchi tuamke!
 
Tatizo letu Watanganyika Ccm imetujaza fikra za uoga tokea mwanzoni, huku tukidanganywa na kuvuli cha Amani, Huku tukijidanganya kuwa Ukombozi Utakuja kama zawadi au kushushiwa na Mwenyezi Mungu,
Ukombozi wa kweli huja kwa Jasho,akili,na moyo uliokufa. Ona mfano Wamisri Mioyo yao wananchi imekufa ganzi. lakini hapa kwetu uoga tulionao mpaka tunachezewa Maka***********oooooo, tumebaki kelele nyingiiiiiii, Unavyoona Bunge lilivyo la Mipasho ktk mambo ya msingi, hata sisi ndivyo tulivyo.
 
It is true hivi sasa kinachopewa kipaumbele ni baseless intra-party conflicts hususani zenye nia ya kuidhoofisha CHADEMA kwenye macho ya watanzania.Ningeshauri viongozi wa chadema hususani Katibu mkuu Dr Slaa waweze kuliona hili na kulifanyia kazi ili jitihada za CCM na wapinzani feki ziifanye chadema ikaonekana haina maana kwa watu.Chadema hivi sasa kinasura ya kitaifa, kimeungwa mkono na mikoa mikubwa (penye high political awareness), na kubwa kuliko vyote ina viongozi na makada wengi wenye best brains (thinkers), hivyo jipangeni kurusha counter-attack kwa hao detractors wa ccm na puppets wao.
 
Hawa wabunge wasifanye wanaongoza population ya mbumbumbu.majadiliano mengi yanayoendelea si tu kwamba si kipaumbele cha taifa hili, vile vile mjadala huo hautatui problems za msingi, za umeme, elimu inayozidi kushuka kiwango siku hadi siku because of poor decision making za hao policy makers.wabunge wajadili major issues na siyo trivial issues ambazo zinasaidia vyama vyao na siyo general public ya watanzania.
 
Wamekataa kujadili issue ya dowans kwa kisingizio cha liko mahakamani.je inakuwa vipi wanajadili suala la arusha ambalo pia liko mahakamani? Waache kutufanya wananchi hatuna akili, huo ni ubabaishaji na wala hautaweza kurudisha imani ya wananchi kwa ccm.the party has lost direction, not respected and also hated by many people, and thus it is in its moribund.in other words, the party is dieng at a fast pace.
 
WanaJF,
Whether mtachukia au la lakini huo ndiyo ukweli. Tusitarajie maendeleo yoyote kutoka kwa rais asiyejua sababu ya umaskini wetu. Ina maana kuwa yupo ikulu ili kutimiza lengo lake la kupata utukufu wa kiti hicho. Ndiyo hasara ya kuwa na rais 'mswahili'. Matumaini yetu tuelekeze 2015.
 
Umasikini wa watanzania uko katika akili. Aliyejifanya daktari wa kwanzaa kutibu tatizo hilo alikuwa mzungu aliyetawala nchi yetu. Aliwanyanyasa sana mababu zetu. Pamoja na hayo, kaacha mifumo ya elimu, sheria, utawala n.k, ambayo haiwezi kumkomboa mtanzania kutoka katika fikra za kishirikina na ndo maana hadi leo nyazifa za kiutawala, michezo n.k. zimejawa na ugandamizaji na ushirikina. Siku ushirikina utakapotoka katika ikulu yetu, Tanzania yenye neema inayotawaliwa na utashi unaongozwa na busara itazaliwa. Lazima tuweke mipango ya muda mrefu ya kitaifa yaani ingawa ya miaka 200 ijayo. Je wewe ungekuwa ndo mtawala wa nchi hii, ungefanya nini ili Tanzania huru na adilifu izaliwe?
 
Hivi wanajamii forum. Hili swala la uchimbaji wa madili ya nchi yetu na wananchi wanabakia maskini mnashauri nini?
 
Mara nyingi siridhiki ninapokula vizuri na kuishi nyumba nzuri na kuendesha my dream car lakini just nje ya gate langu kuna wakina mama wanauza mafungu kumi tu ya mnafu na mchicha ili wapate hela ya kula na kodi ya nyumba.

Kando kando ya maduka hapa mtaani kwetu au vijiweni kwa jina maarufu wakati wa jioni unakuta makundi ya vijana wenye nguvu ambao wamesimama. Wengi wao unagundua walikuwa wana apollo na wamerudi mtaani baada ya sehemu kubwa machimbo ya wachimbaji wadogo wadogo wa Tanzanite kule Mererani kushindwa kupata madini kutokana na kuchimbwa na makampuni makubwa ya makaburu hususani Tanzanite One. Robotatu yao wameoa mara na wanaponiona kama jirani yao wanakusalimia kwa juhudi na matarajio fulani. Baada ya salamu wanakufuata na kukueleza bro hali ni mbaya sana sina kitu kabisa. Hapo unawapa shilingi 2000 then unaingia getini kwako kuendelea na maisha na familia yako.

