Ripoti mgonjwa wa sindano tata MNH yatua kwa wazir

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,080
James Magai
RIPOTI ya uchunguzi wa sakata la kudungwa sindano tata mtoto Imran Mwerangi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), imekamilika na tayari imepelekwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa hatua zaidi.
Imrani alidungwa sindano hiyo miezi sita iliyopita na kumfanya alazwe katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU), baada ya kupata mtindio wa ubongo na mwili kupooza.

Taarifa zilizopatikana jana zilisema kuwa jopo madaktari limegundua ‘madudu’ katika suala hilo hatua ambayo uongozi wa MNH umeona uombe kwanza ushauri wa wizara kabla ya kuanza kulishughulikia.

Alhamisi iliyopita, uongozi wa MNH ulikutana na mama wa mtoto huyo, Amina Mwerangi na kumtaarifu kuwa umeunda jopo la madaktari bingwa kuchunguza suala hilo na kuahidi kutoa taarifa Jumatatu juma hili.
Hata hivyo, juzi uongozi wa hospitali hiyo ulishindwa kuwakabidhi wazazi wa mtoto huyo taarifa hiyo ambayo wamekuwa wakiisubiri kwa hamu ili kujua hatima ya mtoto wao.

Jana, habari zilieleza kuwa tayari jopo la madaktari lililoundwa kuchunguza suala hilo limeshakamilisha kazi yake na liliikabidhi ripoti yake kwa Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Dk Merina Njelekela.

Baba wa mtoto
Baba wa mtoto huyo Iddy Mwerangi ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dodoma, alisema waliitwa jana asubuhi ofisini kwa Dk Njelekela na kuelezwa kuwa ripoti hiyo imekamilika.
“Alisema ripoti imekamilika lakini wameiandikia barua wizara kuomba maelekezo ya hatua za kuchukua,” alisema Mwerangi akimnukuu Dk Njelekela.

Mwerangi alisema licha ya Dk Njelekela kukiri kuipokea taarifa hiyo, hakuikabidhi kwa familia kama alivyoahidi wala familia hiyo haikuelezwa kilichomo zaidi ya kuambiwa kunahitajika kwanza ushauri wa wizara.
Alisema uongozi wa MNH umekiri kuwa tatizo la awali la mtoto huyo yaani mtindio wa ubongo na kuvimba tezi za pua, bado halijashughulikiwa na kwamba linahitaji ufumbuzi wa haraka huku tatizo jipya alilolipata hospitalini hapo likiwa ni la kudumu hali itakayomfanya awe tegemezi.

Alisema pamoja na hayo, wamekubaliana kuwa mtoto huyo ataendelea kuwa chini ya uangalizi wa hospitali mpaka wizara itakapotoa maelekezo.

Baba huyo wa mtoto alisema, Profesa Victor Mwafyongo na Dk Mulungu wataendelea kumwangalia kwa karibu mtoto huyo na kuwasiliana kwa karibu na wazazi.

Hata hivyo, alisema familia yake haikuridhishwa na uongozi wa Muhimbili kushindwa kuchukua hatua za haraka baada ya taarifa hiyo kukamilika ili kupata ufumbuzi wa haraka wa matatizo yanayomkabili mtoto huyo.
Mwerangi alisema baada ya kupata taarifa hizo, walikaa na kuzitafakari na sasa wanatafuta ushauri kwa baadhi ya wataalamu wa tiba ambao nao wameeleza kutoridhishwa na mlolongo wa utaratibu huo ambao unachelewesha kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya mtoto.

Alisema kwa mujibu wa wataalamu hao, baada y ripoti hiyo kukamilika, hospitali ilikuwa na uwezo wa kufanya uamuzi na kuitaarifu tu wizara na si kuomba na kusubiri maelekezo yake.

“Mtoto yuko kwenye critical condition, (hali mbaya) hivyo inaweza kufikia mahali kwamba sasa amepata rufaa kupelekwa kwa mfano, India kwa matibabu zaidi tukaambiwa kuwa tumeshamchelewesha kwa hiyo hata kwa matibabu ambayo yangeweza kufanyika basi yakashindikana,” alisema.

Alisema wanajipanga leo kumwandikia barua Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Haji Mponda kumwomba aingilie kati na kutoa tamko ili hatua za haraka za matibabu ziweze kuchukuliwa, kwa kuwa amekaa ICU muda kwa mrefu na hakuna lolote lililofanyika.

Dk Njelekela pamoja na Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa hospitali hiyo, Aminiel Aligaeshi hawakupatika jana kuzungumzia ripoti hiyo baada ya simu zao za mkononi kuita bila kupokewa.

Yaliyomsibu mtoto
Mtoto huyo alifikishwa hospitalini hapo kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa nyama zilizokuwa puani lakini alidungwa sindano tata iliyomuathiri zaidi afya yake.

Baada ya kudungwa sindano tata, familia iliitaka hospitali hiyo kutoa maelezo ya kuridhisha baada ya baadhi ya madaktari na wahudumu wa hospitali hiyo kutaka kumrejesha nyumbani akiwa katika hali hiyo isiyo na matumaini.
Katika barua hiyo ya Januari 10, mwaka huu, Mwerangi licha ya malalamiko hayo, aliomba maelezo ya kuridhisha kuhusu tatizo hilo na ufumbuzi wake.

chanzo.
Ripoti mgonjwa wa sindano tata MNH yatua kwa waziri
 
Ripoti nyingi zinazohusu madhara ya kusababishwa hucheleweshwa sana au kurekebishwa, au vyote kwa pamoja, ili kuwalinda watu au taasisi fulani.

Lakini kutolewa mara moja kwa taarifa hiyo kungekuwa na manufaa kwa Jumuia yote, na si kwa wazazi wo mtoto huyo tu, kwani bila shaka taarifa hiyo ingechangia kupunguza uwezekano wa tukio kama hilo kujirudia.
 
Back
Top Bottom