Ridhiwani Kikwete Kuchunguzwa Na TAKUKURU Mpaka Aruhusu? Gazeti Jambo Leo

Plato

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
420
94
SAM_2288.JPG

Wakuu nimeikuta hii kule Mjengwablog, eti Ridhiwani amebariki usalama wa taifa na TAKUKURU wamchunguze.

Swali ni kuwa kumbe huyu asipotaka kuchunguzwa haiwezekani kwani ni mpaka atoe ruhusa?
Kwa picha zaidi za magazeti ya leo mnaweza kwenda www.mjengwablog.com
 
Story nyingi ni maneno ya vijiweni, mara ana hili mara hili,watu wakikuona unaingia sehemu basi kitega uchumi chako,watanzania tunaishi kwa dhana tu.
 
Nawashanga Watanzania mnaolalama. Mwaka 2010 wakati Riz1 alipokuwa anazungusha fomu za babaake kusaka saini za wanaChama Cha Magamba kumridhia kuwa mgombea wa Urais kupitia Chama hicho, kulizuka kioja. Baba mtu aliposailiwa inakuwaje 'mtoto' huyo ateke jukumu la chama wakati wako watendaji kibao ndani ya chama na ambao huo ni wajibu wao wa msingi? Unajua 'baba' alisemaje! Alijibu: (nami namnukuu), ''Suala la kugombea urais ni la kwangu mie. Kwani kuna ubaya gani kumwamini mwanangu mpendwa kunitafutia saini za udhamini?'' (mwisho wa kunukuu). Ikiwa urais ni 'ishu' ya familia ya JK, sasa ninyi mnashangaa nini Riz1 kuwaruhusu (tena ataelekeza namna ya kuchunguzwa) TAKUKURU kumfanyia uchunguzi. Au mmekwishasahu kwamba yeye ni sehemu ya utatu mtakatifu wa Ikulu yetu? Teh! Teh! Teh! Ninyi mlie tu na wivu wenu wa kike!! (TAMWA kunradhi)
 
View attachment 55713

wakuu nimeikuta hii kule mjengwablog, eti ridhiwani amebariki usalama wa taifa na takukuru wamchunguze.

Swali ni kuwa kumbe huyu asipotaka kuchunguzwa haiwezekani kwani ni mpaka atoe ruhusa?
Kwa picha zaidi za magazeti ya leo mnaweza kwenda www.mjengwablog.com
kwanini sasa wakati kauli hizi kuhusu shuguli zake zimekua zikipigiwa kelele inaonekana amekamilisha kuficha nyaraka muhimu na kuandikisha makampuni yake kwa majina ya watu wengine and then anasema njooni mnikague kichekesho na usanii wa ccm!
 
Hivi ile kesi aliyosema atamfungulia Dr. Slaa kwa kumuita fisadi imefikia wapi?

Lakini hii nayo ni kali? Kikwete ambaye hataki watuhumia wa ufisadi mkubwa washitakia (ref Hosea and WIKILeaks). Leo hii anabariki TAKUKURU imuchunguze? (Rz1 and JK ni kitu kimoja).
 
kwanini sasa wakati kauli hizi kuhusu shuguli zake zimekua zikipigiwa kelele inaonekana amekamilisha kuficha nyaraka muhimu na kuandikisha makampuni yake kwa majina ya watu wengine and then anasema njooni mnikague kichekesho na usanii wa ccm!
Hivi lile tishio lake la kuwashitaki wanaomchafua liliishia wapi?
 
Mwizi anawaalika polisi waje wamsachi then wakimkkamata na kitu wampeleke jela..wapi na wapi ..hio Takururu yenyewe takururu? mwambieni angoje hadi 2016 ndio aongee hivi vijimaneno

anataka kuuza magazeti tu huyu dogo hana lolote..
 
Takukuru ya Hosea wa JK au nyingine. Mwizi anaomba kukamatwa, hii kali!!!
 
Asilete usanii wa mjini,kuna ushahidi wa kutosha kabisa namna namna wanavyovuja hela za umma,asubir baba yake aachie madaraka waandamwe na kashfa,ni bora uendelee kuiba ukakaa kimya kuliko kuamsha hasira zetu,hayo yote anayokanusha ni ya kweli
 
View attachment 55713

Wakuu nimeikuta hii kule Mjengwablog, eti Ridhiwani amebariki usalama wa taifa na TAKUKURU wamchunguze.

Swali ni kuwa kumbe huyu asipotaka kuchunguzwa haiwezekani kwani ni mpaka atoe ruhusa?
Kwa picha zaidi za magazeti ya leo mnaweza kwenda www.mjengwablog.com

Impunity will never last forever; kama unabisha fuatilia yaliyowakuta hawa hapa! Karim Abdoulaye Wade (Senegal), Gamal na Alaa Hosni Mubarak (Misri), Uhuru Jomo Kenyatta (Kenya), Peter Bingu Wa Mutharika (Malawi), Teodor obiang Nguema (Equatorial Guinea); just to mention a few! leo anatesa; he calls the shots, lakini maisha yako dynamic hayasimami, yakija mabadiliko ambayo lazima yaje tu apende asipende he will be held to account.
 
Toka lini mtu agaoga na nguo? Takukuru hawa hawa? waache kuchezea watanzania.
 
hatutaki abariki cha msingi asubiri 2015 hapo ndipo atakiona cha moto na ndipo atakapojua kuwa kuku hakojoi.
 
Nasubiri kauli ya dr slaa kwani anayajua yake mengi na ilishamtisha kumshitaki.
 
Back
Top Bottom