Wakati mwingine jirani ana piga moyo konde kuja nyumbani na kuomba kumsaidia ada ya shilingi 20,000 ya mtoto aliyeko shule ya kata. Elfu 20 kwa watanzania wengine ni bajeti ya masaa tu machache na kwa wengine haitoshi hata mafuta ya gari wala unywaji wa bia kwa masaa machache Ila kwa huyu mama ni ada ya mtoto ya shule ambayo katika shughuli zake za kuuza mchicha kwa muhula mzima ameshindwa kuipata.

Huwa napata shida zaidi ninapokwenda kusalimia wazazi au kuhudhuria msiba kijijini kwetu unapokutana na kila mtu anayekufahamu akiomba 500 au hata 200. Huwa najiuliza atafanyia nini?

Hali hizi zote zina ashiria hali mbaya ya umaskini unaoikumba jamii ya watanzania na kuna uwezekano wa idadi ya wasio nacho kuongezeka.

Wakati kuna kada ya watanzania ambao suala la nini tunakula na wapi nitapata ada imebaki historia, kuna watanzania walio wengi ambao bado wanahangaika kupata uhakika wa kula na ada ya watoto wao.

Huwa kila siku najiuliza je nini chanzo cha hali kama hii?; Je walaumiwe mababu zao au nani? na ni ipi njia ya kuwatoa katika hali hii? Watatoka lini na kusahau maisha haya magumu ambayo yamekuwa sehemu ya maisha yao toka utotoni? Nani aanzishe mchakato wa kuwatoa katika hali hii?

Wewe mwenzangu unayemshuhudia binadamu mwenzako ambaye bajeti yake kwa mwezi ni nusu ya bajeti yako ya bia kwa siku au robo ya bajeti yako ya mafuta ya gari kwa siku unawaza nini na unamamfikiriaje mwenzio. Sijasema usiweke gari mafuta au usile vizuri lakini woote nataka tujiulize Maswali yafuatayo:

Je unafikiri tukitumia nafasi zetu na rasilimali za ziada tulizojaliwa na Mungu hatuwezi kuwasaidia walio karibu nasi angalau kuchangia ada za watoto wao ili ku break viscious circle ya huu umaskini?

Je viongozi wetu mlioko Nyumba za serikali ambao wengi wenu hamjui maisha halisi ya watanzania na shida zinazowakabili je mnafikiri mkiwa na asilimia tu 10 ya utu tutashindwa kuwainua watanzania?

Viongozi wetu mlioko madarakani tukitumia tu asilimia 25 tu ya rasilimali tulizopewa na Mungu katika nchi yetu kwa uaminifu hamjui tutaweza kuibadili nchi yetu na kuondoa umaskini?

Mnaotuongoza tukiacha kwa asilimia 20 roho mbaya, ubinafsi, kujilimbikizia, mawazo ya kutaka kuwa millionea kwa rasilimali za nchi hamjui kwamba tutawainua watanzania walio wengi kiuchumi?

NB:
Naamini kwa watanzania walio na uchungu na wenzao na nchi yao wanaweza kuchangia point za maana katika hii mada ila kwa yule ambaye anafikiri ninachoongea ni upuuzi basi akae pembeni asichangie
 
Umenena vyema bro...watanzania tumeachana umoja wetu na hii ni laana ya Mwalimu J.K ,naukumbuka usia wake kwamba "mkiliacha kabisa kabisa azimio la Arusha hamtabaki salama" na "mkiwachagua vijana hawa...watawasumbua" mzee alimaanisha (BOYZ II MEN) JK & EL,
tatzo letu kubwa ni kwamba tuliingi kwenye utandawazimu bila kufikiria format yake iweje katika kuhusanisha na mazingira ya watanzania wakati huo,bado watanzania wengi walikuwa masikini,wengi wao walikuwa wakulima na wasiokuwa na elimu za kutosha,nchi haikuwa na viwanda vya maana,hapakuwepo na miundombinu madhubuti na mengine mengi

tatizo jingine lililojitokeza baadae ni kuwapata viongozi wabovu na wabnafsi kupitiliza,waweza kufikiri labda ni watu kutoka nje wamekodishwa kuja kusaidia kuongoza hapa Tanzania,pili watanzania wengi sahvi hatupendani,tunaogopana kama ukoma,hata kusaidiana sahvi ni tabu

usione watu tunaongea,tunacheka na kunywa pamoja,tunaogopana,tunachukiana,tumejaa chuki,hata viongozi wetu wa dini nao hawaendi tena katika kuhubili upendo,amani,utu,uvumilivu n.k,badala yake wanabaguana kwa madhehebu,eti yule ana wateja wengi,what this is it? May God bless Tanzania
 
UNDP inatoa taarifa juu ya "The concentrated poverty". Yaani umaskini wa kutisha, kwa bahati mbaya Tanzania ni moja ya nchi zilizo chini ya mstari mwekundu wa umaskini ambao wao wanaita "below poverty level" au absolutely poverty". Huu ni umaskini unaozidi kawaida ya umaskini, waweza kuita umaskini sana, au umaskini zaidi, ama umaskini mno, lakini yote hayo yanaashiria neno moja tu nalo ni kwamba umaskini unaoikabili nchi yetu ni sawa kabisa na ugonjwa wa ukimwi kwa maana ya kwamba umaskini wetu sasa hautibiki.

