Elections 2010 Ripoti hii si ya kupuuza hasa kutoka kwa shuhuda......isome!!!!

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
Ripoti hizi si za kupuuza hasa ikitoka kwa shuhuda 31/10/2010
0 Comment(s)

Nimekuwa nikifuatilia machapisho ya bloga, Albert Paul na licha ya kuwa blogu yake haina umaarufu zilizonao blogu nyingine, kijana Albert amekuwa akiandika mambo mengi ya msingi na yenye mantiki katika maisha. Si bloga wa habari za kuchota na kubandika kama tufanyavyo wengi, mara nyingi yeye amekuwa akiandika mambo halisi ya maisha anapokutana nayo. Hili ni mojawapo ya toleo lake ambalo halifai kupuuzwa:

5527848.jpg
Albert Paul​
Jana nilikuwa kwenye mchakato wa kuapishwa kwa mawakala watakaosimamia na kuangalia kura za wagombea ili zisiende kusikokusudiwa na kusiko kwa matakwa ya wapiga kura.

Shughuli hii ilifanyikia katika shule ya Msingi Makiungu. Mbali na zoezi hili, pia kulikuwa na semina kwa ajili ya wasimamizi wa uchaguzi.

Zoezi hili la kuapishwa kwa mawakala halikwenda vizuri hata kidogo. Mchakato huu ulikuwa na dosari mbalimbali na ambazo kwa kiasi kikubwa zitakuwa na adhari sana kwa vyama vya upinzani na hasa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA).

Majina mengi ya watu waliojitolea kuwa mawakala wa vyama walijikuta wakikosa nafasi hizo na badala yake kuchukuliwa na watu wengine bila hata kuwa na sababu za kueleweka.

Kwa mujibu wa wananchi wanasema kuwa majina ya watu waliotakiwa kuapishwa ni yale yaliyotolewa na ofisi ya tume ya uchaguzi ngazi ya wilaya ambayo yaliwasilishwa na wagombea wa vyama husika.

Kasoro nyingine iliyojitokeza ni ile ya mtu mmoja kuwa wakala wa vyama viwili kwa wakati mmoja wakati wapo wale waliojitolea kwa dhati katika kusimamia na kulinda kura za vyama husika kizalendo na kwa moyo wote, lakini wakaikosa nafasi.

Miongoni mwa mawakala wa CHADEMA, wapo mawakala wawili ambao watu hawakuweza kuwafahamu kabisa na ilibidi wafuatiliwe kwa ukaribu ili kuweza kutambua uhalali wao wa kuweza kuwa mawakala wa CHADEMA pamoja na kuwa walikuwa wameshaapishwa.

Niliwashuhudia mawakala wa CHADEMA muda mfupi kabla ya kuapishwa. Ni ukweli usiopingika kuwa, wengi wao walikuwa ni wazee na akinamama ambao wengi walionekana wasio na uelewa wa mambo ya uchaguzi na ambao wataweza kurubuniwa kirahisi mno. Tetesi zinasema kuwa chama tawala katika jimbo hili kimetenga takribani Tsh 800,000 kwa kila kituo cha uchaguzi kwa ajili ya kuhonga endapo mambo yatakuwa sivyo kwa upande wao. Kama hili ni la kweli, basi kwa hali ya mawakala wa CHADEMA a kwa jinsi nilivyowaona na namna walivyopatikana, basi kuna hatari kubwa sana ya CHADEMA kuangukia pua. Na kwa hili, CHADEMA itabidi ijilaumu kwani wawakilishi wa CHADEMA waliokuwa wanasimamia zoezi hili angalao nao walitakiwa wapewe list ya majina ya mawakala waliokubalika na chama na ambayo pia ndiyo iliyotumwa kwenye ofisi ya Tume ya uchaguzi ngazi ya wilaya kama kweli utaratibu huu ulikuwepo.

Binafsi nilikuwa miongoni mwa watu niliojitolea kusimamia kura za CHADEMA lakini kwa bahati mbaya ama nzuri, jina langu halikuonekana. Hakukuwa na sababu za kueleweka kwa nini ikawa hivyo. Kilichonishangaza zaidi ni kuwa, mawakala wa chadema walikuwa wengi, na mara baada ya majina kutajwa, ya wale watakaoapishwa, basi kundi lile likawa kama limegawanywa mara mbili. Yani ikawa kama vile idadi ya mawakala ilichukuliwa mara mbili zaidi ya wale waliokuwa wanahitajika. Hapa nina wasiwasi sana wa kuwepo kwa"mapandikizi" ambayo yataweza kufanikisha kirahisi wizi wa kura.

