Ridhiwani Kikwete jina lake linatumika kumdhulumu mjane Arusha

Kwa mtaji wa hayo maneno yako yanayoonyesha kuwa na ukweli ndani yake, hadi hapo nasema HESHIMA MBEEEEEELE KAMA TAI kwa huyu kijana mwenzetu, Ridhiwani Kikwete katika kusaidia mjane huyu asizulumiwe kitu.

Pamoja na yote, bado tuendelee kufuatilia hili jambo kimya kimya hadi tupate ukweli wote kwamba mwisho wake umekua vipi.

Taifa linalodhulumu akina mama wajane na watoto yatima wana laana lisilokomesheka.

Mtoa mada ameweka kinyume kinyume maana ukweli ni kwamba huyo mzee wa madili ni mtu wa Fred Lowassa na haijulikani mambo hayo yote kama huyo kina anajua ama la.

Pia fuatilieni mutajua kwamba hata mali za huyo mama alisaidiwa kuziokoa kwa msaada wa Riz na hata sasa ndiye anamsaidia kuzuia huyo mzee wa madili asimdhulumu huyo mjane.

Huyo mjane namfahamu sana nilipokua Arusha nilikutana naye alisaidiwa kuokoa migodi yake ya Tanzanite na Riz na sasa nasikia mgodi umetema. Kama alimsaidia kuokoa mali za mabilioni na sasa anamsaidia mahakamani (kaangalieni kumbukumbu) itakuaje awe anataka kumdhulumu.

Inawezekana mtoa mada alisikia tu kwamba kuna "mtoto wa kigogo" anayemlinda mzee wa madili anayetaka kumdhulumu mjane.
 
Kijana Mwenzetu, Ridhiwani Kikwete,

ni vema ukapata kuelewa ya kwamba kama sisi wengine huku uswahilini, unalo jukumu lisilokwepeka hata kidogo kwetu sisi WaTanzania wenzako (si kutokana na kuwa mtoto wa rais wa taifa letu) kuturidhisha kwamba wajane na mayatima wote ndani ya mipaka ya taifa hili KAMWE HAWAZULUMI HATA KI-MSUMARI kutoka kwenye mali halali ya m/wazazi wao.

Jukumu hili tunalolizungumzia ni vema ukaanza kulitekeleza tena bila kulazimika kubembelezwa tangu kwa huyu mama wa Jijini Arusha. Hiyo ndio maana tunazaliwa ili tuwe msaada kwa waliotutangulia kuzaliwa.

Ukiwa kidonda, tena kuongezeke na kitu dhuluma juu???????????????
 
salaam kaka
Nimeipenda post yako.. lakini mi nina swali moja nataka kuuliza hvi hizi taarifa ulizotuletea hapa una uhakika nazo au ni blaablaa za vijiweni..Nasema hivyo isije kuwa ni maneno tu ya kusikia mtaani na wewe bila kuyafanyia utafiti uanayapost hapa ili kuonesha baadhi ya watu na makampuni kuwa yanaendesha dhulma mijini... ni hayo tu
 
Kwa upande wa hili ghorofa la mjane ni kweli Njake alimkopesha mume wa huyu mama hela na akawa ameandikishana hii nyumba. Baadaye deni akashindwa kulipa na akaomba grace period aweze kulipa ila njake kwa kuwa ni mhujumu anayejidai mlokole alikataa. Baadaye yule mdaiwa akapata hela yote na riba akampelekea Njake akakataa kupokea kisa anataka kulinganisha vilaki vya mkopo na nyumba ya ghorofa iliyoko sehemu ya biashara ya mabilioni. Kwa kifupi waliendesha kesi huku Njake akihonga sana na mwishowe alishindwa. Kwenye rufaa pia yule mama alishinda baada ya mume kuwa amefariki (sijui kifo cha asili au vipi).
Kwa ufupi utajiri wa Njake ni full maswali, ni mrushaji mkubwa sana anayetumia mgongo wa ulikole kuibia watu wasio na hatia. Kwake bora ufe kuliko shilingi yake ipotee. Kwa ufupi Njake ana umafia mbaya sana kwa mali za watu na ngoja mengine asitiriwe tu maana tukisema yote mtashangaa!!! Hizi ndizo kada za Chama.

Khaa!! Taarifa zilizonifikia mezani kwangu zinasema Njake karudisha jengo kwa mama mjane wiki kadhaa zilizopita. ila sina uhakika kama ni kwa maagizo yake au la ila vijana wake wamefanya uharibifu mkubwa kama vile kuziba njia za maji taka, kuvunja vyoo nk. RIP Njake :shetani:
 
Khaa!! Taarifa zilizonifikia mezani kwangu zinasema Njake karudisha jengo kwa mama mjane wiki kadhaa zilizopita. ila sina uhakika kama ni kwa maagizo yake au la ila vijana wake wamefanya uharibifu mkubwa kama vile kuziba njia za maji taka, kuvunja vyoo nk. RIP Njake :shetani:

Mkuu hakika ni habari njema hizi japo kuna uharibifu but mama atapumzika na kesi sasa. Hakika familia ya Njake ni wahuni wakubwa sana, wanajidai sana na huo utajiri. Hivi yule kijana wake alifia India kwa mazingira tata wakati kesi ya Babake ya EPA ikiwa ndo imeanza kunguruma na mwili ukaletwa akazikwa kimya kimya hivi ilikuaje??????? Utajiri mwingine bwana!!!!! Halafu eti imagine akakutana na rafikia yake mmoja DSM wakati tu ametoka kuzika mtoto na wala hakumwambia kuwa alifiwa!!!!! Ni mshangao wa ajabuuuuuu sana!!!! Rest in Peace motto!!
 
Back
Top Bottom