KATIKA kuufafanua umaskini, mtu aweza kuuweka ama kuugawanya katika mafungu mawili, umaskini wa nchi (au taifa) na umaskini wa watu au "mass poverty" yaani walio wengi katika ujumla wao. Enzi za mkoloni nchi yetu ilikuwa na umaskini wa watu tu yaani "individuals" lakini haikuwa na umaskini wa dola kama uliopo sasa ambapo takribani asilimia 50 ya bajeti ya serikali inatoka kwa wahisani.

Katika uhalisi wa mambo nchi yetu ni ombaomba, hata waliyodai Mkapa alirudisha heshima ya Tanzania kimataifa sijui wanatumia vigezo gani kwani katika ukweli wa maisha hakuna omba omba yeyote aliyepata kuheshimika. Heshima ya Tanzania italetwa kwa kujitegemea na kujitosheleza, kwanza kwa chakula na baadaye kwa mahitaji mengine, yaliyo muhimu kwa taifa. Enzi za mkoloni Tanganyika ilikuwa nchi ya kwanza kwa uzalishaji wa mkonge ambapo ilitoa asilimia 28 ya mahitaji ya dunia ukiacha mazao mengine kama nyonyo, karanga, pamba na ngozi, na kahawa.

Kwa mapato hayo serikali ya mkoloni haikuwa lofa iliweza kujenga mabarabara, njia za mawasiliano, na kutoa elimu bora kwa hao waliobahatika kusoma. Kwa maneno mengine walau serikali iliweza kujitegemea, lakini sasa kila kitu kiko nyang'anyang'a na hoi bin taabani. Hakuna mradi wowote wa kitaifa ambao ungeweza kutoa ajira ya maelfu kama ukoloni, hakuna watu wabunifu ndani ya hiyo kada ya watawala badala yake umahili wao uko kwenye kudhibiti wapinzani na kuendesha mizengwe ya kuwawezesha kubaki madarakani. Wao watawala, ushindi wanaouona muhimu ni ule tu wa uchaguzi mkuu. Ule ukweli kwamba wao baada ya kuwashinda wapinzani, nao wameshindwa na umaskini hawaujali wala hawaoni aibu.

Inapotokea kwamba dola imekuwa maskini hadi kuendeshwa kwa misaada toka nje ya nchi na watu (wananchi) nao wakawa maskini hadi kufikia kiwango cha kushindwa kufanya lolote na kubaki kama walemavu kungojea kudra za Mungu basi hapo kuna tatizo mara mbili yaani tatizo la umaskini na tatizo la watu wenyewe. Lakini papo hapo viongozi wakuu wa serikali wanapokuwa ni matajiri kuliko serikali yao, basi hapo ndipo kinapoinuka kitendawili cha uongozi bora.

Mawaziri walio matajiri, wakuu wa mikoa walio tajiri, makatibu wakuu walio tajiri, na wabunge walio tajiri, je, wamefanya biashara gani madarakani hadi wakaupata utajiri walio nao? Kisha je wameulipia kodi ya mapato? Maana inaonyesha kwa utajiri wao basi wanavyo vyanzo vya uhakika vya mapato na kwa kuwa katika nchi yetu kuna sera ya kutoza kodi ya mapato (wakati mwingine hata kabla ya mtu hajapata) basi na wao watoe mchanganuo wao kuthibitisha kwamba nao ni raia wema wanaoilipa serikali mapato sawa na sheria za nchi zinavyoagiza!!

Kitendawili hiki ni kigumu kuteguliwa ingawa jibu lake liko wazi, kitendawili chenyewe ni kwamba hapa kuna nchi yenye rasilimali za kila namna lakini bado nchi hiyo ni maskini ya kupindukia duniani, nchi hiyo ilipotawaliwa na Wakoloni haikuwa maskini kama ilivyotawaliwa na watawala waliopo sasa, wakati nchi ni maskini, na watu ni maskini mno. Viongozi ni matajiri wa kupindukia. Je kuna mchezo gani umechezwa kuyaleta haya? Jibu wanalo wenyewe watawala, wanajua jinsi walivyofanya hata kuupata utajiri walio nao sasa isipokuwa wanajifanya hawajui wafanye nini ili kuondoa umaskini kwa nchi yao na watu wao, kwa kuwa akili yao imeishia kujitajirisha wao na siyo nchi. Vijana wapatao laki nne wanamaliza elimu ya msingi kila mwaka lakini uongozi uliopo madarakani haujui ufanye nini au uwapeleke wapi,hivyo baada ya kutoka darasani wanaishia "vijiweni".