Kwa utafiti mdogo nilioufanya, mawakala walioachwa, walionekana kujua nini wangetakiwa kufanya na waliokuwa na ujasiri, walikuwa ni watu waliokuwa tayari kusimamia haki na kukitetea chama chao. Inasemekana watu hawa waliwekwa kando kwa makusudi kamili na hili linadhaniwa kuwa lilifanywa baada ya majina yaliyokubaliwa chamani kuwasilishwa kwenye ofisi ya tume ya uchaguzi ngazi ya wilaya.

Jambo jingine ambalo nililishuhudia ni hili la mawakala kuhamishwa kwenda kusimamia vituo ambavyo hawakujiandikisha. Hili nililiona kwa mawakala wa CHADEMA , sijui kwa mawakala wa vyama vingine kama hali hii ilijitokeza. Hii inamaanisha kuwa, mawakala waliopangwa kwenye vituo tofauti na walivyojiandikisha, wataikosa fursa ya kupiga kura. Kwa maana hii, kama kuna mchezo mchafu, na kama mawakala hawa ni wakereketwa wa kweli wa CHADEMA , basi kwa mtindo huu, kura nyingi za CHADEMA zitapotea.

Kuna swali la kujiuliza hapa, CHADEMA ilikuwaje wasiwapatie madiwani wao ambao pia wanagombea (ambao ndio walionekana kuwa watendaji wakuu kwenye zoezi hili) nakala za majina ambayo chama kiliyaafiki? Pengine kwa hili, hawana budi kujilaumu.

Nimalizie kwa kusema kuwa, kwa hali niliyoiona katika mchakato huu wa kuapishwa mawakala, kama hali ndio hii kwenye vingi ya vijiji vyetu, basi upinzani hususani CHADEMA wanaweza kupoteza kura nyingi ambazo zilikuwa halali yao. Na urahisi huu wa kuweka mapandikizi hususani vijijini ni miongoni mwa sababu zifanyazo mara nyingi vijijini vyama vya upinzani kuangukia pua na hatimaye watu wanasema kuwa CCM inapendwa na watu wa vijijini eti kwa sababu ni chama cha Mwalimu Nyerere

from: - Habari
 
Duh imenistua kidogo ila najua mafisadi hawatakubali waachie kirahisi. mapambano yanaendelea.
 
Hizi ndio habari ambazo CHADEMA inabidi izijue.

Duh aiseee kwa hali hii bado tuna wakati mrefu sana wa kufikia hii Democrasia. Hawa jamaa wanatumia kila njia wawezayo kuiba kura. But it wont last long. The same happened in Brazil, chama kilichokua kinatawala, kilikua kinafanya haya haya for 76 years but ilifika wakati hata hao mamluki walichoka na tabia hii. Manake inachosha ukuona unajiibia kura mwenyewe. Hao wanaopewa hela wanasahau kwamba watoto wao ifikapo Jumatatu inabidi waende shule, huko shule hamna madawati wala waalimu kwa sababu ya sera mbovu ya hao CCM ambao wamewapa hela...! Wanasahau hata wakiugua gafla wakati wanasimamia huo uchaguzi watabidi wakimbizwe hospitali (zahanati) ambayo haina dawa kwa sabau ya hio hio CCM ambayo wanaikumbatia.

Anyway, time will tell. Yo may cheat some people for some time but, not all the people for all the time...!
 
Nyamagana tayari kimeeleweka, mawakala kibao wa CHDEMA wametoweka...
 
Ripoti hizi si za kupuuza hasa ikitoka kwa shuhuda 31/10/2010
0 Comment(s)

Nimekuwa nikifuatilia machapisho ya bloga, Albert Paul na licha ya kuwa blogu yake haina umaarufu zilizonao blogu nyingine, kijana Albert amekuwa akiandika mambo mengi ya msingi na yenye mantiki katika maisha. Si bloga wa habari za kuchota na kubandika kama tufanyavyo wengi, mara nyingi yeye amekuwa akiandika mambo halisi ya maisha anapokutana nayo. Hili ni mojawapo ya toleo lake ambalo halifai kupuuzwa:

5527848.jpg
Albert Paul​
Jana nilikuwa kwenye mchakato wa kuapishwa kwa mawakala watakaosimamia na kuangalia kura za wagombea ili zisiende kusikokusudiwa na kusiko kwa matakwa ya wapiga kura.

