Ripoti Mpya: Wanafunzi wa Tanzania hawajui kusoma Kiswahili?

nickodemus

Member
Jan 19, 2011
7
0
Hisabati kwa watoto wa shule za msingi Afrika Mashariki. Ni ajabu kuwa majirani zetu Kenya watoto wao wanawashinda wa hapa kwetu hata kwenye zoezi dogo la Kiswahili!
Ni kweli ripoti inaonesha nchi zote tatu bado zinafanya vibaya ukilinganisha na malengo ya mitaala yao.Hali ni mbaya katika ujifunzaji (learning outcomes) wakati kwa wastani nchi zote zimefanya uwekezaji mkubwa sana kwenye elimu. Sasa tufanyeje? Hivi kweli East Africa federation ama kama ambavyo sasa inapendekezwa, United States of East Africa, itatufaidia? Nimeweka link hizo hapo chini kwa page zenye ripoti ma kurasa nyingine zenye posters zinazofupisha matokeo ya tafiti. Karibuni.

The report and posters and photos from the poster 1 yellow headline.jpg launch are now on-line on the website: Are our Children Learning: Numeracy and Literacy Across East Africa 2011? :: Our publications :: Media :: Twaweza.org and on Facebook http://www.facebook.com/media/set/?set=a.196172990431242.47721.110627155652493#!/media/set/?set=a.196172990431242.47721.110627155652493 and Twitter: http://twitter.com/#!/Twaweza_NiSisi

Please forward, share, retweet and ‘like’.
 
hawajui kisoma kiswaili or ndio wanaiga uzungu?wanajua sana bt wanafunzi wakibongo wanaona kuongea kiingereza ndio usomi ukiongea kiswaili sio msomi na unaonekana mshamba,vilevile kwa upande mwingine labda wanajifunza kiingereza si unaelewa ngeli ndio lugha inayotumika kufundishiwa so wanakariri sio kosa lao lakini si unaelewa sikuzote mbongo alivyo ataonekana vp kama anajua.
 
hawajui kisoma kiswaili or ndio wanaiga uzungu?wanajua sana bt wanafunzi wakibongo wanaona kuongea kiingereza ndio usomi ukiongea kiswaili sio msomi na unaonekana mshamba,vilevile kwa upande mwingine labda wanajifunza kiingereza si unaelewa ngeli ndio lugha inayotumika kufundishiwa so wanakariri sio kosa lao lakini si unaelewa sikuzote mbongo alivyo ataonekana vp kama anajua.
vitabu vyenyewe vimeandikwa kwa kizungu, acha wanafunzi wa watu wakomae na hiyo lugha.
 
Wanafunzi wa Tz si tu hawajui kusoma kiswahili, hata kingereza hawajui pia.
 
Si kweli kuwa wanafunzi wa Tz hawajui kusoma kiswahili. Kichwa cha mada kiko kijumla-jumla sana na waliochangia wameingia kichwakichwa kuchangia. Unatakiwa kujua na wanafunzi wa darasa au kidato cha ngapi? Hiyo tool iliyotumika je, inakubaliana na mitaala ya elimu ya darasa husika kwa nchi zote tatu? Ikiwa 90% walishindwa kusoma mtihani uliowekwa, je hii inamaanisha wanafunzi wote hawajui kusoma? Uwakilishi wa hao waliotahiniwa ulizingitia usawa mf. Ke na me, mijini na vijijini, shule binafsi na serikali, wanaofaulu sana darasani na wale wanaoshindwa.

Ripoti iliyokuwa imetulia ni ile ya Haki Elimu.
 
Back
Top Bottom