Viwanda vingi vimekufa, na mashirika ya umma mengi yameanguka waliokuwa wafanyakazi nao inabidi waungane kwenye vijiwe na vijana wao wanaotoka darasani hadi vijiweni. Kutokana kukosekana sera ya uhakika ya kilimo, kilimo kimebaki duni toka enzi za Mwalimu Nyerere hadi sasa na kwa uduni huo.Kilimo kimejiunga kwenye siasa na kutengenezewa majina mazuri ya kisiasa kama ‘’KILIMO KWANZA’’ wakati uhalisia sio huo. Tumebaki kudanganyana tu ili mradi siku iende. Hakuna elimu ya kuwaelimisha wananchi hasa vijana wajue umuhimu wa kilimo. Mikopo ya Kikwete inatolewa kwa wafanyabiashara badala ya wakulima, na wafanyabiashara wenyewe sio wahitaji halisi wa mikopo hiyo kwania tayari walishakuwa na mitaji ya kutosha. Wakulima wanaachwa kama walivyo, vijana wanaona kilimo kama hakiwezekani kwani hakiwaondoi katika dimbwi la umasikini wa kutupwa. Wakulima hawapendelewi wala hawajengewi mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao kama wanavyofanyiwa wafanyabiashara, hivyo vijana wanaona ni bora kufanya biashara ili wajiingize kwenye mazingira mazuri kuliko kiliko kulimo. Kizazi kipya cha vijana wanakimbia kilimo vijijini na kuja mjini kubahatisha maisha mapya. Wale vijana wanaozaliwa mijini, wao wanakimbilia majuu (wanazamia meli), kizazi cha kale cha wakulima kinazeeka na kudhoofu na hakuna wa kuziba pengo, hivyo usemi wa kwamba Tanzania ni nchi ya wakulima na wafanyakazi umebaki kauli za maandishi tu, lakini katika uhalisi wa mambo Tanzania haina wakulima ndiyo maana ni nchi inayoumwa njaa kila mwaka. Pia Tanzania si nchi ya wafanyakazi maana hakuna kazi nyingi za kufanya kwa sababu hakuna viwanda wala makampuni au mashirika ya kutoa ajira.

Yale yaliyokuwepo yameuawa na watawala waliopo madarakani. Sasa inabidi wote wenye kutazama mambo katika umakini wajiulize nchi ambayo imepukutisha maelfu ya askari wake toka jeshini baada ya kulazimishwa na sera za IMF za kuwa na jeshi dogo, na hivyo kuwalazimisha askari hao kujiunga na walalahoi wengine vijiweni, nchi ambayo imeua mfumo wake wa elimu na kuwafanya vijana wake wasipate elimu ya kuwasaidia kuishi badala yake vijana wake wakawa na elimu ya nadharia ambayo baada ya mtu kumaliza shule (kutoka darasani) anashindwa kuitumia (to apply) aidha hapo kijijini au mjini, mwisho anaishia kijiweni kuvuta bangi au kulamba unga. Ndio vijana hawa wanalaghaiwa na wafanyabiashara wakubwa kujiingiza katika biashara haramu.

Nchi ambayo inashindwa kuzalisha kizazi kipya cha wakulima na waliopo inawaacha wawe wachovu zaidi kwa kuvuruga mfumo wa masoko ya mazao yao na kuwasababishia umaskini usiomithilika, nchi ambayo haina mpango wowote wa kuongeza ajira kwa maelfu ya wananchi wake, nchi ambayo imeua mfumo wa utoaji haki na kusababisha magereza kufurika wafungwa na mahabusu, nchi ambayo haina mikakati yoyote ya kuwatumia wafungwa kuzalisha mali ili kujikimu wawapo magerezani badala ya kutegemea pesa kutoka serikalini, na mahakama zake kuwa na mafuriko ya kesi za jinai. Je nchi ya namna hiyo ina uhakika gani wa kudumisha amani yake wakati inayaacha mabomu yanayongojea wakati wake ufike yalipuke?

Kwa hakika nchi yetu ni mfano wa mtu anayetembea sambamba na gema ambaye kuna uwezekano wa kutumbukia wakati wowote. Hata hivyo ieleweke wazi kwamba tatizo la umaskini ni matokeo tu ya uzembe wa watawala, endapo nchi itapata utawala ulio makini na ulio dhamiria kuondoa tatizo hili, umaskini wa Tanzania unaweza kufutika baada ya muda mfupi na Tanzania ikawa miongoni mwa nchi tajiri na zenye uchumi imara au "economic giant" katika dunia hii.

Mtu hawezi kuamini akielezwa kwamba umaskini wa Tanzania ni sera ya makusudi kabisa ambayo lengo lake kuu ni kudhibiti wananchi na kuwawezesha watawala kuendelea kudumu madarakani hadi siku ya kufa. Watawala wa nchi hii wanajua wazi kwamba wakiwaondoa watu wao katika dimbwi la umasikini hawawezi kutawalika na pia hawawezi kuburuzwa, kwa hiyo umaskini ni silaha yao nzuri ya kuendelea kutawala.

Fikiria kama Watanzania wangekuwa na elimu, shibe, na utajiri, ni wazi kwamba asingekuweko mgombea yeyote wa ubunge, urais, au udiwani wa kuhonga watu soda, pilau, khanga au pombe za kienyeji. Pasingekuweko na mtu wa kuuza shahada yake ya kupigia kura kwa Tshs: 2,000. Hapo ndipo yangekuweko mashindano ya sera na programu za kuendeleza nchi, majimbo, maeneo, au mitaa.

