RIP John Ngahyoma

RIP JOHN NGAHYOMA

Ngayoma.jpg
 
Naamini kama angeamka hata dk tano aone hizi RIP messages angezikataa kabisa. Maana jamaa kasota pale Hospt Segerea hakuna hata mshjikaji wala jamaa wa kumuona. Alikuwa anauliza- hivi fulani yupo, hivi jamaa yangu fulani yupo, hivi yule mwandishi yupo, hivi yule dada fulani yupo. Akijibiwa kuwa wote hao wapo alikuwa anatoa machozi. '' Kila mpatapo msiba basi jifunzeni kwa hilo"

Lakini la muhimu jamani tunapokuwa wazima tujitahidi sana kujali sana familia zetu, wala tusiwanyanyase wake zetu kwa sababu ya kuwa busy na mademu wa hapa mjini, Mungu hakawii kuwalipia kisasi wanaowanyanyasa wake zao wa ujana ( Simaanishi Ngahyoma ndiyo alivyokuwa) ila mwenye macho na aone neno ambalo Roho aiambia JF leo...........................
\\ujumbe mzito
laiti MUNGU ANGAWEZA KUUSAMBAZA KWA KILA MTANZANIA NATUMAINI AKUNA ANGETOKA NJE YA NDOA NAMAANISHA KUZINI
MUNGU AKUPE NGUVU MPWA KATIKA WAKATI HUU WA HUZUNI NI KWELI KUMEKUWA NA WANAFIKI WENGI SANA SANA HASA UNAPOTOKEA MSIIBA NIMEPATA KUWA KARIBU KUMSALIMU HALIMA AKIWA HAI NA HASA KIPINDI AKIWA ANAUMWA HAKIKA UMATI ULIOTOKEA TANGU JUZI NAHISI ASILIMIA 80 ALIONANA NAO MARA YA MWISHO 2006 NA ALIPOPATWA NA STROKE TU KILA MTU AKALA TIME ZAKE..TUFIKE WAKATI TUACHANE NA UNAFIKI WA KISHENZ SISEMI WEWE NASEMA WEWE ULIEHUSIKA KUMJUA AMA KUWAJUA MAREHEMU WAKIWA WANAUMWA NA WENGINE WAMEFIKIA KUULIZA ATI HHE HALIMA ALIENDELEEA KUTANGAZA ULITAKA AMTANGAZIE NANI??NI LIKE IFI HEEE KUMBE MGONJWA ALIKUWA STRONG SO TUSIHISHI HIVI NA TUSISUBIRI MSIBA NDI O TUANZE KUKIMBIZANA ...NIMEONA WAGONJWA WENGI WAKIWA WANAUMWA AWAITAJI PESA ZENU MFANO HALISI NI HALIMA...WENGI WALIJITOLEA KUMTIBIA WAKIONGOZWA NA TBC SO ALIHOKUWA AKIITAJI NI UPENDO WENU TU AKIWAONA ANAKUWA NA FURAHA NA HATA KAMA ANA MAUMIVU YANAKIMBIA JAMANI ..

NATWAKIA MAISHA MEMA YASIYO NA UNAFIKI
 
RIP J Nganhyoma.

Mwaka 2011 utakumbukwa kwa kuondokewa na nguli wa tasnia ya habari. Watu watu ambao watakumbukwa katika habari Tanzania ni
  1. Adam Lusekelo
  2. Halima Mchuka
  3. John Ngahyoma
 
Naamini kama angeamka hata dk tano aone hizi RIP messages angezikataa kabisa. Maana jamaa kasota pale Hospt Segerea hakuna hata mshjikaji wala jamaa wa kumuona. Alikuwa anauliza- hivi fulani yupo, hivi jamaa yangu fulani yupo, hivi yule mwandishi yupo, hivi yule dada fulani yupo. Akijibiwa kuwa wote hao wapo alikuwa anatoa machozi. '' Kila mpatapo msiba basi jifunzeni kwa hilo"

Lakini la muhimu jamani tunapokuwa wazima tujitahidi sana kujali sana familia zetu, wala tusiwanyanyase wake zetu kwa sababu ya kuwa busy na mademu wa hapa mjini, Mungu hakawii kuwalipia kisasi wanaowanyanyasa wake zao wa ujana ( Simaanishi Ngahyoma ndiyo alivyokuwa) ila mwenye macho na aone neno ambalo Roho aiambia JF leo...........................

Maneno Mazito sana Mkuu

Maneno kuntu haya. Ila cha kujiuliza ni je habari za ugonjwa walikuwa nao hao waliokuwa wanaulizwa?. Watu wengi wamepatwa na mshtuko baada ya kupokea taarifa za msiba bila kuwa na taarifa za awali juu ya kuugua kwa nguli huyu. Ni kweli ugonjwa ni issue binafsi ila unapokuwa Public figure kama John Ngahyoma ilitakiwa watu wawe aware maana alitoweka hewani BBC tokea October 2010.
 
Alitoweka oi. Huyu alikuwa anafanya kazi Mbili Mbili hadi Tatu dah alikuwa mchapa kazi wa Ukweli NSSF ITV NA BBC pengine pale NSSF udini ulimkimbiza.... kama bado alikuwepo bahti yake... Dah Huyu nakumbuka Sauti yake kwani nilikuwa naweza kuiigiza. Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rekma Amuweke Pahari Panapo Stahili....
 
Amefariki dunia leo asubuhi nyumbani kwake jijini dar es salaam.hii ni kwa mujibu wa bbc swahili jioni hii.amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu.mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa kaka yake mkunguni,na anatarajiwa kuzikwa siku ya jumapili katika makaburi ya kinondoni.ameacha mjane na watoto watatu (R.I.P).mungu ailaze roho ya marehemu kwa Amani

Kipunguni
 
R.I.P John I will never forget you Brother ulikuwa zaidi ya mtangazaji na reporter katika jamii ya watanzania.
 
Back
Top Bottom