Shughuli hii ilifanyikia katika shule ya Msingi Makiungu. Mbali na zoezi hili, pia kulikuwa na semina kwa ajili ya wasimamizi wa uchaguzi.

Zoezi hili la kuapishwa kwa mawakala halikwenda vizuri hata kidogo. Mchakato huu ulikuwa na dosari mbalimbali na ambazo kwa kiasi kikubwa zitakuwa na adhari sana kwa vyama vya upinzani na hasa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA).

Majina mengi ya watu waliojitolea kuwa mawakala wa vyama walijikuta wakikosa nafasi hizo na badala yake kuchukuliwa na watu wengine bila hata kuwa na sababu za kueleweka.

Kwa mujibu wa wananchi wanasema kuwa majina ya watu waliotakiwa kuapishwa ni yale yaliyotolewa na ofisi ya tume ya uchaguzi ngazi ya wilaya ambayo yaliwasilishwa na wagombea wa vyama husika.

Kasoro nyingine iliyojitokeza ni ile ya mtu mmoja kuwa wakala wa vyama viwili kwa wakati mmoja wakati wapo wale waliojitolea kwa dhati katika kusimamia na kulinda kura za vyama husika kizalendo na kwa moyo wote, lakini wakaikosa nafasi.

Miongoni mwa mawakala wa CHADEMA, wapo mawakala wawili ambao watu hawakuweza kuwafahamu kabisa na ilibidi wafuatiliwe kwa ukaribu ili kuweza kutambua uhalali wao wa kuweza kuwa mawakala wa CHADEMA pamoja na kuwa walikuwa wameshaapishwa.

Niliwashuhudia mawakala wa CHADEMA muda mfupi kabla ya kuapishwa. Ni ukweli usiopingika kuwa, wengi wao walikuwa ni wazee na akinamama ambao wengi walionekana wasio na uelewa wa mambo ya uchaguzi na ambao wataweza kurubuniwa kirahisi mno. Tetesi zinasema kuwa chama tawala katika jimbo hili kimetenga takribani Tsh 800,000 kwa kila kituo cha uchaguzi kwa ajili ya kuhonga endapo mambo yatakuwa sivyo kwa upande wao. Kama hili ni la kweli, basi kwa hali ya mawakala wa CHADEMA a kwa jinsi nilivyowaona na namna walivyopatikana, basi kuna hatari kubwa sana ya CHADEMA kuangukia pua. Na kwa hili, CHADEMA itabidi ijilaumu kwani wawakilishi wa CHADEMA waliokuwa wanasimamia zoezi hili angalao nao walitakiwa wapewe list ya majina ya mawakala waliokubalika na chama na ambayo pia ndiyo iliyotumwa kwenye ofisi ya Tume ya uchaguzi ngazi ya wilaya kama kweli utaratibu huu ulikuwepo.

Binafsi nilikuwa miongoni mwa watu niliojitolea kusimamia kura za CHADEMA lakini kwa bahati mbaya ama nzuri, jina langu halikuonekana. Hakukuwa na sababu za kueleweka kwa nini ikawa hivyo. Kilichonishangaza zaidi ni kuwa, mawakala wa chadema walikuwa wengi, na mara baada ya majina kutajwa, ya wale watakaoapishwa, basi kundi lile likawa kama limegawanywa mara mbili. Yani ikawa kama vile idadi ya mawakala ilichukuliwa mara mbili zaidi ya wale waliokuwa wanahitajika. Hapa nina wasiwasi sana wa kuwepo kwa"mapandikizi" ambayo yataweza kufanikisha kirahisi wizi wa kura.

Kwa utafiti mdogo nilioufanya, mawakala walioachwa, walionekana kujua nini wangetakiwa kufanya na waliokuwa na ujasiri, walikuwa ni watu waliokuwa tayari kusimamia haki na kukitetea chama chao. Inasemekana watu hawa waliwekwa kando kwa makusudi kamili na hili linadhaniwa kuwa lilifanywa baada ya majina yaliyokubaliwa chamani kuwasilishwa kwenye ofisi ya tume ya uchaguzi ngazi ya wilaya.