Kwa ajili hiyo umaskini kama ulivyo katika nchi hii ni kikwazo cha mengi, ni kikwazo dhidi ya demokrasia, ni kikwazo dhidi ya utawala bora kutokana na ukweli kwamba wezi wa mali za umma na walaji rushwa na mafisadi ndio wenye tabia za kuwanunua wapiga kura walio hoi kwa njaa na umaskini wa kupindukia. Pia umaskini ni kikwazo dhidi ya mabadiliko yoyote.

Sasa kwa bahati mbaya tatizo la umaskini haliwezi kuondoshwa na utawala unaoona kwamba kuwatawala watu masikini ni raha zaidi kuliko kuwatawala watu walioridhika kimaisha, wakoloni walijitahidi kuwagawa wananchi ili wabaki hawaelewani kati ya walionacho na wasionacho, waliosoma na wasiosoma ili wapate kinga ya kuwafanya waendelee kutawala bila shida. Wao walihakikisha wananchi wanaowatawala wanabaki wajinga. Wagonjwa, na maskini ili wasiwe na ubavu wa kuwaondoa madarakani. Cha kushangaza ni kwamba takribani miaka 48 (2009-1961) tangu tupate uhuru wetu kutoka kwa Mwingereza watawala wetu bado wanaendeleza mbinu za wakoloni za kutawala za kutufanya tuwe wajinga, masikini na tunaosumbuliwa na magonjwa kila wakati.

Kwa mfano Maasi ya Maji Maji 1905-1907 yalifanya Mjerumani kuyaelewa makabila ya kusini kwamba ni ya watu jeuri na wagumu kutawalika endapo wataachiwa kutulia pasipo kuvurugwa na njaa, umaskini au magonjwa alichokifanya ni kutokupeleka maendeleo makubwa kama vile reli, shule, na mahospitali makubwa. Serikali ya TANU pia ilifuata nyayo za Mjerumani, ilijua wazi kwamba watu wa kusini, Wangoni, Wapangwa, wamatengo, Wamakua, Wamwera, Wanyasa, Wamakonde, Wayao, na Warufiji kwa asili yao ni watu jeuri na wagumu kuburuzwa endapo wataachiwa wawe na uimara wowote ule aidha uimara wa kiuchumi, au uimara wa kielimu au uimara wa kuwa na mshikamano, hivyo basi sera ya ‘’gawanya utawale’’ ikabidi iendelezwe na juu ya hiyo iongezwe sera ya kuwafanya wawe maskini zaidi na pia kuwatenga ama kuwabomolea misingi yote ya maendeleo kwani kama wangekuwa na maendeleo walau nusu tu ya yale yaliyoko kaskazini ingekuwa vigumu kutawalika. Kwa hiyo kwa makusudi kabisa reli ya TAZARA ambayo kimsingi ingekuwa kama ilivyo reli ya kati kwa mikoa ya kusini ikapitishwa porini badala ya kupita Rufiji, Mtwara,Lindi, Songea hadi Itungi Port (Kyela) na kuingia Zambia. Reli ilikwepeshwa maeneo hayo ili tu kuzuia kasi ya maendeleo ya kusini na pia kuzuia kukua kwa uchumi wa kusini.

Kusini ambayo ina rasilimali nyingi na utajiri mwingi kuliko kaskazini na pengine maeneo mengine yote ya nchi hii sasa imekuwa chemi chemi ya kutoa Wamachinga kwa sababu tu watoto wake wamenyimwa elimu. Rasilimali zake zinaoza na huenda siku za usoni watapewa wageni kama ilivyotokea kwa SongoSongo na machimbo ya Alexandrite huko Tunduru.
Baadhi ya wasomi wachache wa kusini walipewa nyadhifa katika serikali ili ziwe kama takrima na uchawi wa kuloga akili zao wasijejali tena maendeleo ya kusini wala kuwahurumia ndugu zao ambao wanahitaji ukombozi kwa njia ya maendeleo.
Umasikini wa Tanzania ni wa Kujitakia
Africar T Kagema

UNDP inatoa taarifa juu ya "The concentrated poverty". Yaani umaskini wa kutisha, kwa bahati mbaya Tanzania ni moja ya nchi zilizo chini ya mstari mwekundu wa umaskini ambao wao wanaita "below poverty level" au absolutely poverty". Huu ni umaskini unaozidi kawaida ya umaskini, waweza kuita umaskini sana, au umaskini zaidi, ama umaskini mno, lakini yote hayo yanaashiria neno moja tu nalo ni kwamba umaskini unaoikabili nchi yetu ni sawa kabisa na ugonjwa wa ukimwi kwa maana ya kwamba umaskini wetu sasa hautibiki.

KATIKA kuufafanua umaskini, mtu aweza kuuweka ama kuugawanya katika mafungu mawili, umaskini wa nchi (au taifa) na umaskini wa watu au "mass poverty" yaani walio wengi katika ujumla wao. Enzi za mkoloni nchi yetu ilikuwa na umaskini wa watu tu yaani "individuals" lakini haikuwa na umaskini wa dola kama uliopo sasa ambapo takribani asilimia 50 ya bajeti ya serikali inatoka kwa wahisani.

Katika uhalisi wa mambo nchi yetu ni ombaomba, hata wanaodai Mkapa amerudisha heshima ya Tanzania kimataifa sijui wanatumia vigezo gani kwani katika ukweli wa maisha hakuna omba omba yeyote aliyepata kuheshimika. Heshima ya Tanzania italetwa kwa kujitegemea na kujitosheleza, kwanza kwa chakula na baadaye kwa mahitaji mengine, yaliyo muhimu kwa taifa. Enzi za mkoloni Tanganyika ilikuwa nchi ya kwanza kwa uzalishaji wa mkonge ambapo ilitoa asilimia 28 ya mahitaji ya dunia ukiacha mazao mengine kama nyonyo, karanga, pamba na ngozi, na kahawa.

Kwa mapato hayo serikali ya mkoloni haikuwa lofa iliweza kujenga mabarabara, njia za mawasiliano, na kutoa elimu bora kwa hao waliobahatika kusoma. Kwa maneno mengine walau serikali iliweza kujitegemea, lakini sasa kila kitu kiko nyang'anyang'a na hoi bin taabani. Hakuna mradi wowote wa kitaifa ambao ungeweza kutoa ajira ya maelfu kama ukoloni, hakuna watu wabunifu ndani ya hiyo kada ya watawala badala yake umahili wao uko kwenye kudhibiti wapinzani na kuendesha mizengwe ya kuwawezesha kubaki madarakani. Wao watawala, ushindi wanaouona muhimu ni ule tu wa uchaguzi mkuu. Ule ukweli kwamba wao baada ya kuwashinda wapinzani, nao wameshindwa na umaskini hawaujali wala hawaoni aibu.

Inapotokea kwamba dola imekuwa maskini hadi kuendeshwa kwa misaada toka nje ya nchi na watu (wananchi) nao wakawa maskini hadi kufikia kiwango cha kushindwa kufanya lolote na kubaki kama walemavu kungojea kudra za Mungu basi hapo kuna tatizo mara mbili yaani tatizo la umaskini na tatizo la watu wenyewe. Lakini papo hapo viongozi wakuu wa serikali wanapokuwa ni matajiri kuliko serikali yao, basi hapo ndipo kinapoinuka kitendawili cha uongozi bora.

Mawaziri walio matajiri, wakuu wa mikoa walio tajiri, makatibu wakuu walio tajiri, na wabunge walio tajiri, je, wamefanya biashara gani madarakani hadi wakaupata utajiri walio nao? Kisha je wameulipia kodi ya mapato? Maana inaonyesha kwa utajiri wao basi wanavyo vyanzo vya uhakika vya mapato na kwa kuwa katika nchi yetu kuna sera ya kutoza kodi ya mapato (wakati mwingine hata kabla ya mtu hajapata) basi na wao watoe mchanganuo wao kuthibitisha kwamba nao ni raia wema wanaoilipa serikali mapato sawa na sheria za nchi zinavyoagiza!!

Kitendawili hiki ni kigumu kuteguliwa ingawa jibu lake liko wazi, kitendawili chenyewe ni kwamba hapa kuna nchi yenye rasilimali za kila namna lakini bado nchi hiyo ni maskini ya kupindukia duniani, nchi hiyo ilipotawaliwa na Wakoloni haikuwa maskini kama ilivyotawaliwa na watawala waliopo sasa, wakati nchi ni maskini, na watu ni maskini mno. Viongozi ni matajiri wa kupindukia. Je kuna mchezo gani umechezwa kuyaleta haya? Jibu wanalo wenyewe watawala, wanajua jinsi walivyofanya hata kuupata utajiri walio nao sasa isipokuwa wanajifanya hawajui wafanye nini ili kuondoa umaskini kwa nchi yao na watu wao, kwa kuwa akili yao imeishia kujitajirisha wao na siyo nchi. Vijana wapatao laki nne wanamaliza elimu ya msingi kila mwaka lakini uongozi uliopo madarakani haujui ufanye nini au uwapeleke wapi,hivyo baada ya kutoka darasani wanaishia "vijiweni".