Jambo jingine ambalo nililishuhudia ni hili la mawakala kuhamishwa kwenda kusimamia vituo ambavyo hawakujiandikisha. Hili nililiona kwa mawakala wa CHADEMA , sijui kwa mawakala wa vyama vingine kama hali hii ilijitokeza. Hii inamaanisha kuwa, mawakala waliopangwa kwenye vituo tofauti na walivyojiandikisha, wataikosa fursa ya kupiga kura. Kwa maana hii, kama kuna mchezo mchafu, na kama mawakala hawa ni wakereketwa wa kweli wa CHADEMA , basi kwa mtindo huu, kura nyingi za CHADEMA zitapotea.

Kuna swali la kujiuliza hapa, CHADEMA ilikuwaje wasiwapatie madiwani wao ambao pia wanagombea (ambao ndio walionekana kuwa watendaji wakuu kwenye zoezi hili) nakala za majina ambayo chama kiliyaafiki? Pengine kwa hili, hawana budi kujilaumu.

Nimalizie kwa kusema kuwa, kwa hali niliyoiona katika mchakato huu wa kuapishwa mawakala, kama hali ndio hii kwenye vingi ya vijiji vyetu, basi upinzani hususani CHADEMA wanaweza kupoteza kura nyingi ambazo zilikuwa halali yao. Na urahisi huu wa kuweka mapandikizi hususani vijijini ni miongoni mwa sababu zifanyazo mara nyingi vijijini vyama vya upinzani kuangukia pua na hatimaye watu wanasema kuwa CCM inapendwa na watu wa vijijini eti kwa sababu ni chama cha Mwalimu Nyerere

from: - Habari

Hali hii ni mbaya. Kweli CHADEMA wamekamiwa kuangushwa na kura zao kwenda kusiko. Duh! Mola tunusuru!
 
Miimi nimeshangaa kituo nilichopigia kura yangu hapa Dar es Salaam asubuhi saa 1 na nusu mwakala walikuwa hawajafika. Walikuwepo wale wa tume lakini si wa kutoka kwenye vyama. Eneo nililo pigia vilikuwepo vituo takribani 8, wasi wasi wangu huenda vyma vilijiandaa kutuma wakala mmoja kwa kituo kimoja yaani centre moja, lakini sasa ndani ya hiyo centre unakuta kuna section nyingi za kupigia mfano A1, A2, A3, VIVYO VIVYO KWA B, C nk..,

Hii pia inatia shaka kwani wakitaka chakachua itakuwa rahisi sana kwani hao mawakala wa vyama hawapo kila ki section! Cjui walichelewa fika ama ni kweli hawakupanga hao wawakilishi?
 
Kuna swali la kujiuliza hapa, CHADEMA ilikuwaje wasiwapatie madiwani wao ambao pia wanagombea (ambao ndio walionekana kuwa watendaji wakuu kwenye zoezi hili) nakala za majina ambayo chama kiliyaafiki? Pengine kwa hili, hawana budi kujilaumu.

Kazi nzuri iliyofanyika muda woooote inaweza kuharibiwa kwa uzembe tu (tena labda wa mtu mmoja) na ukosefu wa umakini. Tuombe Mungu aweke mkono wake na mbinu chafu zishindwe vibaya
 
Jamani kuna kitengo ndani ya chadema kinachoratibu na kushughulikia haya mambo wakati hizi habari zinajitokeza? Au nao chadema makao makuu wamechakachuliwa?
 
Kama ni kweli chadema hawakuwa makini kwenye mawakala ili kuhakikisha wako makini na hawawezi kurubuniwa basi tumeshaliwa. Inasikitisha sana.
 
Kwa hali hii tushaliwa,inaelekea ni sehemu nyingi tu mpaka huko Nyamagana,sijui lakini...
 
The last thing turn to is Prayers.
Mungu hamtupi mja wake, and finally hakuna marefu yaiyokuwa na ncha.

Kupambana watapambana, lakini hawatashinda! By the grace of The Lord Jesus!
 
Back
Top Bottom