Viwanda vingi vimekufa, na mashirika ya umma mengi yameanguka waliokuwa wafanyakazi nao inabidi waungane kwenye vijiwe na vijana wao wanaotoka darasani hadi vijiweni. Kutokana kukosekana sera ya uhakika ya kilimo, kilimo kimebaki duni toka enzi za Mwalimu Nyerere hadi sasa na kwa uduni huo.Kilimo kimejiunga kwenye siasa na kutengenezewa majina mazuri ya kisiasa kama ‘’KILIMO KWANZA’’ wakati uhalisia sio huo. Tumebaki kudanganyana tu ili mradi siku iende. Hakuna elimu ya kuwaelimisha wananchi hasa vijana wajue umuhimu wa kilimo. Mikopo ya Kikwete inatolewa kwa wafanyabiashara badala ya wakulima, na wafanyabiashara wenyewe sio wahitaji halisi wa mikopo hiyo kwania tayari walishakuwa na mitaji ya kutosha. Wakulima wanaachwa kama walivyo, vijana wanaona kilimo kama hakiwezekani kwani hakiwaondoi katika dimbwi la umasikini wa kutupwa. Wakulima hawapendelewi wala hawajengewi mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao kama wanavyofanyiwa wafanyabiashara, hivyo vijana wanaona ni bora kufanya biashara ili wajiingize kwenye mazingira mazuri kuliko kiliko kulimo. Kizazi kipya cha vijana wanakimbia kilimo vijijini na kuja mjini kubahatisha maisha mapya. Wale vijana wanaozaliwa mijini, wao wanakimbilia majuu (wanazamia meli), kizazi cha kale cha wakulima kinazeeka na kudhoofu na hakuna wa kuziba pengo, hivyo usemi wa kwamba Tanzania ni nchi ya wakulima na wafanyakazi umebaki kauli za maandishi tu, lakini katika uhalisi wa mambo Tanzania haina wakulima ndiyo maana ni nchi inayoumwa njaa kila mwaka. Pia Tanzania si nchi ya wafanyakazi maana hakuna kazi nyingi za kufanya kwa sababu hakuna viwanda wala makampuni au mashirika ya kutoa ajira.

Yale yaliyokuwepo yameuawa na watawala waliopo madarakani. Sasa inabidi wote wenye kutazama mambo katika umakini wajiulize nchi ambayo imepukutisha maelfu ya askari wake toka jeshini baada ya kulazimishwa na sera za IMF za kuwa na jeshi dogo, na hivyo kuwalazimisha askari hao kujiunga na walalahoi wengine vijiweni, nchi ambayo imeua mfumo wake wa elimu na kuwafanya vijana wake wasipate elimu ya kuwasaidia kuishi badala yake vijana wake wakawa na elimu ya nadharia ambayo baada ya mtu kumaliza shule (kutoka darasani) anashindwa kuitumia (to apply) aidha hapo kijijini au mjini, mwisho anaishia kijiweni kuvuta bangi au kulamba unga. Ndio vijana hawa wanalaghaiwa na wafanyabiashara wakubwa kujiingiza katika biashara haramu.

Nchi ambayo inashindwa kuzalisha kizazi kipya cha wakulima na waliopo inawaacha wawe wachovu zaidi kwa kuvuruga mfumo wa masoko ya mazao yao na kuwasababishia umaskini usiomithilika, nchi ambayo haina mpango wowote wa kuongeza ajira kwa maelfu ya wananchi wake, nchi ambayo imeua mfumo wa utoaji haki na kusababisha magereza kufurika wafungwa na mahabusu, nchi ambayo haina mikakati yoyote ya kuwatumia wafungwa kuzalisha mali ili kujikimu wawapo magerezani badala ya kutegemea pesa kutoka serikalini, na mahakama zake kuwa na mafuriko ya kesi za jinai. Je nchi ya namna hiyo ina uhakika gani wa kudumisha amani yake wakati inayaacha mabomu yanayongojea wakati wake ufike yalipuke?

Kwa hakika nchi yetu ni mfano wa mtu anayetembea sambamba na gema ambaye kuna uwezekano wa kutumbukia wakati wowote. Hata hivyo ieleweke wazi kwamba tatizo la umaskini ni matokeo tu ya uzembe wa watawala, endapo nchi itapata utawala ulio makini na ulio dhamiria kuondoa tatizo hili, umaskini wa Tanzania unaweza kufutika baada ya muda mfupi na Tanzania ikawa miongoni mwa nchi tajiri na zenye uchumi imara au "economic giant" katika dunia hii.

Mtu hawezi kuamini akielezwa kwamba umaskini wa Tanzania ni sera ya makusudi kabisa ambayo lengo lake kuu ni kudhibiti wananchi na kuwawezesha watawala kuendelea kudumu madarakani hadi siku ya kufa. Watawala wa nchi hii wanajua wazi kwamba wakiwaondoa watu wao katika dimbwi la umasikini hawawezi kutawalika na pia hawawezi kuburuzwa, kwa hiyo umaskini ni silaha yao nzuri ya kuendelea kutawala.

Fikiria kama Watanzania wangekuwa na elimu, shibe, na utajiri, ni wazi kwamba asingekuweko mgombea yeyote wa ubunge, urais, au udiwani wa kuhonga watu soda, pilau, khanga au pombe za kienyeji. Pasingekuweko na mtu wa kuuza shahada yake ya kupigia kura kwa Tshs: 2,000. Hapo ndipo yangekuweko mashindano ya sera na programu za kuendeleza nchi, majimbo, maeneo, au mitaa.

Kwa ajili hiyo umaskini kama ulivyo katika nchi hii ni kikwazo cha mengi, ni kikwazo dhidi ya demokrasia, ni kikwazo dhidi ya utawala bora kutokana na ukweli kwamba wezi wa mali za umma na walaji rushwa na mafisadi ndio wenye tabia za kuwanunua wapiga kura walio hoi kwa njaa na umaskini wa kupindukia. Pia umaskini ni kikwazo dhidi ya mabadiliko yoyote.

Sasa kwa bahati mbaya tatizo la umaskini haliwezi kuondoshwa na utawala unaoona kwamba kuwatawala watu masikini ni raha zaidi kuliko kuwatawala watu walioridhika kimaisha, wakoloni walijitahidi kuwagawa wananchi ili wabaki hawaelewani kati ya walionacho na wasionacho, waliosoma na wasiosoma ili wapate kinga ya kuwafanya waendelee kutawala bila shida. Wao walihakikisha wananchi wanaowatawala wanabaki wajinga. Wagonjwa, na maskini ili wasiwe na ubavu wa kuwaondoa madarakani. Cha kushangaza ni kwamba takribani miaka 48 (2009-1961) tangu tupate uhuru wetu kutoka kwa Mwingereza watawala wetu bado wanaendeleza mbinu za wakoloni za kutawala za kutufanya tuwe wajinga, masikini na tunaosumbuliwa na magonjwa kila wakati.

Kwa mfano Maasi ya Maji Maji 1905-1907 yalifanya Mjerumani kuyaelewa makabila ya kusini kwamba ni ya watu jeuri na wagumu kutawalika endapo wataachiwa kutulia pasipo kuvurugwa na njaa, umaskini au magonjwa alichokifanya ni kutokupeleka maendeleo makubwa kama vile reli, shule, na mahospitali makubwa. Serikali ya TANU pia ilifuata nyayo za Mjerumani, ilijua wazi kwamba watu wa kusini, Wangoni, Wapangwa, wamatengo, Wamakua, Wamwera, Wanyasa, Wamakonde, Wayao, na Warufiji kwa asili yao ni watu jeuri na wagumu kuburuzwa endapo wataachiwa wawe na uimara wowote ule aidha uimara wa kiuchumi, au uimara wa kielimu au uimara wa kuwa na mshikamano, hivyo basi sera ya ‘’gawanya utawale’’ ikabidi iendelezwe na juu ya hiyo iongezwe sera ya kuwafanya wawe maskini zaidi na pia kuwatenga ama kuwabomolea misingi yote ya maendeleo kwani kama wangekuwa na maendeleo walau nusu tu ya yale yaliyoko kaskazini ingekuwa vigumu kutawalika. Kwa hiyo kwa makusudi kabisa reli ya TAZARA ambayo kimsingi ingekuwa kama ilivyo reli ya kati kwa mikoa ya kusini ikapitishwa porini badala ya kupita Rufiji, Mtwara,Lindi, Songea hadi Itungi Port (Kyela) na kuingia Zambia. Reli ilikwepeshwa maeneo hayo ili tu kuzuia kasi ya maendeleo ya kusini na pia kuzuia kukua kwa uchumi wa kusini.

Kusini ambayo ina rasilimali nyingi na utajiri mwingi kuliko kaskazini na pengine maeneo mengine yote ya nchi hii sasa imekuwa chemi chemi ya kutoa Wamachinga kwa sababu tu watoto wake wamenyimwa elimu. Rasilimali zake zinaoza na huenda siku za usoni watapewa wageni kama ilivyotokea kwa SongoSongo na machimbo ya Alexandrite huko Tunduru.
Baadhi ya wasomi wachache wa kusini walipewa nyadhifa katika serikali ili ziwe kama takrima na uchawi wa kuloga akili zao wasijejali tena maendeleo ya kusini wala kuwahurumia ndugu zao ambao wanahitaji ukombozi kwa njia ya maendeleo.
 
mkuu post yako nzuri lakini ndefu kweli kweli, sijui kama itapata wasomaji wa kutosha labda uipunguze asilimia 90
 
Kama kawaida wabongo tunapenda vitu vya mkato. We don't want to read much. Tunapenda vitu vya juu juu. Probably ndio maana tunasaini mikataba mibovu b'se we dont care to read the small details.
 
mzee ndio hivyo, umaskini wetu ni wakujitakia kabisaaa, nchi nyingi za kiafrika na tanzania ikiwemo tumejidumaza katika kupokea misaada ambayo kimsingi inakuja na masharti magumu ambayo hayatekelezi, jamani tujifunze kutoka kwa wenzetu wa asian tiger economies
 
Lakini mkuu wa Kaya amesema hali sio mbaya. Mapato yameongezeka miaka mitano iliyopita.
[video]www.youtube.com/watch?v=3q7btXj7bh4[/video]
 
YOUR post is excellent sir, but in the future try as much as possible to put few words, go straight to the point. Succintly, you need to be precise and concise in your presentation.

This is important because very few people, particularly those with moderate intelligent, are interested to read long articles. Most important, however, many people are too busy not only physically but also intellectually, and therefore they are interested to short but comprehensive articles.

Thank you very much for your insight sir
 
Back
Top Bottom